Ukiwa mtaani au kwenye mikusanyiko ya kijamii unajihisi huru kutoa maoni yako juu ya mambo mbalimbali nchini?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wakuu,

Screenshot 2023-09-11 004118.png

Uhuru wa kutoa maoni umehakikishiwa na katiba katika ibara ya 18 kwa kila mtu bila kuathiri sheria za nchi. Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa mawazo yake nje. Uhuru wa kutoa maoni hautakiwi kubaki kwenye makaratasi, badala yake watu wajisi kuwa huru na waweze kutoa maoni yao bila uoga.

Mtu anapotoa maoni yake huwezi kumpangia cha kusema, anachosema kinaweza kuwa kinyume na unachoamini, kukukasirisha au kupingana na wewe, ili mradi havunji sheria yoyote mtu huyo hatakiwi kuingiliwa kwenye uhuru wake wala kuminywa kutoa maoni yake.

Je, uko huru kusema mawazo yako?
 
Uhuru upo ila sio uhuru kam uhuru yani uhuru uliopo ni uhuru uhuru tu maan ukijichanganya cha mtema utakiona😆
 
Uhuru wa kutoa maoni ndiyo uliosababisha kupotea kwa memba mwenzetu hapa jf Ben Saanane.
Kuwa mwangalifu dhidi ya uhuru wako
 
Wakuu,

Uhuru wa kutoa maoni umehakikishiwa na katiba katika ibara ya 18 kwa kila mtu bila kuathiri sheria za nchi. Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa mawazo yake nje. Uhuru wa kutoa maoni hautakiwi kubaki kwenye makaratasi, badala yake watu wajisi kuwa huru na waweze kutoa maoni yao bila uoga.

Mtu anapotoa maoni yake huwezi kumpangia cha kusema, anachosema kinaweza kuwa kinyume na unachoamini, kukukasirisha au kupingana na wewe, ili mradi havunji sheria yoyote mtu huyo hatakiwi kuingiliwa kwenye uhuru wake wala kuminywa kutoa maoni yake.

Je, uko huru kusema mawazo yako?
ndio hasa humu jukwaani.
licha ya baadhi ya nyuzi kufutwa na kupingwa ban.
Kwa kiasi kikubwa sana kuna uhuru wa kusema upo.
 
Sio huru kivile inabidi nitumie mbinu za werevu wa nyoka, lahaja za lugha na tamathali za semi ili kuruka viunzi vya wasiopenda kukosolewa
07a35b9b495260b7cea572ed7901b77a.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naogopa maadui zangu wasije kuniharibia bora nikae kimya tu nishuhudie na kuchangamsha genge nyuma ya keyboard
Kuna njia nyingi kuchangia mabadiliko, sio lazima kila mtu awe mbele kabisa.... hapo hapo ulipo nyuma ya kibodi unaitendea haki nafasi hiyo?
 
Ukila kiapo cha kutunza siri utagundua kuwa hauna uhuru wa kutoa maoni
Sio tu viapo wapo ambao hawajafanya viapo ila wanabugudhiwa pindi wakiwasema wale wanaolitendea taifa ndivyo sivyo kwa misaada wa wale wasiotumia weledi ila utashi,kwa msukumo wa wanasii hasa.
 
ndio hasa humu jukwaani.
licha ya baadhi ya nyuzi kufutwa na kupingwa ban.
Kwa kiasi kikubwa sana kuna uhuru wa kusema upo.
Nje ya jukwaa hili je, uko huru kujimwaga kutoa maoni yako kwa kuzingatia kuwa huvunji sheria?
 
Kwamfano wewe kwa kutoa hayo maoni yako mtu akatokea akasema hayo ni maoni ya kijinga umefikiria kwa kutumia makalio utafanyaje?

Maoni ya staha ni kupinga kinachosemwa na yeyote ambacho unaamini kuwa hakiko sawa lakini lazima uje na hoja mbadala au suluhisho.
 
Back
Top Bottom