Yegomasika
JF-Expert Member
- Mar 21, 2009
- 13,164
- 61,249
Nadhani hapo alikuwa na maana kwa jinsi ilivyokaa shaghala baghala humo ndani~he he !.Kuna AF one zingine ukiziona unachanganyikiwa hii mbona ya kawaida tu:lol::lol::lol:
Nadhani hapo alikuwa na maana kwa jinsi ilivyokaa shaghala baghala humo ndani~he he !.Kuna AF one zingine ukiziona unachanganyikiwa hii mbona ya kawaida tu:lol::lol::lol:
Mambo ya Ajabu sana haya...
Hiyo Risiti ukiiangalia kwa makini utagundua ina walakini...
1. Haisemi imetolewa lini.
2. Ililipiwa lini
3. Imelipwa na nani
4. Je inawezekana kukodisha ndege ya serikali kabla ya malipo maana inaonekana kukodishwa kulifanyika 28/08/2010 na malipo yakafanyika 31/08/2010
5. Risiti pia haizungumzii ni ndege gani imekodishwa kama ambavyo ilikuwa described na akina slaa inasema air fleight number... sasa kwa wanao fanya kazi airport watakubaliana kwamba fleight number inategemea na siku ndege inaposafiri ndo itajulikana...
6.Nilifikiri kwamba serikali inapiga marufuku matumizi ya dollar... sasa iweje leo hii malipo hayo yafanyike kwa dollars ... kwa nini sasa they dont practise what they preach?
7. Usd 15000 Kwa masaa matano? Kwa kazi gani anayofanya huyo mama... hii inaonesha kwamba hawa watu ni anasa tu..Dollar elfu 15 kwa kazi gani anayofanya maana WAMA ni charity tu na sidhani kama sisi wachangiaji wa hiyo charity tungeruhusu matumizi makubwa ya ku-hire private govt jet ya namna hiyo... huu ni mfano mmbaya wa public figures kama hawa... they are setting dangerous examples...hata kama ingelipiwa na CCM... hili pia haliko wazi maana inasema tu Secretary General Chama cha mapinduzi.. sasa sijui ni yeye aliyelipa au ni CCM ... Kama alikuwa analipa wa niaba ya CCM basi tisiti ingeandikwa received from CCM for accounting purposes ndani ya serikali na huko CCM Kwenyewe.
8. Mwihso Mbona hatujawahi ambiwa kwamba ndege ya serikali ni ruksa kukodi kwa watu binafsi wakiwemo serikali mbadala (wapinzani)?
Ni hayo tu wakuu... free to make additional observations.
Hiki ndicho nilichotaka kusema kwa sababu nilikuwa na mashaka sana na mpangilio wa namba za risti hizo, ila nikakwama katika kutafuta sheria iliyotunga agency hiyo. Nilitaka kujua pia majukumu ya agency hiyo kisheria; nimetafuta pale Bunge nikachoka na kukata tamaa. Ila nina wasiwasi mkubwa sana na legitimacy ya invoice hizo alizoonyesha Kinana na uhalali wa matumizi ya ndege hizo kwa shughuli za binasfi; nilikuwa ninaamini kuwa ndege zile zinakodishwa na wizara kwa shughuli za kiserikali tu, ila nilitaka kujiaminisha kwa kusoma sheria inasemaje.
Kilichonishangaza zaidi ni lile pengo liliopo baina ya invoice hizo mbili katika kipindi cha wiki mbili tu ukichukulia kuwa wao wanaandika invoce zao kinyume nyume, utadhani kuwa Agency hiyo ina biashara nyingi sana kiasi cha kuwa na wateja zaidi ya 500 kwa wiki!!
.Kwa kweli likizo hii ya X-mass nataka kuikodisha, jamani narudia tena kuomba utaratibu wa kuikodi na bei!
Kinachotakiwa Kinana akaonyeshe mahakamani kama risti ni za kweli au kugushi itajulikana si vitabu vitaletwa, na vile vile watuambie walianza lini kukodi ndege za serikali ina maana serikali inafanya biashara ya kukodi. Mimi nafikiri Chadema wasonge mbele tu wapeleke suala hili mahakamani ili waendelee kuwaweka CCM kwenye defensive position wakati wote wa kampeni.
hiyo kwenye red naomba clarification, kwasababu nakumbuka tulishawahi kuambia kile kitengo kinaweza kukodisha ndege kwa watu binafsiNi invoice kwa Katibu Mkuu wa CCM. Kuna matatizo haya:
(1) Kitengo cha ndege za serikali si cha biashara. Hakina kibali cha kufanya biashara.
(2)Serikali ya CCM hairuhusiwi kufanya biashara na CCM. Kunakuwepo na conflict of interest.
(3) Sidhani Mtendaji Mkuu wa hicho kitengo angeandika USD 15,000/=. Hiyo alama" /= " ni kifupisho cha "shilingi".
Mkuu watachoma moto ofisi ya Wakala wa Ndege sasa hivi. Vitabu vyote vitapotea, sasa ushahidi utatokea kwenye majivu? Kwa serikali hii hakuna baya linaloshindikana!
Huku kutapatapa kunaweza kuwapeleka kubaya sasa. Ina maana serikali inafanya biashara ya kukodisha ndege? Na hizo fedha zinapelekwa kwenye account gani? Namna nyingine ya kujibu mambo inatia mashaka umakini wa hawa watu. Imefikia mahali kuwa nchi hii inaendeshwa kwa matakwa ya mtu na familia yake. Serikali inafanyaje biashara ya kukodisha ndege? Ina maana ikitokea mtu akataka kukodi ile convoy ya magari ya Rais kwa ajili ya harusi inawezekana? Hawaachi kutushangaza kwa kweli...
Kinana alisema jana kwamba Mama Salma anafanya kazi nzuri sana kwa CCM na mikutano ya kampeni anayofanya ni ya "ndani" sio ya hadhara. Mimi nadhani tuachane na hili kwani sidhani kama litampunguzia kura Dr Slaa. Urais ni TAASISI ambayo familia ya Rais huwezi kuitenganisha nayo. Afya ya JK ni mgogoro na huyu mama analijua zaidi hilo na mjue tu kwamba ana-play role kubwa zaidi ya hiyo mnayoiona kwenye majukwaa.
.
Mwanamayu,
Nijuavyo mimi, Shirika la Ndege za Serikali, halikodishi ndege zake kwa shughuli zozote zisizo za serikali.
Wakati wa Wiki ya Utumishi wa Umma, toka kwenye viwanja vya CCM Kirumba mjini Mwanza, Afisa Mtendaji Mkuu wa TGFA, alisema ndege za serikali, hazikodishwi!.
Sasa kama CCM nayo ni serikali, naamini by kesho ataissue statement kufafanua hili.
Anachoonyesha Kinana ni Hati ya Madai (invoices). Naomba nieleweshwe na wenye ufahamu wa hizi taratibu za ununuzi. 'HATI YA MADAI' inakuwaje risiti?
risiti (invoice) iliyotolewa tarehe 31/08/2010 ikawa na serial no. 00868727
tarehe 14/09/2010 ikawa na serial no. 00867609
mambo ya ajabu sana haya...
Hiyo risiti ukiiangalia kwa makini utagundua ina walakini...
1. Haisemi imetolewa lini.
2. Ililipiwa lini
3. Imelipwa na nani
4. Je inawezekana kukodisha ndege ya serikali kabla ya malipo maana inaonekana kukodishwa kulifanyika 28/08/2010 na malipo yakafanyika 31/08/2010
5. Risiti pia haizungumzii ni ndege gani imekodishwa kama ambavyo ilikuwa described na akina slaa inasema air fleight number... Sasa kwa wanao fanya kazi airport watakubaliana kwamba fleight number inategemea na siku ndege inaposafiri ndo itajulikana...
6.nilifikiri kwamba serikali inapiga marufuku matumizi ya dollar... Sasa iweje leo hii malipo hayo yafanyike kwa dollars ... Kwa nini sasa they dont practise what they preach?
7. Usd 15000 kwa masaa matano? Kwa kazi gani anayofanya huyo mama... Hii inaonesha kwamba hawa watu ni anasa tu..dollar elfu 15 kwa kazi gani anayofanya maana wama ni charity tu na sidhani kama sisi wachangiaji wa hiyo charity tungeruhusu matumizi makubwa ya ku-hire private govt jet ya namna hiyo... Huu ni mfano mmbaya wa public figures kama hawa... They are setting dangerous examples...hata kama ingelipiwa na ccm... Hili pia haliko wazi maana inasema tu secretary general chama cha mapinduzi.. Sasa sijui ni yeye aliyelipa au ni ccm ... Kama alikuwa analipa wa niaba ya ccm basi tisiti ingeandikwa received from ccm for accounting purposes ndani ya serikali na huko ccm kwenyewe.
8. Mwihso mbona hatujawahi ambiwa kwamba ndege ya serikali ni ruksa kukodi kwa watu binafsi wakiwemo serikali mbadala (wapinzani)?
Ni hayo tu wakuu... Free to make additional observations.