Umeme umegoma kupita kanisani kwa Kakobe

jamani hilo la umeme kugoma kupita hapo kwa kakobe na mimi nimelisikia ,ila sishangai kwani sehemu nyingi tu ilishatokea hilo mfano iringa kuna sehemu(jina silikumbuki) ina makaburi mawili ambapo nguzo ilibidi zipindishwe baada ya umeme kutopita juu ya makaburi hayo na sinza makaburini pia ni same prob ilijitokeza wakapitisha nguzo kwingine



:frusty:.
 
Kile kituo pale Victoria (Kijitonyama) ndicho bado hakijakamilika vizuri. Acheni hizo!
 
Mambo mengine yanatia aibu hata kuyasoma. Hivi kuna mtanzania mwenye uwezo wa kutype kwenye keyboard hapa kwenye jamii forums ambaye akili yake inamtuma kabisa kuwa umeme hauwezi kupita eti kwa sababu ya Kakobe au mungu amekataa???? TANESCO wamesema umeme unapita kwa viwango walivyoamua kuweka kwa sababu bado substation ambako ule umeme unatakiwa upekelewe bado inafanyiwa kazi!! Baada ya miezi sita kazi ya pale kwenye substation ikiisha umeme unapita full swing. HATA LEO UNAPITA KWA VIWANGO AMBAVYO WANAOPITISHA WAMEAMUA VIPITE HIVYO!!!

Imani kama hizi (ashakum si matusi) za kijinga ndo zinafanya baadhi ya watu wajiulize hivi MUNGU Ni kitu kidogo au cha CHINI hivyo kuwa anaweza kuwa manipulated na watu kama akina KAKOBE na kupindisha mambo??? Kuweni na akili mtumie vichwa vyenu kufikiri. Hata kama mnataka kuamini kuwa kakobe amezuia umeme ili mjifurahishe kuwa ni mtu wa mungu, aminini uchafu wenu huo bila kutaka kuwadanganya wengine. Mwandishi huyo wa gazeti la Dira angekuwa ni mwandishi competent angewahoji contractor wanaojenga umeme pale.

Haya mawazo ya kishirikina hayawezi kuwasaidia wenye nayo wala mtu yeyote. Umeme unapita na utapita milele hadi ile LINE ITAKAPOCHOKA YENYEWE. MSIDANGANYWE!!
 
Hivi tangu lini watu waliokwenye utawala wakakubali kushindwa? Hata kama umegoma kupita watadanganya tu kuwa ni jambo la kiufundi na kuongeza mbwembwe nyingi. Mambo yote huanza hivi hivi na baadaye ukweli unakuja kugundulika, Hivyo ukweli utajulikana tu hata kama wataficha.
 
Hili la umeme kutokupita kanisani linawezekana kabisa, kule Iringa kuna eneo linaitwa isimila, mahali hapo umeme ulishindwa kupita juu ya makaburi ya wazee wa eneo hilo. Sasa kama waliokufa wanaweza kuzuia umeme usipite itashindikana kwa Kakobe ambaye anafanya maombi kila kukicha? Tutafute uthibitisho wa taarifa, lakini pia tuamini kwamba hilo linawezekana.
 
kwa imani kila jambo linawezekana, Sayansi na Imani ya dini ni vitu viwili tofauti kabisa. Usishangae kwamba kuna wanasayansi kibao wanazunguka na kuabudu kwenye haya makanisa yanayohubiri uzima - sasa uliza wanafanya nini humo wakati hospitali kubwa zenye madaktari bingwa zipo kibao.

Mtu asiyejua kutenganisha vitu hivi viwili Sayansi na Imani ya dini basi atakuwa anajichanganya wenyewe kauli zake na matendo yake. kuweni makini na watu hawa.
 
Washirikina mko wengi hata humu mmo? Mwambieni Kakobe aisaidie Ghana ichukue kombe la dunia.
 
Waheshimiwa nimepata taarifa mda si mrefu kuwa ule umeme wa tanesco umeshindwa kupita kanisani kwa kakobe. Kama kuna mtu anataarifa zozote tunaomba mtujulishe.

Nahisi wewe na wenzako mnao mwabudu kakobe mmefilisika kimawazo na hamna tofauti na vijana wanaokuwa brain-washed na al-qaeda.
 
Hao wanasema miungu mingine wanamaanisha nini? kwa hyo wewe upo tayari kumuumiza ndugu yako ili upate maendeleo? wewe ndo muhubiri miungu mingine! MUNGU wa kakobe ndo tunamuabudu! PRAISE THE LORD
 
Hamna kitu kibaya kama kumeza kila kitu bila kutafuna. Inaonekana there is a chunk of folks humu bongo who could easily be tricked that there is chocolate in every box..Ndo maana JK alisema kuwa 70% ya wabongo ni wafuata upepo..So sad indeed.
 
Kama umeme unaingia ndani ya kanisa lake inakuwaje huu wa kupita ushindwe? Je, tatizo lipo kwenye eneo la Kakobe tu na kwingine kama Mawasiliano Towers hakuna shida hiyo? Kama tatizo lipo kwenye lines zote na nzima kutoka Ubungo mpaka Victoria basi si kwa sababu ya sala za Kakobe.

Mimi ni RC, tuna amri kumi za Mungu; ya kwanza inasema,"Mimi ndimi bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine". Sasa kwa wale ambao mnamsifia Kakobe kwa maombi yake kuwenu makini kwani anaweza kuwa anatumia miungu mingine au nguvu za giza. Haiwezekani kitu cha manufaa kwa nchi na wananchi unakizuia na kusema eti mungu atazuia. Kwanza huo uaskofu alipewa na nani? Kwanza sala gani muda wote ni sadaka, fungu la kumi na kuombea tu, hakuna kushukuru?

angalia kwenye red alafu usiwaaibishe RC wenzio hapa...upofu wako wa kujua neno ndo unakufanya kuongea hivyo...ndio maana huwa tunawaambia muachane na huyo papa anayewablind mje mfundishwe neno muelewe Bible....haohao wakatoliki ndo wamekuwa adui mkubwa wa kakobe enzi zote, na hii unaionyesha hata wewe muumini wao...pole sana. I hope Roman catholic wenzio watakusaidia kukuelewesha hapa...

kwa upande wa mada, mimi naomba source yake, na ihakikishwe kama ni kweli au watu wanaanza kuzusha tu. hii itakuwa ni kwa faida ya wengi na kwa utukufu wa Mungu....
 
Back
Top Bottom