Ukosefu wa maadili unatisha kwa kasi unayoporomoka Tanzania

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,883
109,212
Bila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozidi miaka 40 watanielewa.

Tanzania yetu iliyokuwa inasifika ndani na nje ya nchi kwa maadili na nidhamu imeenda "arijjojo", wale waliowahi kucheza na vishada (kites) watanielewa nikisema "arijojo".

Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie, nikamwambia mbona wachumba wapo wengi na vijana siku hizi hakuna anaetaka kutafutiwa, akanambia hujanielewa, hataki mchumba tu, anataka mchumba kutokea Tanzania. Akanielewesha nikamuelewa, nikamuunganisha na watu Dar., Nafurahi kusema akapata mke na mpaka sasa wanazeeka pamoja, watoto zao wameshafikia umri wa kujukuu, kama bado, sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.

Hiyo siyo point yangu bali ni mfano tu. Kama hayo yalikuwa mengi sana si kutokea Ulaya tu, hata nchi za jirani walitamani kuoa mwanamke wa Kitanzania, sababu kuu ikiwa ni maadili.

Leo hayo kukutana nayo ni nadra sana, sisemi yamekwisha kabisa, lakini yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Ni nini kilichotufikisha hapo? Nafahamu wengi sana maisha wanayokutana nayo ndivyo yalivyo, hawatoweza kunielewa kabisa, kwani hawana cha kulinganisha nayo hayo, sisi wa zamani tunaoyaona kuwa ni maadili mema.

Wewe unayenisoma, maadili mema kwako ni yepi? Tutajie japo moja tu. Inawezekana kabisa nnavyoviona mimi kuwa si maadili mema, kwako ikawa ni ajabu kwanini hilo hayo si maadili mema.

My take; Maadili mema hayafundishwi tu, bali huanzia kwa kuigwa, je ni wazazi na walezi ndiyo tulikosea?
 
Utandawazi una mchango mkubwa sana katika kuporomoka kwa maadili mema,
Wazazi nao wamekua too busy na kutotafuta hata muda wa kulea watoto wao au kufuatilia mienendo yao,maadili ya Walimu pia yameporomoka,zamani walimu walikua wanaheshimiwa na wanafunzi kuliko walivyokua wakiwaheshimu au kuwaogopa wazazi wao,

Hapa tatizo linaanzia kwenye malezi,So wazazi/Walezi hawana pa kukwepea hizi lawama.
 
Kama wewe zee Zima kutwa kueneza chuki za udini unategemea maadili wawe nayo wajuu zako


Ajuza mzima unaleta udini Karne hii





Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
Ulitaka nieneze chuki za upagani?


Kama wewe huna dini unataka wote tusiwe na dini? Kukosa dini ndiyo chanzo kikuuu cha ukosefu wa maadili.

Kama huna dini hayo maadili utajifunza kutokea wapi?
 
Ugumu WA maisha na ukosefu WA ajira vinawafanya vijana kuishi kinamna nyingine kabisa .....! Unaweza vipi kuwa mstaarabu na maadili kwenye njaa na Dunia ya uhuni...

Wenyewe wanasema ...unyama unyama tu ,strong will survive..
 
Bila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozido miaka 40 watanielewa.

Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikiuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie.
Iliozido= Uliozidi
nilikiuwa = Nilikuwa
nawasiliano = Nawasiliana
nami = Na mimi

Ni kweli maadili yameporomoka...

we unafikiri Familia kama hii itakuwa na Maadili
BAba kazaliwa 2000 ,Mama kazaliwa 2003 , mtoto kazaliwa 2018 unategemea Familia hiyo itakuwa na Maadili wayatoe wapi ....Wote watoto wa 2000s
 
......mi binafsi huwa najiuliza mabinti wa leo kuzaa zaa ovyo ovyo sijui wanajisikiaje, sijui wazazi tumefeli wapi. Binti mdogo kabisa anabeba mimba tena niseme isiokua na baba, mzazi nae atashiriki kumuandalia baby shower shame!! Shame!! Akikaa kidogo kaenda tena kuzaa na mwingine, yani kawaida sahivi kila mtoto kuwa na baba ake.
 
Utandawazi una mchango mkubwa sana katika kuporomoka kwa maadili mema,
Wazazi nao wamekua too busy na kutotafuta hata muda wa kulea watoto wao au kufuatilia mienendo yao,maadili ya Walimu pia yameporomoka,zamani walimu walikua wanaheshimiwa na wanafunzi kuliko walivyokua wakiwaheshimu au kuwaogopa wazazi wao,

Hapa tatizo linaanzia kwenye malezi,So wazazi/Walezi hawana pa kukwepea hizi lawama.
Nini kifanyike?
 
Wazazi wa sasa hasa wanawake ambao ni msingi bora kabisa wa maadili kwa watoto wapo bize kutafuta pesa , mtoto anakua bila malezi kutoka kwa mama , mgawanyiko wa majukumu wa zamani upo vizuri sana hasa katika nia ya kujenga maadili kwa mtoto , mama anabaki nyumbani kuangalia usalama wa watoto baba anaenda kutafuta , hii ilijenga misingi bora kabisa ya uadilifu , kwa sababu mama alikua anafuatilia tabia za mwanae kwa ukaribu zaidi.

Licha ya mwanamke kuwa bize kwenye utafutaji , sasa kuna wimbi la malezi ya mtoto ambayo yamemwelemea mzazi mmoja , single mother na single father, huko tunapoenda ni kubaya zaidi ya hapa tulipo .

Nini kifanyike , kila abiria achunge mzigo wake.
 
Back
Top Bottom