Ujumbe wa Freeman Mbowe wabadili wengi Houston

Nilisha sema na leo narudia tena! Hakuna mwenyekiti wa chama chochote cha siasa kwa sasa anae tema madini mdomoni akiongea kama kamanda Mbowe! Jamaa anaongea issues zinazogusa watanzania. Asie amini atafute audio ya speech yake pale Serena Hotel au hata akiwa anahojiwa.

Kamanda amekomaa ajabu ya maulana!
Mkuu huyu jamaa nilimsikia nikiwa na miaka chini ya 16 na hadi leo sijasahau.Yani nikikumbuka ni kama namsikia na kumwona.Na wakati huo sasa wala hakuwa maarufu kiasi hiki.Na la msingi lilikuwa hilo la ujengaji wa hoja.Ukimsikiliza,ana convincing power ya ajabu.
 
Mwenyekiti wa Taifa Chadema Bwana Freeman Mbowe akiwa ameongozana na Mbunge wa mbeya mjini bwana Joseph Mbilinyi (Sugu) wametembelea jiji la Houston Texas USA kuanzia tarehe 24 hadi 26 August. Ujio huu ni mwaliko wa Tawi la Chadema Houston TX .

Tawi la Chadema Houston linaonekana kuwa tishio kwa uhai wa CCM sio Houston pekee bali USA. Wanachadema wa Houston ambao ni wengi wanaojiamini, wenye malengo na nia ya dhati kuikomboa Tanzania kisiasa, kiuchumi na kijamii wamekuwa mstari wa mbele kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kiuchumi nchini Tanzania kwa kushiriki moja kwa moja.

Ujio huu wa Mbowe ambao uliingiza wanachama wapya zaidi ya 100 kwenye idadi ya wanachadema wa Houston, ulifana sana. Mkutano huu uliofanyika kwenye hotel ya Marriot Westchase Houston TX ulifanyika kwa utulivu na furaha kubwa sana.

Mkutano huu ulihudhuriwa na watanzania wengi na kuvunja rekodi ya mkutano wowote wa kisiasa ambao umewahi kufanyika Houston TX kwa historia ya uwepo wa Watanzania jijini hapa.

Mwenyekiti Mbowe akiwa anajiamni aliweza kuwafanya Watanzania kutokwa na machozi kwa jinsi alivyokuwa akielezea ugumu wa maisha, ubovu wa elimu, afya, barabara nk waliyonayo/walivyonavyo watanzania kila siku. Mwenyekiti aliwaasa watanzania kuacha kulalamika badala yake kuwa chanzo cha ufumbuzi kwa kushirikiana na Chadema.

Mwenyekiti aliwaambia Watanzania hawa kuwa Chadema inawahitaji Diaspora kwa uwingi wao ili kupeleka nchini ujuzi wao, elimu, utamaduni wa kuwajibika, kuaminiwa, na kila chema walichojifunza kutoka nje. Bwana Mbowe aliwahakikishia watanzania kuwa chadema kinaingia ikulu mwaka 2015 kwani kinafanya na kimefanya maandalizi ya kutosha.

Wakiwa na hamu ya kushiriki moja kwa moja kusaidia mabadiliko haya ya kisiasa na kiuchumi Tawi la Chadema Houston liliahidi kutoa pikipiki mia ishirini na sita (126), gari la kampeni na vifaa mbali mbali vya computer utaalamu na wataalamu wake kutumika katika njanja mbali mbali ili kusaidia chama na watanzania kwa ujumla.

Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi kwa upande wake alisema, Chadema inawataka na kuwahitaji sana, inawathamini sana diaspora na wakazi wa Houston kama watanzania wote ndio maana imewafuata. Alisema, Chadema hakitaki kumwacha mtu yeyote nyuma kwenye kujenga nchi hususani pale itakapochukua dola 2015.

Akiongea kwa kujiamini Sugu alisema anajua kazi kubwa iliyofanywa na watanzania na sasa walioko nje nao wanaletewa neno la ukombozi kwa ajili ya nchi yetu.

Naye Mwenyekiti wa Tawi Bwana Fue Fue akiongea na wananchi aliwaasa kuwa wasiwe waoga kwani makamanda wa Chadema wamepitia mengi ila bado wanasonga mbele. Aliwaambia watanzania wenzake kuwa hakuna wa kuisaidia Tanzania isipokuwa Watanzania wenyewe. Alisisitiza ujasiri, kujiamini na kufanya kwa vitendo. Akiongea kwa msisitizo alisema uongozi ulioshindwa hauwezi tena kuaminiwa, kwa miaka 50 sasa serikali ya CCM imeshindwa na imeishiwa ubunifu hivyo kuwa na ugumu wa kuweza hata kutambua matatizo halisi ya Mtanzania. Lazima kubadili uongozi mzima ili kuweza kusonga mbele kiuchumi, ni kazi yetu kufanya hivyo na wajibu wetu kuindoa CCM madarakani, alisema bwana Fue Fue

Mbowe aliwaaga watanzania kwa kuwaambia Chama kina wahitaji na kinathamini sana mchango wao.

Watanzania wengi walimsifia Mbowe kwa uwezo wake wa kuongea kujenga hoja na kujibu maswali ya Watanzania na kumaliza kiu yao. Mkutano huo ulichukua takribani masaa manne.

Majibu ya watanzania ni kuwa wengi wamehamasika na kukubali kushiriki moja kwa moja kwenye kuikomboa nchi.
Shukuran Mwenyekiti, hizi ndio taarifa tunazopenda kuzisikia..Siku zote nimesema Mbowe ni mwanasiasa, na mwenye Uzalendo wa pekee. Hongera sana mheshimiwa.
 
Utaelewa tu mkuu! Ni kutwanga kotekote Tanzania na Ulaya! Huoni kuwa hizo pikipiki 126 zitasadia sana kwenye M4C? Stay tuned!
Okay, ni kutwanga kote kote, sasa hizo pikipiki 126 zisingeweza patikana bila kwenda kufungua tawi nje??
Gharama ya safari na uendeshaji wa mikutano haununui hizo pikipiki??
Achia mbali gharama ya muda na nguvu zilizotumika??

Taratibu. Siku moja utaelewa tu.

Hapa nataka kuelewa, ndio maana nimeuliza

Tanzania sio kisiwa ina watanzania wengi wanaoishi ndani ya nchi na wengine wachache wametapakaa duniani. Watanzania waliopo nje wanafaida kubwa sana kwa taifa letu, hawa Watanzania wenzetu huko walipo ama wanasoma, wanafanyakazi, au biashara vile vile wanafamilia zao.

Manufaa yao kwetu sisi, kila mtanzania anafamilia yake Tanzania, mara nyingi huwatumia fedha ndugu zao za kigeni kama sikosei kwa miaka miwili iliyopita Watanzania hawa walituma zaidi ya dola za kamarekani milioni mia sita zikaingia kwenye mzunguko wetu kama foreign income, kupitia ndugu, jamaa, au biashara zao.

Watanzania hawa wengi wanafanyakazi kwenye viwanda na makampuni yaliyoendelea hivyo kuchota utaalamu na vitendo. Watanzania wanapata elimu na kujifunza mambo mbali mbali amabyao ni muhimu kwa kukua kwa Taifa lolote duniani.

Mapinduzi ya kiuchumi ya nchi kama Singapore, Italy, Israel, Ghana nk ni Diaspora zao.

Tukiwatumia Diaspora wetu vizuri tutasonga mbele. tutoe mawazo mgando ya CCM kuwaogopa kwani wanaogopa changamoto zao.

Kuonekana tunawatumia vizuri diaspora hawa ni lazima tuwafuate huko walipo tuwafungulie matawi ya vyama vyetu vya siasa???

Kuna hajka gani ya kuwa na tawi thabiti Houston afu Tandahimba huna hata mwakilishi??

Na matawi ya vyama yasipofunguliwa nje, kunaathiri vipi pesa za kigeni zinazotumwa nchini na diaspora hawa?? Hizo 2bilioni ulizoongelea?

Matawi nje ya nchi maana yake ni kwamba chadema kwa kuwa ni chama makini kinahakikisha kinawawekea uzalendo watanzanzania walioko nje ya nchi,wale waliokata tamaa baada ya kuona uozo wa uongozi legelege wa chama cha magamba,kuwapa tumaini jipya ili waisaidie nchi yao kwa kutumia taaluma zao waliozopata wakiwa nje ziwasaidie na ndugu zao watanzania, watumie pesa zao kwa kusaidia mabadiliko makubwa yanayoenda kutokea. Ukumbuke kuwa chadema sio omba omba kama chama cha magamba ambao wanaenda kuwakenulia meno watu weupe ili wawasaidie jinsi ya kupora pesa za walipa kodi na kwenda kuziweka uswisi. Hii ndio maana halisi ya kuanzisha matawi nje ya nchi. ili kuhakikisha kuwa roho ya vuguvugu la mabadilikoni inaambukizwa dunia nzima na wa tz wenzetu watusaidie kuitangazia dunia kuwa tz na wa tz wamechoshwa na magamba. umeelewa kaka au niendeleee kutoa darasa la bure hadi unielewe.

Red: Kipi bora, kuwekeza kwa mwanajeshi aliyevitani na mwenye ari, au kwenda kutafuta aliyekimbia uwanja wa mapambano na kukata tamaa??

Blue: Labda kweli, labda si kweli. Je hiyo roho ya vuguvugu, imewekezwa kiasi cha kutosha hapa nchini hadi kuamua kwenda nje?? na je tunahitaji kutangazia dunia ili tufanye mabadiliko ndani ya nchi yetu?? Na je unadhani mabadiliko yetu yatafanikiwa kwa kushirikisha dunia badala ya watanzania wenyewe kwa wenyewe kuamua kutafuta mabadiliko haya??

Green: Naweza kuwa nahitaji darasa zaidi aisee
 
Okay, ni kutwanga kote kote, sasa hizo pikipiki 126 zisingeweza patikana bila kwenda kufungua tawi nje??
Gharama ya safari na uendeshaji wa mikutano haununui hizo pikipiki??
Achia mbali gharama ya muda na nguvu zilizotumika??



Hapa nataka kuelewa, ndio maana nimeuliza



Kuonekana tunawatumia vizuri diaspora hawa ni lazima tuwafuate huko walipo tuwafungulie matawi ya vyama vyetu vya siasa???

Kuna hajka gani ya kuwa na tawi thabiti Houston afu Tandahimba huna hata mwakilishi??

Na matawi ya vyama yasipofunguliwa nje, kunaathiri vipi pesa za kigeni zinazotumwa nchini na diaspora hawa?? Hizo 2bilioni ulizoongelea?



Red: Kipi bora, kuwekeza kwa mwanajeshi aliyevitani na mwenye ari, au kwenda kutafuta aliyekimbia uwanja wa mapambano na kukata tamaa??

Blue: Labda kweli, labda si kweli. Je hiyo roho ya vuguvugu, imewekezwa kiasi cha kutosha hapa nchini hadi kuamua kwenda nje?? na je tunahitaji kutangazia dunia ili tufanye mabadiliko ndani ya nchi yetu?? Na je unadhani mabadiliko yetu yatafanikiwa kwa kushirikisha dunia badala ya watanzania wenyewe kwa wenyewe kuamua kutafuta mabadiliko haya??

Green: Naweza kuwa nahitaji darasa zaidi aisee
Mkuu. Kamanda hakufunga safari kwenda kufungua tawi ughaibuni. alialikwa na chama cha upinzani cha huko kwenye kumsimika mgombea wao wa u-rais. Hivyo aliitumia nafasi ndogo aliyopata kukutana na makamanda wa H-Town. Na gharama zote zilizo nje ya mwaliko wake zililipwa na makamanda wa H-town.
 
Mkuu. Kamanda hakufunga safari kwenda kufungua tawi ughaibuni. alialikwa na chama cha upinzani cha huko kwenye kumsimika mgombea wao wa u-rais. Hivyo aliitumia nafasi ndogo aliyopata kukutana na makamanda wa H-Town.
Waeleze Mkuu!!!! wao wanafikiri ni ule upromota anaofanya Mwenyekiti wao wa kumpeleka Diamond kuburudisha watoto wao huko USA kwa kisingizio cha kufungua matawi
 
vikao vya wana ccm kwa sasa ni kuilaumu chadema tuu!huu moto wa M4C hawakuutegemea!MBOWE kafanya mabadiliko makubwa

HATA mtu niliyemheshimu kama Mr6 anamtukana na kumkejeli!! Ama kweli Mr6 ni "la kuvunda halina ubani"
 
Halafu anapoongea huwa hatoki povu kama magamba

Ukimwona mtu anaongea mpaka povu linamtoka ujue kwamba maneno anayosema percent kubwa ni uongo. Mtu mwenye kujiamini , mwenye busara, mwenye anazungumza kitu anachoelewa, mwenye kueleza mpaka msikilizaji aelewe , ni mtu asemaye UKWELI . Ni mwalimu ni kiongozi . Mbowe ni kiongozi . Tumwombee na tuwaombee CHADEMA ndilo tegemeo tulilobaki nalo kama nchi tunataka iendelee kuishi kwa Amani na Utengamano. Hatuna tena tumaini na CCM inavyoendesha nchi kwa uongozi wao nchi inaelekea kwenye maangamizi. Mwenye sikio na asikie
 
Mkwawa umenifanya nitamani kufika Houston nikija huko Marekani. Safi sana makamanda. Sisi huku hata fungu la dagaa shida. Watu wanawaonea wivu mbwa na paka wa matajiri wanapowaona kliniki.

Tunasema yana mwisho.
 
Kweli kabisa Mbowe ni jembe yani ana busara lukuki we acha!

Naunga mkono hoja yako!

Nilisha sema na leo narudia tena! Hakuna mwenyekiti wa chama chochote cha siasa kwa sasa anae tema madini mdomoni akiongea kama kamanda Mbowe! Jamaa anaongea issues zinazogusa watanzania. Asie amini atafute audio ya speech yake pale Serena Hotel au hata akiwa anahojiwa.

Kamanda amekomaa ajabu ya maulana!
 
Gharama ya safari na uendeshaji wa mikutano haununui hizo pikipiki??
Ndiyo! Haziwezi kununua. Lakini Kongosho, bado hujaweza kuona thamani ya diaspora mmoja kuwa na moyo uliorejezwa hata kushiriki ktk mapambano ya ukombozi wa watu wake. Nafikiri yapasa kujua kichwa kimoja(one brain) is worth millions times one motorbike.

Red: Kipi bora, kuwekeza kwa mwanajeshi aliyevitani na mwenye ari, au kwenda kutafuta aliyekimbia uwanja wa mapambano na kukatamaa??
Siku zote Kamanda Hodari huwa anafikiri uwingi na uwezo wa jeshi lake akijumlisha wale waliopo ktk vikosi viliuyo kazini kwa wakati huo, na wale wa akiba (reserve soldiers). Ndivyo vinavyompa jeuri ya kutangaza vita.
Kwa hili walifanya CHADEMA, huon kuwa ni jambo zuri la kuzidi kujiongezea hao makamanda wa akiba ambao katiki siku usiyodhani watawatumia?
 
Last edited by a moderator:
Ukisikia Hotuba za Mbowe unaweza kutamani kulia.Jamaa yuko very emossional.Ifact AMEIVA
 
Back
Top Bottom