Shida ya Umeme wanaohusika wajiuzuru

Super Msouth

Senior Member
Dec 28, 2014
133
121
Nipo Newala Mjini wiki ya pili sasa hali ya umeme ni mbaya kupita kiasi.

Tangu nimefika na sasa shida imezidi wiki iliyopita umeme ulikua unawaka kati ya masaa 4-6 kwa siku.

Wiki hii Jumatatu umeme uliwaka masaa 6 kwa siku, Jumanne masaa 3 kwa siku, Jumatano umeme uliwaka chini ya saa 1 kwa siku, Alhamisi uliwaka kwa dakika 14 tu.

Kwa hali hii Meneja wa TANESCO Newala, Meneja wa TANESCO Mtwara, Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Naibu waziri na Waziri Wizara ya Nishati wana uhalali gani wa kuendelea kukaa ofisini?

Kama tatizo linazidi kwa kiasi hiki, na tatizo hili mwisho wake nini?

Tunarudi nyuma kimapato ya Wananchi na nchi kwa kuwa na viongozi mizigo.
 
Halafu wakiulizwa shida nini wanaishia kutoa majibu ya kisiasa..

Wapigieni simu huko ofisini kwao muwaukize kwanini wanakata umeme hovyo..
 
Back
Top Bottom