Jinsi ya kupata kazi za remote katika mashirika ya kimataifa yaliyo nje

TheCrocodile

JF-Expert Member
May 31, 2021
1,077
2,814
Leo ningependa kuzungumzia namna kijana yoyote wa Kitanzania ambae una utaalamu na/au ujuzi katika eneo fulani unavyoweza kupata kazi katika mashirika na makampuni ya kimataifa yaliyopo popote duniani na kuweza kufanya kazi remotely ukiwa hapa hapa nchini. Kwa mfano mimi nafanya kazi katika mradi wa kimataifa; makao makuu yao yako USA, lakini mimi nafanyia hapa hapa bongo. Kupata hii nafasi nilishindana na watu kutoka ataifa mbalimbali kama vile USA, Ehtiopia, Nigeria, na Kenya. Nilifanya raundi tano, nakumbuka hadi raundi ya mwisho tulibaki mimi na jamaa mwingine wa kutoka Ethiopia. Hivyo, inawezekana kabisa hata wewe kijana wa Kitanzania ukapata kazi za namna hii, you just have to be competent, and know where to look. Kufanya kazi remote kuna faida kubwa sana, kwani ukiacha kutokua na mizunguko ya kwenye magari/daladala kila siku asubuhi na jioni, pia unakua unalipwa kwa dola za Kimarekani, wakati wewe matumizi unafanya kwa pesa za madafu (Tshs), hakuna kitu kizuri kama kulipwa kwa $$ halafu unafanya matumiz kwa Tshs.

Nitaongelea kila kitu hapa hapa jukwaani, yeyote mwenye swali aliweke hapa hapa, nitalijibu hapa hapa, nitamaliza kila kitu kwenye uzi huu huu, hakuna cha PM wala wapi.
NItaongelea platforms ambazo unaweza pata kazi hizi, pamoja na nini ufanye ili uweze kuji position na kuwa competitive katika kupata hizi kazi.

Kitu cha kwanza kabisa ambacho ni muhimu kuliko vyote, lazima uwe VIZURI SANA kwenye kazi yako, yaani you have to be one of the best...!! Uwe COMPETENT kweli kweli, maana hizi nafasi unakwenda kushindana na mashine kutoka Nigeria huko, Kenya, USA, na kadhalika...! Na hao watu wako nondo kweli kweli, they do not joke, so na wewe inabidi uwe level hizo za hali ya juu! Ukienda kichwa kichwa, hata ukifanikiwa kuitwa interview utambwela balaa hadi utajiona bonge la kilaza!

1. Andaa resume yako na iwe imenyooka, iwe katika mfumo ambao ni very competitive. Kuna tools nyingi sana za kuandaa resume yako na kuifanya competitive. Kwa mfano, Canva:https://www.canva.com/resumes/templates/professional/; Novoresume, Free Resume Templates for 2024 [Download Now]
Ni muhimu sana uandae resume yako iwe ya kibabe kabisa, sio unaandaaa resume ya kichovu, hutafika popote katika competition ya kimataifa.

2. Hakikisha unakua na a very STRONG ONLINE PRESENCE: Unataka kufanya kazi remote na mashirika ya kimataifa halafu hata hauijui LinkedIn? Bro, are you serious? Kama hauna account LinkedIn, baada tu ya kusoma hii post, kitu cha kwanza unatakiwa kufanya haraka sana ni kwenda LinkedIn, kujisajili kule na kuhakikisha una profile very strong (5 star profile), baada ya hapo hakikisha unaomba connection na watu walio katika industry yako una connect nao as many as possible. Kisha, mdogo mdogo anza kupost masuala yanayohusiana na kazi yako au vitu unavyovifanya. Are you a tech wizard and you are working to solve a challenge through technology? Why not post what you are doing there? Are you employed somewhere and today you had a workshop with some stakeholders to discuss on something? Why not share over LinkedIn with some nice photos? Pamoja na LinkedIn, pia kuna platform zaingine kulingana na industry yako, mfano watu wa tech wana zile platform zao ambazo zinakua na communities, wana discuss ma solution, na ma code; wewe ni programer, kwa nini usijiunge huko?
Niwaambie kitu, hii kazi yangu niliyoipata, mimi hata sikuiomba, I was just contacted on LinkedIn na mtu ambae yupo huko, akaniambia kuna nafasi huku nilipo naona inakufaa sana based on what you have been sharing here on LinkedIn, akaniambia kama nipo interested aniunganishe na recruiter wao, ikawa imeisha hiyo.

3. Ongeza zaidi ujuzi wako:
Sawa, umemaliza degree ya Information, Communication, and Technology hapo UDSM; Lakini je, una nini cha ziada? Kuna platforms kama Coursera, Udacity wanatoa courses fupi fupi katika maeneo tofauti tofauti- Zipo za bure na za kulipia, anza na zile za bure angalia ipi itakuongezea kitu, zipige nyingi nyingi.... Ukijipanga pia ukapiga hata na zile za kulipia kwa kutoboka kidogo mfuko sio mbaya, YES. Kama unaweza kutoa hadi shilingi 150,000 - 200,000 kugharamia kumgonga demu why not usitumie gharama inayokaribiana na hiyo kujiongezea ujuzi na skills ambazo zitakusaidia pia? Pia, usisahau YOUTUBE kuna madini ya kutosha kule, bure kabisa. Badala ya kupoteza bundle lako kuangalia umbea wa insta, ingia kule ucheki madini ujiongezee SKILLS. Niwaambie tu, dunia ya sasa hivi skills na ujuzi wako ni muhimu sana sana, usije ukaingia kwenye mtego wa kukusanya vyeti huku huna unacho-gain...!! Mimi hadi nimepata hii kazi ya remote, hawajawahi kuniambia hebu tuone vyeti vyako hata mara moja..!! Kwa hiyo zingatia sana katika kuongeza ujuzi na skills zako, vyeti viwe ushahidi tu.

4. CONNECTION
Usijifungie tu chumbani kwako, connect na ongea na watu mbalimbali kwenye industry yako hasa walio katika nafasi za juu kimaamuzi na wale waliokuzidi uzoefu. Hkikisha wanajua ujuzi na skills zako na what you can bring on the table. Hii ianzie kote kuanzia kwenye mtandao, ndio maana kwenye point namba 2 nikaongelea presence yako kwenye mitandao kama LinkedIn, ukiwa kule unaweza ku connect na watu walio katika industry yako na wakiangalia posts zako na profile yako wanajua kuwa huyu ana skills hizi na zile. Pia, vile vile offline hudhuria zile events zinazohusiana na sekta yako na hakikisha unaongea na wale watu waliokuzidi na kubadilishana nao mawazo.. Ni rahisi mtu kukupa referral namna hiyo, kama ambavyo ilinitokea mimi alienipa referral alifanya hivyo kutokana na kuona posts zangu na profile yangu LinkedIn.

5. Platform unazoweza kupata remote jobs: Hapa chini nitapost link za platforms ambazo unaweza pata hizi kazi za remote zile ambazo nazifahamu. Wadau wengine wanaweza kuongezea links zaidi.
Jobgether is the Largest Remote Job Platform worldwide with more than 160k remote jobs available across the world.

Karibuni kwa yoyote mwenye swali au anaetaka kujua zaidi kuhusu chochote, nipo hapa, maswali yote yaulizwe hapa na nitajibu kila kitu hapa hapa sebuleni!!

DA HUSTLA karena
Stv Mkn
 
MKuu uko right mzee ukujibrand vizuri kule linkedin unapokea sms za michongo ya romote jobs that pays in foreign currency... especially USD
Mimi last week nimepokea sms jamaa amesema amepitia profile yangu na ameona nafaa kwenye kazi ya Technical Writer in machine Learning/Data science field
Najua atakuwa amepitia nondo zangu ninazondikaga za Quantum Machine Learning.

Vile vile three days back nimepokea sms jamaa ananambia kwamba kuna mchongo wa Business analyst role kama niko interested nimchek.....

Michongo yote inatoka USA... Noma Sanaaaaaa

Five years back kuna jamaa now yupo UK Alikuwa anasema kwamba yeye anapokea michongo kutoka Uber na Google etc na wanamfata mwenyewe... nilikuwa namuona kama mchawi vile... now its happening to me.. anyway nimeanza kutumia pc 2003 and nlianza kucode since 2012, so Its a long journey

NB. Kama huna hela ya kulipia courses za coursera za online unaweza apply financial aid ... just google how to apply for financial aid to coursera courses.....
Thanks in advance.
 
Safi sana mkuu, ushuhuda mzuri kabisa huo, excellent!!
Ndio maana nimesema kwa kijana atakaesoma huu uzi na hana account LinkedIn na ana ndoto za kulipwa in USD akiwa Bongo, kitu cha kwanza inabidi immediately aende LinkedIn, ajisajili na kuwa na akaunti kule!!
Asante sana mkuu kwa ushuhuda!!
 
Asante kwa uwasirishaji mzuri! Ebu tupe your job daily routine within a week!
My daily routine revolves around kutoa support katika nchi ambazo mradi unakua implemented kwenye issues za data pamoja na reporting of indicators. Kwa mfano leo I was working on an annual report ya mwaka jana, na pia nilikua na virtual meeting na our team in Nigeria kutoa technical support kwa issues zao za data, kuna data zao zilikua na discrepancies kidogo, so niliziflag ili waweze kuziangalia na kuaddress.
Morning_star
 
Kama kaz ya kushindana had na wanaija hiyo ni zaid ya kuomb kaz tra we bro ilikubeba nathibitisha kwa kusema jamaa yangu ilikubeba bahati/ nazan ushawah sikia matangazo michezo ya bahati nasibu ndio hiyo
Unaweza ukawa sahihi, lakini hata bahati ya lifti huwa inampata mtu alie barabarani.
Kwanza, ina maana nisingekua na active presence LinkedIn ina maana hata nisingejua kuhusu hiyo kazi.
Pamoja na bahati lazima uwe fiti pia, ningekua siko fiti hiyo bahati isingenisaidia kitu. Ndio maana nimesisitiza sana, lazima uwe COMPETENT in every sense of it!
 
Mkuu Linkedln ni mtandao professional tu kwa ajili ya watu wenye elimu kubwa.
Unaweza kuweka kama ni tour guide na kazi zingine? Au ni zile proffesional kubwa?
Mkuu, unaweza ukawa na akaunti yako kule kwa level yoyote ile uliyonayo.
Mfano, kuna jamaa yangu elimu yake yeye ni Form 4 na vyeti vya NIT na VETA, ni dereva NGO fulani hivi; Ana akaunti LinkedIn na yupo very active, anapost mara nyingi akiwa field huko, mfano changamoto za njia za kufika field, namna anavyosadia timu yake waweze kufika field kwa usalama, na kadhalika. Na jamaa anajikusanyia point sana, juzi kati alikua contacted na HR wa NGO nyingine shindani akimuuliza kama yuko interested wampandie dau wambebe...!!
Tena kama uko kwenye issue za tourism huko mambo mbona mengi sana ya ku share? Ukiwa field huko, mambo unayokutana nayo, vitu unavyofanya, ukiwa na wageni wako huko, na kadhalika. Hapo utajibrand vizuri sana kama tour-guide wa kipekee kabisa!
The Lastdream
 
Kama kaz ya kushindana had na wanaija hiyo ni zaid ya kuomb kaz tra we bro ilikubeba nathibitisha kwa kusema jamaa yangu ilikubeba bahati/ nazan ushawah sikia matangazo michezo ya bahati nasibu ndio hiyo
Nimepata bahadi ya kunetwork na wanaija... Wale jamaa ni next level lakini IQ zetu watz na wanaija ni zile zile sema wao ni wapambanaji. Yuko radhi ashinde njaa miezi sita huku hela ya kula akinunua bando la kujifunza code
 
Absolutely true mkuu! You are very right.
 
Back
Top Bottom