najua hii topiki haitokuwa poplar na baadhi ya watu humu ndani na hata wenye website lakini potelea mbali
je ni kweli wizara hizo zimejaa makabila ya wachagga,wanyakyusa na wahaya?
Mimi nilikuwa siamini mpaka pale nilipo ambiwa kuwa kuna ukabila wa hali ya juuu kule ikulu na vile vile namba mbili kwa ukabila ni tra je kuna ukweli katika haya?
Japo kuna watu wanasema kuwa ni udini lakini sumu ambayo hatuko tayari hata kuijadili ni hii ya ukabila na ndio inayoturudisha nyuma je mnakubaliana nayo?
-jambo forums where we dare talk openly
Asante san kwa michango yako yote na siku zote huwa naomba Mungu Akusaidie na akupe Uzima Daima Asante sana juu ya yoteunajua mtu usipojua historia yako.. kuna hatari ya kujaribu kuiandika upya! Ili kuelewa hapa tulipo sometimes we have to look back where we are coming from. Historia yetu haikuanza jana au juzi (kama baadhi wanavyotaka tuamini) matatizo tuliyonayo leo hayakuanza jana (isipokuwa haya ya kina Richmonduli!) lakini mengi yana msingi toka huko nyuma. Binafsi, nitashtuka zaidi kama kwenye nafasi fulani kwenye taasisi kumejaa Wakerewe, Wanyali, au Watindiga.. kwa sababu hakuna jibu zuri la kihistoria linaloweza kuonesha kujaa huko!!
La maana ni kuongeza jitihada ili baadaye hali ielekee uwiano kwani Waha na Wamang'ati na wenyewe watakuwa na shule nyingi na wanapata nafasi nyingi za kusoma.. kwani hata hivi sasa bado Uchagani, Mbeya n.k wanaendelea kuwa na shule nyingi na zenye kutoa wanafunzi wengi (angalia matokeo ya hivi karibuni!)..
Do we need some kind of affirmative action which would not be translated as reverse discrimination?
tuipendenchiyetu, karibu na tunafurahi kuwa umeweza hatimaye kuamua kuchangia badala ya kuwa mtazamaji tu.
a. Katika maendeleo yote ya elimu hadi hivi sasa, Makabila hayo yamerudi nyuma au yameendelea mbele?
b. Ili kuweza kufikia uwiano, je tuamue kuyafunga breki, kwa mfano kusitisha kwa miaka mitano kuchukua wanafunzi wa elimu ya juu toka makabila hayo?
c. Tukiamua kufanya hivyo, tuhakikishe kuwa hawaendi kusoma nje ya nchi pia kwa muda huo?
d. Je, tunapopokea CV ya mtu au kumchagua mtu tukiona jina la "Kagaruki", "Mwakipesile" au "Lyimo" tuwaengue moja kwa moja?
e. Kwenye ofisi ambazo zimejaa watu wa makabila hayo tuzipangue na kuwaaingiza watu wa makabila mengine ilimradi isionekane wamejaa watu wa kabila moja?
f. Tukishaanza kufanya hivyo na tukagundua kuwa watu warefu ndio wengi zaidi, tuanze kuhakikisha watu wafupi nao wanaingizwa? tukifanya hivyo tukagundua kuwa wengi wanaofanya kazi maofisini wanatumia mikono ya kulia, tuanze kutafuta watumiaji wa mikono ya kushoto? na tukimaliza hivyo na kugundua kuwa wengi waliojariwa ni wanaume, tuwapunguze ili tuongeze wanawake? Tukishamaliza hivyo na kugundua kuwa wanawake wengi waliojariwa ni waislamu, tuwaombe wastaafu ili wawapishe wakristu? tukifanya hivyo na kugundua kuwa wakristo hao wengi ni wakatoliki tuwatake wawamegee nafasi hizo waprotestanti?.. ni jinsi gani tutasitisha zoezi hilo la kibaguzi?
Mzee Varisanga uko sahihi kabisa! wakati mwingine woga tu unamkosesha mtu ajira kwa kuogopa kuomba kazi mahali fulani akiamini kuwa kwa vile yeye si wa kabila fulani basi hawezi kupata kazi.Kwa kawaida ukishakuwa na Umri Mkubwa unakuwa umeona mambo mengi sana.
Mimi nina Umri wa kutosha sasa.
Naomba ni kanushe kuwa maeneo yote yaliyotajwa hayana Ukabila.
Wafanyakazi walioko pale wako kwa ajili ya elimu zao.
Kama umesoma na unafiti kwenye Fani lazima utapewa kazi.
Ukiuliza hapo utaambiwa wachaga wengi wako Ikulu, TRA, BOT n.k
Wote hao wamesoma Shule ndiyo Maana wako pale.
Watu wanaolalamikia Ukabila ni wale ambao hawakusoma na kama wamesoma sehemu kubwa wametawaliwa na majungu.
Kabila la Wahaya lilikuwa likisakamwa kwa kuwa na ukabila lakini si kweli, Wahaya ni watu wanaopenda sana kusoma na kujiendeleza Ndiyo maana Wanakuwa sehemu muhimu za kazi kwa ajili ya Uwezo walio nao.
Ukabila tanzania hauko kabisa.
unajua mtu usipojua historia yako.. kuna hatari ya kujaribu kuiandika upya! Ili kuelewa hapa tulipo sometimes we have to look back where we are coming from. Historia yetu haikuanza jana au juzi (kama baadhi wanavyotaka tuamini) matatizo tuliyonayo leo hayakuanza jana (isipokuwa haya ya kina Richmonduli!) lakini mengi yana msingi toka huko nyuma. Binafsi, nitashtuka zaidi kama kwenye nafasi fulani kwenye taasisi kumejaa Wakerewe, Wanyali, au Watindiga.. kwa sababu hakuna jibu zuri la kihistoria linaloweza kuonesha kujaa huko!!
La maana ni kuongeza jitihada ili baadaye hali ielekee uwiano kwani Waha na Wamang'ati na wenyewe watakuwa na shule nyingi na wanapata nafasi nyingi za kusoma.. kwani hata hivi sasa bado Uchagani, Mbeya n.k wanaendelea kuwa na shule nyingi na zenye kutoa wanafunzi wengi (angalia matokeo ya hivi karibuni!)..
Do we need some kind of affirmative action which would not be translated as reverse discrimination?