Ujumbe wa wazi kwa Mhe. Edward Lowassa: Uchaguzi ni wako

Ahsante Mwanakijiji. Kama ningekuwa Lowassa nisingeona aibu kuitisha press conference na kukiri kuisoma barua yako na kuitafakari na kuamua kuifanyia kazi. Tatizo la viongozi wetu na watanzania kwa ujumla ni kuona aibu au kudhani kuomba radhi ni udhaifu. Hili ndilo linalomponza Mkapa sasa.

Sijui kwa nini hawaioni logic simple kiasi hiki. Kusimama na kuwaambia watanzania "I am sorry for what i did" ni virtue ya hali ya juu sana na inaweza kumsafisha mtu yeyote hata Rostam!

sio rahisi kuomba samahani
na kuomba samahani ni ustaarabu wa hali ya juu. inaambatana na kukubali kuwa wewe ni binadamu kama wengine - kuwa wewe sio malaika - kwamba unaweza kukosea kama kila mtu awezavyo kukosea

hata hivyo kuomba samahani kunaambatana na nia ya kutotaka kurudia tena. sasa kwa mfano rostam kama ni fisad kama tunavyotaarifiwa kwenye vyombo vya habari ana nia ya kutorudia kutuhujumu tena mpaka aombe samahani? subutu! huenda ndo kwanza kunakucha

na kuomba samahan kwa ukweli kunaambatana na kurudisha ulichokichukua pasipo uhalali. je, mkapa, yona etc wako tayari kuurudisha ule mgodi wa kiwira na vinginevyo? subutu! mkewe atakubali? say

kuomba sanahan sio rahis kihivyo
 
SOURCE RAIA MWEMA

NAJISIKIA niko huru sana. Wiki iliyopita niliandika makala iliyobeba kichwa cha habari kilichohusu kujivua gamba kwa Chama cha Mapinduzi, lakini makala hiyo ikitoa changamoto mbili ambazo CCM na viongozi wapya waliopewa hatamu za kuongoza chama hicho wanapaswa kuzisimamia na kuzitekeleza.

Mosi, nilisema hatua hiyo ya CCM kujivua gamba isiishie tu kuwaondoa watuhumiwa wa ufisadi katika nafasi za uongozi wa ngazi za juu za chama, bali chama hicho kiende mbele zaidi kwa kuwasaka mamuluki na mawakala wa mafisadi hao, ambao kwa miaka mingi wamewatengeneza na kuwasimika katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama, serikali, idara na asasi zake ili waweze kulinda na kusimamia maslahi yao katika kila maamuzi yatakayofikiwa.

Pili, nilizungumzia haja ya CCM kuondokana kabisa na usanii unaofanywa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wanaomiliki vyombo vya habari, ambao wamekuwa wakitumia vyombo vyao hivyo kujifanya wanakitetea Chama na Serikali.

Nilisema hatua hiyo inaendelea kuwaaminisha wananchi wazalendo wenye uchungu na nchi yao kwamba CCM na Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete na serikali yake wamefungamana na mafisadi hao, na ndiyo maana vyombo hivyo vimekuwa mstari wa mbele kujibu makombora yanayotoka upande wa pili wa wapinzani.

Kwa hakika, nimefarijika sana na mrejesho nilioupata kutoka kwa wasomaji wangu, na zaidi nilifarijika nilipomsikia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, siku hiyo hiyo ya Jumatano iliyopita, pengine baada ya kusoma makala yangu hiyo, katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma, akiwaasa wanaCCM na Watanzania kwa ujumla kuyapuuza magazeti yanayomilikiwa na mafisadi, ambao katika maandiko yao wanajifanya wanakisaidia CCM wakati ukweli ni kwamba wanakiharibia.

Ndugu zangu, kabla sijaingia katika mada ya leo, ningependa kutoa angalizo moja kwa kada zote za Watanzania wenye itikadi zao tofauti za kisiasa. Mapambano haya mapya yaliyoanzishwa na CCM baada ya vikao vya NEC Dodoma, ambayo kimsingi ni mwendelezo tu wa mapambano ya kweli yaliyokwishaanzishwa na watu wenye uchungu wa nchi hii kwa takriban miaka mitano sasa iliyopita dhidi ya ufisadi na vitendo vingine vya rushwa, yatakuwa hayana maana yoyote kama yatamwangalia tu Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge.

Watatu hawa kama tulivyoelezwa kwamba majina yao yalitawala katika vinywa vya wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, mjini Dodoma, wanaweza kuwa vinara tu waliokubuhu katika suala hilo, lakini katika mfumo wa sasa wa uongozi wa nchi yetu na vyama vyetu vya siasa, ufisadi umeenea kila kona na kila mahali.

Kwa hiyo, ninachoshauri katika angalizo langu hili ningependa kuona mapambano haya mapya yakilenga katika kuhimiza ujenzi wa uzalendo wa kweli vichwani na mioyoni mwa Watanzania katika kuhakikisha mambo kadhaa yanasimamiwa, yakiwamo ya ulinzi wa raslimali za nchi yetu, ufufuaji wa maadili ya viongozi na kujenga mshikamano miongoni mwetu ambao utahakikisha kiongozi mkuu wa nchi anapatikana kutokana na utashi wa Watanzania wenyewe badala ya kiongozi huyo kuchaguliwa na kundi la watu wachache wenye maslahi binafsi.

Nasema hivyo kwa sababu Taifa letu, kwa sasa, linakabiliwa na ufisadi mkubwa wa wizi wa mali za umma kwa upande mmoja, lakini linakabiliwa pia na ufisadi katika mifumo ya utawala wa nchi yetu. Ilifika mahali kundi la mafisadi ndio waliokuwa na nguvu na mamlaka ya kuamua ni nani awe mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na au mkurugenzi mkuu wa shirika fulani la umma.

Mipango yote hiyo wameendelea kuiratibu kwa ustadi mkubwa kabisa; kiasi kwamba hata linapotokea tatizo au janga linaloligusa taifa, mafisadi hao walihakikisha kuwa utatuzi wa tatizo au janga hilo lazima ulinufaishe kundi hilo kwa namna moja au nyingine. Kwa umoja wetu, kama wazalendo wa kweli, bila kujali itikadi za vyama vyetu, tukatae, tuseme kwa sauti moja kwamba inatosha!

Tuje kwenye mada ya leo. Wakati mwingine, nadhani ujinga wangu pengine ndio unaonifanya niwaze tofauti na weledi wetu tulionao katika nchi hii, na hasa katika masuala ya kisiasa na uongozi wa umma. Tunao wanasiasa wasomi na wenye uweledi wa kutosha, lakini mawazo yao na fikra zao vinafanana na mtu mjinga tu kama mimi na wengine wa aina yangu.

Katika ujinga wangu huu na weledi wa wanasiasa wetu hao, nitazungumzia kwa mifano mambo mawili. Nafasi ya waziri mkuu wa Tanzania kukwea hadi kuufikia urais na madai ya baadhi ya wanasiasa wetu kwamba wanao uswahiba na Rais wa Jamhuri hii ya Muungano.

Nianze na hili la pili. Yapo madai, ambayo binafsi hayaniingii akili, kwamba wapo baadhi ya watu fulani fulani wanaojiona wao ni maswahiba wa Rais Kikwete, na kwa hiyo hata wakifanya lolote chafu, ukiwamo ufisadi wa kuifilisi nchi hii, hawawezi kuguswa na Rais wala mkono wa dola. Watu hao, wanadaiwa ndio waliomwingiza Rais Kikwete Ikulu mwaka 2005, na kwa hiyo wanaweza wakafanya chochote wanachokitaka bila kushughulikiwa.

Nasema ni kweli katika mkakati wa kutaka kuingia Ikulu, Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa na watu wake wa karibu katika uratibu wa mikakati yao hiyo. Huyo alikuwa Jakaya Kikwete, ambaye mwaka 2005 alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Lakini, Kikwete huyu baada ya kupata ridhaa ya chama chake na Watanzania kwa ujumla wao kuongoza nchi hii, hawezi kuwa rafiki wala swahiba wa mtu yeyote anayerudisha nyuma jitihada zake za kuwatumikia Watanzania na nchi yake katika kuitoa hapa ilipo na kuipeleka kwenye neema ya ndoto zake alizokuwa nazo wakati anaweka nia ya kutaka kuwa Rais wa nchi hii.

Kikwete kama Jakaya Kikwete anao marafiki wa damu, anayo familia na anao ndugu zake, ambao anaweza akawaita wakanywa naye kahawa au chai mgahawani na nyumbani kwake. Lakini Rais Jakaya Kikwete, kama taasisi, ni rafiki na swahiba wa kila Mtanzania aliyezaliwa leo na kikongwe cha miaka zaidi ya 100 kilichopo kwa sababu hao ndio alioapa kuwalinda na kuwatumikia chini ya Katiba ya nchi yetu.

Labda tukumbushane kwa mifano michache baadhi ya waliojiita maswahiba wa marais katika nchi hii, ambao hata hivyo hatima yao ya kisiasa iliishia kubaya. Karibu Watanzania wote wanaujua urafiki au uswahiba waliowahi kuwanao Oscar Kambona na Mwalimu Nyerere wakati wa harakati za kutafuta uhuru wa nchi. Ni katika urafiki huo au uswahiba huo, Mwalimu alipomuoa Mama Maria Nyerere alimfanya Kambona kuwa ‘bestman’ wake! Lakini Kambona huyo huyo, akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani mwaka 1964 ndiye aliyeokoa uhai wa Mwalimu katika tukio la kuasi kwa jeshi lililokuwa limeachwa na Wakoloni wa Kiingereza.

Hata hivyo, mwaka 1967, baada ya Kambona kukataa kukubaliana na Mwalimu juu ya misingi ya Azimio la Arusha, iliyolenga kuwa na Taifa la kijamaa na linalojitegemea, Mwalimu alimtimua serikalini, na akakimbilia uhamishoni Uingereza. Kambona hakurudi nchini tangu mwaka huo hadi mwanzoni mwa 1990 baada ya kuruhusiwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Ipo mifano mingi ambayo wanasiasa wetu waliofanya kazi na Mwalimu wanaweza kuitoa juu ya yaliyowakuta wale wote waliojitia kimbelembele na kujifanya wao wako karibu na Rais.

Nafasi ya Waziri Mkuu wa Tanzania kukwea hadi kuufikia urais. Hili ni jambo langu la pili ninalotaka kulijadili katika makala haya katika ujinga wangu ule ule unaonitofautisha na wanasiasa weledi. Kama kuna msingi au mfumo imara ambao Baba wa Taifa aliuweka CCM katika uteuzi wa mgombea urais, basi, ni sifa ya mwanachama wa chama hicho anayestahili kuteuliwa kuwa mgombea urais, iwe kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Zanzibar.

Nitashangaa kama siku moja nitakuja kusikia kwamba ‘mtoto wa mkulima’, Mizengo Pinda, ana matamanio ya kuwa Rais baada ya Rais Kikwete. Ndugu zangu, si kila kitu katika masuala ya uongozi wa nchi lazima kiandikwe katika Katiba. Ndiyo maana naendelea kusikitika na kumhurumia kaka yangu, Edward Lowassa, kila ninaposikia baadhi ya wapambe wake wakisema bado ana nia na dhamira ya kumrithi Kikwete mwaka 2015!

Tuanzie kwa Rashid Mfaume Kawawa hadi kwa Frederick Sumaye: Ni nani katika hao amewahi kupitishwa na CCM ili awe mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho? Waziri Kiongozi gani wa Zanzibar amewahi kutoka nafasi hiyo na kuwa moja kwa moja Rais wa Zanzibar? Hawakuwahi kuteuliwa kugombea urais kwa sababu ya bahati mbaya, au mawaziri wakuu na waziri kiongozi waliojaribu kugombea hawakuwa na mtandao imara wala fedha za kutosha?

Katika mfumo wa utawala wa Taifa hili ambao Rais ana mamlaka ya ki-alfa na ki-omega, mwanasiasa yeyote yule anapobahatika kuupata uwaziri mkuu, anapaswa amshukuru Mungu na aridhike na ngazi hiyo aliyofikia. Kinyume cha hapo, ni kujimaliza mwenyewe kisiasa.

Orodha ya waliowahi kuwa mawaziri wakuu na wakajaribu kugombea urais tunaijua. Aidha, mawaziri kiongozi wa Zanzibar waliojaribu kugombea urais wakaishia njiani tunawajua. John Malecela na David Msuya walikuwa na sifa zote za kuwa marais mwaka 1995, lakini sote tunajua kilichowakuta. Tunaambiwa kwamba faili lenye jina la Malecela halikutakiwa hata kuingia jumba lile la White House, Dodoma. Sumaye naye alikuwa na sifa zote mwaka 2005, lakini tunajua kilichomkuta.

Nimalizie makala hii kwa kuwakumbusha weledi hao wanaodhani bila wao Tanzania haiwezi kuwa na Rais bora kwamba, Waziri Mkuu ni mteule wa Rais kama alivyo mkuu wa mkoa na wilaya. Kazi kubwa ya watu hao ni kumsaidia Rais kusimamia yale aliyowaahidi wananchi.

Hao (mawaziri wakuu) ni tofauti na mawaziri ambao kazi yao kubwa ni utendaji na kusimamia sera za nchi. Kwa hiyo, jaribio lolote la waziri mkuu, mkuu wa mkoa au wilaya kutaka kumfunika aliyemteua ili yeye aonekane bora mbele ya watu kuliko rais, kwa mtazamo wangu, kisiasa ni jambo hatari sana.
 
Unafiki wa mwandishi huyu nao anatakiwa alitoe gamba! Mbona haungami kwamba alipokuwa kwenye chombo cha habari cha hao mafisadi aliwadefame watu wangapi in favor of magamba!:banplease:
 
Kwa muda sasa wafuasi wa Edward Ngoyai Lowassa, ambaye imeshatamkwa wazi (japo siyo rasmi) kwamba atawania nafasi ya kugombea urais mwaka 2015, wamekuwa wakidai kwamba Lowassa anakubalika na wengi na kwamba kutokana na kukubalika kwake na uchapa kazi wake ana nafasi kubwa ya kuwa rais wa nchi hii. Maneno haya yamekuwa pia yakijadiliwa hata humu JF kwa baadhi ya wapambe wake kuanzisha thread zinazompamba.

Hata hivyo, wakati majigambo haya yakiendelea, tumekuwa tukisikia visa vya Lowassa na kundi lake kurubuni watu mbalimbali wakiwemo viongozi, wamiliki wavyombo vya habari na hata waandishi na wahariri kununliwa kwa kupewa fedha na ahadi kadha wa kadha ili harakati zake zifanikiwe. Amekuwa akiwatisha pia wale wote wanaoonekana hawako katika kundi lake au wale wanaoonekana kumpinga. Wengine wamepoteza kazi au hata kutishiwa na mashitaka bandia.

Swali linalokuja ni kwamba, kama Lowassa ni mtu anayekubalika na watanzania, kuna haja gani ya kuwarubuni na kuwanunua watu? Si awaache wampende kwa vile alivyo na kile anachokisimamia na siyo kununua mapenzi. Ni kwa nini awatishe wale wanaompinga (ambao ni wengi). Kwa nini kwa miaka karibu mitatu sasa hajawahi hata kushiriki shughuli za kisiasa zaidi ya zile za jimboni mwake? Anawezaje kupima kukubalika kwake wakati hakutani na watu?

Hivi ni kweli Lowassa ni kipenzi cha Watanzania?
 
Kwa muda sasa wafuasi wa Edward Ngoyai Lowassa, ambaye imeshatamkwa wazi (japo siyo rasmi) kwamba atawania nafasi ya kugombea urais mwaka 2015, wamekuwa wakidai kwamba Lowassa anakubalika na wengi na kwamba kutokana na kukubalika kwake na uchapa kazi wake ana nafasi kubwa ya kuwa rais wa nchi hii. Maneno haya yamekuwa pia yakijadiliwa hata humu JF kwa baadhi ya wapambe wake kuanzisha thread zinazompamba.

Hata hivyo, wakati majigambo haya yakiendelea, tumekuwa tukisikia visa vya Lowassa na kundi lake kurubuni watu mbalimbali wakiwemo viongozi, wamiliki wavyombo vya habari na hata waandishi na wahariri kununliwa kwa kupewa fedha na ahadi kadha wa kadha ili harakati zake zifanikiwe. Amekuwa akiwatisha pia wale wote wanaoonekana hawako katika kundi lake au wale wanaoonekana kumpinga. Wengine wamepoteza kazi au hata kutishiwa na mashitaka bandia.

Swali linalokuja ni kwamba, kama Lowassa ni mtu anayekubalika na watanzania, kuna haja gani ya kuwarubuni na kuwanunua watu? Si awaache wampende kwa vile alivyo na kile anachokisimamia na siyo kununua mapenzi. Ni kwa nini awatishe wale wanaompinga (ambao ni wengi). Kwa nini kwa miaka karibu mitatu sasa hajawahi hata kushiriki shughuli za kisiasa zaidi ya zile za jimboni mwake? Anawezaje kupima kukubalika kwake wakati hakutani na watu?

Hivi ni kweli Lowassa ni kipenzi cha Watanzania?

Huu ni udanganyifu wa hali ya juu. Inanikumbusha kauli ya Dr. Mwakyembe ambaye aliwapa changamoto Lowassa na wenzie kwamba kama wanataka wapime kukubalika kwao basi waende naye wakahutubie Kariakoo halafu tuone kama watu wengine watarudi na nguo za ndani. Panic inayoonekana kwa jamaa na wapambe wake inaonyesha kwamba hana uhakika na maisha yake.
 
Sasa mbona hiyo haiwezekani. Wenzie wameshamvua gamba labda atafute chama kingine na watanzania watakaopiga kura wabadilike maana hawa waliopo wanasubiri kwa hamu waonyeshe hasira zao.
 
Hata wamasai wenyewe wanamuona siyo mwenzao, sembuse sie akina mgosi. Jamaa will not see his name in the ballot oaoers in 2015.
 
Lowassa ni kama Godfather wa mafia anayetaka kutumia fedha zake na influence zilizotokana na fedha kununua urais wa Tanzania. Mahali pekee anapostahili kuwa godfather yeyote yule ni jela.
 
A wate of time. This country cannot afford a Lowassa presidency. He should relax and take care of his ill gotten wealth and let the people from whom he stole forget him. The more he makes noice the bitter and astounded the Tanzanians are with him. Nyerere's conviction against Lowassa will never be lifted!
 
Lowassa ni kama Godfather wa mafia anayetaka kutumia fedha zake na influence zilizotokana na fedha kununua urais wa Tanzania. Mahali pekee anapostahili kuwa godfather yeyote yule ni jela.

Mimi natabiri kwamba jela yake haiko mbali maana huku kuropoka ropoka kwa wapambe wake kutawaamsha Watanzania halafu watamtia kitanzini.
 
Huu ni udanganyifu wa hali ya juu. Inanikumbusha kauli ya Dr. Mwakyembe ambaye aliwapa changamoto Lowassa na wenzie kwamba kama wanataka wapime kukubalika kwao basi waende naye wakahutubie Kariakoo halafu tuone kama watu wengine watarudi na nguo za ndani. Panic inayoonekana kwa jamaa na wapambe wake inaonyesha kwamba hana uhakika na maisha yake.

Lowassa Mwenyewe (Personally) hajawahi Kutangaza Kama Anagombea Urais 2015!Ila wanaotangaza tangaza ndio ni Wapambe, Labda watanufaika na Urais wake.Lakini Kupata Urais si Kiulaini kwa Kutangaza au Kutangaziw!
Laukama MTZ kutaka kugombea Urais si Haramu!
Na nadharia ya Kusema Ngoyai Kahonga watu wote naona nimfu kwani Ana Hela Kiasi Gani kuhonga kila Mtu?
Watakao Amua nani awe Rais ni Watanzania watakao kuwepo,Jiandikisha na Kujitokeza kupiga kura mwaka Huo wa 2015!
Mie Mkweche wa Mkangufu, Mgaya sida wa Igangudungu Sijawahi kumwona Lowasa zaidi ya Kwenye Magazeti Ila nimewahi Kusikia Mtu Mmoja akisema kwa Kujiamini kabisa kwamba Yeye anaamini Lowasa alikuwa ni Waziri Mkuu Mchapa Kazi na Toka ameondoka 2008 anahisi kama serikali imeenda nae!Kwani watu wamebaki kulia lia tu na wanachokifanya hakionekani na Hata Halmashauri zimesinzia tofauti na wakati Lowasa akiwa Waziri mkuu, Viongozi Halimashauri walwajibika kwani walijua Lowasa akisikia Uzembe atatia timu na Atakemea na Ikibidi Kumwajibisa mtu papo hapo!
Mie nikasema kweli Kila Mpiga Siasa ana wanaompenda na Wasilazimishwe Kumchukia!
Jibu wapo Watanzania Wanaompenda na Kumkumbuka!Ila idadi ya wanaompenda au Kumchukia ni Yakufikirika!Na Kuhonga wote hawezi!
 
Lowasa hatofautiani sana na Viongozi wetu walio madarakani na hata wale wanaofikilia kuwa madarakani hapo baadae kupitia CCM. Tumpe nafasi atubu, atuponye majeraha aliyotusababishia. Lowasa anaonekana anakubali kukosolewa, nani asiyekuwa shahidi kwa hili. Alikubali kuachia U-waziri mkuu, hivi karibuni atakubali kuachia U-CCM. Ameonyesha mfano nzuri kwa wenzake, ingawaje wao hawataki kufuata nyao zake. Pia namwona Lowasa kama kiongozi mzuri nikimlinganisha na BOSS wake Kikwete, ana ndoto na anaweza kusimamia mipango yake, moja kati mipango yake ilikuwa kumweka KIkwete madarakani na kumtumia atakavyo, kwa kiasi kikubwa amelitimiza hilo, alisimamia Richmond na Dowans amefanikiwa pia. alisimamia ujenzi wa shule za sekondari kila kata, hili halina ubishi amefanikiwa japowatoto wake hawasomi huko. Kwa maoni yangu Lowasa ni kipenzi cha watanzania zaidi ya wenzake ndani ya CCM.
 
Lowassa ni kipenzi cha mke wake na familia yake, at least hilo tuna uhakika nalo.
Watanzania wengine tungefarijika kuelewa kiini cha utajiri wake na umahiri wake wa kutengeneza fwedha(akiwa serikalini) ulikotoka ili na sisi tumpende.
 
Hivi ni kweli Lowassa ni kipenzi cha Watanzania?

Simple research kujua jibu mtoe Lowasa nje ya moduli au arusha
eg

Mpeleke Lowasa na Pinda na Zitto kabwe kama wagombea ubunge pekee katika majimbo haya. tena bila k kmapeni.


  • Mwanza
  • tabora
  • Dodoma
  • Bukoba
  • Shinyanga
  • Ilala, Dar au Kinondoni
Katika hayo majimbo yeote hata nafasi ya Pili Lowasa hawezi kushika......

Hata ungemuongeza chenge kwenye list bado Lowasa atakuwa wa Mwisho.

Hiyo ndo hali ya Lowawa ni just Media ndo inamuweka barabarani.
 
lowasa kweli ni gamba lakin lakin wadau tukubali huyu jamaa ni mtendaji wa ukweli, hata alipokuwa PM kweli watendaji waliokuwa chin yake walikuwa wanawajibika vya kutosha, lakin kwa sasa utadhan hatuna mtu ambaye alichukua nafas yake. kwa upande wa pili ni kweli ana madhaifu na kashfa za ufisad, ajipime mwenyewe aone kama anadeserve kuwa president wa bongo kupitia chama kingine akijiona anafaa agombee tu
 
Back
Top Bottom