Ukodishaji wa ndege za serikali, Risiti za Salma Kikwete

Lakini jamani, unawezaji kuruhusu ndege kuruka bila kulipwa, hii ni invoice na pamoja sio mtaalamu wa mahesabu ya fedha, sioni aliyeandikiwa. Na itakuwaje tarehe ya madai yawe ni siku ile ile ya kusafiria. Je viwango vya kukodisha vimepangwa na nani. Mtu mzima anapoamua kudanganya kwa kufoji virisiti na invoice tunaelekea pabaya. Nisingeweza kulala nikijua nimefoji kwa kiasi hicho. Kwa nini wasiseme ndio tumetoa ndege kwa Mama wa Taifa, sidhani Slaa angeweza kumpiku huku ndani ya mahakama. Hii ikienda mahakamani ni rahisi kumshinda!

Ni kweli Kinana kaonesha proforma invoice na sio receipt! Sasa inabidi atuonesha kila kitu - proforma invoice mpaka receipt. Halafu nyinyi waandishi wa habari mmekubali vipi kuwa hizo proforma invoices ni receipt? Kwa nini msimuulize na kumuonesha receipt ya serikali? Au na nyinyi hamjui tofauti? Halafy proforma imeandikwa 1st lady kwenye details badala ya service tu, yaani , plane hiring for say 10 hours. 1st lady maanake mke wa Rais, hivyo proforma invoice hizo zinahusiana na Ikulu! Na wewe Silva kwa nini usemi kitu wakati masaidizi wako alisema IKULU ina bajeti ya Salma kwenye shughuli za kiserikali, ni zipi hizi?
 
Kinachosikisha zaidi waTZ anaoweza kudadavua mambo kama haya wapo wachache sana,wengine wote wadanganyika hawaelewi hata maana ya invoice ni nini..
 
Ni kweli Kinana kaonesha proforma invoice na sio receipt! Sasa inabidi atuonesha kila kitu - proforma invoice mpaka receipt. Halafu nyinyi waandishi wa habari mmekubali vipi kuwa hizo proforma invoices ni receipt? Kwa nini msimuulize na kumuonesha receipt ya serikali? Au na nyinyi hamjui tofauti? Halafy proforma imeandikwa 1st lady kwenye details badala ya service tu, yaani , plane hiring for say 10 hours. 1st lady maanake mke wa Rais, hivyo proforma invoice hizo zinahusiana na Ikulu! Na wewe Silva kwa nini usemi kitu wakati masaidizi wako alisema IKULU ina bajeti ya Salma kwenye shughuli za kiserikali, ni zipi hizi?


Hivi ndugu yangu huwezi tu kuona hiyo haraka waliyokuwa nayo kuandaa risiti; jamani, be fair to the guy who was given the assignment; kapigiwa simu ya kuitwa mahali[mi sijasema ni wapi niacheni!] akapewa amri ya kutengeneza risiti za kupinga madai ya Slaa; hivi unategemea angepata akili ya haraka ya kugundua madhara ya kuandika 'first lady'? Halafu; Kinana angepata wapi ufahamu wa haraka kwamba kuna watu wata question utofauti wa invoice na risiti?; Kukurupuka is the order of the day.

Trust Slaa to hit them below the belt
 
Nimechoka na Hii Bana kila mara Ufisadi haya Hizi Hela za Wadanganyika hawana pesa mlo mmoja kwa siku taabu eti bado upo upo tu na kuisapoti hiki chama cha mafisadi, Wananchi tujiunge kwa pamoja tuung'oe huu utawala wa walionacho CHAGUA CHADEMA CHAGUA DR.SLAA.
 
Kinachosikisha zaidi waTZ anaoweza kudadavua mambo kama haya wapo wachache sana,wengine wote wadanganyika hawaelewi hata maana ya invoice ni nini..

Waandishi wetu wengi wa habari hawana uzoefu wa kuuliza maswali ya papo kwa papo, na pia hawana uelewa wa mambo mengi. Wangeweza kumhenyesha palepale na documents zake na angeshindwa kutoa majibu ya haraka.
 
Namshukuru Dr. Slaa kwa uamuzi wake wa kumshaki Mama Salma Kikwete. Hilo limesaidia kufichua uozo mwingine tena wa hawa viongozi wa CCM. Wamezoea kufoji mno? Hawajazoea utawala wa kisheria. Kama hawangekuwa wamefoji, wala malipo hayangekuwa kwenye dola.

Hakuna msomi au accountant ataandika UDS 15,000/=. Hawachanganyi shilingi na dola. Hiyo no forgery ya watu hao hao wanaofoji documents za kuingiza meno ya tembo kwenye meli. Wamezoea.

Jamani msaada tutani, hivi dollar elfu kumi na tano, au Tshs elfu kumi na tano, au Rupia elfu kumi na tano au Rand elfu kumi na tano zinaandikwaje??? Hii alama (/=) nilifikiri inamaanisha bila cent!!!

Anyway, CCM wameshikwa pabaya!!
 
This is not about Kikwete...I've said about this now and again kuwa CCM is a wrong party...hiki ni chama cha wanyan'ganyi, mabepari wanyonyaji...kura yako usiipe CCM na mgombea yeyote wa CCM, asilimia 50 ya watanzania wakifikia hapa basi hayo yote yatapunguwa kama si kwisha kabisa.

Mkuu mara nyingi huwa sikuelewi elewi..lakini kwa leo umenigusa moyoni na nimelazimika kukuunga mkono. Na kuhusu ushauri wako kwa kura zetu mesema tusimpe ccm lakini hujasema tumpe nani. Mimi nasema Dr Slaa anaweza kukomesha huo ujambazi wa ccm.. kwahiyo KURA YAKO MPE Dr W. Slaa.
 
Nadhani Kinana amelewa madaraka na sasa hajui analolifanya, kutuonyesha risiti haitoshi - watueleze hizo gharama zinalipwa na nani? Mama Salma anatumia misafara ya magari ya Ikulu kwa bajeti ipi? Anapewa mapokezi ya viongozi wa serikali kwa gharama za walipa kodi, au hata hao anazo risiti za matumizi yao?

Hebu nieleweshwe hivi muda wa kazi kwa hao viongozi wa serikali mikoani na wilayani, wanapokwenda kumpokea First lady anekuwa kwenye ziara ya kampeni za chama na kuattend shughuli , hao viongozi kikatiba still wanalipwa na kodi zetu wananchi (serikali) kwa masaa wanayokuwa wanaattend huko au huwa wanaclock out masaa hayo from kazi za serikali manake mie naona kama sio sawa hapo hebu nielewesheni!!!
 
USD 15,000/=, LOL kama kufoji kwenyewe ni kwa kijinga namna hii CCM wamefulia.
 
Wakuu tuache ushabiki lakini kwenye hili Kinana inabidi awajibike kwa kuwadanganya watanzania na possibly kufanya forgery. CCM need to immediately come clean on this..............

Inawezekana vp risiti (invoice) iliyotolewa tarehe 31/08/2010 ikawa na serial no. 00868727

na ile iliyotolewa tarehe 14/09/2010 ikawa na serial no. 00867609


:becky::becky::becky: hapo mzee wa meli amekosea kuchakachua sasa tusubiri swaiba wake aje amsaidia kubwatuka
 
USD 15,000/=


hivi wadau usd huwa ina hii hitu /=?

Kinana!!!!!!!!
 
Wakuu

Nimewasoma ila naomba niwakumbushe mambo machache ambayo wengi wenu vijana hamyafahamu na ni kwa sisi wazee tunaweza dadafua:

Kwa kifupi Wakala wa Ndege za Serikali, ilizinduliwa mwezi Mei, 2002 kutoka kilichokuwa Kitengo cha Ndege za Serikali na ina majukumu yafuatayo:

1.Kumhudumia Mhe. Rais na Viongozi Wakuu wa Serikali.

2.Kusimamia, kutunza, kuendesha na kuendeleza ndege za Serikali pamoja na karakana yake.

3.Kutumia nafasi ya ziada kwa kutoa huduma kwa umma kwa msingi wa biashara.

4.Kutoa ushauri kwa Serikali juu ya mafunzo ya wafanyakazi wake na shughuli za usafiri wa ndege kwa jumla.

Baada ya kusema hayo naomba kuchangia mjadala huu

1.CCM wako sahihi kabisa kukodi ndege ya serikali kutokana na kifungu cha tatu hapo juu na yeyote yule anaweza kufuata utaratibu wa kukodi ndege za serikali.

2.Sifahamu ni gharama zipi ambazo mtu anatakiwa kulipa ili kukodi ndege hizi kwa sasa ila nitafuatilia na kuwapa majibu baadaye

3.Dr. Slaa anatakiwa ajenge hoja nyingine za kuleta mapinduzi na hili ndiyo jukumu kubwa alkilokabidhiwa na watanzania.

4.Asipoachana na kukurupukia hoja za mafisadi na kuendelea kuwaambia wananchi mambo ambayo hayawagusi kila siku basi wapinzani wataendelea kushindwa vibaya.

5.Mkuu Mwanakijiji utakubaliana na mimi tatizo la wagombea wa upinzani ni kukosa 'focus' katika kunadi sera zao na siku zote hubebwa kirahisi na propaganda za chama cha mapinduzi(CCM).

6.Wananchi wa vijijini wanapenda kusikia utawaletea maji,umeme utajenga shule na siku zote CCM imekuwa inashinda kwa kufanya hivi ila tatizo la wananchi wanashindwa kuchagua watu watakaoleta mabadiliko.kwa sasa kuna CDF ambao kama ukitumiwa vizuri basi unaweza kuleta mabadiliko madogo madogo kwanza katika kila jimbo.

7.Suala la risiti siyo hoja sababu wana uwezo wa kulijibu.CHADEMA wajipange zaidi kuwaleza wananchi nini wanaweza kuwafanyia na kwa kipindi gani

8.siku zote maendeleo yatakuja pale viongozi watakapoweza kuwajibishwa kwa kushindwa kutekeleza kile ambacho huwa wanakihaidi.kuwepo adhabu kali kama kunyongwa,kutolewa macho ama kukatwa mdomo na koromeo ili watu wajue uongozi si lelemama!

Wenu Mkuu Gembe!

 
Name AOC Number Base/ Area of Operation Type of operationCOASTAL TRAVELSCAA/AOC/023DAR-ES-SALAAM /WITHIN TANZANIA AND ADJACENT STATESCOMMERCIAL AIR TRANSPORTGOVERNMENT FLIGHT AGENCYCAA/AOC/053PUBLIC TRANSPORT,AIR CHARTER WITHIN TANZANIA AND ACOMMERCIAL AIR TRANSPORT

frm tcaa
 
wapendwa haki anayo huyo mama swala libaki kwenye risiti tu

AOC Holder
spacer.gif
Home › Operator › AOC Holder › Aircraft Operating Certificate Detail
print_icon2.gif


Aircraft Operating Certificate DetailsAOC Number:CAA/AOC/053Name :GOVERNMENT FLIGHT AGENCYBase Address:P.O.BOX 1493 DAR ES SALAAM. ceo@tgf.co.tzApproved Maintenance Base:Engineers:0 Pilots:0 Type of Aircraft / Registration:F-50,PA-31Base / Area of operation:PUBLIC TRANSPORT,AIR CHARTER WITHIN TANZANIA AND AType of Operation:COMMERCIAL AIR TRANSPORTIssue Date:04/03/2010Expiry Date: 05/03/2011
 
Risiti za serikali karatasi zake ziwe na quality mbovu namna hiyo kama risiti unayopewa unaponunua kilo ya maharage, CCM wamebugi step huo ni uongo wa mchana kweupe.

Luteni taratibu basi umesahau kuwa bado una kadi yao? ebanaeee.. Marando ujiko huooo kiulainiiiiiiiiiiiii kama kumsukuma mlevi
 
Wakuu najua hii issue imejadiliwa kwenye post nyingine. Nimeiangalia kwa umakini mkubwa nimeona kinana ameonyesha hati ya madai a.k.a bili, ankara - INVOICE na siyo risiti ya malipo.

154cdtv.jpg


4rarnb.jpg


Nilitegemea kuwa kwa kuwa ni ndege za serikali, risiti ilipaswa kuwa ya njano. Ni wazi kuwa hakuna malipo yaliyofanyika ndiyo maana hakuna risiti. Wametumia ubabe tu kuchukue hiyo ndege.
 
Back
Top Bottom