Waziri Mwigulu ashangaa Tanzania kuishi kwa kutegemea Misaada!

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
"Lazima kama Taifa tuwe na mikakati ya kujitegemea sio heshima Nchi kama Tanzania tunaishi kwa misaada ili tufikie huku lazima tulipe na kukusanya kodi ambapo bado tunapata shida katika maeneo haya."

Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amesema hayo leo, Jumanne 23/1/2024 Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST).




 
Ndo mlikuwa mnafikiria kuwa huyu anaweza hata kugombea nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea uraisi wa JMT?

Sidhani hata kama Singida wenyewe wakiambiwa wawe na raisi wa kuchagua wa mkoa, watamfikiria huyo!
 
Sasa mheshimiwa anashangaa kweli? na yeye ndio yuko kwenye baraza la mawaziri na ni waziri wa wizara muhimu sana, anacuwezo wa maamuzi au kumshauri rais nini kifanyike.

Kwa kweli hata mie nashangaa kwa kinacho mshangaza
 
Tutajitegemea vipi wakati serikali inatumia kodi za wananchi kufafhili maisha ya anasa kwa viongozi wake?

Familia masikini ambayo kipaumbele cha baba ni iphone 15 pro max itaendelea kuwa masikini tu.

Kipaombele cha serikali yetu ni maisha ya anasa ma wizi wa mali za umma.

Mwigulu acha hadaa!
 
Raisi ajaye Job. NDUGAI ARUDISHWE BUNGENI HARAKA SANA-Arejeshewe Uspika wake!

😆😆😊😅
NB:Iwekwe kwenye Bango kesho.
 
Back
Top Bottom