SoC03 Umefika wakati wa kujikwamua kutoka kwenye misaada isiyoheshima

Stories of Change - 2023 Competition

jemsic

Member
Jul 1, 2020
21
51
Screenshot_20230710-231058~2.jpg

Picha: Swahilitimes
UTANGULIZI
Mara nyingi sana mataifa maskini yamekopa kwa mataifa yenye uwezo lakini hatukuwahi kuona nchi tegemezi zikijikwamua katika hali zake duni za kiuchumi kupitia misaada zinayopewa kwani misaada mara zote hudumaza. Tukitathmini kwa makini tutagundua hata katika nchi zilizoendeea duniani mfano China na Japan hakuna iliyoweza kupata maendeleo makubwa kwa kutegemea misaada zaidi ya kutumia rasilimali walizonazo kujikwamua na kushinda vita dhidi ya umaskini. Nchi nyingi za afrika zimekuwa zikiomba na kupokea misaada mingi kutoka kwenye nchi zenye uwezo kama vile Marekani na Uingereza ili kutatua changamoto zinazoikumba, cha kusikitisha misaada hii imegeuka kuwa tishio na fimbo ya kuchapia pale ambapo tunafanya maamuzi yenye tija kwa ustawi wa taifa lakini yanayokinzana na matakwa ya nchi wafadhili.ni wakati sasa wan chi yetu Tanzania iachane na misaada na kuangalia mbinu mbadala za kujikwamua na kupata maendeleo ya kiuchumi na kufanya hivyo tutadumisha utawala bora.

Misaada ni mbinu ambayo imekuwa ikitumiwa mara nyingi na nchi zinazoendelea kama namna ya kutatua matatizo katika kutafuta maendeleo. Na tumeshuhudia nchi nyingi maskini zikipokea misaada yenye riba na mingine isiyo na riba lakini yenye masharti magumu. Tukumbe ya kwamba mara chache ambapo watu hutoa pasina kutegemea kitu fulani kutoka kwako na tukizingatia kwamba binadamu huishi kwa kutegemeana vivyo hivyo hata kwa nchi. Na vitu vya kubadilishana hujumuisha vitu halisi mfano kama madini, madawa na chakula na vingine dhahania mfano baadhi haki, uhuru na taratibu. Mambo haya ya misaada yamepelekea baadhi ya nchi maskini kukubali hata masharti magumu ambayo yamekuwa yakiiweka nchi na watu wake katika matatizo na zahama kubwa. Vita zinazoendelea katika nchi za Afrika tunaweza kusema zinasababishwa kwa namna moja ama nyingine kwa utegemezi uliokithiri hadi mambo ya msingi ya taifa kama uchaguzi na utawala bora vinatiwa dosari na wahisani. Kwa hiyo misaada imekuwa chanzo kikubwa sana cha kuhafishisha utawala bora kwa sababu ya kutegema misaada hadi kufikia kutawaliwa kwa ukoloni mamboleo. Na ukoloni mamboleo hujumuisha kuwa na serikali yenye meno lakini yasiouma kwa sababu maasi mengi yatashindwa kuzuilika hasa yale yanoyosababibishwa na wahisani wenyewe.

AINA ZA MISAADA NCHINI TANZANIA
Kuna aina tofauti za misaada ya kifedha inayoleta na wahisani wakiwemo Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na mataifa yenye uwezo kama Marekani, Urusi na China kwa ajili ya kusaidia nchi maskini na misaada hii ni pamoja na:​
  • Ruzuku: hizi ni hujumuisha ufadhili wa fedha ambazo hazihitaji kulipwa. Mara nyingi huwa zinatolewa kulingana na mahitaji makubwa ya kifedha nchini kama mbinu ya kusaidia katika kupambana na changamoto wanazopitia.​
  • Mikopo: hizi ni fedha ambayo nchi hukopa na hulipwa kwa kujumuisha na riba kutokana na makubaliano husika nah ii mara nyig huwa ndio hatari kwa sababu huambatana na masharti mengi amabayo huhatarisha uwajibikaji na utawala bora​

NAMNA MISAADA INAVYOHAFIFISHA UTAWALA BORA
  • Matumizi mabaya ya dola: Mara nyingi misaada imkuwa ikichochea viongozi kutumia dola vibaya hasa pale ambapo watapokea misaada yenye masharti na pengine wanapohongwa pesa nyingi kufanya hivyo.​
  • Utegemezi uliokithiri: Misaada imekuwa ikisababibisha nchi kuacha mbinu nyingine za kujikwamua dhidi ya umaskini na kutegemea misaada katika kuendesha miradi yake mingi hasa miradi mikubwa. Misaada inapokithiri huisababishia nchi husika kuwa na utegemezi kwa mataifa yanatoa misaada mpaka kuonekana kwamba bila misaada yao basi shughuli haziwezi kwenda.​
  • Ukiukwaji wa katiba: watoaji wa misaada huja na masharti na mikataba mingi ambayo kama isipoangaliwa na kupitiwa kwa umakini mkubwa huwa na baadhi ya vifungu au vipengele vinavyoenda tofauti na katiba za nchi. Kama katiba ikishakiukwa ni hakika hata utawala hautabaki imara.​
  • Kuongezaeka sana kwa deni la taifa: Nchi zinazoendelea zimekuwa zikipanga bajeti zake za mwaka wa fedha bila kuwa na kiasi cha kutosha bajeti pangwa. Tunaweza jiuliza wapi huwa wanatoa fedha nyingine za kuendesha nchi? Hili litabaki dhahiri ya kwamba bajeti inayopitishwa na bunge hutegemea misaada kama moja ya vyanzo vya mapato na kuongeza deni la taifa.​

NJIA ZA KUWEZA KUJIKWAMUA DHIDI YA MISAADA YENYE KUDHOOFISHA UTAWALA BORA.
  • Kuongeza uwazi na usimamizi serkalini kwa kufatilia kwa ukaribu taasisi au nchi zinazoikopesha serikali. Taarifa zinatolewa kama vigezo vya watoaji wa mikopo na misaada zifafanuliwe na keuleweka bayana wakijumuisha na athari zinazoambatana na mikopo inayopokelewa. Pia iundwe mihili inayojitegemea ili kuchunguza na kutoa uhakika na usahihi na ubora wa mikopo na misaada tunayopewa kama taifa.​
  • Kukuza tabia ya kukopa kiasi tunachoweza kukilipa ndani ya wakati uliokubaliwa ili kukwepa athari zinazoweza kujitokeza kama vile kuongezeka kwa riba ya deni baada ya muda wa kulipa kupita au kushindwa kabisa kulipa deni linapoelemea.​
  • Kukomesha ubadhilifu wa mali za umma itasaidia kuwa na akiba ya kutosha ya fedha katika mfuko wa bajeti kuu. Ubadhilifu wa mali za umma mfano pesa za kuendesha miradi huipeleka nchi kwenye kuomba misaada, hivyo basi tukitokomeza ufisadi na ubadhilifu tutaepuka misaada isiyo na tija kwa taifa.​
  • Kupunguza asilimia za bajeti ya matumizi na kuongeza asilimia za bajeti ya kufanyia shughuli za maendeleo. Kwa kufanya hivyo miradi ya imaendeleo mfano bwawa la Mwl. Nyerere itapewa kipaumbele ili ikikamilika izalishe na kuongeza pato la taifa kwa kasi hivyo kujiepusha na misaada.
  • Kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani hasa kodi kupitia uhamasishaji na watu kufundishwa umuhimu wa kulipa kodi ili wafanye kwa moyo wa kupenda na bila shuruti. Tukiondoa vizuizi vya uwekezaji itaboresha ukusanyaji wa kodi na kuleta mapato ya kutosha.

HITIMISHO
Kuweka kando misaada ndiyo njia pekee ambayo itasimama na kuifanya Tanzania kufikia uhuru wa kiuchumi na yenye kujitegemea Matumizi mazuri ya raslimali na fursa zilizopo nchini zitakuwa namna bora ya kukuza demokrasia na kukwepa kuingiliwa kwenye maamuzi ya mambo ya msingi kwa kushurutishwa kukubali yasiyofaa kwa sababu tu ya misaada tunayoipokea kama nchi inayoendelea. Kwa kutoa elimu kwa walipa kodi, kuzuia ubadhilifu, kukuza uwekezaji na kukopa kiasi kilicho ndani ya uwezo wetu itadumisha heshima mbele ya matifa wahisani. Ifike mahali tuache kuyaona madeni kwa nchi kama kitu cha kawaida kwani huleta fedheha kwa sababu sio jambo zuri kwa nchi kudaiwa na sasa muda umefika tujikwamue na kuachana na misaada isiyoheshima.​
 
DIBAJI
Mara nyingi sana mataifa maskini yamekopa kwa mataifa yenye uwezo lakini hatukuwahi kuona nchi tegemezi zikijikwamua katika hali zake duni za kiuchumi kupitia misaada zinayopewa kwani misaada mara zote hudumaza. Tukitathmini kwa makini tutagundua hata katika nchi zilizoendeea duniani mfano China na Japan hakuna iliyoweza kupata maendeleo makubwa kwa kutegemea misaada zaidi ya kutumia rasilimali walizonazo kujikwamua na kushinda vita dhidi ya umaskini. Nchi nyingi za afrika zimekuwa zikiomba na kupokea misaada mingi kutoka kwenye nchi zenye uwezo kama vile Marekani na Uingereza ili kutatua changamoto zinazoikumba, cha kusikitisha misaada hii imegeuka kuwa tishio na fimbo ya kuchapia pale ambapo tunafanya maamuzi yenye tija kwa ustawi wa taifa lakini yanayokinzana na matakwa ya nchi wafadhili.ni wakati sasa wan chi yetu Tanzania iachane na misaada na kuangalia mbinu mbadala za kujikwamua na kupata maendeleo ya kiuchumi na kufanya hivyo tutadumisha utawala bora.

UTANGULIZI
Misaada ni mbinu ambayo imekuwa ikitumiwa mara nyingi nan chi zinazoendelea kama namna ya kutatua matatizo katika kutafuta maendeleo. Na tumeshuhudia nchi nyingi maskini zikipokea misaada yenye riba na mingine isiyo na riba lakini yenye masharti magumu. Tukumbe ya kwamba mara chache ambapo watu hutoa pasina kutegemea kitu fulani kutoka kwako na tukizingatia kwamba binadamu huishi kwa kutegemeana vivyo hivyo hata kwa nchi. Na vitu vya kubadilishana hujumuisha vitu halisi mfano kama madini, madawa na chakula na vingine dhahania mfano baadhi haki, uhuru na taratibu. Mambo haya ya misaada yamepelekea baadhi ya nchi maskini kukubali hata masharti magumu ambayo yamekuwa yakiiweka nchi na watu wake katika matatizo na zahama kubwa. Vita zinazoendelea katika nchi za Afrika tunaweza kusema zinasababishwa kwa namna moja ama nyingine kwa utegemezi uliokithiri hadi mambo ya msingi ya taifa kama uchaguzi na utawala bora vinatiwa dosari na wahisani. Kwa hiyo misaada imekuwa chanzo kikubwa sana cha kuhafishisha utawala bora kwa sababu ya kutegema misaada hadi kufikia kutawaliwa kwa ukoloni mamboleo. Na ukoloni mamboleo hujumuisha kuwa na serikali yenye meno lakini yasiouma kwa sababu maasi mengi yatashindwa kuzuilika hasa yale yanoyosababibishwa na wahisani wenyewe.

  • Utegemezi uliokithiri: Misaada imekuwa ikisababibisha nchi kuacha mbinu nyingine za kujikwamua dhidi ya umaskini na kutegemea misaada katika kuendesha miradi yake mingi hasa miradi mikubwa. Misaada inapokithiri huisababishia nchi husika kuwa na utegemezi kwa mataifa yanatoa misaada mpaka kuonekana kwamba bila misaada yao basi shughuli haziwezi kwenda hivyo.​
  • Ukiukwaji wa katiba: watoaji wa misaada huja na masharti na mikataba mingi ambayo kama isipoangaliwa na kupitiwa kwa umakini mkubwa huwa na baadhi ya vifungu au vipengele vinavyoenda tofauti na katiba za nchi. Kama katiba ikishakiukwa ni hakika hata utawala hautabaki imara.​
  • Kuongezaeka sana kwa deni la taifa: Nchi zinazoendelea zimekuwa zikipanga bajeti zake za mwaka wa fedha bila kuwa na kiasi cha kutosha bajeti pangwa. Tunaweza jiuliza wapi huwa wanatoa fedha nyingine za kuendesha nchi? Hili litabaki dhahiri ya kwamba bajeti inayopitishwa na bunge hutegemea misaada kama moja ya vyanzo vya mapato na kuongeza deni la taifa.​

NJIA ZA KUWEZA KUJIKWAMUA DHIDI YA MISAADA YENYE KUDHOOFISHA UTAWALA BORA.
  • Kuongeza uwazi na usimamizi serkalini kwa kufatilia kwa ukaribu taasisi au nchi zinazoikopesha serikali. Taarifa zinatolewa kama vigezo vya watoaji wa mikopo na misaada zifafanuliwe na keuleweka bayana wakijumuisha na athari zinazoambatana na mikopo inayopokelewa. Pia iundwe mihili inayojitegemea ili kuchunguza na kutoa uhakika na usahihi na ubora wa mikopo na misaada tunayopewa kama taifa.​
  • Kukuza tabia ya kukopa kiasi tunachoweza kukilipa ndani ya wakati uliokubaliwa ili kukwepa athari zinazoweza kujitokeza kama vile kuongezeka kwa riba ya deni baada ya muda wa kulipa kupita au kushindwa kabisa kulipa deni linapoelemea.​
  • Kukomesha ubadhilifu wa mali za umma itasaidia kuwa na akiba ya kutosha ya fedha katika mfuko wa bajeti kuu. Ubadhilifu wa mali za umma mfano pesa za kuendesha miradi huipeleka nchi kwenye kuomba misaada, hivyo basi tukitokomeza ufisadi na ubadhilifu tutaepuka misaada isiyo na tija kwa taifa.​
  • Kupunguza asilimia za bajeti ya matumizi na kuongeza asilimia za bajeti ya kufanyia shughuli za maendeleo. Kwa kufanya hivyo miradi ya imaendeleo mfano bwawa la Mwl. Nyerere itapewa kipaumbele ili ikikamilika izalishe na kuongeza pato la taifa kwa kasi hivyo kujiepusha na misaada.
  • Kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani hasa kodi kupitia uhamasishaji na watu kufundishwa umuhimu wa kulipa kodi ili wafanye kwa moyo wa kupenda na bila shuruti. Tukiondoa vizuizi vya uwekezaji itaboresha ukusanyaji wa kodi na kuleta mapato ya kutosha.

HITIMISHO
Kuweka kando misaada ndiyo njia pekee ambayo itasimama na kuifanya Tanzania kufikia uhuru wa kiuchumi na yenye kujitegemea Matumizi mazuri ya raslimali na fursa zilizopo nchini zitakuwa namna bora ya kukuza demokrasia na kukwepa kuingiliwa kwenye maamuzi ya mambo ya msingi kwa kushurutishwa kukubali yasiyofaa kwa sababu tu ya misaada tunayoipokea kama nchi inayoendelea. Kwa kutoa elimu kwa walipa kodi, kuzuia ubadhilifu, kukuza uwekezaji na kukopa kiasi kilicho ndani ya uwezo wetu itadumisha heshima mbele ya matifa wahisani. Ifike mahali tuache kuyaona madeni kwa nchi kama kitu cha kawaida kwani huleta fedheha kwa sababu sio jambo zuri kwa nchi kudaiwa na sasa muda umefika tujikwamue na kuachana na misaada isiyoheshima.​
Andiko la mabadiriko
 
View attachment 2700481

👏👏👏👏 Kazi Nzuri Mtaalamu
 
Back
Top Bottom