Umeniharibia maisha! ...what?

Duh hiyo bold imenikamata sana, well mi nadhani ni mtu kushindwa kuelewa au kujua anataka mwnza wa aina gani, anajiingiza kwa mtu na kuanza kumsoma wakati anakuwa tayari kwenye mahusiano, cha muhimu ni mtu ku focus, kujua nini ni nini, na kitu gani hakipendi......kuchagua mwenza sio jambo la kukurupuka, wengi wetu tunafanya maamuzi ya haraka na kuja kujuta badae, tunapokatishwa ndio tunaanza kujutia maamuzi yetu, mwisho nahitimisha "hakuna kuharibiwa maisha na mtu ni wewe mwenyewe ndio ulijiharibia" kwa kushindwa kuchagua nazi mpaka ukapat koroma

Nice Gaga,

hapo kwenye kosa la kujiingiza kwenye mahusiano kwanza, kisha unaanza kumsoma mtu ndio kosa mojawapo!
Lakin i hebu twende mbele tukirudi nyuma.
Mfano; wazee wetu wa miaka ya 60s kurudi nyuma, wengi hawakuwa Boyfriend na Girlfriend kwenye ujana wao. Wengi wao walikutanishwa through mawifi, mashemeji, mashangazi nk...
Wengi wao walioana na kuja fahamiana ndani ya ndoa. Wengi wao wameleana mpaka vifo vinawatenganisha.

Tatizo lipo wapi miaka hii ya leo kiasi kwamba "tunaona kuna umuhimu wa kufahamiana kwanza" kabla ya kuoana?
Je, ni muda gani unahitajika kumfahamu mwenzako ndipo muoane? na kujiridhisha nini mnataka maishani?

Bado nataka kuamini nhili neno 'umeniharibia maisha' halina maana yeyote kwa anayelitamka ila kukupandikizia lawama.
 
Michango mizuri wakuu.

Tukitoa wale wapumbavu ambao wanajua kabisa hawana malengo na mtu lakini wanaamua kuwa na mtu hili kukamilisha mambo yao binafsi,kuna mengine watu huwa wanajitakia wenyewe. Na mengi yameelezwa juu na wadau wengine mie ningependa kuongeza kwamba mawasiliano muhimu kwenye mahusiano yetu. Tuwe na moyo wa kuuliza pale tunapoona kasoro sio kukaa kimyaa mpaka siku inafika kwamba damage iliofanyika kubwa kihasi cha kuhisi kwamba maisha yako yameharibiwa.

Unapozungumza tatizo lolote na mpenzi wako mapema unampa nafasi ya kujirekebisha na unajipa nafasi wewe mwenyewe ya kufanya maamuzi mapema kama hato jirekebisha.
 
Mbu... signature ya Gaga imemaliza yote kwenye hili la kuharibiana maisha, and it is a quote from MJ1...

No one screw your life, unless you gave them the screw driver!
 
Nadhani ni aina flan ya uselfish.... Maisha mmeishi pamoja iweje ulalamike yako ndo yameharibiwa? Na unapotishia kujiua lengo lako ni nini?

I have bn there and believe me usipokuwa makini utajikuta unastick kwa mtu si kwa kuwa unampenda la hasha ni kwa kuwa unaogopa kumwacha kwani atajiua!

It is selfishness mydear, hakuna justification yeyote kumtambulisha mtu wa aina hii.
Yeye hupima thamani ya matamshi yake kwa reaction yako,...ukijikubalisha kuwa msukule kila siku utaishia
kumkimbiza A&E au kumnywesha maziwa...wahka kila siku maishani...! Hawafai watu wa aina hii acha tuitwe 'makatili' wa mapenzi.

Easier said than...

vipi, nawe una tendency za u suicidal? Unaamini ukijiua ndio utakuwa umemkomoa mhusika?

Mkuu
Mimi hii imenitokea MARA 2 recently
Kwanza wanaanza kujiapiza NAFUTA NAMBA ZAKO ZOTE
Then baadae anakuja na NAONA BORA NIFE TU, SIWEZI KUISHI BILA WEWE CPU, UKISIKIA NIMEKUFA USISHANGAE, NIMESHAKUAGA RASMI.
Finally inakuja "Kumbe kweli umeshani-delete kwenye mind yako"

Dah, pole sana CPU...sasa mnaendeleaje? au ndio ushachukuliwa msukule kwenye maamuzi magumu?

Ningependa kusikiliza upande wapili wa hii mada.
Wenye mioyo midogo na kufikiria kutishia kujiua ndio solution ya matatizo...
Kwanini mnafikiria hivyo?
 
mimi kwa upande wangu hakuna kuharibiwa maisha...Labda kupotezewa muda....Ntarudi tena, ngoja nitafakari!..
mimi nafikiri kama ni maisha wote wawili tunashirikiana kuyaharibu ila kwenye swala la kupotezeana muda mmoja ndio anaweza akawa anapotezewa muda.
 
Duh we bwana nafikiria kuku'rudishia' proposal yako! We have too many things in common loh hahhh

Yes kwa hapo ilikuwa emotional blackmailing... Nimejifunza what RR hav just put down, enjoy the love while it last....if it last forever I concider myself blessed and if it last shortly I consider my self lucky. Life has to go on and no one is responsible for your life, only you.

....looollllllll!!!!.....ha ha ha! kwa PM au?
 
Nice Gaga,

hapo kwenye kosa la kujiingiza kwenye mahusiano kwanza, kisha unaanza kumsoma mtu ndio kosa mojawapo!
Lakin i hebu twende mbele tukirudi nyuma.
Mfano; wazee wetu wa miaka ya 60s kurudi nyuma, wengi hawakuwa Boyfriend na Girlfriend kwenye ujana wao. Wengi wao walikutanishwa through mawifi, mashemeji, mashangazi nk...
Wengi wao walioana na kuja fahamiana ndani ya ndoa. Wengi wao wameleana mpaka vifo vinawatenganisha.

Tatizo lipo wapi miaka hii ya leo kiasi kwamba "tunaona kuna umuhimu wa kufahamiana kwanza" kabla ya kuoana?
Je, ni muda gani unahitajika kumfahamu mwenzako ndipo muoane? na kujiridhisha nini mnataka maishani?

Bado nataka kuamini nhili neno 'umeniharibia maisha' halina maana yeyote kwa anayelitamka ila kukupandikizia lawama.
Mbu wazee wa zamani walilelewa kwa misingi imara na sheria kali ambazo waliweza kuzidhibiti kwa kipindi kile, nafikiri pia population ilikuwa ndogo hivo ikawa rahisi watu wanajuana hadi vijiji vya jirani, sio siku hizi hata jirani yako humjui ni nani, utaweza kweli mpa mwanawe maadili hata ukiona anapotoka?
Mahusiano ya siku hizi yametupa nafasi ya kusomana na bado tunafeli hapo utajua kwamba mapenzi hayana darasa, nikirudi kwa wazee, pia walikuwa na matatizo ila kuyajua utayajuaje?globalization imatusaidia sana in one way or another, embu ona leo hii najua mbu alipitia nini katika mahusiano yake wakati maybe unaishi london, na mbu leo anajua Gaga alipitia nini na niko mbali kabisa
Mie nawashauri vijana ambao bado mnatafuta wapenzi wa kuishi nao mtumie hii advantage ili kupembenua mabo ya mahusiano, ingawa hayawezi kuwa perfect asilimia mia moja lakini kuna ambacho kitakusaidia
 
Hahahh CPU duh kweli limekutokea.... Ila reminder si kina dada tu ambao hukimbilia huko bali kuna wakaka pia haah

Yaani nilivyoona Mbu kaweka hii mada nikajiapiza na mimi . . . " Hapa na mimi nasema kila kitu"
Ni kweli MJ1 hii haina jinsia. Mi nimeelezea upande wangu kama mwanaume. Atakuja mwanamke ataelezea upande wake.
 
mimi nafikiri kama ni maisha wote wawili tunashirikiana kuyaharibu ila kwenye swala la kupotezeana muda mmoja ndio anaweza akawa anapotezewa muda.

Husninyo nakushukuru sana kwa uwazi wako hapa.
Now, sit back and reflect what you've just written there...
  1. kuharibiana maisha maana yake nini?
  2. malengo yako (maishani na mapenzi) ni nini?
Maswali yangu ni guidance tu, ...nahisi nimekuelewa umesimamia upande gani kwenye mada hii...
It's ok...kuwa muwazi tu. Karibu tujadiliane kwa mtazamo wako, kwa mapana zaidi.
 
Dah, pole sana CPU...sasa mnaendeleaje? au ndio ushachukuliwa msukule kwenye maamuzi magumu?

Mi kwa kweli naogopa sana watu wa aina hii. Yaani hata kama nimempenda vipi, akifikia hatua ya kusema ANAJIUA KWA AJIRI YANGU nabadilisha mawazo fasta. Maana naamini hii kauli ina maana zaidi ya hapo aliposema. Inaweza kugusa hata ktk maeneo mengine pia. Ipo siku akisikia tetesi tu kwamba CPU anatembea na MJ1 akaamua "Bora nimwekee sumu kwenye msosi afe kuliko kumuona akitesa na MJ1"
Baadae baada ya kumuua CPU anagundua kwamba MJ1 hana mawasiliano na CPU mwaka umepita, na wala hajawahi hata kujua sura ya CPU
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mkuu una maanisha anaeacha asilaumiwe? lawama lazima ziwepo coz kuna upande wa pili ambao umeathirika na kitendo chako, na kila mtu ana haki ya kujisikia au kufanya afanyalo ili ajisikia au ujumbe ukufikie kwamba kaumia kiasi gani, then utampa reason kazi inabaki kwake, kwa mwenye upeo atafurahi kwamba umemwambia umemchoka kwa sasa, ila king'ang'anizi ndio atakuja na single ya kujiua

Kama hanipendi tena, kwa nini azuge bado ananipenda? japo hoja yangu haiwajumuishi wale wanaAsante kwa mj1 kwa kunirahisishia maana....mapenzi sio lazima yawe ya milele...binadam si tunabadilika?
 
Mkuu..mimi nadhani vitu vyote vinatokana na Journey of love”.. unajua wakati mapenzi yanaanza yanakuwa kama asali..yaani watu wanachanganyikiwa na wengine wanakosa hata uwezo wa kufikiria mazuri na mabaya..yaani hasa kina dada wanashindwa kujua kama porojo za wanaume ni zina ukweli au vipi..as a human instinct ..wanaume wamejaliwa uwezo wa kucheza na akili za kina dada hivyo ni sehemu ndogo ya kina dada wanakuwa ngangari na mtego huu.. Sasa, ukiangalia vizuri suala la kuharibiana maisha lipo sana toka kwa kinadada ..kuwaambia kinakaka..kwani kinadada wanapenda kiukweli wakati asilimia kubwa ya wanaume wana .. “artificial feelings ambazo zinasukumwa sana na tamaa za mwili.

Mimi nafikiri..Katika kipindi hiki ambacho mapenzi ni asali hapo ndipo porojo za wanaume zinapom-maliza mwanamke..wakati mwanamme anatunga porojo ili alidhishe tamaa yake ..masikini mdada anapenda kwa ukweli ..na zile sense za kuhisi hatari zinakuwa zimezima..Sasa mwanaume akishashiba ..ile graph ya mapenzi inashuka ghafla..na mwanamke anazinduka toka katika usingizi..huu ni wakati wa panic anaweza fanya lolote..lakini kama akitulia ile panic itaisha.. kwa upande wa mwanaume kwa sababu alikuwa na artificial life’ hatotilia maanani..hivyo basi hata rafiki ya kike akimwambia amemuharibia maisha haitoingia kichwani kwani yeye alikuwa anataka kitu fulani tena kwa muda fulani..yaani hata msichana kama hatajiua hii haitaingia akilini kwa mwanume ..yaani hata msichana hakikuambia maisha yake hayana thamani yaani ni kumpigia mbuzi gitaa ..kwani ni kweli maisha ya msichana yalikuwa hayana thamani toka mwanzo..kilichokuwa na thamani ni mwili..

Lakini, in contrast..kama wote wawili..mlipendana kiukweli..na mkapanga mambo mengi kwa ajili ya baadaye..halafu ikatokea kitu nje ya uwezo wenu kutofanikisha malengo yenu..Kama dini..wazazi..n.k..Hapo wote wawili mtayumba kisaikolojia..na hata kama mtapata wapenzi wapya hapo baadaye..lile jeraha halitofutika kamwe..
 
Mkuu..mimi nadhani vitu vyote vinatokana na Journey of love".. unajua wakati mapenzi yanaanza yanakuwa kama asali..yaani watu wanachanganyikiwa na wengine wanakosa hata uwezo wa kufikiria mazuri na mabaya..yaani hasa kina dada wanashindwa kujua kama porojo za wanaume ni zina ukweli au vipi..as a human instinct ..wanaume wamejaliwa uwezo wa kucheza na akili za kina dada hivyo ni sehemu ndogo ya kina dada wanakuwa ngangari na mtego huu.. Sasa, ukiangalia vizuri suala la kuharibiana maisha lipo sana toka kwa kinadada ..kuwaambia kinakaka..kwani kinadada wanapenda kiukweli wakati asilimia kubwa ya wanaume wana .. "artificial feelings ambazo zinasukumwa sana na tamaa za mwili.

Mimi nafikiri..Katika kipindi hiki ambacho mapenzi ni asali hapo ndipo porojo za wanaume zinapom-maliza mwanamke..wakati mwanamme anatunga porojo ili alidhishe tamaa yake ..masikini mdada anapenda kwa ukweli ..na zile sense za kuhisi hatari zinakuwa zimezima..Sasa mwanaume akishashiba ..ile graph ya mapenzi inashuka ghafla..na mwanamke anazinduka toka katika usingizi..huu ni wakati wa panic anaweza fanya lolote..lakini kama akitulia ile panic itaisha.. kwa upande wa mwanaume kwa sababu alikuwa na artificial life' hatotilia maanani..hivyo basi hata rafiki ya kike akimwambia amemuharibia maisha haitoingia kichwani kwani yeye alikuwa anataka kitu fulani tena kwa muda fulani..yaani hata msichana kama hatajiua hii haitaingia akilini kwa mwanume ..yaani hata msichana hakikuambia maisha yake hayana thamani yaani ni kumpigia mbuzi gitaa ..kwani ni kweli maisha ya msichana yalikuwa hayana thamani toka mwanzo..kilichokuwa na thamani ni mwili..

kiwango sana hii post
 
Mbu wazee wa zamani walilelewa kwa misingi imara na sheria kali ambazo waliweza kuzidhibiti kwa kipindi kile, nafikiri pia population ilikuwa ndogo hivo ikawa rahisi watu wanajuana hadi vijiji vya jirani, sio siku hizi hata jirani yako humjui ni nani, utaweza kweli mpa mwanawe maadili hata ukiona anapotoka?
Mahusiano ya siku hizi yametupa nafasi ya kusomana na bado tunafeli hapo utajua kwamba mapenzi hayana darasa, nikirudi kwa wazee, pia walikuwa na matatizo ila kuyajua utayajuaje?globalization imatusaidia sana in one way or another, embu ona leo hii najua mbu alipitia nini katika mahusiano yake wakati maybe unaishi london, na mbu leo anajua Gaga alipitia nini na niko mbali kabisa
Mie nawashauri vijana ambao bado mnatafuta wapenzi wa kuishi nao mtumie hii advantage ili kupembenua mabo ya mahusiano, ingawa hayawezi kuwa perfect asilimia mia moja lakini kuna ambacho kitakusaidia

that's deep! hongera sana.
wenye macho, akili na utambuzi wasome, watafakari na kuelewa.
Shukran sana Gaga.

Mi kwa kweli naogopa sana watu wa aina hii. Yaani hata kama nimempenda vipi, akifikia hatua ya kusema ANAJIUA KWA AJIRI YANGU nabadilisha mawazo fasta. Maana naamini hii kauli ina maana zaidi ya hapo aliposema. Inaweza kugusa hata ktk maeneo mengine pia. Ipo siku akisikia tetesi tu kwamba CPU anatembea na MJ1 akaamua "Bora nimwekee sumu kwenye msosi afe kuliko kumuona akitesa na MJ1"
Baadae baada ya kumuua CPU anagundua kwamba MJ1 hana mawasiliano na CPU mwaka umepita, na wala hajawahi hata kujua sura ya CPU

kweli wewe una experience nzuri ya hii kitu!
utawajua haraka kwani tendency yao mojawapo ni attention seekers wa hali ya juu.
Ni wepesi ku claim wanakuwa victimized...wanajidekeza kupita kiasi!

By the time unakuja gundua janja yao, wanakuwa wesha infiltrate kwa ndugu jamaa na marafiki zako wote
ambao nao wanakuangalia kwa jicho la "kwanini unamtesa mwenzio!?"...akisha wa win trust yao, anatoa makucha yake!

Anyway, wengi wao ni tabia walizokua nazo tangu utotoni.
'Born to (?)' manipulate others!
 
  • Thanks
Reactions: CPU
kama hanipendi tena, kwa nini azuge bado ananipenda? japo hoja yangu haiwajumuishi wale wanaAsante kwa mj1 kwa kunirahisishia maana....mapenzi sio lazima yawe ya milele...binadam si tunabadilika?[/QUOTE
Ni kweli kabisa RR ila yule mtendwaji hataondoka kimya lazima atakupa maneno mawili matatu ili aweze ku move on, haijawahi kukutokea umekosana na mpenzi na unataka ku move on ila unahitaji siku moja tu uongee yaliyo moyoni ayasikie then unajisikia kama umetua zigo zito moyoni na unajihisi mwepesi unaendelea na maisha hapo hata aje na maelezo gani tena hurudi nyuma
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Husninyo nakushukuru sana kwa uwazi wako hapa.Now, sit back and reflect what you've just written there...
  1. kuharibiana maisha maana yake nini?
  2. malengo yako (maishani na mapenzi) ni nini?
Maswali yangu ni guidance tu, ...nahisi nimekuelewa umesimamia upande gani kwenye mada hii...It's ok...kuwa muwazi tu. Karibu tujadiliane kwa mtazamo wako, kwa mapana zaidi.
tunaharibiana maisha pale ambapo tunatenda mambo ambayo kwa kujua au kutojua yataharibu mafanikio yetu ya baadae au yatakuwa ni vikwazo kwa sasa tukapohitaji kusonga mbele. Mfano mmoja mkubwa ni mimba wakati bado tunasoma. Lawama tunawapa wanaume ila na binti husika umechangia kiasi kikubwa kujiharibia maisha, umechangia kujiwekea vikwazo vya kutosonga mbele katika maisha yako ya kielimu. Umechangia kwa sababu ulikuwa unajua matokeo ya kufanya ngono, (kwa case hii exclude waliopata mimba kwa kubakwa). Na kwa mwanaume pia amechangia kwa maana anajua binti unasoma na asingetakiwa kukurubuni au angekulinda kwa namna yoyote asikupe mimba. Hvyo wote hapo mmeyaharibu maisha yenu.Kuhusu swali la malengo yangu mbu, malengo yapo mengi ila kimahusiano ni kutengeneza familia nitakapoona nipo tayari kufanya hvyo.Nafikiri nimeeleweka.
 
...mkuu tunahitaji michango ya kiwango hiki mara kwa mara.
Huu mchango wako umekwenda shule kwa asilimia kubwa sana...kama ni maksi nimgetoa A*...

Safi sana! Na matarajio kina dada wengi kwa nia nzuri tu watafaidika na hii posting yako, na sisi wanaume tujifunze ni kwa kiasi gani tunachangia kulaumiwa sana kwenye maisha haya ya mapenzi.

Let us all be responsible, please!

Mkuu..mimi nadhani vitu vyote vinatokana na Journey of love".. unajua wakati mapenzi yanaanza yanakuwa kama asali..yaani watu wanachanganyikiwa na wengine wanakosa hata uwezo wa kufikiria mazuri na mabaya..yaani hasa kina dada wanashindwa kujua kama porojo za wanaume ni zina ukweli au vipi..as a human instinct ..wanaume wamejaliwa uwezo wa kucheza na akili za kina dada hivyo ni sehemu ndogo ya kina dada wanakuwa ngangari na mtego huu.. Sasa, ukiangalia vizuri suala la kuharibiana maisha lipo sana toka kwa kinadada ..kuwaambia kinakaka..kwani kinadada wanapenda kiukweli wakati asilimia kubwa ya wanaume wana .. "artificial feelings ambazo zinasukumwa sana na tamaa za mwili.

Mimi nafikiri..Katika kipindi hiki ambacho mapenzi ni asali hapo ndipo porojo za wanaume zinapom-maliza mwanamke..wakati mwanamme anatunga porojo ili alidhishe tamaa yake ..masikini mdada anapenda kwa ukweli ..na zile sense za kuhisi hatari zinakuwa zimezima..Sasa mwanaume akishashiba ..ile graph ya mapenzi inashuka ghafla..na mwanamke anazinduka toka katika usingizi..huu ni wakati wa panic anaweza fanya lolote..lakini kama akitulia ile panic itaisha.. kwa upande wa mwanaume kwa sababu alikuwa na artificial life' hatotilia maanani..hivyo basi hata rafiki ya kike akimwambia amemuharibia maisha haitoingia kichwani kwani yeye alikuwa anataka kitu fulani tena kwa muda fulani..yaani hata msichana kama hatajiua hii haitaingia akilini kwa mwanume ..yaani hata msichana hakikuambia maisha yake hayana thamani yaani ni kumpigia mbuzi gitaa ..kwani ni kweli maisha ya msichana yalikuwa hayana thamani toka mwanzo..kilichokuwa na thamani ni mwili..

Lakini, in contrast..kama wote wawili..mlipendana kiukweli..na mkapanga mambo mengi kwa ajili ya baadaye..halafu ikatokea kitu nje ya uwezo wenu kutofanikisha malengo yenu..Kama dini..wazazi..n.k..Hapo wote wawili mtayumba kisaikolojia..na hata kama mtapata wapenzi wapya hapo baadaye..lile jeraha halitofutika kamwe..

...ila experiences zinatofautiana, nilikuwa kwenye relationship iliyodumu miaka zaidi ya kumi. Kama ni 'Love Joint acount' - banking, basi nilihakikisha naweka akiba ya kutosha kunufaisha account,...bahati mbaya, wakati mimi naamini figure kwenye 'Love deposit receipts', mwenzangu alikuwa anacheza na 'Love ATM'... Siku nakurupuka, account tayari ilishakuwa overdrawn....---maisha yakabakia tunaishi kwa 'Overdraft!' - Mapenzi haya...!
 
...

Duh! Pole sana.. ilibidi uwe unatumia "internet banking" na ku-check statements mara kwa mara..hapo ungeshagundua kabla "account haija-overdraft" si unajua tena kuna "salesmen" wanawadanganya sana wapenzi wetu kununua bidhaa zao..
 
Husninyo nakushukuru sana kwa uwazi wako hapa.
Now, sit back and reflect what you've just written there...
  1. kuharibiana maisha maana yake nini?
  2. malengo yako (maishani na mapenzi) ni nini?
Maswali yangu ni guidance tu, ...nahisi nimekuelewa umesimamia upande gani kwenye mada hii...
It's ok...kuwa muwazi tu. Karibu tujadiliane kwa mtazamo wako, kwa mapana zaidi.

Swahiba... kwenye tima na maendeleo ya jamiii wanasema the first step towarsd healing is accepting that you have problems, and in this case ni kwamba youare part of the problem

sasa unapoona mtu anahamisha shida au lawama zote kwa one party ujue kabisa huyo mtu hana dalili ya kuerevuka au kuelewa nini maana ya mapenzi.... it takes two to tangle and at any particular time, wote wanakua part ya furaha na wanakua part ya huzuni

to me mtu akiniambia nimemaribia maisha napata mawazo haya;
yeye si mtu bali ni kitu and i was using it
yeye hana utut wala utashi wa kung'amua chochote, i am the driver, screw drive and a screwer
yeye hajui kwanini alikua na mimi... irresponsible etc

the only place where this statement is valid ni kama ntakua nimemvictimize kazini, kumbaka, kumuibia, kumtapeli etc

otherwise the sentence is a blanket to cover up for ones ignorance
 
Ndio maana nimekufa nimeoza kwa JF.........Ni zaidi ya darasa yaani.....

Thank you Mbu,MJ1,Gaga,Husninyo,MTM,RR,CPU,AW na wengine for your Useful Posts......

Nikiri kwamba kwa muda mfupi tu nilioptia bandiko hili nimejifunza mengi kweli.......Mbarikiwe sana.....

Hakika 'No one screw your life, unless you gave them the screw driver!'-Gaga's signature
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom