Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Mkjj,
Kwanza ninawapa pongezi wanajambo wote kwa kukata issue!.mimi nimsomaji wa siku nyingi toka bcs lakini si mchangiaji.Lakini hii maada imenikumba hata mimi katika harakati zangu za maisha ya kazi,nilipokuwa ndani ya mfumo wa serikali
Hili swala ni gumu kwa kuangalia kwa inje,nikiwa na maana ya kuwa kama mtu si mwajiriwa wa serikali au shirika la umma lolote.
unachokisema ni sahihi kwa wakati huo,lakini kwasasa hivi makabila mengi wamesoma,lakini kwa sababu waliotangulia ni wa makabila hayo,basi kazi zitakwenda kwa kuangalia kama muombaji anatoka kwenye kabila lake au laa.hapa ninamaana hakuna usawa,hata hizo nafasi za shule zitakwenda kwa mfumo huo.kwa hiyo labda tujadili nia mbadala lakini ukweli ndiyo huo kwa mtu ambaye yupo ndani ya mfumo wa serikali unaona hili,lakini kwa mtu ambaye haupo ndani ya mfumo huo unaweza usikubaliane na mtoa hoja.Ninaomba kutoa .01%

SIMPLY UNTRUE!
Mimi namuunga mkono mia kwa mia M-kijiji, kwamba kweli ajira ziko skewed kuelekea kwenye makabila fulani kwa sababu ambazo zimetajwa. Tunaona kwamba sasa makabila mengine nayo sasa yamo vizuri tu kwenye ajira kutegemea na uwezo wao.

Hata hivyo ni vigumu kumwondoa mtu ambaye tayari ni "insider". Kufanya hivyo kunahitaji matayarisho pamoja na level playing field.

Sasa kama una evidence ya kutokuwepo kwa usawa huo katika kinyanganyiro cha kazi, then unatakiwa kuyasema hayo.
 
mbona ile thread MSIBA WA MANGI MAREALLE imefutwa? ilikuwa na ubaya gani...peple would like to know whts going on since all leaders would be there for the burial which starts today and end tommorow,and ccm in moshi is doing all what it can to make the burial a ccm affair ,i think so as to seal the mass support it is about to enjoy in kilimanjaro region...

YES why delete it?
 
sasa tunapoongelea UKABILA au CHUKI si ndio kama hivi,sasa ukiondoa thread ya yule mzee anayeendaa kupumzika kwa amani MANGI MAREALLE OBE tukueleweje? INA MAANA humu ndani mtu akiwa mchagga au wakuja ni kosa..thats whaat it sound like ...hata hivyo if you have decide to delete it its okay,you dont need to restore it..but we now undestand that some people here inside who we discuss there issues ,we may have be biased with there origin..yes stiff debate to WAKUJA or WAMLIMA,but for wa mjini are UNTOUCHABLELES..

Please lets look on issues in national and internatinal perspective way ,and not biased to our homestead boerders!!!! call spade a spade !!!!!@>//;.
 
Sasa Phelemon ndo umefanya nini hivi? Hiyo ni Flooding ndugu.

Halafu kama hujaangalia vema usilaumu tu kuwa thread flani imefutwa. Nadhani hujaangalia vema au ku-search for it walau uone iko wapi.

Aidha sidhani kama suala la ukabila lina nafasi katika maamuzi ya thread ipi ifutwe ama ipi ikae.

Nadhani ukiiona thread yenyewe utajua umehukumu visivyo. Nitaandika kwenye thread husika ujue ipo ila haijachangiwa. Sijapenda reaction yako as long as najua hujajishughulisha kuitafta thread husika.

Anyway, you're welcome
 
pm

duuuhh sasa nawewe unaleta mpya hapa, hii sijawahikuona, yaani thread kufutwa kwa kufuata ukabila!!!!!!!!!!!!!!, NEVER ON JF or not to my experience either

punguza jazba ndugu, thats absolute-overreaction
 
tuipendenchiyetu...

Kama nilivyokuonesha hapo juu madai kuwa "Ukabila unakua kwa kasi" siyo mageni! makabila yanayolaumiwa kuwa na ukabila ni yale yale Wahaya, Wanyakyusa, na Wachagga! Unioneshe ukabila kama ungetaja makabila kama wandegereko wamejaa ofisi fulani, wamakuwa wamejaa ofisi fulani hapo ningeshtuka kidogo. Siyo kwa sababu hawajasoma au hawana watu wengi la hasha!

Nimeuliza hapo juu sasa tufanye nini ili TUPUNGUZE wingi wa Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa katika ajira mbalimbali bila kuwafanyia ubaguzi? Of course njia ya kwanza ni ya kuwaruka na kuwapita katika ajira! Kama kwenye cheo fulani wanaofuatana ni mchagga, mmwera, mbena, na mndele...japokuwa mchagga anazo sifa zaidi (kielimu na kiuzoefu) bati tumruke na tumchukue mndele ili tupunguze wachagga!
 
hABARI ZA MASIKU WANA JAMBO!
UKABILA UPO ANAYESEMA HAUPO NI MKABILA MWENYEWE!

HAYA MAKABILA YANAENDEKEZA UKABILA HAYATAKI KABISA KUSIKIA MTU ANASEMA AU ANALALAMIKIA UKABILA! CHA AJABU MKABILA HUYU ANAAJIRI WATU 2O WA KABILA MOJA HALAFU HATAKI MTU MWINGINE ASEME HUO NI UKABILA, YULE ATAKAYESEMA ATANYOSHEWA VIDOLE ETI YEYE NDIY MKABILA KAMA UNAVYOONA HAPA!

JE MWAJUA SIKU HIZI BONGO KUNA HOTEL AMBAZO KUNA VYAKULA VYA MAKABILA MBALI MBALI?

SIKU MOJA NILIKUTA KATIKA HOTEL/BAR MOJA KUNA WATU WA KABILA MOJA WAJARUO WANAKURA, WANAKUNYWA NA KUSIKILIZA MIZIKI YA BENGA(luo).

SASA HAPA UNADHANI UKIGOMBEA AU WAKATI WA KAMPENI UKABILA HAUTAKUWEPO?

JE MWAJUA SIKU HIZI K=MAKABILA MENGI YA TANZANIA YAMEIBUKA NA KUANZA KUIMBA NYIMBO KWA KUTUMIA LUGHA ZAO!
WAHAYA, WANYAKYUSA, WAKURYA NK!

YOTE HAYA MNADHANI YA MWELEKEO GANI??!!

NINAMALIZI KWA KUSEMA ONENI AIBU HUKO TRA, BENKI KUU ETC, ACHENI UKABILA UTAWATAFUNA TU!!
 
Mkira,
Mjaluo kuwa na hotel yake yenye chakula cha Kijaluo sio Ukabila ndugu yangu acha kuongeza chunvi. Mbona Wachina, Wahindi wanazo hotel zao kila kona duniani nao tuseme ni wakabila hali Mkira hapo ulipo chakula chako ukipendacho ni hicho cha wahindi na Wachina!. tena yaonyesha wewe mwenyewe ktk hotel za Wajaluo maanake hata nyimbo zao unazimanya!
Sasa unataka kunambia leo hii Mkandara nikipika viazi vitamu na samaki wangu Furu basi nimekuwa mkabila maanake watakao penda mapishi yangu ni watu wa ziwa?...
Duuuh, ama kweli Ukabila una tafsiri mia moja!

Kisha huyo aliyeajiri watu 20 ktk ofisi moja ndiye Mkabila... hizo ofisi ni asilimia 000.1 ya sehemu zinazotoa ajira na watu kama hawa ndio tunaowapiga vita. Tupe jina tutalipiga vita lakini sio kusema tanzania kuna Ukabila. Rudia tena hotuba ya Mwalimu.
Ukisema Ukabila upo nchini ina maana swala hilo la kuajiri kabila yako bila vigezo vya uwezo wa kiutendaji unakubalika na kutumika ktk ofisi nyingi hapa nchini.
I don't think so,..
Leo hii tunaposema hakuna Ujambazi TZ haina maana hakuna kabisa jambazi na mifano kama hii ndio akina Mkapa na JK wamekuwa wakiitumia sana ktk vita ya Rushwa ati rushwa lipo kila sehemu duniani?... Ujinga mtupu kwa sababu hata wavuta unga wapo kila kona duniani na imekuwaje wanapigwa vita na kufunguliwa mashtaka.
RUSHWA, Tanzania limekubalika na linatumika karibu kila ofisi kama vile ni kitendo halali, hii ndiyo lugha tunayozungumza.
 
hiyo flooding mnaweza kuifuta ...ila siwezi kusema sikuiona ,kwa sababu nipo makini sana always kuangalia chochote kabla ya ku complain..and what i did niliangalia thread hadi thread hadi kufikia feb 14..mara tatu na sikuona kitu na still nikamuomba na mtu mwingine kwenye pm anisaidie kuitafuta naye kama mimi hakuiona...
anyway tuendelee kukata issues tusitafute mchawi.peace!!!!
 
Mkira, inaonekana huelewi maana ya ukabila na unachangaya ukabila na watu wa kabila moja kushikiriana na kufanya mambo fulani kwa pamoja au kutunza mila za kabila lao. Ukabila si kuzungumza lugha ya kabila lako au kula chakula cha kikwenu. Na zaidi ya yote ukabila si kuwa ofisi moja na mtu wa kabila lako! Nikiwakuta wafipa wanne kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa kule Rukwa, naweza kuita huo Ukabila? Je nikienda Songea kwenye uwanja wa Majimaji karibu na soko kuu pale na kukuta wengi waliojiriwa pale ni wangoni na wandendeule nitasema pana ukabila hapo? Au niende pale Makorola, au barabara ya 11 na kumi na mbili karibu na soko "Mjinga" na kukuta kuna wasambaa wengi wanafanya vibarua pale, wabondei na wazigua nitasema kuna ukabila?

Kwa vile umejifatutia ugumu usio wa lazima wa kutokuelewa ukabila ni nini, nimeamua basi kukusaidia kuweza kuona ni wapi umepotoka katika hoja.

Ukabila ni hisia isiyo na msingi katika ukweli (biased) ambayo inamfanya mtu au jamii ya watu kuamini na kukubali kuwa kabila lao ni bora zaidi, lenye kustahili zaidi, na lenye tunu iliyo ndani (intrinsic value) inayotofautisha kabila hilo na makabila mengine. Watu wenye hisia hizi huamini kuwa makabila mengine ni duni kiuwezo na kinafasi na pia makabila hayo mengine hayastahili nafasi zile ambazo mtu wa kabila hilo (linalojihisi bora) anazo. Kwa maneno mengine, Ukabila ni hisia ya ubaguzi utokanao na habari zisizokweli kuwa kabila fulani ni bora zaidi kuliko makabila mengine na hivyo linastahili zaidi katika jamii.

Mara nyingi msingi wa ubaguzi wa namna hii siyo tofauti kubwa ya kabila hilo na makabila mengine bali ni tofauti inayoonekana (perceived difference) ya watu wa kabila hilo na makabila mengine. Inaweza kuwa ni tofauti ya lugha, maumbile, na makazi. Hivyo unaweza kukuta watu wanaozungumza lugha moja wakibaguana kwa misingi ya nani anatoka familia au ukoo gani katika kabila hilo. Hata hivyo hapa tuzungumzie ukabila unaotokana haswa na tofauti ya lugha ya watu na tamaduni za watu ambao rangi yao ni moja (weusi).

Mtu mwenye ukabila wa aina hii hudharau watu wa makabila mengine kwa kuwaona duni na hivyo hujaribu kwa kila aina kukwepa kuhusiana nao na kuwapa nafasi. Je Tanzania kuna ukabila wa namna hii? Kwa ujumla si kweli kwani licha ya watu wa Tanzania kuoleana (wachagga wanaoana na wamasai, wapare), (wangoni wameoana na wasukuma, wahehe, wanyakyusa) n.k... Hivyo katika mahusiano ya watu wetu hakuna ukabila wa namna hiyo kwani tumeingiliana sana kiasi cha kwamba ukianza kumbagua mtu utajikuta unambagua shemeji yako!!

Sasa ni nini kinachotokea maofisini? Mwalimu aligundua tatizo lililoko maofisini ambalo watu wanalitafsiri kama ukabila. Kinachotokea maofisini na sehemu nyingi za kazi ambacho ni cha hatari zaidi kuliko ukabila hewa unaotajwa ni undugunization ambao unatokana na kujuanization. Wengi wanaopata nafasi za kazi, masomo, biashara n.k swali la kwanza ni "je namfahamu", "Je familia yake inafahamika"? Watu hawaulizi je "ni mhaya, mchagga, au mnyakyusa"?! sasa.. bahati mbaya ni kuwa tunafahamiana na kujuana na watu ambao tunatoka zaidi sehemu moja au shule moja n.k Hivyo, kiongozi mchagga yuko tayari kumpa nafasi mtoto wa rafiki yake mkurya kwa vile yeye na huyo baba wa kijana walikuwa wote Tabora Boys miaka ile!!! Sasa mchagga mwingine ambaye anawania nafasi ile ile kwa vile hajuani na huyo bosi.. usitarajie kuwa atapata nafasi!!

Sasa, kama alivyosema Mkandara kwa umahiri mkubwa watu wa kabila moja kuimba nyimbo za kikwao, kula chakula cha kikwao n.k siyo ukabila ama sivyo sisi watanzania tulioko nje ya nchi ambao tumeunganika katika jumuiya mbalimbali za Watanzania tunafanya ubaguzi kwa wale ambao si Watanzania! Watu wajumuiya moja wanaposhirikiana katika shughuli mbalimbali bila ya kujijengea hisia ya kuwa wao ni bora kuliko wote wa makundi mengine au wanastahili zaidi hao siyo wabaguzi. KKK ni wabaguzi kwa sababu wanashirikiana mambo yao nk lakini msingi wa ushirikiano huo ni chuki yao dhidi ya watu wengine. Watusi na Wahutu walipouana mwaka 1994 ni kwa sababu hiyo kuwa lile kabila jingine ni duni na lisilostahili!!

Katika Tanzania, ukabila wa namna hiyo haupo kwa watu wetu kama jumuiya. Hata hivyo, kuna watu ambao mmoja mmoja wanazo hisia hizo. Siku moja nilikuwa nazungumza na rafiki yangu ambaye katika kuzungumza akaamua kujisifia "unajua wachagga ndio most intelligent na smart tribe katika Tanzania, ndio maana wamesoma sana". Sasa, aliyesema maneno hayo binti wa miaka 18 tu na ni wazi hajui historia imetoka wapi, yeye akiona wachagga wamepata nafasi za uongozi hapa na pale anafikiri ni kwa sababu wachagga ndio smart kuliko watu wote! Of course, nilimsaidia kuona kosa la maoni yake na kuanzia wakati huo amekuwa akisahihisha mtazamo huo uliopotoka. Bila ya shaka wapo watu kwenye makabila au dini ambao kutokana na kutokuwa na habari sahihi wamefikia masuluhisho ya kujiona kuwa wao ni bora kuliko watu wa dini au makabila mengine. Watu wanamna hiyo ni lazima waoneshwe upotofu wa mawazo yao ili wajisahihishe! Wale wanaokataa na kung'ang'ania uduni wa watu wa makabila mengine, hao ndiyo wenye ukabila!
 
MKJJ:Umelifafanua vizuri sana jambo hili, na nadhani wengi watalielewa hivyo, hasa 'huyo' na wengineo wanaodhani kula kijaluo ndio kuwa mkabila. Ninakubali kabisa, kuwa "Mangi" aliyeko Songea akiuza bia na nyama choma zake si lazima aonekane kuwa mkabila kwa vile tu ati kuwepo kwake hapo kumesababisha 'Mangi' wengine nao kuanza kumiminikia Songea kuanzisha biashara za nyama choma na bia; na wala sio wangoni wa pale. This was (is?) the beauty and genious of Tanzania - you can (could) go anywhere and feel very welcome anytime!(sijui kama bado ni hivyo leo. I am a bit ignorant or outdated). Ni watu kama huyo rafiki yako uliyemzungumzia katika aya yako ya mwisho ndio wanaonitia wasiwasi na kuwa na hofu ya kurudishwa nyuma. Sina uhakika sana ya kwamba Tanzania imekwishapiga hatua kubwa katika mambo haya kiasi kwamba haiwezi ikatumbukia huko, tena kwa kishindo kikubwa na cha kuwashangaza walimwengu! Usisahau, it takes only a small spark to start an inferno where condusive conditions exist. Most of those conditions are due to "Ignorance."
Tumewaajiri akina Kikwete na wenzake waendeleze 'darasa' hili; lakini sijui kama kweli wataliendeleza ipasavyo.
 
Mwanakijiji & Kalamu,

It looks like people are confusing between tribalism and cronyism/nepotism
 
Mtz.. that is what is going on.. na Tanzania inatishiwa na huo "undugunization" kuliko ukabila. Believe me, kama una mtu unamjua kwenye ofisi fulani you have a better chance of getting hired than kama mtu aliyeko ni wa kabila lako!
 
That is very true! sasa hivi kuna hii trend watoto wa vigogo wa serikali nao "kufuata nyayo" si kitu kibaya kama kweli they are capable, lakini hao can we draw a line between the two i.e kupendelewa kwa sababu baba/mama na kigogo au uwezo halisi wa uongozi!
 
MWANAKIJIJI.

Naona unataka kupindisha mada na kuleta upofu sio siri ukabila umetawala sana hivi sasa.
Mama Mkapa alipokuwa Ikulu alifanya kila linalowezekana kuhakikisha anaingiza wachagga kila kona, na hata deal za rada na ndege ni wafanyabiashara wa kichagga wana mikono yao.

chukulia mfano daktari wa mkapa alikuwa dr.Maro mchagga na ni ndugu wa mama Mkapa, mpiga picha wa Mkapa na sasa Rais Kikwete ni mchagga na ndugu wa mama mkapa freddy Maro. na Ikulu imejaa wachagga wengi tu. foreign nako ni hivyo hivyo.

vipi TRA nako imetokea kama ajali? hujui kama ukiwa na jina Kittlya, mrema, mushi, lyimo, tesha, mbowe, Lauo, yaani TRA yote imeshikwa na watu wa moshi. jiulize hadi kituo cha ushuru kilichotakiwa kiwe Tanga lakini kiko Holili.
haya ni masuala ya ukabila ndani ya TRA ambayo ina mahusiano na wizara ya fedha ambako ni ngome ya watu wa kaskazini.

suala la uchagga TRA limefikishwa hadi bungeni. na kama ulifuatilia bajeti ya wizara ya ujenzi ambapo Mramba alihakikisha kila kitu kinakwenda Kilimanjaro na kuzua mtafaruku kwenye bajeti ya mwaka huu.

nchi yetu inakwenda kubaya hivi sasa. wanyakyusa nao wanataka kutawala JKT na Jeshi kwa nguvu hivi sasa labda kwa vile uko nje ya nchi. ndio maana hujui ukabila unavyotafutana nchi.
 
Mswahili,

Mimi sintaweza kubisha ktk hili ila nataka utupe mifano ya wazi ktk TRA.
Kuhusu Ikulu, dakrari wa rais na mpiga picha wake nadhani hivi ni vitu ambavyo hata na wewe na wananchi wote tuna nafasi ya kuchagua. Yawezekana nafanya makosa lakini sio Tanzania au Mkapa na JK peke yao. Viongozi wote wanachagua wao madakari na sio kuletewa mtu yeyote!..Tena Ikulu ndugu yangu ndio usiseme maanake hata Marekani, kumejaa watu waliokuwa wamefuatiwa maisha yao toka waanze hasa elimu ya sekondari.

Kifupi, tupe majina ya watu walioko TRA kwa sababu mimi nawafahamu jamaa kibao wanaotoka kila kona wako pale. Sielewi kabisa uachozungumza hasa kuhusu JKT na jeshi kwa sababu hivi vitengo vipo wazi kwa kila mtu kujiandikisha, sasa ikiwa wewe hujawahi kuomba kujiunga na jeshi inakuwaje leo iwe ni jeshi la Wanyakyusa hali wao wamejaa toka JKT hadi jeshi la wananchi kama kuruta! mbona hatusemi mafundi viatu wengi na wauza matairi used wengi ni Wachagga?
 
Naam Maalim Mkandara.

Mboma aliposhika jeshi akavuta sana watu wake.

na JKT kuna Mwamnyange akiwa na kina Mkissi uliza huko upate habari zao.

TRA GENERAL COMMISSIONER ni Kittlya Harry huyu ni mchagga na ndio mkuu wa TRA NI mchagga aliyebebwa na Mramba basil mchagga mwenzake.

TRA ina idara ya ushuru na forodha ambayo ndio idara nyeti inashikiliwa na George Lauwo mchagga anaripoti kwa Kittlya (mchagga), huyu ndiye commissioner wa ushuru na forodha.

msaidizi wake ni yusuf salim anatoka kilimanjaro na anatumia vyeti vya uongo kwani yeye ni mkristu anatumia majina haya. ila kwa vile anatoka kilimanjaro hakuna hatua zozote zinachukuliwa kuchunguza kashfa ya vyeti vyake.

Mkandara fuatilia makamishina wote wa TRA HALAFU utaona mwenyewe kilimanjaro ilivyodhibiti kitengo hiki nyeti.

pia tizama press realease ya TRA ya mwezi julai 2006 ambapo ilitamkwa wazi kuwa ' wanaoshangaaa ukabila TRA waende jeshini wakaulize wakyulya' aliyetoa statement hiyo ni mchagga. hata Tanzania Daima waliiandika hiyo habari.

suala hili limefika bungeni lina kila chembe ya usahahidi.
 
Ndugu zangu wana Jf nadhani nyote hapa (wale wanaosema ukabila haupo na wale wanaodai upo) mwaweza kuwa sahihi na madai yenu. Mimi ningependekeza tujiulize masuali haya matatu:
1) Je katika nchi yetu ya Tanzania hakujawahi kuwa na ukabila tangu tupate uhuru?
2) Kama jibu kwa suali hilo la kwanza ni ndiyo, sasa kwa nini kati ya mambo ambayo Serikali za mwanzo za Tanganyika ziliyakemeya vikali ilikuwa ni ukabila?
3) Kama jibu la suali la kwanza ni hapana, je ni lini ubaguzi ulikwisha kabisa nchini Tanzania?
 
Back
Top Bottom