Ujumbe wa wazi kwa Mhe. Edward Lowassa: Uchaguzi ni wako

Kuna Rais mwingine zaidi ya Dr.waukweli?
Naamini hata Kikwete anajuta kimoyomoyo kwa nini aliukurupukia Urais

Wacheni kutuletea mavuvuzela hapa Tanzania sio inji ya majaribio .
Tanzania ni inji iliyojaliwa karibu kila kitu na aina ya kiongozi inayo muhitaji si jamii ya mabwanyenye waliopo sasa wasiojua hata vipaumbele vya msingi kwenye inji iliyo na utajiri wa aina tulio nao.

Serikari iliyojijngea utaratibu wa kuendesha mambo yake kimizengwe mizengwe utadhani imejiweka yenyewe madarakani unatarajia kuona wanainji wake watatoka kwenye shimo lililo wachimbia?watatolewa na nani?

Natamani 2015 iwe kesho CCM ione ilipo jifikisha na hivyo vi miamia mnavyokula ili kusafishana vitwagharimu.
Kwa hali ilivyo kwenye huu mpango wao wa kuvuana magamba siku moja natarajia kuona Kikwete na swahiba wake wanachapana mkono hadharani
 
CCM mtajiju wenyewe hata mkimtaka Tambwe kazi kwenu ila sisi tunajua raisi wa Tanzania ajaye ni Dr.Slaa
 
Kwakweli, kama kuna mwana ccm halisi basi ni Lowasa, ni mvumilivu, hajhusika katika kuanzisha ccj. alileta kampuni ya kufua umeme, amesubiri tu kwa muda mrefu Uraisi bila vurugu, il hal ndani ya CCM hakuna mwenye sifa za kukibeba chama kama yeye. Uchafu wote wa CCM mmemtwisha yeye.

2015 anachukua ugombea ndani ya CCM kiulaini tu. Komaa Lowasa usikubali, maana wamekuzoea sana.

Hebu angalieni alivyo na haiba ya Uongozi katika hii Picha



mc07011464.jpg
 
Katika hotuba yake kwa Bunge hakuwasiliana na Rais juu ya yeye kujiuzulu. Na believe me, JK hakumtaka ajiuzulu; JK kama wabunge wengine hawakujua Lowassa atajiuzulu vile vinginevyo Spika Sitta angejua juu ya hilo vile vile. Ninachojua ni kuwa JK alikataa kuiona ripoti ya Mwakyembe kabla.

JK alikuwa Dodoma kwa ajili ya mkutano wa baraza la Mawaziri (soma maelezo yake mweenyewe kwa wazee wa Dar wiki chache baadaye; suala la Waziri Mkuu kujiuzulu halikuwepo). EL alifanya vile wakijua watu kama wanne tu. Yeye, mkewe na wabunge angalau wawili (Hawa nina uhakika walijua).


ziko tatu; ya Mwang'onda (loyal to Mkapa, EL na RA), ya RO (loyal to JK), na Patriots (loyal to the standard of professionalism ya kazi ya intelligence). Njia pekee ni kuhakikisha TISS inaundwa upya baada ya mabadiliko ya sheria.

c) Uchambuzi wa Mwanakijiji, unaonyesha kuwa Lowassa anamhitaji sana JK kuliko kinyume chake. Ukweli uliopo, unaosema, unaoonekana ni kuwa JK anamhitaji sana Lowassa na watu ili awe salama katika nafasi na kazi zake.

Naamini JK hamuitaji Lowassa at all, hakuna lolote ambalo EL anaweza kufanya dhidi ya JK. Hakuna. Lakini JK akiamua kumfanyizia anaweza to extreme measures. Hili ndilo the message behind mada yangu. EL na RA bado hawaliamini hili. It'll be too late when they grasp its eventual implications.



Nadhani hapa uko sahihi sana; tulishadokeza huko nyuma juu ya suala la afya yake. Watu wengi wamekuwa wakizungumzia gonjwa lile lakini kwa karibu mwaka mzima baadhi yetu tunajua juu ya hali yake ya kiafya. Siyo blood clot. It is something more serious. I won't get into that.[/QUOTE]


"the trouble with the world is that people know so many things which are ain't so"

kipofu hawezi kumtangulia kipofu mwenzake.....................................
 
UJUMBE WA WAZI KWA MHE. EDWARD LOWASSA: “Uchaguzi ni wako”
Na. M. M. Mwanakijiji


mc07011464.jpg


Endapo aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Edward Lowassa (CCM-Monduli) ataendelea na mwelekeo wake wa sasa wa kisiasa na mahusiano yake ya sasa ya kimkakati basi njozi zake za kuja kushiriki tena katika uongozi wa juu wa taifa letu zitakuwa zimefikia ukingoni bila kupiga kelele ya breki. Na endapo nitakachoandika hapa hatakipa uzito wake unaostahili naomba niwe wa kwanza kutanguliza habari mbaya kwake na wale wanaomuunga mkono kuwa atashindwa. He will lose.

Ninaandika kwa sababu kubwa tatu; kwanza ni kwa sababu ninaamini anapoteza muda kwa kuendelea na machungu ya matukio ya mwaka jana; pili, anapoteza kipaji chake cha uongozi kwa kukaa pembeni ya mijadala ya kitaifa na hivyo kuonekana yuko upande kinyume na maslahi ya taifa na tatu, ni kwa sababu naamini hakuna mtu mwingine anayeweza kumuambia kile nitakachomuambia hapa kwa heshima na taadhima kubwa. Wengine aidha wanamuonea soni, wanamuogopa au kwa namna fulani wanagwaya mbele yake.


Inaendelea katika attachment...

Nimeonelea nijitafsiri mwenyewe maana watu wengine wanatafsiri zaidi ya kile nilichosema.

a. Lowassa anawajibika kwa kujiuzulu kwake Uwaziri Mkuu. Hana wa kumlaumu.

b. Amechagua upande usio sahihi baada ya kuachia ngazi.

c. Hawezi kurudi kwenye uongozi wa kitaifa na hivyo ni bora aendelee kukaa upande huo mwingine. It is too costly.

Huyo ndye anayependwa na CCM wengi, hamna jinsi. Huyu ndie mgombea 2015
 
Back
Top Bottom