Umeme umegoma kupita kanisani kwa Kakobe

Hamna kitu kibaya kama kumeza kila kitu bila kutafuna. Inaonekana there is a chunk of folks humu bongo who could easily be tricked that there is chocolate in every box..Ndo maana JK alisema kuwa 70% ya wabongo ni wafuata upepo..So sad indeed.
The Following User Says Thank You to Abdulhalim For This Useful Post:

Bigirita (Today)​
 
Kama umeme unaingia ndani ya kanisa lake inakuwaje huu wa kupita ushindwe? Je, tatizo lipo kwenye eneo la Kakobe tu na kwingine kama Mawasiliano Towers hakuna shida hiyo? Kama tatizo lipo kwenye lines zote na nzima kutoka Ubungo mpaka Victoria basi si kwa sababu ya sala za Kakobe.

Mimi ni RC, tuna amri kumi za Mungu; ya kwanza inasema,"Mimi ndimi bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine". Sasa kwa wale ambao mnamsifia Kakobe kwa maombi yake kuwenu makini kwani anaweza kuwa anatumia miungu mingine au nguvu za giza. Haiwezekani kitu cha manufaa kwa nchi na wananchi unakizuia na kusema eti mungu atazuia. Kwanza huo uaskofu alipewa na nani? Kwanza sala gani muda wote ni sadaka, fungu la kumi na kuombea tu, hakuna kushukuru?

Yesu mwenyewe walimsingizia anatumia nguvu za baalizebubu, sembuse sisi wanadamu..tatizo wewe umedanganywa na kina pengo na kilaini huko, na kuabudu kwamo maria, ndo unaleta upupu wako hapa, unawaaibisha wakatoliki wenzio! ni ajabu kuwa hadi leo hii mtu kujiita m RC anaona proud..hahaha, jamani poleni kwa kweli.
 
Very funny stuff.......Kakobe mwenyewe ana umeme nyumbani kwake...wa TANESCO....three phases na wakikata tu kwa mgao au vinginevyo anakuwa mbogo :pound:.......hapa tunataka kutoana roho...oooh ana nguvu sijui nini....:twitch:
 
Kama umeme unaingia ndani ya kanisa lake inakuwaje huu wa kupita ushindwe? Je, tatizo lipo kwenye eneo la Kakobe tu na kwingine kama Mawasiliano Towers hakuna shida hiyo? Kama tatizo lipo kwenye lines zote na nzima kutoka Ubungo mpaka Victoria basi si kwa sababu ya sala za Kakobe.

Mimi ni RC, tuna amri kumi za Mungu; ya kwanza inasema,"Mimi ndimi bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine". Sasa kwa wale ambao mnamsifia Kakobe kwa maombi yake kuwenu makini kwani anaweza kuwa anatumia miungu mingine au nguvu za giza. Haiwezekani kitu cha manufaa kwa nchi na wananchi unakizuia na kusema eti mungu atazuia. Kwanza huo uaskofu alipewa na nani? Kwanza sala gani muda wote ni sadaka, fungu la kumi na kuombea tu, hakuna kushukuru?

.
Kalaga bao!! Kwanza wewe jiulize ni Mungu yupi unaemwabudu, je ni yule ambae alimwamuru mfalme Sauli kuwauwa Wamidiani wote kuanzia mfalme, mzee hadi mtoto mchanga na wanyama wote au? Kama ni huyo swali lako halina maana yeyote, ila tu ni wivu wa kile atendacho mungu nje ya kanuni za asili ya kimaumbile. Kwa nini mtizamo wako umemweka Shetani juu ya Mungu? Maana kila pakiwepo na ishara na miujiza sawa na neno la Mungu wa biblia kwa waaminio, wewe unakimbilia kumpa Shetani huo uwezo kwa kuziita nguvu za giza. Dini yako imekupofisha maana imejengwa juu ya msingi wa kuitawala dunia hii kiintelijensia, kwani dini na wokovu vimeachana kama mashariki ilivyo mbali na magharibi. Nakushauri ndugu utafute wokovu wa Yesu Kristo na achana na hayo mapokeo ya kizee yaliyo maagizo ya wanadamu.
 
Maendeleo yememuua nani?

.
Watu wote waliokufa kwa ajali za vyombo vya moto, visingelikuwepo wasingekufa. Tena mabadiliko ya maumbile nchi yanayosababishwa na shughuli za kimaendeleo za binadamu yamewaua watu zaidi ya chochote kile ulichowahi kufikiri.
 
Hivi umeme bado umegoma kupita kwa Kakobe?? Mboni hamtupi updates wajameni ??? -_-
 
Bwana amesikia kilio cha baba askofu kakobe

Hivi Umeme Ukipita Utakuwa Tayari kukiri kama Mungu ameshindwa? Jamani tusipende sana kumsingizia Mungu Mambo mengine halafu yasipokuwepo tunamruka
 
HTML:
.
Kalaga bao!! Kwanza wewe jiulize ni Mungu yupi unaemwabudu, je ni yule ambae alimwamuru mfalme Sauli kuwauwa Wamidiani wote kuanzia mfalme, mzee hadi mtoto mchanga na wanyama wote au? Kama ni huyo swali lako halina maana yeyote, ila tu ni wivu wa kile atendacho mungu nje ya kanuni za asili ya kimaumbile. Kwa nini mtizamo wako umemweka Shetani juu ya Mungu? Maana kila pakiwepo na ishara na miujiza sawa na neno la Mungu wa biblia kwa waaminio, wewe unakimbilia kumpa Shetani huo uwezo kwa kuziita nguvu za giza. Dini yako imekupofisha maana imejengwa juu ya msingi wa kuitawala dunia hii kiintelijensia, kwani dini na wokovu vimeachana kama mashariki ilivyo mbali na magharibi. Nakushauri ndugu utafute wokovu wa Yesu Kristo na achana na hayo mapokeo ya kizee yaliyo maagizo ya wanadamu.

Ukiristo siyo mapokeo pia?
 
HTML:

Ukiristo siyo mapokeo pia?

.
Ukristo kwa maana ya badiliko la nafsi kwa kuzaliwa upya ndani ya ufalme sio mapokeo. Ila kujifariji kwa majina ya kikristo bila badiliko la nafsi ndio haswaa mapokeo.
 
Mitanzania bana!

Kweli Mkuu, kuna mijitu imepewa akili kwa ajili ya kufikiri, wenyewe wameweka akili zao rehani.
Kinachoongelewa hakina uthibitisho watu wanadiriki kuonyesha ukasuku wa kutotumia akili kabisa!!
Mijitu mingine bwana!!!!
 
mbona hamna habari maalumu? kama umegoma kweli, tuambieni basi, sio speculations tu hapa...
Jamani hakuna watu wa Tanesco hapa? Hao ndio wanaweza kutujuza kulikoni!
Mimi nimesikia asubuhi likiongelewa kwenye vichwa vya magazeti lakini sina hakika nalo.
 
Umeme haujagoma kupita kwa kakobe, kinachosubiriwa ni transformer iliyoagizwa kutoka japan, ikiingia inakuwa fitted kisha unawashwa, by the way ile sio distribution line ya kupeleka umeme majumbani bali ni transmission line ( njia kuu ya usafirishaji umeme ) na unapelekwa makumbusho substation kupoozwa ukiwa unatokea kwenye gridi; kisha kusambazwa dar es salaam, na hiyo itaboresha quality of power and availability
 
Jamani hakuna watu wa Tanesco hapa? Hao ndio wanaweza kutujuza kulikoni!
Mimi nimesikia asubuhi likiongelewa kwenye vichwa vya magazeti lakini sina hakika nalo.

Umeme haujagoma kupita kwa kakobe, kinachosubiriwa ni transformer iliyoagizwa kutoka japan, ikiingia inakuwa fitted kisha unawashwa, by the way ile sio distribution line ya kupeleka umeme majumbani bali ni transmission line ( njia kuu ya usafirishaji umeme ) na unapelekwa makumbusho substation kupoozwa ukiwa unatokea kwenye gridi; kisha kusambazwa dar es salaam, na hiyo itaboresha quality of power and availability
 
Kama umeme unaingia ndani ya kanisa lake inakuwaje huu wa kupita ushindwe? Je, tatizo lipo kwenye eneo la Kakobe tu na kwingine kama Mawasiliano Towers hakuna shida hiyo? Kama tatizo lipo kwenye lines zote na nzima kutoka Ubungo mpaka Victoria basi si kwa sababu ya sala za Kakobe.

Mimi ni RC, tuna amri kumi za Mungu; ya kwanza inasema,"Mimi ndimi bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine". Sasa kwa wale ambao mnamsifia Kakobe kwa maombi yake kuwenu makini kwani anaweza kuwa anatumia miungu mingine au nguvu za giza. Haiwezekani kitu cha manufaa kwa nchi na wananchi unakizuia na kusema eti mungu atazuia. Kwanza huo uaskofu alipewa na nani? Kwanza sala gani muda wote ni sadaka, fungu la kumi na kuombea tu, hakuna kushukuru?

Mimi sisali kwa kakobe, lakini hapo kwenye red pananitia mashaka. Hv askofu ni lazima achaguliwe na papa ndy awe askofu. Huyo babu yenu anmekolonaiz sana akili zako. Biblia yako hiyohiyo inasema Mungu ni mmoja, na hashindwi jambo, amini nakwambia ukisali utaweza kuhamisha milima iliyoshindikana. Aaamen.
 
Mambo mengine yanatia aibu hata kuyasoma. Hivi kuna mtanzania mwenye uwezo wa kutype kwenye keyboard hapa kwenye jamii forums ambaye akili yake inamtuma kabisa kuwa umeme hauwezi kupita eti kwa sababu ya Kakobe au mungu amekataa???? TANESCO wamesema umeme unapita kwa viwango walivyoamua kuweka kwa sababu bado substation ambako ule umeme unatakiwa upekelewe bado inafanyiwa kazi!! Baada ya miezi sita kazi ya pale kwenye substation ikiisha umeme unapita full swing. HATA LEO UNAPITA KWA VIWANGO AMBAVYO WANAOPITISHA WAMEAMUA VIPITE HIVYO!!!

Imani kama hizi (ashakum si matusi) za kijinga ndo zinafanya baadhi ya watu wajiulize hivi MUNGU Ni kitu kidogo au cha CHINI hivyo kuwa anaweza kuwa manipulated na watu kama akina KAKOBE na kupindisha mambo??? Kuweni na akili mtumie vichwa vyenu kufikiri. Hata kama mnataka kuamini kuwa kakobe amezuia umeme ili mjifurahishe kuwa ni mtu wa mungu, aminini uchafu wenu huo bila kutaka kuwadanganya wengine. Mwandishi huyo wa gazeti la Dira angekuwa ni mwandishi competent angewahoji contractor wanaojenga umeme pale.

Haya mawazo ya kishirikina hayawezi kuwasaidia wenye nayo wala mtu yeyote. Umeme unapita na utapita milele hadi ile LINE ITAKAPOCHOKA YENYEWE. MSIDANGANYWE!!

Katika Wachangiaji Wote waliochangia hii Mada ( including Me), Wewe Ndiye Uliyeongea Jambo la Msingi Sana
 
Back
Top Bottom