Kujutia kunakuelemea maisha yako je, unawezaje kuishi bila kujutia?

Nov 2, 2023
60
50
Kujutia maana yake ni kutochukua hatua yoyote kwenye tukio lililotokea na kubaki nalo umelikumbatia kimawazo. Na matokeo yake litachukua nasafi na kuharibu mambo mengine kuweza kufanyika kwa nafasi yake. Majuto ni chanzo cha kufanya maovu mengi, utajikuta unahamasika kufanya uamuzi usio na maana kwa lengo la kupunguza au kutaka kujitoa kwenye majuto yako na kuongeza madhara zaidi.

Watu wengi wameharibu furaha ya maisha yao kwa kujutia waliyoyafanya kwakujitendea wao au watu wengine. Kujutia kunamadhara mengi sana ya kiakili ya kukufanya ushindwe kufanya mambo yako ya msingi uliyo na mudi nayo kwa kukufadhaisha akili yako bila kujua. Maamuzi mengi yasiyo na maana hutokea muda huu kwa kujiona huna thamani na kukufanya ujione upande wa ubaya wako peke yake.

Kitu gani kinachotupelekea tuumie sana na yaliyopita na tushindwe kabisa kuyaacha yapite. Raha ya maisha nikuyaishi kwa furaha 'sherehekea' . Tunawezaje kuishi kwa furaha na bado tukafanya makosa juu yetu na kwa wengine. Lazima tujiulize kwanza je, tunaweza kuishi bila kufanya kosa lolote?. Au mifumo yetu tunavyoishi imetujengea kosa linakushusha thamani yako na kuonekana hufai.

Ujinga wetu wenyewe ndio unamchango mkubwa kwenye kutufanya tujutie. Makosa kwenye maisha hayaepukiki, huwezi kujua hata jambo jema la sasa litakujakuwa na matokeo gani badae. Hatuwezi kuwa na mawazo chanya kiasi cha yakadhibiti makosa yetu yote. Kwa ufupi mfumo wetu wa kimawazo na hisia kwa ujumla haupo mikononi mwetu na ndio huwa chanzo kikubwa cha matendo yetu.

Kama tumeshaona ushawishi wa matendo yako upo nnje ya uwezo wako jambo la muhimu ni lipi kujua. Tunahitaji matendo yetu yatoke kwenye zao la kuelewa na matokeo yake yatabaki kama yalivyo na thamani yake ilivyotakiwa kutendeka muda huo. Ufahamu unatakiwa uchukue nafasi kubwa kuliko hisia za mawazo. Kuweza kutofanya kitu kitachokupa hisia ya kuumia wewe au mtu mwingine kuna muda hilo jambo haliwezekani.

Ila una ubora gani wa ufahamu wa kuelewe na kujitambua hilo ndio lamuhimu zaidi.

Nb: Kujutia hakuna maana yoyote kimsingi na niugonjwa unaohitaji kuutibu. Ni kama umebeba begi kubwa linalokuelemea ambalo halina faida yoyote kwenye safari yako zaidi linakupunguzia nguvu za unapotaka kuelekea.
 
Yesterday is History, Tomorrow is mystery, but today is Gift...

Ishi leo, achana na historia, historia hipo kutukumbusha, ila hatupaswi kuikumbatia... Kujitia maana yake unalazimisha unalazimisha kuishi kwenye wakati uliopita badala ya kujifunza kuishi leo na kesho yenye fumbo.
 
Back
Top Bottom