Jamani tuacheni propaganda. Si kubaliani na yeyote anayesema kuwa viongozi wote ni mafisadi. Kwani hawa viongozi ni akina nani. Si ni baba zetu, wajomba zetu, mama zetu, kaka zetu n.k. Mimi ninaamini kuwa tatizo lilopo Tanzania si la viongozi tu, bali ni la watanzania wote. Na tukisimama kuwasaidia viongozi wazuri waliopo madarakani waraka wenye maslahi ya Taifa.
Zawadi ,Pili ndio kuwaelimisha wananchi jinsi ya kuwangoa mafisadi. Nilichokigundua mimi kuwa rythm tunayoipiga bado aslimia 70 ya wananchi hawawezi kucheza. Mpaka huo ndio ukweli tutalalama sana na wapinzani tukidhani tunaonewa.
.
""Sema ukweli, propaganda zisikupofue macho. Ulitembelea vijiji gani Tabora? Tazengwa, Lusu, Uyumbu, Kazaroho, , Uyowa au Izimbiri? Hali halisi ya Wakulima wa Tumbaku ninaijua manake Familia yetu ni wakulima wa Tumbaku. Please tell the truth and shame the devil. Ukweli ni kwamba Muungwana ameona umaarufu wake unashuka kwa style ya Free-fall ndiyo maana amekuja na style ya kuongea na wananchi kwa njia ya TV(ambayo nadhani haikuwa na mafanikio) na sasa anawatumia makada wake kwa nguvu kumuuza kwa Watanzania".
Nashukuru kwa maelezo yako. Lakini upungufu mkubwa katika habari yako ni kutotoa namba. Kwa sababu hata kutoka 80% mpaka 75% bado ni kushuka lakini vilevile nibado juu. Kwasababu rais ana hitaji 51% tu ya kura. Si unakumbuka Mkapa alipita kwa 52%.Ndugu Zawadi, Waingereza wanasema "Dont re-invent the wheeel". Yaani gurudumu lilishagunduliwa zamani kwa nini kama unataka kutengeneza gari model yako uanze tena kugundua gurudumu lingine? Kuna kampuni zamani ilijulikana kama Steadman(sasa hivi imenunuliwa na kubadili jina) imekuwa ikifanya utafiti mara kwa mara na juzi juzi imetoa matokeo yanayoonyesha kwamba ingawa Kikwete bado ana mvuto kwa wapiga kura Tanzania lakini mvuto huo umeshuka chini kulinganisha na mwaka 2005 na sababu za kupungua zimetolewa.
"Steadman" wana utaalam wa hali ya juu kuliko JF na Magazeti ambayo unataka wafanye utafiti yaani "they should re-invent the wheel!" kama Zawadi alivyofanya ingawa hana utaalam katika mambo ya research. Tena kumbuka kwamba katika kutafiti kuna kitu kinaitwa "incumbency factor" kinachangia sana katika kuongeza mvuto wa Rais aliye madarakani kwa wakati huo. Hata Idd Amini kule Uganda alikuwa na mvuto kwa Waganda akiwa madarakani lakini JWTZ walipomtimua toka Kampala wananchi walikesha wakisherekea kwa kucheza ngoma!
Kazi kwelikweli. Tujifunze kujiamini na kusema ukweli bila woga. Maisha yetu hayamilikiwi na mtu awaye yote. Kujipiga bei chee kwa mtu kama ndo njia ya kutokea, sio tu ni kujidharirisha, bali pia ni kupoteza thamani yetu bila sababu. Utawala huu, kama tawala nyingine zote, utakuja na kwenda na watakaobaki salama ni wale waliosimamia ukweli bila kujiingiza kwenye siasa za kuendekeza njaa. Na kubwa kuliko yote, hii ni nchi yetu. Tukiibomoa, tunajibomoa wenyewe.Zawadi Ngoda, molimoli mkwamisi: Nakumbuka hoja yako ya jana, naona umeachana nayo kabisa leo. Hata hivyo nimekupata vizuri, bila shaka unatokea kitengo cha Tabwe Hiza pale Lumumba. Mkuu njaa njaa ziangalie sana, zitatupeleka pabaya.
Ukweli ni kwamba JMK hapingiki wala hatetereki uchaguzi ujao, Rais, kama atakuwa hai, na InshaAllah atakuwa hai na Mwenyeezi Mungu ampe maisha marefu. Amin.
Hakuna Rais yeyote katika Tanzania aliyepita kabla ya JMK, aliyefanya mambo anayoyafanya JMK. Kwa hilo nampa pongezi.
Hata humu ndani ya ukumbi kila anaempinga JMK analeta upupu tu na hana kamili la kumponda. Mimi nna challenge aanzishe mtu mada ya kusema hili JMK hakulifanya inavyotakiwa na anioneshe Rais gani wa Tanzania kabla yake kalifanya! Nakuhakikishieni hakuna anaeweza kuja na hata moja, labda upupu tu.
Ahsante JMK, wenye macho na masikio, tunaona na tunasikia unavyopambana na adui Ujinga, Maradhi, Umaskini, Ubadhirifu, na mengine mengi. Heko na shukrani zangu za dhati kwako.
Ndugu zanguni, msione vyaelea, vimeundwa. Wengi wanapozungumzia Demokrasia, picha zao zipo ulaya nchi ambazo zimechukua miaka zaidi ya 300 kujenga Demokrasia ukilinganisha na ya kwetu miaka 15. Jamani ujenzi wa Demokrasia ni mgumu kuliko kitu chochote kile.Zawadi,
Mimi nataka kukuuliza kwenye mambo ya takwimu. Sijui hizi takwimu umechukuliaje,
- Kwenye hizi chaguzi bado watu wanaoishi vijijini wenywewe wanapiga kura tuu ilimradi mtu amepata khanga, au sukari kwa umaskini au kudanganywa na ahadi - hii yote ni kukosekana kwa Elimu ya Uraia.
- Katiba, kwenye hili nikuwa hapa kuna vitu vingi, kutangaza mshindi ambapo unakutana na wizi wa kura ilimradi Serikali inayotawala ikitaka atangazwe anatangazwa tena kwa ulinzi mkali hata muda mwingine kura zikiwa zinakusanywa vituoni.
Kama nchi yetu tungekuwa na uwanja wa Demokrasia bila hivi vitu vya vurugu hapo ndo ungesema kuwa takwimu ni sahihi zinazotangazwa, vinginevyo kama Katiba haitabadilishwa, na Elimu ya Uraia kutolewa hakuna Demokrasia na takwimu zitakuwa ni kupaka poda mshindi.
Ndugu yangu mkono mtupu haulambwi! Tabasam peke yake bila vitendo halisaidii hata kidogo. Tuacheni uongo Rais Kikwete kafanya kazi. Nitakuorodheshea baadhi ya matatizo sugu yaliyokera sana wananchi katika maeneo mbalimbali.Kweli tabasamu la JK limewapofusha watu! Usemi pekee wa JK kwamba anashindwa kuelewa kwa nini TZ ni maskini inatosha kum-disqualify, tukiacha ahadi zake nyingi hewa na mbwembwe zake za "maisha bora kwa kila mtz"! Angejuaje wakati yuko busy na safari za majuu! Kasi yake mpya ya kupambana na ufisadi imeishia pale alipodai kuwa mzee BWM "aachwe apumzike" kwa kazi nzito ya kufanya biashara ikulu!
Ndugu yangu mkono mtupu haulambwi! Tabasam peke yake bila vitendo halisaidii hata kidogo. Tuacheni uongo Rais Kikwete kafanya kazi. Nitakuorodheshea baadhi ya matatizo sugu yaliyokera sana wananchi katika maeneo mbalimbali.
.......
N.B Muundo wowote wa uchumi usioshirikisha wananchi hautafanikiwa. Na hapo ndipo Kikwete anapojitahidi kupafikia, Njia yake si rahisi lakini tutafika tu.
Unaweza ukajitahidi kum-bomoa mtu kumbe ndio unajenga na kumpandisha chati...!
Uhuru huu haukuwepo enzi zile za Musa (Julius) na che Mkapa, thanx God... watu wanazungumza sasa.
Ukweli ni kwamba JMK hapingiki wala hatetereki uchaguzi ujao, Rais, kama atakuwa hai, na InshaAllah atakuwa hai na Mwenyeezi Mungu ampe maisha marefu. Amin.
Hakuna Rais yeyote katika Tanzania aliyepita kabla ya JMK, aliyefanya mambo anayoyafanya JMK. Kwa hilo nampa pongezi.
Hata humu ndani ya ukumbi kila anaempinga JMK analeta upupu tu na hana kamili la kumponda. Mimi nna challenge aanzishe mtu mada ya kusema hili JMK hakulifanya inavyotakiwa na anioneshe Rais gani wa Tanzania kabla yake kalifanya! Nakuhakikishieni hakuna anaeweza kuja na hata moja, labda upupu tu.
Ahsante JMK, wenye macho na masikio, tunaona na tunasikia unavyopambana na adui Ujinga, Maradhi, Umaskini, Ubadhirifu, na mengine mengi. Heko na shukrani zangu za dhati kwako.
Shukran kwa maoni yako. Lakini ni vyema kama ungeiangalia shilingi kwa pande zote mbili, na si kwa mapenzi ya moyo kama ushabiki wa mpira.
Ukweli ni kwamba, wananchi si kama wanamuona Kikwete kama Raisi aliyewatimizia yote, bali wananchi hawawaamini wanasiasa. Na kwa maana hii, hawana imani kuwa kama watambadili na kuuweka upinzani ndio mambo yao yatakuwa mazuri. Maana Zimwi likujualo halikuli likakwisha.
CHADEMA ni moja kati ya vyama vilivyopata heshima sana nchini Tanzania. Lakini tukio la hivi karibuni la kumtoa katika kinyanganyiro cha uenyekiti, mbunge maarufu Zitto Kabwe kimeishushia hadi sana chama hicho. Na wananchi wanajiuliza hivi tukiwapa Urais watawezaje kugawana post za Uwaziri na nyinginezo. Hivi hawa wapo pamoja au wanatuhadaa tu.
Watanzania mpaka leo si watu wa kuchukua Risk kubwa kiasi hicho. Kwa hili wengi tutakubaliana.
"
Ongezeko la tumbaku: RUVUMA, toka tani milioni 1.5 mwaka 2007 hadi tani milioni 3 mwaka 2008. Tabora ongezeko la asilmia 40 toka mwaka 2007 hadi 2008. Tazama shirika la takwimu au TAT. Sina maelezo zaidi. Tafadhali nipe takwimu zako, tuache hizi longo longo.
Longo longo. Dola inayumba hiyo inaeleweka. Maisha i utatuzi wa matatizo.
Ukisoma JF na magazeti mengine unaweza kudhani kwamba, mwaka 2010 Kikwete hawezi kuambulia hata 20% ya kura za watanzania. Lakini hali halisi nchini ni nyingine kabisa. Nimetembelea Mwanza, Lindi,Tabora, Ruvuma, Dodoma, Dar es Salaam na baadhi ya vijiji na kupata picha halisi.
Nimetembelea vijiji sita, na nikajaribu kueleza jinsi Kikwete alivyowaangusha wakulima kwa ahadi hewa. Vijiji vya Tabora na Ruvuma, walinieleza kuwa wao ni wakulima wa Tumbaku na toka Kikwete aingie madarakani wamesikilizwa sana kwa kuwabana wawekezaji katika eneo hilo. Aidha wale wa Ruvuma walifurahia kuona mwaka jana zao hilo liliongezeka mara mbili, na kila mmoja alihisi tofauti katika mfuko wake. Hali kama hiyo nilielezwa na wananchi wa Tabora. Kifupi katika mikoa yote nilipata majibu ya kuonyesha wanaimani na Rais Kikwete.
.