Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa lengo la maandamano si machafuko bali ni kupeleka ujumbe kwa watawala.
Akizungumza Katika mkutano wa hadhara uliofanyika baada ya maandamano jijini Arusha, Mbowe aligusia kuwa mpaka sasa hakuna madhara yoyote yaliyojitokeza tangu walipoanza maandamano, huku akisema kuwa ni kielelezo tosha kwamba maandamano hayo lengo lake ni kupeleka ujumbe kwa wahusika waliopo madarakani.