Kaunga
JF-Expert Member
- Nov 28, 2010
- 12,530
- 13,469
Natumia mchina . . . . . .!
Kila siku????? Hata mchina waweza weka desktop mode just for that!
Natumia mchina . . . . . .!
Afu bora huyo mtoto awe wa kiume. Wababa wengi wana mapenzi yalopitiliza kwa watoto wao wa kike. Which is natural. Akiwa mwanao ukiona baba ana mspoil utavumilia; na labda unaweza hata ukafurahia. Lakini kuna watu nawajua wanafikia kukasirikia kitendo cha waume zao kuwa na attention zaidi kwa watoto zao wa kike. Sasa nambie mtoto huyo si wako. Ndo hapo mtu anamchukulia mtoto kama mke mwenzie. Kazi kweli kweli. Je wewe kama baba utaacha kuonyesha mapenzi kwa bintiyo usimchukize mkeo? Je utampenda tu mkeo atajiju???
Maana kuna wanaume kila unapomkuta amemkumbatia bintiye. Lol.
nyumba kubwa, mie awe mtoto wangu au si wangu, binti akishafikisha miaka 10 sikubali akumbatiane na baba yake.
Naona kama sijawa tayari kulea wanangu katika utamaduni wa kimagharibi kwa kiwango hicho.
Kumpenda mtoto ruksa as long as haingilii malezi bora ya mtoto. Hivi unaweza mwonea wivu mtoto kwa baba yake? Kiaje?
Mimi sina mtoto wa kike sina jibu la hapo kwenye bold. Lakini hicho kitu kipo labda wanaofanya hivyo wakiwa tayari kufunguka na kutuambia sababu.
Kuhusu kukumbatia mtoto wewe hupendi kwa nini au ndo wivu wenyewe.Lol.
Na kama uliruhusu akiwa mdogo utaanzaje kumwambia mmeo au mtoto kuwa sasa basi una miaka 10???
Hii mada ni ngumu kuliko tunavyofikiri. Kwa yale niliyopitia kwa mama wa kambo...niliapa kamwe sitazaa kabla ya ndoa, na namwomba Mungu anipe mume asiye na mtoto. Si rahisi kulea mtoto wa mwenzio kama wako, huyo wa ndugu yako wa damu tu ni shida. Mama waweza kuwa mwema lakini watoto na mume wasione, kuna watoto nao ni vimeo.. Kuna mambo mengi sana juu ya hili.
kweli kabisa, mimi baba yangu ananipenda mpaka mama ananiita mtoto wa baba, na sometimes nahisi nampa baba wakati mgumu kama kuna kitu anatakiwa achague kati yangu na mama.............na naona watoto wa kiume walivyo karibu na mama.Afu bora huyo mtoto awe wa kiume. Wababa wengi wana mapenzi yalopitiliza kwa watoto wao wa kike. Which is natural. Akiwa mwanao ukiona baba ana mspoil utavumilia; na labda unaweza hata ukafurahia. Lakini kuna watu nawajua wanafikia kukasirikia kitendo cha waume zao kuwa na attention zaidi kwa watoto zao wa kike. Sasa nambie mtoto huyo si wako. Ndo hapo mtu anamchukulia mtoto kama mke mwenzie. Kazi kweli kweli. Je wewe kama baba utaacha kuonyesha mapenzi kwa bintiyo usimchukize mkeo? Je utampenda tu mkeo atajiju???
Maana kuna wanaume kila unapomkuta amemkumbatia bintiye. Lol.
watoto kama ni wa kiume hawatampa shida mama wa kambo ila kama ni wa kike shida itakuwepo..........muhimu mke na mume muwe na msimamo mmoja lakini mmoja akionyesha kulega lega basi ndoa itakuwa ngumu kama nyie wawili mtashindwa kuelewana vizuri katika kuwalea hao watoto.
Hongera shosti,manake mwanamke mwenzio kukusomea mbovu ukakakimnya jina lako linafanana na upole wako.Mie nimeolewa nikamkuta mumewangu anawatoto wawili wamechwa na mama yao wakiwa na umri wa miaka3 na mwengine miezi 10 na sababu kubwa nilikua nawaonea huruma wale watoto vp mwanamke unagua na moyo wa kiume kumuachia mwanamme watoto wako wadogo sababu anasema atalijua jiji,leo hii watoto wako 16 na 13yrs nawapenda sana na watoto wangu wanajua kama wale ni dada na kaka yao wa kwanza na sijawambia kama sio mama mmoja,mama yao watoto nilimpigia cm nikamwambia njoo uwaone watoto alinambia usione raha yakulala na baba yao ujue na raha yakulea pia unao hao nilishangaaa! lakini nimezowea na maisha yanakwenda,sasa ukipenda boga upende na majani yake...
Eiyer sio kwamba natarajia ila nimeshaona kwa wengi kwamba watoto wanapokuwa wakubwa na mama yao bado yu hai sio rahisi sana wakamheshimu mama wa kambo automatically. Kwa maana ya kuwa, wengi hua trained na mama mzazi kutomheshimu mama wa kambo. Hivyo wanahitaji kuonyeshwa kwamba hiyo heshima ni muhimu ili familia yote iwe na furaha. Ndio maana ntajitahidi/hakikisha tunaelewana lugha. . .na hilo likishindikana basi lazima maisha yatatuwia magumu, especially kama baba yao nae wanamwendesha tu.
Wanaume wasiokuwa na watoto ni adimu sana siku hizi mithili ya bikra ya mwanamke mwenye miaka 20!