Ujenzi wa Miradi hii Bagamoyo ni wa Lazima Kiasi Hiki?

..JK alikuwa mbunge kwa miaka 15 lakini jimbo lake lilikuwa limechoka huwezi kuamini kwamba liko karibu na DSM.

..wasiwasi wangu na miradi kama hii ni kwamba wenjeji wa Bwagamoyo watakuwa kama watazamaji tu. ardhi yao itachukuliwa, watalipwa fidia mbuzi, na baada ya hapo watahamia sehemu nyingine yenye umasikini.

..Bwagamoyo wanahitaji bottom up approach ktk kuchochea maendeleo. wanahitaji miradi ambayo itakuwa na direct impact kwa wananchi wa kawaida wa eneo hilo kama masoko ya kisasa ya mazao, miradi ya kilimo cha umwagiliaji, kuboresha shule za msingi na sekondari na kufungua vyuo vya ufundi stadi etc etc.
 
Miradi kama hii inaweza ikawa 'stimulus'! Amesema mwana JF Mmoja na mimi nakubaliana naye kabisa. Kwa muda tafakari kwamba mradi huu unalenga kuchochea maendeleo ya Bagamoyo(the sleeping giant ukitaka!). Kwa wale mnaotembelea Bagamoyo mtakuwa mmeona upande wa Dar yaani maeneo ya Kiroma, Zinga, Kerege na Mapinga yalishaanza kuinukia kimaendeleo. Bei za mashamba pale Kerege zilikuwa shs 250,000 miaka ya 2005 na kabla ya mradi huu (2009) tayari ilikuwa Tshs 2,500,000 na kando kando ya barabara zaidi ya hapo. Lakini upande wa pili wa Bagamoyo, kuelekea Mkata(au ni Msata nini?) hali ni tofauti mno, watu wanaishi maisha duni sana.

Nilidhani kama ni kuleta kichochozi cha maendeleo, Mheshimiwa angewekeza kule nyuma ya Bagamoyo(away from Dar) na awaachie wawekezaji ambao walishaanza kufuata Bagamoyo (from the Dar side) waendelee kujenga upande huu, na kwa kuwa mradi ungekuwa upande wa pili, kasi ya kuufikia ingekuwa kubwa.

Lakini kinachofanyika sasa Bagamoyo ni kuvunja nguvu za wale wawekezaji wadogo wadogo(wa mashamba, shule na biashara) kwa kuwanyanganya ardhi waliyoinunua na kuwaahidi fidia, kuwafanya wahame na kuwaacha wale wana-Bagamoyo upande wa pili wakitoa mimacho wakishangaa ni nini kinaendelea huko Dar (maana hata kufikiria sehemu ile ni ya kwao ni vigumu). Kwa ajili hii jiji la Dar na Bagamoyo zitakuwa pamoja na kukutana. Upande wa kule Mkata na Saadani utabaki kama zamani...hii ndio hadithi. Hapakuwepo na mchakato au master plan....
 
1. Bandari ya Dar lazima ife haifai kuwepo...Fedha zilizokusudiwa kujengwa bandari mpya Bagamoyo itumike kuboresha bandari za Tanga na Mtwara ikiwa ni pamoja na njia za usafiri nchi kavu.
2. Uwanja wa Ndege mpya Bagamoyo utakuwa hauna maana yeyote ikiwa huo wa Dar hauna traffic ya kutosha...demand na Supply haikubali.
3. Bwagamoyo ni mji wenye kumbukukumbu kubwa sana ya Utumwa. Mji huu ungepewa sifa hizi kimataifa na kuboresha sehemu zote zenye magofu ya historia ili kuvutia Watalii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Beach Hotels za kimataifa, viwanja vya Golf na misafara ya majahazi kwenda Zanzibar kama ilivyokuwa wakati wa utumwa..

Bagamoyo kuwa mji wa viwanda ni kuharibu mazingira safi ya kiasili ya mji huo kwani hauhitaji msongamano ulioko Dar na hakika tutakuja sahau kabisa historia..
Dar es Salaam inahitaji kupumua na misululu ya viongozi kama mji mkuu wa biashara, waondoe makao makuu kwenda Dodoma,huko watajenga Uwanja wa ndege wa kimataifa..
 
"...Bwagamoyo ni mji wenye kumbukukumbu kubwa sana ya Utumwa. Mji huu ungepewa sifa hizi kimataifa na kuboresha sehemu zote zenye magofu ya historia ili kuvutia Watalii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Beach Hotels za kimataifa, viwanja vya Golf na misafara ya majahazi kwenda Zanzibar kama ilivyokuwa wakati wa utumwa..." by Mkandara

UNESCO walishaupa huu mji hadhi ya hifadhi ya kimataifa, na kule mji mkonge kuna kazi nyingi zinazoendelea katika kukarafati majengo ya kale. Lakini una point kali, demand and supply na mwingine amesema tena vizuri tu, Kikwete alishindwa nini kuwahamasisha wenyeji wa Bagamoyo miaka yote 15 ya ubunge na sasa ameona heri awaletee miradi ambayo hata kushiriki kwao katika ujenzi ni ndoto, itakuwa wanayadokolea macho kama wale wenzangu mimi wanaoishi maeneo ya Savei wanavyoshangaa mle Mlimani City kuna nini
 
wanayajua hayo uroho unawasumbuwa wanasema feasibility study imefanyika wantaka kufunga kila mahala maajabu na kweli wajinga ndio waliwao
 
Hiyo miradi (mipango) kama ni sehemu ya iliyopangwa tangu zamani, sina utata nayo. Lakini ya ulimbukeni wa kuamka na kujenga Chuo Kikuu ni ufinyu wa mawazo,kama sio kupendelea kwao!
 
Hiyo miradi (mipango) kama ni sehemu ya iliyopangwa tangu zamani, sina utata nayo. Lakini ya ulimbukeni wa kuamka na kujenga Chuo Kikuu ni ufinyu wa mawazo,kama sio kupendelea kwao!

La kupendelea kwao silioni kama ni la msingi sana, kwani hiyo miradi itawafaidisha vipi locals wa hiyo sehemu? Ninavyowafahamu watahama watasogea porini zaidi na kutuachia 'wakuja' kupambana na hizo nafasi. Cha msingi ni kama huo uwekezaji umefuata taratibu na kama una tija kwa taifa. Haijalishi uwekezaji unafanyika wapi, provided hakuna anayezuiwa kusafiri na kuishi popote, wahangaikaji wataifaidi huko huko iliko. Hii mambo ya kusema eti watu fulani hawajaendelea kwa sababu eneo lao halikuwekezwa ni visingizio tu na hatuna budi kuachana navyo sasa.
 
"...Bwagamoyo ni mji wenye kumbukukumbu kubwa sana ya Utumwa. Mji huu ungepewa sifa hizi kimataifa na kuboresha sehemu zote zenye magofu ya historia ili kuvutia Watalii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Beach Hotels za kimataifa, viwanja vya Golf na misafara ya majahazi kwenda Zanzibar kama ilivyokuwa wakati wa utumwa..." by Mkandara

UNESCO walishaupa huu mji hadhi ya hifadhi ya kimataifa, na kule mji mkonge kuna kazi nyingi zinazoendelea katika kukarafati majengo ya kale. Lakini una point kali, demand and supply na mwingine amesema tena vizuri tu, Kikwete alishindwa nini kuwahamasisha wenyeji wa Bagamoyo miaka yote 15 ya ubunge na sasa ameona heri awaletee miradi ambayo hata kushiriki kwao katika ujenzi ni ndoto, itakuwa wanayadokolea macho kama wale wenzangu mimi wanaoishi maeneo ya Savei wanavyoshangaa mle Mlimani City kuna nini
unajua kunatafsiri mbili za maendeleo, kuna watu wanaona kuwepo kwa majengo mazuri, barabara nzuri nk hata kama hazina msaaada kwao ni maendeleo, au wanachukulia ile approach ya top down, wakati kuna wengine wanachukulia msingi wa maendeleo ni kuwepo kwa vitu vinavyo chochea uchumi/maendeleo kataka hali ya ku-balance na kuwafaidisha wahusika na pia kuwa endelevu, bottom- up, ndio maana kuna wengine kuwaleta brazili wanaona tumepiga hatua, hata kama mpira hatuuwezi, lakini wengine wangeenza na kujenga uwezo wa mpira na si dar-salaam tu bali kwa uwigo mpana zaidi ndio kutawezesha kuleta nigeria, ghana mpaka mjerumani.
 
"Bandari ya Dar es Salaam imeelemewa na bado nchi nyingi za jirani zinahitaji kutumia bandari zetu hapa Tanzania, hivyo serikali ina mpango wa kujenga bandari ya kisasa huko Bagamoyo hili kukabiliana na changamoto hii".
TANZANIA imeingia makubaliano na Kampuni ya Ujenzi ya (Merchants Holding Company) ya nchini China kwa ajili ya ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, alisema makubaliano ya awali yalifanyika Septemba 5, mwaka huu.

Alisema ujenzi huo unaenda sambamba na uendelezaji wa miradi mingine inayoambatana na ujenzi wa bandari hiyo kwenye Eneo Maalumu la Kiuchumi la Bagamoyo (SEZ).

"Leo tunashuhudia uzinduzi rasmi wa kikosi kazi cha pamoja kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya China Merchants Holding kitakachosimamia utekelezaji wa mradi huu," alisema Dk. Nagu.

Katika hilo, alieleza kuwa kikosi hicho kitasimamia miradi yote itakayojumuisha ujenzi wa barabara kuunganisha bandari hiyo, mtandao wa barabara nyingine na ujenzi wa reli itakayounganisha bandari hiyo, Reli ya Kati na Reli ya TAZARA.

Kwa mujibu wa Dk. Nagu mradi huo utakuza kwa kiasi kikubwa ushindani wa Tanzania kikanda na kimataifa kwa kuzingatia kwamba utaongeza uwezo wa kuhudumia shehena za mizigo zinazoingia na kwenda nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Congo (DRC) na Malawi.

Chanzo: Tanzania Daima | 17 Novemba 2012

Nimeshtushwa kuisikia hii kauli kuto kwenye kinywa cha waziri na viongozi mbalimbali ktk taarifa ya habari ITV huku waziri mkuu akiwepo, walikuwa wanaongea na wachina ambao wanategemea kuchukua hilo dili.

Hii nchi sijui tunaipeleka wapi, hivi tuna haja kweli ya kuingia garama kubwa ya ujenzi wa Bandari ilhali tuna Bandari kubwa huku Mtwara ama pale Tanga?. Naanza kuingiwa na mashaka na hii plan B ya kuipeleka gas yetu Bagamoyo kwa kigezo cha kuwa inakwenda kutumiwa na viwanda vikubwa vinavyotarajiwa kujengwa huko, kwanini isiwe Mkuranga?.

Kwanini kila kitu siku hizi ni Bagamoyo? Hivi viongozi wetu hamlioni hili?. Msitulazimishe tuanze kuangaliana kibaguzi ktk nchi ambayo haikuwa na hivi vitu vinavyopandikizwa sasa.

Kama waliopita wangekuwa na hurka za ubinafsi kama hizi basi Butiama, Lupaso na Dole yangekuwa majiji muda huu!
 
Si mkuranga wala Bagamoyo ni sahihi. Tanga ni kuzuri zaidi kusave Kaskazini na Uganda. Wakirekebisha miundo mbinu.

Kuweka Bagamoyo ni kuongeza hatari ya kanda ya Dar na Pwani kupanuka huku ikiwa haina plan ya Kufanya evacuation kubwa na ya haraka. Kupanua mianya ktk nchi ni kusambaza maendeleo haraka
 
Kumbuka msemo huu, in Tanzania if you are not confused then your head is not working properly.

Ukisikia kauli za viongozi wetu wanazotoa mikutanoni you get confused, if you get confused that's when you realise that your head is working properly.
 
Basil Mramba alijenga rami kwao

Wasira alipeleka maji kwao

Hao wakaadhibiwa kwa kubadilishwa wizara.

Mkulu yeye anapeleka bandari kwao. The leader is always right( IL DUCE HA SEMPRE RAGIONE)
 
Ndugu yangu usiligeuza suala hili muhimu la kiuchumi kuwa la kisiasa. Umuhimu wa bandari kwa uchumi wa Tanzania hauna ubishi. Yapo mambo ya msingi muhimu kufahamika:

Bandari ya Dar imeelemewa kwasababu ya wingi wa mizigo inayopitia katika bandari hiyo ndio maana kuna foleni za meli kuingia hapo Bandarini. Kuelemewa huko, kunasabasha jiji kuzidiwa na wingi wa magari ya mizigo na abiria (traffic congestion) yanayoingia na kutoka Bandarini. Zipo jitihada za kufanya upanuzi wa bandari hiyo kwa kujenga gati mpya no 13 na 14. Upanuzi huo ni suluhu ya muda mfupi katika handling ya mizigo, lakini hakutoa suluhu ya tatizo la congestion jijini....sana sana utaongeza congestion. Ni kwa msingi huo ujenzi wa bandari mpya ni jambo la muhimu.

Kwanini Bagamoyo?
Eneo la ujenzi wa bandari la Bagamoyo, lina kina kirefu na mlango mpana wa kuingizia meli zitakazohitaji kutia nanga. Hizo ni sifa kubwa zinazopelekea interest ya Wawekezaji wa sekta ya bandari kupendelea kuwekeza kule. Miaka 20 ijayo, meli zitakazojengwa zitakuwa ni 4th Generation zenye size kubwa kwa ajili ya kubeba mizigo mingi. Meli hizo hazitoweza kuingia kwenye lango la bandari ya Dar es salaam unless lifanyike zoezi la kupanua mlango wa bandari na kuchimba zaidi kuongeza kina....jambo ambalo itabidi kuchimba eneo kubwa mpaka ilipo Ikulu. Bandari ya Tanga na ile ya Mtwara vilevile zina disadvantage ya kutokuwa na Kina kikubwa kinachotakiwa kwa ajili ya hizo 4th generation ships. Sisemi kwamba haziwezi kutengenezwa zika accomodate meli za aina hiyo, la hasha. Inawezekana, lakini kwa gharama kubwa. Hivyo mtu anayetaka kuwekeza kwenye bandari ni rahisi zaidi kuwekeza Bagamoyo kule eneo lingine.

Lakini pia,duniani kote, bandari huwa zinafanya vizuri panapokuwa na eneo la Export Processing Zone na miundombinu mingine. Kule Bagamoyo next to eneo la BandAri, kuna eneo kubwa la mamlaka ya EPZA kwa ajili ya viwanda vya uzalishaji kwa ajili ya mauzo ya nje. Hivyo, muwekezaji yoyote mwenye kutaka kuwekeza kwenye bandari, atavutiwa kuwekeza kwenye bandari iliyo karibu na EPZ.

Tatu biashara ya bandari inahitaji kuwa karibu na eneo la biashAra (Business/commerical district) kwa ajili ya kuwezesha transactions mbalimbali. Kwa TZ commercial district ipo Dar es salaam. Hivyo muwekezaji wa bandari ata prefer kwenda bagamoyo iliyopo karibu na Dar kuliko mahala pengine. Lakini pia, Bagamoyo ina potential ya kutengeneza new business district.

Mtwara
Bandari ya Mtwara ipo sorted. Wale investors wa kuchimba gesi wameshaelezea nia yao ya kuitumia bandari ile kama sehemu ya usafirishaji wa gesi. Pia tayari eneo la uzalishaji wa viwanda karibu na bandari limechukuliwa na makampuni yatakayowekeza kwenye viwanda vya kuzalisha mbolea kwa kutumia gesi, na makampuni mengine ya uzalishaji wa cement kama lile la Dangote......hivyo, investor mpya anayekuja sasa, hawezi kuwa na interest na Mtwara kwani tayari kuna strategic investors wa bandari ile.

TANGA
Tanga itaendelezwa soon kwa hesabu za kuitumia ku serve eneo la kaskazini, na pia ni altenative ya Mombassa na pia inahitajika na waganda. Mipango yake ipo. Soon utaona nayo inashughulikiwa.
 
unajua viongozi wetu wengi ni watu wenye IQ ndogo sana,mimi naamini kuwa bandari ya Mtwara ilipaswa kujengwa kabla ya Bagamoyo,na pia naamini hatuhitaji bandari Dar na Bagamoyo.kati ya hizi mbili tunataka moja tu,ya ukweli na kwakuwa ya Dar ipo,basi ingeboreshwa tu.Naamini tz tunahitaji bandari tatu tu,Tanga,DSM na Mtwara,vilevile tunahitaji reli,Mtwara to Mbeya,mtwara to Iringa,etc
 
Hiyo bandari mpya imo kwenye mpango wa maendeleo 2011-2016? Labda kuna sababu muhimu za kujenga bandari nyingine mpya 50 km away toka bandari ya Dar. Lakini nilidhani, kwa changamoto tulizonazo -hasa kwenye sekta ya usafiri na usafirishaji, tungeimarisha bandari ya Dar, then change itakayobakia itumike kuboresha usafiri wa Train.

Tuna hela kidogo, tuwe na priority areas otherwise tutajikuta na miradi mingi ambayo haitakuwa na 'impact' kwa wananchi walio wengi. Hakuna kitu ambacho kina-miss nchi hii kama usafiri wa train and unless hili liangaliwe kwa jicho la karibu tutakuwa na uchumi wa makaratasi. Uchumi wa makaratasi ndio unachangia sana 'social unrest' maana watu wengi wanaachwa wakati wakubwa wanatupa GDP za ajabu ajabu.

It will be interesting kujua wachina wanaojitokeza kwenye hii Bandari mpya ya Bagamoyo wanafanya hivyo kwa makubaliano gani? Tunawapa/tunawalipa nini? China kwa sasa wana kiu ya 'raw-materials' na Africa ndio wamefika. Tayari wameshachukua mgodi wa makaa ya mawe in exchange watujengee bomba la gesi, sasa Bandari wanataka kulipwa vipi?
 
We hujui kule ni kwa Jk? Kila m2 na kwao bana! Hivi hujui nchi hii ilivyo! Tanga na bagamoyo kuna umbali gani mpaka kuwe na bandari 2!
 
"Bandari ya Dsm imeelemewa na bado nchi nyingi za jirani zinahitaji kutumia bandari zetu hapa Tz,hivyo serikali ina mpango wa kujenga bandari ya kisasa huko Bagamoyo hili kukabiliana na changamoto hii".
Nimeshtushwa kuisikia hii kauli kuto kwenye kinywa cha waziri na viongozi mbalimbali ktk taarifa ya habari ITV huku waziri mkuu akiwepo,walikuwa wanaongea na wachina ambao wanategemea kuchukua hilo dili.Hii nchi sijui tunaipeleka wapi,hivi tuna haja kweli ya kuingia garama kubwa ya ujenzi wa Bandari ilhali tuna Bandari kubwa huku Mtwara ama pale Tanga?.Naanza kuingiwa na mashaka na hii plan B ya kuipeleka gas yetu Bagamoyo kwa kigezo cha kuwa inakwenda kutumiwa na viwanda vikubwa vinavyotarajiwa kujengwa huko,kwa nini isiwe Mkuranga?.

Kwa nn kila kitu siku hizi ni Bagamoyo?,hivi viongozi wetu hamlioni hili?.Msitulazimishe tuanze kuangaliana kibaguzi ktk nchi ambayo haikuwa na hivi vitu vinavyopandikizwa sasa.Kama waliopita wangekuwa na hurka za ubinafsi kama hizi basi Butiama,Lupaso na Dole yangekuwa majiji muda huu.

ALIE SEMA raisi janga alimaanisha ni TUFANI ndo hayo sasa.
 
Ndugu yangu usiligeuza suala hili muhimu la kiuchumi kuwa la kisiasa. Umuhimu wa bandari kwa uchumi wa Tanzania hauna ubishi. Yapo mambo ya msingi muhimu kufahamika:
Bandari ya Dar imeelemewa kwasababu ya wingi wa mizigo inayopitia katika bandari hiyo ndio maana kuna foleni za meli kuingia hapo Bandarini. Kuelemewa huko, kunasabasha jiji kuzidiwa na wingi wa magari ya mizigo na abiria (traffic congestion) yanayoingia na kutoka Bandarini. Zipo jitihada za kufanya upanuzi wa bandari hiyo kwa kujenga gati mpya no 13 na 14. Upanuzi huo ni suluhu ya muda mfupi katika handling ya mizigo, lakini hakutoa suluhu ya tatizo la congestion jijini....sana sana utaongeza congestion. Ni kwa msingi huo ujenzi wa bandari mpya ni jambo la muhimu.

Kwanini Bagamoyo?
Eneo la ujenzi wa bandari la Bagamoyo, lina kina kirefu na mlango mpana wa kuingizia meli zitakazohitaji kutia nanga. Hizo ni sifa kubwa zinazopelekea interest ya Wawekezaji wa sekta ya bandari kupendelea kuwekeza kule. Miaka 20 ijayo, meli zitakazojengwa zitakuwa ni 4th Generation zenye size kubwa kwa ajili ya kubeba mizigo mingi. Meli hizo hazitoweza kuingia kwenye lango la bandari ya Dar es salaam unless lifanyike zoezi la kupanua mlango wa bandari na kuchimba zaidi kuongeza kina....jambo ambalo itabidi kuchimba eneo kubwa mpaka ilipo Ikulu. Bandari ya Tanga na ile ya Mtwara vilevile zina disadvantage ya kutokuwa na Kina kikubwa kinachotakiwa kwa ajili ya hizo 4th generation ships. Sisemi kwamba haziwezi kutengenezwa zika accomodate meli za aina hiyo, la hasha. Inawezekana, lakini kwa gharama kubwa. Hivyo mtu anayetaka kuwekeza kwenye bandari ni rahisi zaidi kuwekeza Bagamoyo kule eneo lingine.

Lakini pia,duniani kote, bandari huwa zinafanya vizuri panapokuwa na eneo la Export Processing Zone na miundombinu mingine. Kule Bagamoyo next to eneo la BandAri, kuna eneo kubwa la mamlaka ya EPZA kwa ajili ya viwanda vya uzalishaji kwa ajili ya mauzo ya nje. Hivyo, muwekezaji yoyote mwenye kutaka kuwekeza kwenye bandari, atavutiwa kuwekeza kwenye bandari iliyo karibu na EPZ.

Tatu biashara ya bandari inahitaji kuwa karibu na eneo la biashAra (Business/commerical district) kwa ajili ya kuwezesha transactions mbalimbali. Kwa TZ commercial district ipo Dar es salaam. Hivyo muwekezaji wa bandari ata prefer kwenda bagamoyo iliyopo karibu na Dar kuliko mahala pengine. Lakini pia, Bagamoyo ina potential ya kutengeneza new business district.

Mtwara
Bandari ya Mtwara ipo sorted. Wale investors wa kuchimba gesi wameshaelezea nia yao ya kuitumia bandari ile kama sehemu ya usafirishaji wa gesi. Pia tayari eneo la uzalishaji wa viwanda karibu na bandari limechukuliwa na makampuni yatakayowekeza kwenye viwanda vya kuzalisha mbolea kwa kutumia gesi, na makampuni mengine ya uzalishaji wa cement kama lile la Dangote......hivyo, investor mpya anayekuja sasa, hawezi kuwa na interest na Mtwara kwani tayari kuna strategic investors wa bandari ile.

TANGA
Tanga itaendelezwa soon kwa hesabu za kuitumia ku serve eneo la kaskazini, na pia ni altenative ya Mombassa na pia inahitajika na waganda. Mipango yake ipo. Soon utaona nayo inashughulikiwa.

Tanga ni karibu sana na Bagamoyo hivyo hizo sabaubu za Bagamoyo si za msingi. Tanga tayari kuna miundo mbinu kuna barabara na maeneo ambayo tayari yana mpangilio. Tanga ni mji ambao una mpangilio kuliko miji yote Tanzania!. Hivyo hata kama wakichimba bado gharama za kuendeleza Tanga zitakuwa ndogo kuliko kuanzisha mji mpya wa Bandari bagamoyo. Vilevile kuna viwanda Tanga na Hotel kwani Bagamoyo patajaa kama Dar hakuna mpangilio mzuri.
 
Back
Top Bottom