Ujenzi wa Miradi hii Bagamoyo ni wa Lazima Kiasi Hiki?

Basil Mramba alijenga rami kwao

Wasira alipeleka maji kwao

Hao wakaadhibiwa kwa kubadilishwa wizara.

Mkulu yeye anapeleka bandari kwao. The leader is always right( IL DUCE HA SEMPRE RAGIONE)

Bado kesho utasikia Bagamoyo international airport na bagamoyo University ni lazima ijengwe kabla hajaondoka madarakani
 
Nimekukubari bro umewezakunielewesha sababu ya kujenga port bagamoyo, watu wengine wanaingiza siasa ndani yake.Nimetembelea port nyingi duniani haziko town Kama dar port jinsi ya kuipanua ni utata sehemu ni ndogo, nimuhimu kuwa na port nyingine hapo karibu na dar. Kuna wakati niliketa mzigo ikapitia Mombasa nilijilaumu Sana gharama opioids kubwa Sana.Kama London ina port mbili Tilbury na Sherness na zote ziko busy.
 
Ndugu yangu usiligeuza suala hili muhimu la kiuchumi kuwa la kisiasa. Umuhimu wa bandari kwa uchumi wa Tanzania hauna ubishi. Yapo mambo ya msingi muhimu kufahamika:
Bandari ya Dar imeelemewa kwasababu ya wingi wa mizigo inayopitia katika bandari hiyo ndio maana kuna foleni za meli kuingia hapo Bandarini. Kuelemewa huko, kunasabasha jiji kuzidiwa na wingi wa magari ya mizigo na abiria (traffic congestion) yanayoingia na kutoka Bandarini. Zipo jitihada za kufanya upanuzi wa bandari hiyo kwa kujenga gati mpya no 13 na 14. Upanuzi huo ni suluhu ya muda mfupi katika handling ya mizigo, lakini hakutoa suluhu ya tatizo la congestion jijini....sana sana utaongeza congestion. Ni kwa msingi huo ujenzi wa bandari mpya ni jambo la muhimu.

Kwanini Bagamoyo?
Eneo la ujenzi wa bandari la Bagamoyo, lina kina kirefu na mlango mpana wa kuingizia meli zitakazohitaji kutia nanga. Hizo ni sifa kubwa zinazopelekea interest ya Wawekezaji wa sekta ya bandari kupendelea kuwekeza kule. Miaka 20 ijayo, meli zitakazojengwa zitakuwa ni 4th Generation zenye size kubwa kwa ajili ya kubeba mizigo mingi. Meli hizo hazitoweza kuingia kwenye lango la bandari ya Dar es salaam unless lifanyike zoezi la kupanua mlango wa bandari na kuchimba zaidi kuongeza kina....jambo ambalo itabidi kuchimba eneo kubwa mpaka ilipo Ikulu. Bandari ya Tanga na ile ya Mtwara vilevile zina disadvantage ya kutokuwa na Kina kikubwa kinachotakiwa kwa ajili ya hizo 4th generation ships. Sisemi kwamba haziwezi kutengenezwa zika accomodate meli za aina hiyo, la hasha. Inawezekana, lakini kwa gharama kubwa. Hivyo mtu anayetaka kuwekeza kwenye bandari ni rahisi zaidi kuwekeza Bagamoyo kule eneo lingine.

Lakini pia,duniani kote, bandari huwa zinafanya vizuri panapokuwa na eneo la Export Processing Zone na miundombinu mingine. Kule Bagamoyo next to eneo la BandAri, kuna eneo kubwa la mamlaka ya EPZA kwa ajili ya viwanda vya uzalishaji kwa ajili ya mauzo ya nje. Hivyo, muwekezaji yoyote mwenye kutaka kuwekeza kwenye bandari, atavutiwa kuwekeza kwenye bandari iliyo karibu na EPZ.

Tatu biashara ya bandari inahitaji kuwa karibu na eneo la biashAra (Business/commerical district) kwa ajili ya kuwezesha transactions mbalimbali. Kwa TZ commercial district ipo Dar es salaam. Hivyo muwekezaji wa bandari ata prefer kwenda bagamoyo iliyopo karibu na Dar kuliko mahala pengine. Lakini pia, Bagamoyo ina potential ya kutengeneza new business district.

Mtwara
Bandari ya Mtwara ipo sorted. Wale investors wa kuchimba gesi wameshaelezea nia yao ya kuitumia bandari ile kama sehemu ya usafirishaji wa gesi. Pia tayari eneo la uzalishaji wa viwanda karibu na bandari limechukuliwa na makampuni yatakayowekeza kwenye viwanda vya kuzalisha mbolea kwa kutumia gesi, na makampuni mengine ya uzalishaji wa cement kama lile la Dangote......hivyo, investor mpya anayekuja sasa, hawezi kuwa na interest na Mtwara kwani tayari kuna strategic investors wa bandari ile.

TANGA
Tanga itaendelezwa soon kwa hesabu za kuitumia ku serve eneo la kaskazini, na pia ni altenative ya Mombassa na pia inahitajika na waganda. Mipango yake ipo. Soon utaona nayo inashughulikiwa.

Mkuu kama ni kina utakuwa unachekesha, Bagamoyo haina tofauti sana na Dar na kama ni gate kubwa basi ilipo oysterbay, ukanda wa Mbezi hadi Kunduchi ni kupo wazi sana.Pia sababu ya dar kusemwa hivyo hiana msingi kwani Haiwezekani hata kwa miaka 50 ijayo, pakawa na Meli inayozidi ule ukubwa.Masuala ya kina si kweli kwani hata iwe vipi kwa bahari zinazoangalia EAST mawimbi yanaleta mchanga mfululizo na mara nyingi kutahitajika uondoa.


Saabua kubwa zipo nje ya maswalahi yetu ila kwa sifa za JK kadhani ataibadili Bagamoyo iwe dubai.Bagamaoyo ni front ya kufanya unyonyajia wa nchi, itakuw anjia ya kupitisha uranium, madini mengine na uwekezaji mkubwa wenye siri nyingi.

Sisemi kuwa haiwezekani kufungua njia ya mafanikio ila ni wazi kuwa hiyo project ni challenging sana kwa serikali corrupt na dhaifu kama ya CCM.Watafungua bagamoyo kwa mikataba ambayo si TRA,Si PCB,wala Sumatra watakaoweza thubutu ingia bila adabu.

Sioni processing itakayofanyikia bagamoyo yenye maana kam hakuna miundombinu ya train na barabara, JK angeleta plan ya kuwa na barabara zenye lane si chini ya 8, ziktokea pale na kwenda kusini kupitia dar, kuptia challinze ktk ya mapori , kupitia lugoba hadi dodoma, kupitia wami kwenda Arusha, kupitia Pangani kwenda tanga.Rel nayo iwe ya kati, kusini kaskazini itakayokwenda gawanyika mahali fulani kwenda tanga,ili kukwepa bahari na uwezekanao wa kukwama pakiwa na tsunami miak aijayo na pia Tanga ianweza fikiwa kwa bahari pia,mombasa na nyingine kwenda Arusha hadi Mwanza kupitia singida. Ila wakiweka hivi vinjia na vidaraja ambavyo hakuna hta nafasi ya mpita kwa baiskeli nina mashaka na evacuation siku za kawaida tu achilia mbali pakitokea uvamizi au tsunami.
 
Tanga ni karibu sana na Bagamoyo hivyo hizo sabaubu za Bagamoyo si za msingi. Tanga tayari kuna miundo mbinu kuna barabara na maeneo ambayo tayari yana mpangilio. Tanga ni mji ambao una mpangilio kuliko miji yote Tanzania!. Hivyo hata kama wakichimba bado gharama za kuendeleza Tanga zitakuwa ndogo kuliko kuanzisha mji mpya wa Bandari bagamoyo. Vilevile kuna viwanda Tanga na Hotel kwani Bagamoyo patajaa kama Dar hakuna mpangilio mzuri.

Naona umeamua kupick sababu moja tu ya distance....ukaacha sababu nyingine za msingi nilizoziongelea. Hapa ni suala la numbers.......mwekezaji yoyote mpaka aamue kuwekeza mahala lazima aangalie factors zote kwa marefu na mapana yake. Feasibility study na business plan aliyofanya inamuonyesha Bagamoyo ndiko akiwekeza pesa yake itarudi, having considered all the factors....hakuna siasa hapa, ni uchumi tu na hesabu za muda wa kati na muda mrefu. Bagamoyo haijajengwa bado....hivyo kusema patajaaa kama Dar ni assumptions tu.
 
Hiyo bandari mpya imo kwenye mpango wa maendeleo 2011-2016? Labda kuna sababu muhimu za kujenga bandari nyingine mpya 50 km away toka bandari ya Dar. Lakini nilidhani, kwa changamoto tulizonazo -hasa kwenye sekta ya usafiri na usafirishaji, tungeimarisha bandari ya Dar, then change itakayobakia itumike kuboresha usafiri wa Train.

Tuna hela kidogo, tuwe na priority areas otherwise tutajikuta na miradi mingi ambayo haitakuwa na 'impact' kwa wananchi walio wengi. Hakuna kitu ambacho kina-miss nchi hii kama usafiri wa train and unless hili liangaliwe kwa jicho la karibu tutakuwa na uchumi wa makaratasi. Uchumi wa makaratasi ndio unachangia sana 'social unrest' maana watu wengi wanaachwa wakati wakubwa wanatupa GDP za ajabu ajabu.

It will be interesting kujua wachina wanaojitokeza kwenye hii Bandari mpya ya Bagamoyo wanafanya hivyo kwa makubaliano gani? Tunawapa/tunawalipa nini? China kwa sasa wana kiu ya 'raw-materials' na Africa ndio wamefika. Tayari wameshachukua mgodi wa makaa ya mawe in exchange watujengee bomba la gesi, sasa Bandari wanataka kulipwa vipi?

Bandari hiyo itajengwa kwa PPP.....hivyo hofu yako ya prioritisation ya utekelezaji wa mambo kutokana na ufinyu wa rasilimali iko taken careof. Investor ata finance mradi 100 percent kwa utaratibu wa BOT
 
Bandari hiyo itajengwa kwa PPP.....hivyo hofu yako ya prioritisation ya utekelezaji wa mambo kutokana na ufinyu wa rasilimali iko taken careof. Investor ata finance mradi 100 percent kwa utaratibu wa BOT

100% halafu kodi mje anza mdia lini?nanani ataangalia kuwa kesharudisha hela yake na riba zihusianazo na hiyo investment?Vipi mrabaha na mambo mengine?Vipi baada ya miaka aje wauzia bei kichaa,ili mbadili infrastructure iliyochakaa ,halafu arudi itumia yeye kwa mikataba ya muda mrefu.

Sijui kwa vijana weye vichwa vitupu waliojiufnza life kwa hadith za baba zao wataona kuw ahii ni bonge ya project kwa vile watakuwa na vishughuli fulani vinavyowafanya wafaidi leftovers tk ujenzi na baadaye,basi wanadhani hiyo project ni viable.project kama hizi ni loopholes ya kuzipora nchi masikini hela nyingi sana.Ipo wapi sheraton sasa kauziwa Akgaha kahani hea ya kunywa bia, na huo utakuwa mwendo wa nchi nyingi.Soon mtasikia wajenzi wa bagamoyo wanashika top ten duniani kwa utajiri.halfu ndipo mlolongo kama wa issue ya rad utakavyoibuka.
 
Badala ya kwenda imeza mombasa mnaenda shindannisha dar na bagamoyo?Tanga ingeweza pitisha bidhaa za Uganda na South Sudan,Rwanda na Burundi,tena Museven na kagame wangeshwishika kuwekeza ktk reli itakayopitia Arusha ,Singida hadi mwanza bila kuharibu mbuga zetu.

Kenya wanaejnga Airport mpakani kabisa, warushe wageni karibu kabisa na wageni wafurahie kuuona mlima Kilimnajaro toka angani, wachukue wageni wa KIA, wainuke na maua, na matunda yetu, n.k

Mtwara Ivutwe hadi lake Nyasa tukawashike malawi na mikoa yetu kusini, Dar isaidie dar mikoa ya kati hadi zambia hadi sumbawanga ili tukafaidi upade wa pili wa DRC.
CCM as usual ina another suicidal move.
 
Kwa upuuzi huu wasubiri hukumu kutoka kanda ya ziwa .kanda hii imetelekezwa ingawa ndio inaongoza ktk mchango wa kiuchumi ktk Taifa hili.mwaka 2005 rais kikwete ktk moja ya hotuba zake aliahidi kujenga kiwanda kimoja cha cement kwa kanda ya ziwa ktk mji wa shinyanga,sasa ni miaka 7 imepita hakuna kinachoendelea.wameua reli yetu,wanaimarisha pwani na kutelekeza kanda nyingine.kama nyerere angekua hivyo kama wao basi kanda ya ziwa ingekuwa mbali sana
 
100% halafu kodi mje anza mdia lini?nanani ataangalia kuwa kesharudisha hela yake na riba zihusianazo na hiyo investment?Vipi mrabaha na mambo mengine?Vipi baada ya miaka aje wauzia bei kichaa,ili mbadili infrastructure iliyochakaa ,halafu arudi itumia yeye kwa mikataba ya muda mrefu.

Sijui kwa vijana weye vichwa vitupu waliojiufnza life kwa hadith za baba zao wataona kuw ahii ni bonge ya project kwa vile watakuwa na vishughuli fulani vinavyowafanya wafaidi leftovers tk ujenzi na baadaye,basi wanadhani hiyo project ni viable.project kama hizi ni loopholes ya kuzipora nchi masikini hela nyingi sana.Ipo wapi sheraton sasa kauziwa Akgaha kahani hea ya kunywa bia, na huo utakuwa mwendo wa nchi nyingi.Soon mtasikia wajenzi wa bagamoyo wanashika top ten duniani kwa utajiri.halfu ndipo mlolongo kama wa issue ya rad utakavyoibuka.


Shida yetu watanzania tupo very persimistic na hatupendi kufanya utafiti kabla ya kuaza kulaumu na kuwa na negative opinion. Kujibia swali lako, hizo details za kodi itaanza kutozwa lini ndio zitajulikana kwenye mazungumzo baina ya Serikali na Mwekezaji. Bahati nzuri sheria za PPP zimeweka bayana mwongozo wa nini cha kufanyika. Definately Serikali itapata mrahaba, kodi ya ardhi, hisa katika mradi(ikiamua kununua) na kubwa zaidi ajira kwa vijana wasiopungua 2000 katika bandari hiyo mpya.
Mikataba ya aina hii Tanzania haitokuwa ya kwanza kuingia. Singapore majuzi wamejenga bandari mpya na ya kisasa kwa utaratibu huu. sri-Lanka (Colombo South Container Terminal) na Uturuki vilevile (Mersin Container Port), Uingereza-Great Yarmouth Terminals.....hii ni mifano michache tu ya karibuni.....chukua muda ku google usome zaidi kuhusu miradi hiyo upate kuelewa.

Kuhusu suala la mkataba utakuwa ni wa miaka mingapi litakuwa determined na uwekezaji utakayofanyika na muda wa return of investment utakaokadiriwa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali vya kiutaalam wa masuala ya fedha na biashara. Ofcourse the more money invested, the longer it may take kurejesha faida. Ipo mifano kadhaa inayoweza kutupa picha..mfano uwekezaji wa treni iendayo kasi kutoka Uingereza kwenda Ufaransa (The Channel Tunnel) iliyojengwa kwa utaratibu huu wa PPP..iligharimu kiasi cha USD 10billion...mkataba wa miaka 55 (google taarifa hizi zipo wazi); mradi wa Mersin Container Terminal huko Uturuki umegharimu USD 755 Million na wameingia mkataba wa miaka 36, kule Pakistan wamejenga Quasin Container International Terminal 2 kwa USD 211 na wameingia mkataba wa miaka 21. Nimekupa mifano hiyo ili upate picha kwamba miaka ya mkataba inategemea aina ya uwekezaji- returns, na mambo mengine. Tanzania haitokuwa ya kwanza, na tusiwadanganye watu na cheap arguments za kuwaonyesha kwamba tunaibiwa n.k

Hoja unayotoa kwamba vijana watanzania watafaidi leftovers na kwamba project za namna hii ni za kuzipora nchi masikini pesa nyingi kwakweli ni ya kisiasa zaidi. Why are you so persimistic kwenye mambo makubwa na ya kuleta maendeleo nchini?
Labda nikuulize, wewe ulitaka nini kifanyike? Pasijengwe kitu? Tubakie tu na umasikini....miradi isifanyike,ajira zisitengenezwe watanzania wenzako wasipate fursa?
Shida ya baadhi yetu, tushajiset na "maisha bora" ya ughaibuni, hatupendi kuona nchi yetu inaendelezwa kwa miradi mikubwa ili ndugu zetu tuliowaacha Nyumbani nao maisha yao yanaboreka kama sisi....

Miradi ya aina hii tuii structure vizuri (win-win) itakuwa na impact kubwa.....pengine hata mliopo mtoni mnaweza kurejea nchini kupata ajira zenye ujira unaofana na huo mnaopata ughaibuni. Kitu ambacho tungetegemea kutoka kwenu, ni kufanya utafiti huko mlipo project za aina hii zimekuwa structured vipi, nchi mlizopo zinafaidika vipi? Wale ambao wameingia kwenye such arrangement wakapata matatizo, walikosea wapi ili sisi tusirudie makosa yao.....etc etc......hayo ndio mambo ya kizalendo ya kufanya sio kuponda tuuuuuu haisaidii. Sisi tupo hodari kusifia vya wenzetu na kuponda vyetu....we need to change that negative attitude ili tuendelee
 
unajua viongozi wetu wengi ni watu wenye IQ ndogo sana,mimi naamini kuwa bandari ya Mtwara ilipaswa kujengwa kabla ya Bagamoyo,na pia naamini hatuhitaji bandari Dar na Bagamoyo.kati ya hizi mbili tunataka moja tu,ya ukweli na kwakuwa ya Dar ipo,basi ingeboreshwa tu.Naamini tz tunahitaji bandari tatu tu,Tanga,DSM na Mtwara,vilevile tunahitaji reli,Mtwara to Mbeya,mtwara to Iringa,etc

Hivi hapa mwenye IQ ndogo ni viongozi au ni wewe unayetoa hoja bila sababu za msingi. Unasema unaamini bandari tatu zinatosha nchini....ulifanya utafiti lini wa kukufanya uamini hivyo? Unaishi Tanzania kweli? Ukitembelea dar angalia meli zilizopanga foleni wiki nzima kuingia bandari ya dar..... Ukiagiza mzigo wako, angalia jinsi unavyochelewa kutoka kwasababu ya bandari ya dar kuzidiwa....mpaka watu wanakimbilia Mombasa. Masuala ya uwekezaji yanakuwa determined na numbers na sio imani! Kama kuna faida katika uwekezaji nchini.....hata bandari kumi zinaweza kujengwa....achilia tatu unazosema.
 
Mkuu salaama bigup for ur best analysis,watu wengine wamezoea kuponda tu.jaman hasira za kuichukia ccm na mwenyekiti wake zisihamie kwenye mipango ya kitaifa.
 
Mkuu kama ni kina utakuwa unachekesha, Bagamoyo haina tofauti sana na Dar na kama ni gate kubwa basi ilipo oysterbay, ukanda wa Mbezi hadi Kunduchi ni kupo wazi sana.Pia sababu ya dar kusemwa hivyo hiana msingi kwani Haiwezekani hata kwa miaka 50 ijayo, pakawa na Meli inayozidi ule ukubwa.Masuala ya kina si kweli kwani hata iwe vipi kwa bahari zinazoangalia EAST mawimbi yanaleta mchanga mfululizo na mara nyingi kutahitajika uondoa.


Saabua kubwa zipo nje ya maswalahi yetu ila kwa sifa za JK kadhani ataibadili Bagamoyo iwe dubai.Bagamaoyo ni front ya kufanya unyonyajia wa nchi, itakuw anjia ya kupitisha uranium, madini mengine na uwekezaji mkubwa wenye siri nyingi.

Sisemi kuwa haiwezekani kufungua njia ya mafanikio ila ni wazi kuwa hiyo project ni challenging sana kwa serikali corrupt na dhaifu kama ya CCM.Watafungua bagamoyo kwa mikataba ambayo si TRA,Si PCB,wala Sumatra watakaoweza thubutu ingia bila adabu.

Sioni processing itakayofanyikia bagamoyo yenye maana kam hakuna miundombinu ya train na barabara, JK angeleta plan ya kuwa na barabara zenye lane si chini ya 8, ziktokea pale na kwenda kusini kupitia dar, kuptia challinze ktk ya mapori , kupitia lugoba hadi dodoma, kupitia wami kwenda Arusha, kupitia Pangani kwenda tanga.Rel nayo iwe ya kati, kusini kaskazini itakayokwenda gawanyika mahali fulani kwenda tanga,ili kukwepa bahari na uwezekanao wa kukwama pakiwa na tsunami miak aijayo na pia Tanga ianweza fikiwa kwa bahari pia,mombasa na nyingine kwenda Arusha hadi Mwanza kupitia singida. Ila wakiweka hivi vinjia na vidaraja ambavyo hakuna hta nafasi ya mpita kwa baiskeli nina mashaka na evacuation siku za kawaida tu achilia mbali pakitokea uvamizi au tsunami.

Nicholous sio kweli kwamba Bagamoyo haina tofauti sana na Dar kwenye kina. Kina kinachotakiwa standard ni 13.9 M ili kukidhi meli zenye ukubwa wa kwenda chini mita 12. Kina cha Dar es salaam katika eneo lililopo la kupanua bandari hakifiki 13.9M, kwa sasa kipo kwenye 12M hivyo inabidi kufanya zoezi la kuchimba zaidi. Kina cha Bagamoyo ni 13.4M hivyo uchimbaji unaotakiwa ni kidogo ukilinganisha na Dar.

Umeongelea kwamba Oysterbay,mbezi, kunduchi kuna gate kubwa.....are you serious na hoja hii? Kweli unataka kutuaminisha kwamba sasa bandari ijengwe Oysterbay? mbezi? Kunduchi? Kwenye eneo lipi hilo ambalo lina space kubwa ya ku accomodate operations za bandari na mpaka kuwa na Export Processing Zone? Na hata kama space ingekuwepo...tunataka kuongeza congestion ya traffic zaidi ya iliyopo sasa? Maana shghuli za bandari lazima ziongeze idadi ya movement za magari kwenye eneo la bandari kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo.

Unasema bagamoyo ni front ya kufanya unyonyaji- hebu tupatie mawazo bora zaidi! From where am standing Bagamoyo project ni front ya kutoa ajira kwa vijana wengi ambao hivi sasa wamenitimu masomo yao katika ngazi mbalimbali na hawana ajira. Ni front ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara cha kuaminika; ni front itakayotuwezesha tuimili ushindani katika sekta ya bandari kwenye region yetu....wakenya wanapanua Mombassa, wanajenga bandari mpya Lamu.....sisi tumo humu kupiga porojo kwamba Bagamoyo ni front ya unyonyaji.

ume raise valid argument ya umuhimu wa kuwa na miundombinu ya kuisupport bandari mpya ya bagamoyo. Kama wewe umetambua umuhimu huo, hata yule anayetaka kuwekeza pesa yake kujenga ile bandari keshatambua hilo pia. Ndio maana ya kufanyika feasibility study na busines plan.....katika mpango mzima wa uwekezaji ule kuna ujenzi wa reli kuumganisha Tazara na reli ya kati kwenda Bandari ya Bagamoyo. Pia kuna mpango wa ujenzi wa Expressway ya Chalinze-Ubungo (alisha announce Magufuli bungeni) na express way ya Bagamoyo-Dar es salaam....na zile barabara za kati kuunganisha Bagamoyo na Kibaha zipo.
 
Hili jambo nilishalisikia mara nyingi sana.Nadhani sasa wameamua kulitekeleza.NILIDHANI BAADA YA MUDA MREFU WA KUTAFAKARI SENSE WOULD PREVAIL.Mambo haya yana fanana kabisa na yale ya Mobutu,to develop his village into a town.Na hii nadhani ndiyo nia.Jamani Dar es Salaam ni karibu mno na Bagamoyo, kiasi kwamba it would make sense kuongeza capacity ya Dar ili iweze ku-cater for Bagamoyo.Na hata hivyo viwanda vinavyodaiwa vinajengwa Bagasmoyo, for God's sake, why Bagamoyo and not Mtwara or Tanga kwa kuwa kama nilivyokwisha sema,Bagamoyo iko karibu mno na Dar.We need to develop other areas also.Mimi nadhani nia hapa ni ku-develop Bagamoyo for a very simple reason:Ni nyumbani kwa Rais aliyeko madarakani.Lakini hii ni mbaya, kwa kuwa people are inteligent enough to see.Ninaogopa haya mamba yasije yaka kaa kwenye mioyo ya watu halafu yakatuletea matatizo baadae.
[h=5]"Bandari ya Dsm imeelemewa na bado nchi nyingi za jirani zinahitaji kutumia bandari zetu hapa Tz,hivyo serikali ina mpango wa kujenga bandari ya kisasa huko Bagamoyo hili kukabiliana na changamoto hii".
Nimeshtushwa kuisikia hii kauli kuto kwenye kinywa cha waziri na viongozi mbalimbali ktk taarifa ya habari ITV huku waziri mkuu akiwepo,walikuwa wanaongea na wachina ambao wanategemea kuchukua hilo dili.Hii nchi sijui tunaipeleka wapi,hivi tuna haja kweli ya kuingia garama kubwa ya ujenzi wa Bandari ilhali tuna Bandari kubwa huku Mtwara ama pale Tanga?.Naanza kuingiwa na mashaka na hii plan B ya kuipeleka gas yetu Bagamoyo kwa kigezo cha kuwa inakwenda kutumiwa na viwanda vikubwa vinavyotarajiwa kujengwa huko,kwa nini isiwe Mkuranga?.

Kwa nn kila kitu siku hizi ni Bagamoyo?,hivi viongozi wetu hamlioni hili?.Msitulazimishe tuanze kuangaliana kibaguzi ktk nchi ambayo haikuwa na hivi vitu vinavyopandikizwa sasa.Kama waliopita wangekuwa na hurka za ubinafsi kama hizi basi Butiama,Lupaso na Dole yangekuwa majiji muda huu.[/h]
 
Nimekukubari bro umewezakunielewesha sababu ya kujenga port bagamoyo, watu wengine wanaingiza siasa ndani yake.Nimetembelea port nyingi duniani haziko town Kama dar port jinsi ya kuipanua ni utata sehemu ni ndogo, nimuhimu kuwa na port nyingine hapo karibu na dar. Kuna wakati niliketa mzigo ikapitia Mombasa nilijilaumu Sana gharama opioids kubwa Sana.Kama London ina port mbili Tilbury na Sherness na zote ziko busy.
Kama great thinker ungehoji ni vipi bandali ioanuliwe mpaka ikulu? Kweli una amini hilo?
Mbili nimesoma tokea mtoto kuwa bandali ya kina kirefu ni Mtwara, iweje leo aja ukuongopee na wewe hukubali?


Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Vipi kuhusu kilimo cha michikichi? Au ndio wanajenga bandari kwa ajili ya kuexport mawese!

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Siasa ni uchafu mkubwa ikiruhusiwa kwenye long term plans za maendeleo. Nilishiriki kidogo kuandaa feasibility study kwa ajili ya bandari 4 years ago. Timu ya wataaalamu wa hali ya juu kutoka ndani na nje ya nchi ilifanya kazi nzuri sana. Bandari hizo zote ulizotaja zilipitiwa na kuchambuliwa kwa undani ( 15 days kwa kila bandari). Matoeko kwa ufupi ni haya.Kujenga Tanga ni sawa ila gharama ya kuharmonise huduma nyingine ni kubwa sana. Pia kutakuwa na advantage (SPILL OVERS) fulanni kwa bandari ya Mombasa ambao ni rivals wetu. Mtwara pia ni nzuri ila kama Tanga service harmonization ni gharama. Pia miundombinu mingine ipo chini. DSM ina saffocate.


Bagamoyo - ipo karibu na huduma nyingi sana , imeshapangika ki miundo mbinu ikiwemo ujenzi wa viwanda na storage facilities ambazo zinafanywa na sekta binafsi ambayo haivutiwi na mazingira ya uwekezaji mbali sana na Dsm.

PAYBACK PERIOD - Mtwara ni 69 years. Tanga 52 years, Bagamoyo 35 years.

Yapo mengi kwenye andiko lile ila Nadhani kwa haya machache uamuzi ni wa kupigiwa saluti. Huwa siungi mkono serikali ila kwa hili MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI.

HEKO SERIKALI
 
.Nimetembelea port nyingi duniani haziko town Kama dar port
Bandari ya Cape Town ipo mjini, ukifananisha ilipo ni sawa na pale kivukoni

Bora hata yetu ni kubwa inaanzia Posta hadi Kurasini
 
Back
Top Bottom