Ujenzi wa Miradi hii Bagamoyo ni wa Lazima Kiasi Hiki?

Lakini jamani tutazame upande mwingine wa Shilingi. Hii miradi yote imefanyiwa feasibility study na kuonekanaa inafaa na italeta tija. Sasa ni sawa kusema hao wataalam hawana uwezo wa kutosha?
Sidhani kama Rais akishauriwa na wataalam kwamba mradi haufai yeye akaendelea nao kwa sababu za kisiasa ama sivyo itakuwa yale ya "Alex stewwart" ya viongozi waliopita.
Mbona barabara na kiwanja cha ndege kitajengwa Serengeti?
Tujaribu kwenda ndani zaidi katika uchambuzi kabla ya kutoa hoja.

Feasibility study gani? Imefanywa na kampuni gani? Imeonyeshaje kwamba Bagamoyo ndiyo sehemu nzuri kabisa ya kutumia fedha zetu chache za kigeni? Utatuhakikishiaje kwamba hizi projects hazijapita kwa pressure ya top down? Kwamba mkulu anaagiza kiwanja cha ndege na bandari vijengwe kwanza, halafu feasibility study hata kama inakuja inachongwa ku fit matakwa ya mkulu?

Tumetumia hela kibao kuhamiha "mji mkuu" kwenda Dodoma, miaka kibao baadaye wizara zote, mabalozi wote na serikali yote kwa ujumla iko Dar bado.Hata hilo bunge lililohamia Dodoma wabunge wake kibao bado wako Dar. Hili halijatufundisha?

Katika wakati huu wa global economic crises, tunapata wapi confidence ya kuweka mihela kibao katika projects kubwa hizi? Historia ya kukuza miji kwa kumwaga fedha imejaa matokeo ya kushindwa, kuanzia Brasilia, Canberra mpaka Dodoma. Binafsi napenda zaidi mipango ya miji inayoipa miji organic growth, from bottom to top. Hizi habari za top down zimewashinda Waarabu na hela zao, zimewashinda Wa South Korea na teknolojia yao, other than a bottomless pit for our money, hizi pprojects hazina kazi nyingine.

While one can make a coherent case that the Dar business hub needs to be decentralized, and Bagamoyo may be the place to start, I feel that not enough justification is given.In addition tayari tuna bandari na viwanja vya ndege vinavyohitaji kuboreshwa. Tunakuwa sawa na yule mtu maskini lakini asiyetaka kufua nguo, nguo ikichafuka yeye anataka kununua nguo mpya tu. Hii si akili.

To make matters worse, projects zinaonekana kutolewa kwa sababu ya nasaba ya Kikwete kuwa Bagamoyo
 
Mara kadhaa nimeona watu wanauliza hoja kuwa kama ingekuwa kaskazini ingehojiwa. Mi naona huo ni upuuzi wa mawazo. Ni kujaribu kufanya cheap politics ambazo nafikiri hapa jamvini sio mahali pake.

Sitoki kaskazini wala Bagamoyo so I have no interest na maeneo yote hayo, ila kama mlipa kodi nina haki ya kimsingi ya kuhoji ninapoona watu wanafanya sivyo. Kuna mdau anasema tuombe miradi ifanikiwe! Siku hizi uchambuzi yakinifu ukishafanyika huhitaji tena maombi. What is the big picture kwa hiyo miradi ya Bagamoyo?
Mi ningedhani tungepanua Bandari ya Mtwara tumwage two way road kutoka Mtwara hadi Border ya Malawi na Zambia tuanze kushusha mizigo yao kama wenda wazimu tupate pesa, mkopo unarudi tunabali na infastructure na tunaendelea kukamua.

Sasa Bandari ya Bagamoyo barabara yenyewe ya Bagamoyo ina foleni saa sita mchana tukianza kupitisha malori ya bandarini yanayopeleka vitu Dar na mabasi ya mikoani mbona watu itabidi waondoke home saa kumi usiku badala ya 11:30 wanayofanya sasa kuwahi kibaruani?

Ningesikia kuwa panajengwa na reli fupi kulelekea mjini kupeleka Bidhaa au Bandari kavu karibu na chalinze kwa mizigo ya Rwanda, Burundi na Congo ningeelewa. Hapa usanii ni mwingi kuliko maelezo and I can smell something "FISHY"

Kukurupuka kumeshatuponza sana I hope not this time again,

Mpiga kura
 
Mchapakazi,

Hiyo habari ya Mtwara corridor mbona tushafanya mipango ya awali, kila kitu kipo katika makabrasha, lakini badala ya kukamilisha tulichoanza tunaanza mipango mingine. Bandari ya Mtwara ingehudumia a biggr hinterland mpaka Zambia huko, instead tuna duplicate mi bandari kibao kutoka Tanga, Bagamoyo na Dar.
 
Kuweka port mpya Bagamoyo hakuna ulazima, koz tayari tuna bandari safi tu ya tanga..1/4 ya hy pesa inaweza kuifanya bandari ya Tanga Kuifunika ya Mombasa. Trust me wanajamvi, kuna wakazi kibao wa Dsm wanapitishia Mizigo Bandari ya Mombasa then Holili to Dsm na sio kama bandari ya Salama haina uwezo la hasha ni utendaji mbovu wa Vigogo wa TPA DSM na TICS kwa Ujumla. kabla hawajafikiria kuestablish bandari mpya huko B'Moyo it could be very wise to eradicate all TPA's n TICS Bosses from Dsm port na kupata watu ambao wanauwezo wa kuiutilize Dsm Port to the Maximum.

Na sio kwanba JK halijui hili...How many times kafanya suprise visit pale?? anapiga mkwara mbuzi then hakuna utekelezaji juu ya mkwara wake so na those guys wameshamjua kuwa ni mbabaishaji so they are doing what the want and not what tehy r suppose to do...How many times vyombo vya habari vimeripoti juu ya ubadhirifu wa kodi ya Forodha na so far hakuna lolote lililofanyiwa kazi??? hawa jamaa bado wanakusanya mizigo kama kawaida 400$ per CBM tax inclusive from China to Dsm. nani kwagusa???

Take ggod care of what you have before u think of something New. kama cha zamani kimekushinda kukirun dont ever espect to run in a better way kipya ukijengacho. Kifupi ni upuuzi mtupu...Siku tukichapana na kuwa kama rwanda Burundi ndo hashima itakuja.......

Hakuna marefu yasio na ncha...
 
tumiisha fanya mikakati (kuhalalisha) uwepo uwanja wa ndege na Bandari na vitaka taka vyake navyo ni kuwepo kwa Karmal Investment hapo bagamoyo, sasa hawa wekezaji hawawezi kukaa Ghost town, lazima na wengine wawepo ili muweze kutumia bidhaa zao na majengo yao iwe hotel, play ground/michezo ya kitoto, majumba ya senema/cinema
 
Hizo ni plani mbovu tu za kupendezeshea eneo la nyumbani kwa Rais:

(a) Hata kama feasibility studies zimefanyika, inategemea terms of reference zilizotumika katika studies hizo. Kama study ilikuwa ni kutafuta sehemu ipi inafaa kujenga bandari nyingine ya kisasa, sidhani kama matokeo yangeonyesha kuwa ni Bagamoyo. Lakini kama study ilikuwa ni kutafuta kama Bagamoyo panafaa kujengwa bandari basi jibu lake litakuwa ni panfaa kwa sababu kuna bahari.

(b) Huwezi kujenga Bandari hapo Bagamoyo kwa sababu hakuna infrastructure ya kutosha kuisupport. Hakuna reli, hakuna barabara, ndiyo maana mradi unahusisha na ujenzi wa barabara za kwenda Tanga na Dar es salaam. Nina imani kuwa gharama za kukamilisha mambo hayo ni kubwa sana kuliko kupanua na kuboresha bandari za Mtwara, Tanga na Dar es Salaam kwa pamoja.

(c) Ujenzi wa Chuo Kikuu cha serikali hapo Bagamoyo nao ni muujiza wa ajabu sana hasa ukizingatia population iliyoko pale wakati kuna vyuo vikuu vingi vya serikali hapo Dar. Kuna sehemu nyingine za nchi zenye watu wengi lakini hazina vyuo vikuu vya serikali hata kimoja. Sehemu zote za kanda ya kusini, kanda ya ziwa na kanda magharibi hakuna chuo kikuu cha serikali hata kimoja. To the best ningetegemea serikali ifikirie kuweka chuo Kikuu Tabora, Mwanza, Mbeya, na Mtwara kuliko hapo Bagamoyo ambapo hakuna tofauti na Dar es Salaam.

(d) Hata kama ni kweli tunahitaji uwanja mpya badala ya ule JKN ambao umechoka, bado sijaona sababu ya kuujengea Bagamoyo ukilinganisha na Mkuranga ulikokuwa umepangiwa. Ninaanza kutambua kwa nini mbunge wa Mkuranga alipewa madaraka serikalini ili kumnyamazisha asipigie kelele jambo hilo la kuhamishwa uwanja kutoka Mkuranga kwenda Bagamoyo.
 
Tatizo la nchi yetu, mikakati inayo tumika katika kupeleka miradi in tilia maanani divide and rule, badala kuangalia strategy ya taifa ni nini ili kuleta maendeleo, na sio ili tujitajirishe au tuendele kutawala.

Na tatizo la strategy kama hii ni kuleta momonyoko wa kitaifa, na pia wa watu.

Watu hawa wamekaaa katika kile kinachoitwa mkao wa kula, lakini ndani yao wengi ni walafi zaidi ya wengine, wengine watakata paja kubwa kuliko wengine, matokeo yake wataanza kuona kwamba huyu, kumbe si mwenzetu, huyu anatatizo hili na lile. nk nk.

Kama watu wanaamini njia bora ya kutawala na kuleta maendeleo, basi tusubiri maafa makubwa tu katika taifa.

Ndio maana leo hii Taifa halina umeme wa kutosha, lakini wazeee wamekaa kutafuta ni njia gani watakayo tumia ili wale.

Maendeleo hata ukiwa na biliioni ngapi kama hutafuata mikakati endelevu , hutafanikiwa wala huwezi kudumisha huo utajiri.

Matatizo kama haya ndio yanayo mliza Mkapa, maana alifikiria kwamba kuwa kubalia WB,IMF, na wafadhili ndio kutaletezela maendeleo , na kuwekeza kwa wingi bila kujali ni mikakati ipi atumie ili hao wawekezaji waje. na wale ile tija iliyo tarajiwa.
 
hawa viongozi kama kina kikwete ndio stahili yetu watanzania.lame leaders for lame citizens.Siku tukiwa na quality population itakayoweza pambanua mambo kwa kina ndio tutapata viongozi bora.

Kwa sasa hivi kufosi kuna na Raisi muwajibikaji ni sawa na kutaka Tanzania kuwe na Lionel Messi.U need a bigger talent pool,otherwise it;'s pure luck..,that takes time!
FOR OUR CASE A FEW HUNDRED YEARS.
 
Hiyo miundombinu ingekuwa inajengwa kaskazini watu wangepiga kelele????????

Ni swali tu wadau, nothing personal.
Ingejengwa Arusha, Mtwara au Mwanza hamna atakayepiga kelele maana haitakuwa white elephants! kuna biashara huko na potentials nyingi
 
Fallacy ya argument yako inatokana na kujikita kwake katika averages.

Si kila mtanzania ni "lame", na hata kama wasio lame ni wachache, bado wana wajibu wa kutaka uongozi bora na kutoa ushawishi kwa wale wasiojua/ tegemea uongoi bora.

Kauli yako imekata tamaa. Concept nzima ya maendeleo inatokana na kuelewa limitations za the human condition, lakini kuelewa pia kwamba hata kama tuna limitations, tunaweza kufanya gradual advancement.

Kama si hivyo dunia nzima ingekuwa inalala na kuishi kijima tu.
 
Hiyo miundombinu ingekuwa inajengwa kaskazini watu wangepiga kelele????????

Ni swali tu wadau, nothing personal.

swala ndani ya 65km unaweka bandari nyingine na uwanja wa ndege mwengine ni upuuzi uliotukuka!
Ni sababu za kisiasa hakuna mtaalamu atakaye kubaliana na hizo pumba kwa nini visiboreshwe vya Dar maana ni kama vipo bagamoyo tu.
 
..naona Dr.Kawambwa kaamua kukomba kila kitu -- barabara,bandari,uwanja wa ndege.

..upendeleo huu angeufanya Mramba, ungesikia kelele za kina Selelii na wenzake.
 
Ingejengwa Arusha, Mtwara au Mwanza hamna atakayepiga kelele maana haitakuwa white elephants! kuna biashara huko na potentials nyingi
Mkuu,

Kwa kifupi ni kwamba hatuna vipaumbele, dira wala muelekeo. Kama vipo havifuatiliwi au havipo kimbinu. Hata hivo sitegemei miujiza kwene current system, ndivyo tulivo na hatutobadilika unless tuamue kubadilika.
 
hawa viongozi kama kina kikwete ndio stahili yetu watanzania.lame leaders for lame citizens.Siku tukiwa na quality population itakayoweza pambanua mambo kwa kina ndio tutapata viongozi bora.

Kwa sasa hivi kufosi kuna na Raisi muwajibikaji ni sawa na kutaka Tanzania kuwe na Lionel Messi.U need a bigger talent pool,otherwise it;'s pure luck..,that takes time!
FOR OUR CASE A FEW HUNDRED YEARS.

100% sure..this has been the case. Sad but true.
 
Mara kadhaa nimeona watu wanauliza hoja kuwa kama ingekuwa kaskazini ingehojiwa. Mi naona huo ni upuuzi wa mawazo. Ni kujaribu kufanya cheap politics ambazo nafikiri hapa jamvini sio mahali pake.
Nadhani wewe umeamua kujifutika kichwa chako mchangani kama mbuni..fair enough, uamuzi ni wako.

Lakini binafsi siamini influx ya miradi ya maendeleo kaskazini comes as a coincidence kama kunguru kwenda haja kichwani kwa mtu..there is explanation to that.Wakati barabara nyingine kule zinajengwa kiwango cha lami, majuzikati Kigoma ilikuwa haifikiki walau hata kwa treni la mjeremani au barabara za vumbi, yet it is the same Government. Sasa kuhoji mashuzi kama haya huezi kuniambia eti ni cheap politics.
 
mkuu bora angemalizana na suala la kuendeleza kigamboni kwanza............

haya mambo ya kuendeleza mikoa yote ni mazuri, lakini akamilishe moja kwanza ndio afanye jengine, laa si hivyo tutajikuta tuna vitu nusu nusu daima.
 
Naona wapo wenye hoja za msingi na wengine wanachuki zisizo na mantiki. Ukweli wa hoja ni kuwa maamuzi mengi yanafanywa na wanasiasa badala ya wataalamu,na siku zote tunajua ukitaka ufanikiwe kisiasa ni kufungia degree zako kabatini na kumsikiliza 'ma-rope' anasema nini.

Uwanaja wa JKN hauna tatizo kinachotakiwa ni kuuboroesha uendane na wakati. Eneo la kufanya hivyo lipo. Mwl aliupanua kulingana na mahitaji ya wakati ule,lakini tunapaswa kujiuliza ATC imekufa,ndege zinazotua ni za nje na waala hakuna inayolala hapo,sasa uwanja tunaotaka kuujenga ni kwa matumzi gani. Kwani tusiukarabati uwanja wetu uwe wa kisasa kama tulivyofanya uwanja wa mpira? Hatukwenda Bagamoyo au Mkuranga.

Pili, eneo la viwanda linajengwa kabla ya kuimarisha miundo mbinu, sasa sijui tunategemea nini endapo tu kutoka lugalo kwenda tegeta ni saa moja kwa mwendeshaji wa gari.

Tatu,bandari ya Dar inafanya kazi chini ya kiwango, tumempa TICTS ukiritimba na kwa vile kuna 10% hakuna anayesema lolote.Hatuhitaji bandari mpya,ile ya Tanga na mtwara zinatosha kama tutainua ufanisi kwa kuweka management mpya hata kama ni za kigeni. Kwa kumbukumbu tu,bandari ya Dar peke yake ingeweza kuchangia nusu ya pato la taifa, wajinga watabisha lakini tujiulize Norway na Dubai wanafanikiwa vipi.

Mwisho,hatuna haja ya kuwa na majengo mengi,UDSM ina eneo kubwa kwanini tusiliendeleze ili kupata wanafunzi wengi. Ubora wa elimu si kusambaza majengo kila mahali bali kutumia resource vizuri.

Mfano kwanini chuo cha ufundi mbeya kisiendelezwe ili kuchukua wanafunzi hata 100,000, kwanini chuo cha butimba kisiendelezwe kuchukua wanafunzi wengi zaidi, kwani chang'ombe kispanuliwe et etc. Hatuhitaji majengo kila mkoa tunahitaji ubora wa wahitimu.

Mwisho, nachukia sana ukaskazini au umagharibi na ukusini watu wanaoongelea. Kuna mambo yapo kutokana na historia na geographical position. Mathalani dhahabu na almas na pamba ndizo zilikuza mji wa mwanza na kwahiyo uchumi ndio una dictate priority. Kahawa na utalii ndizo ziliendeleza miji ya kilimanjaro na Arusha, na hii imebaki lifeline ya uchumi hadi leo.

Nitashangaa kama kuna mtu ana wazo la kujenga uwanja wa ndege Malinyi ulanga badala ya KIA. Hata ukiangalia mtiririko wa kiuchumi, unalazimisha pengine hata miundo mbinu kuelekezwa huko. Angalia Tanga baada ya mkonge kufa na kila kitu kimedorora. Hii haina maana eti tulazimishe bwawa la kidatu lijengwe Lindi, lakini kama upo umuhimu wa kiwanda cha uvuvi kujengwa na basi kiwe Lindi au mtwara. Ukitaka kujua geography inachangia vipi maendeleo,nenda mtwara. Mwaka 1985 nilikuwa Mtwara, hakika hali ilikuwa inahuzunisha, leo baada ya Songo Songo gas Mtwara imezaliwa upya, na uwekezaji umeanza kwa kasi na hiyo ndiyoitainua hata umuhimu wa miundo mbinu.

Lakini pia maendeleo yanaletwa na watu wenyewe, kule kwetu milimani kilimanjaro wazee wetu walichimba bara bara ingawa hawakuwa na magari kwa njia ya kujitolea, leo tunaongelea upanuzi wa kingo za bara bara na si kupasua miamba. Wazee wetu walijenga shule zao leo wilaya moja ina shule zaidi ya mkoa mmoja. Ni kwa kutumia elimu waliyopata huenda ndio maana wanaonekana wanapendelewa.

Angalia Bukoba, miaka ya 60 walishafikiria kuwa na chuo kikuu, ni mizwengwe tu wangeweza, lakini hawajakata tamaa, Josia Kibira University inapanda. Sasa tujiulize jitihada gani wana Kigoma wanafanya ambazo zinahitaji usaidizi wa serikali ili wasaidiwe. Vinginevyo wakikaa kimya wasubiri chuo kikuu cha serika shauri yao maana watakapokipata wale wa Bukoba na Kimanjaro watakuwa na 20.
Ni mawazo tu.
 
Uwanja wa ndege mpya ulishatafutiwa eneo zamani kabla muungwana hajaingia madarakani. Eneo lilishatengwa wilaya ya Mkuranga, inakuwaje ahamishie Bagamoyo? kwao for that matter! sasa huu ni ulimbukeni. Jamani Nyerere angetaka kupeleka vyote Musoma nchi ingekuwaje? Muraaa, ri uwanja riko kwetu muraa... Maslahi ya taifa yaangaliwe, huo sasa ni ubinafsi...watu wataanza kuchagua kiongozi kikanda ili miradi iletwe nyumbani. Hata huo Bwagamoyo internattional Airport itahamishwa na kupelekwa BK...oooh...mmh Kamachumu International Airport.....awamu nyingine kuleee Tuykuyu.....awamu nyingine kuleee Zenj...Kibandamaiti International Airport. Watanzania tuige mwalimu alivyo allocate rersources.

Umenena! Ni kweli TAA walishafanya mikakati ya kujenga extension ya Dar Airport huko Mkuranga (60km kutoka Dar kuelekea Kilwa) ambapo ni karibu sana na Airport ya sasa kwa maana ya kuzungukia Chanika/Kisarawe, pia hakuna makazi yanayohitajika kuondolewa kupitisha barabara ya kuunganisha viwanja vya Dar na hicho kipya. Lakini mkulu anataka na yeye airport, lakini fikiria kuunganisha Uwanja wa sasa kwa barabara na Bagamoyo! Mama yangu!

Lakini ninachoona zaidi ni UBINAFSI! Ni kwangu Bagamoyo, Ni kwangu Songwe(Prof Mwandosya naye alingangana akapata Uwanja wa International pale Songwe!). Sasa hivi taifa linajadili miliki ya taasisi zinazoanzwa na wake wa maraisi( yaani first lady hasa yule wa Mkapa na Kikwete). Wenye upeo mdogo wanabishia eti ni kuwaonea wivu hawa kina mama, hawataki kuona kuwa ni kwa ajili ya nafasi za waume zao wameweza kujenga hizo taasisi na kwa kuwa wao ni wachaguliwa wa taifa, basi mali hizo sio zao binafsi. Ni kama huyo anayeuliza kama ingekuwa 'kaskazini'....acha mabishano ya namna hii, tuangalie maslahi ya taifa na dira ya maendeleo yetu.

Nisingeona shida kama miradi yote ya Bagamoyo ingekuwa inatokana na fedha za ndani ya Bagamoyo, lakini tunajua fika tunachangia wote kama taifa. Huko Rufiji, kule Kibondo, na kungineko, hali ya maisha bado inatisha, iweje mwenye kukampeni maisha bora zaidi kwa waTZ analundika miradi Bagamoyo, tena kwake, na je miradi hii kweli itawaondolea umaskini wana-Bagamoyo! NGOJA Tuone, maana hata kina ngosha kule Mwadui na wazaramo waliokuwa kando kando kule Kipawa hali zao zilibaki pale pale wakati miradi hiyo ilivyoanza KAMA sio kudorora.

Mungu kwa nini hujapenda kutupa viongozi wenye kuona mbali? Kwa nini huturudishii Nyerere
 
Naona wapo wenye hoja za msingi na wengine wanachuki zisizo na mantiki. Ukweli wa hoja ni kuwa maamuzi mengi yanafanywa na wanasiasa badala ya wataalamu,na siku zote tunajua ukitaka ufanikiwe kisiasa ni kufungia degree zako kabatini na kumsikiliza 'ma-rope' anasema nini.

Uwanaja wa JKN hauna tatizo kinachotakiwa ni kuuboroesha uendane na wakati. Eneo la kufanya hivyo lipo. Mwl aliupanua kulingana na mahitaji ya wakati ule,lakini tunapaswa kujiuliza ATC imekufa,ndege zinazotua ni za nje na waala hakuna inayolala hapo,sasa uwanja tunaotaka kuujenga ni kwa matumzi gani. Kwani tusiukarabati uwanja wetu uwe wa kisasa kama tulivyofanya uwanja wa mpira? Hatukwenda Bagamoyo au Mkuranga.

Pili, eneo la viwanda linajengwa kabla ya kuimarisha miundo mbinu, sasa sijui tunategemea nini endapo tu kutoka lugalo kwenda tegeta ni saa moja kwa mwendeshaji wa gari.

Tatu,bandari ya Dar inafanya kazi chini ya kiwango, tumempa TICTS ukiritimba na kwa vile kuna 10% hakuna anayesema lolote.Hatuhitaji bandari mpya,ile ya Tanga na mtwara zinatosha kama tutainua ufanisi kwa kuweka management mpya hata kama ni za kigeni. Kwa kumbukumbu tu,bandari ya Dar peke yake ingeweza kuchangia nusu ya pato la taifa, wajinga watabisha lakini tujiulize Norway na Dubai wanafanikiwa vipi.

Mwisho,hatuna haja ya kuwa na majengo mengi,UDSM ina eneo kubwa kwanini tusiliendeleze ili kupata wanafunzi wengi. Ubora wa elimu si kusambaza majengo kila mahali bali kutumia resource vizuri.

Mfano kwanini chuo cha ufundi mbeya kisiendelezwe ili kuchukua wanafunzi hata 100,000, kwanini chuo cha butimba kisiendelezwe kuchukua wanafunzi wengi zaidi, kwani chang'ombe kispanuliwe et etc. Hatuhitaji majengo kila mkoa tunahitaji ubora wa wahitimu.

Mwisho, nachukia sana ukaskazini au umagharibi na ukusini watu wanaoongelea. Kuna mambo yapo kutokana na historia na geographical position. Mathalani dhahabu na almas na pamba ndizo zilikuza mji wa mwanza na kwahiyo uchumi ndio una dictate priority. Kahawa na utalii ndizo ziliendeleza miji ya kilimanjaro na Arusha, na hii imebaki lifeline ya uchumi hadi leo.

Nitashangaa kama kuna mtu ana wazo la kujenga uwanja wa ndege Malinyi ulanga badala ya KIA. Hata ukiangalia mtiririko wa kiuchumi, unalazimisha pengine hata miundo mbinu kuelekezwa huko. Angalia Tanga baada ya mkonge kufa na kila kitu kimedorora. Hii haina maana eti tulazimishe bwawa la kidatu lijengwe Lindi, lakini kama upo umuhimu wa kiwanda cha uvuvi kujengwa na basi kiwe Lindi au mtwara. Ukitaka kujua geography inachangia vipi maendeleo,nenda mtwara. Mwaka 1985 nilikuwa Mtwara, hakika hali ilikuwa inahuzunisha, leo baada ya Songo Songo gas Mtwara imezaliwa upya, na uwekezaji umeanza kwa kasi na hiyo ndiyoitainua hata umuhimu wa miundo mbinu.

Lakini pia maendeleo yanaletwa na watu wenyewe, kule kwetu milimani kilimanjaro wazee wetu walichimba bara bara ingawa hawakuwa na magari kwa njia ya kujitolea, leo tunaongelea upanuzi wa kingo za bara bara na si kupasua miamba. Wazee wetu walijenga shule zao leo wilaya moja ina shule zaidi ya mkoa mmoja. Ni kwa kutumia elimu waliyopata huenda ndio maana wanaonekana wanapendelewa.

Angalia Bukoba, miaka ya 60 walishafikiria kuwa na chuo kikuu, ni mizwengwe tu wangeweza, lakini hawajakata tamaa, Josia Kibira University inapanda. Sasa tujiulize jitihada gani wana Kigoma wanafanya ambazo zinahitaji usaidizi wa serikali ili wasaidiwe. Vinginevyo wakikaa kimya wasubiri chuo kikuu cha serika shauri yao maana watakapokipata wale wa Bukoba na Kimanjaro watakuwa na 20.
Ni mawazo tu.

Mkuu umeongea vizuri tu...

Lakini kuna ubaya gani kuifanya Bwagamoyo kuwa kitovu cha kibiashara?. kumbuka kuwa wawekezaji wa viwanda kwenye EPZs wanatumia pesa zao na inaelekea wawekezaji wengi wangependa kuwa nje ya Dar sehemu ambazo hawatakuwa na shida ya usafiri. EPZs ni kwa ajili ya kuuza nje kwa hiyo ni lazima bandari ya uhakika iwepo hapo, uwanja wa ndege kwa ajili ya mizigo n.k.

Pia nadhani hata hiyo bandari inayozungumziwa inajengwa na wawekeaji toka Qatar au UAE kama sikosei. Hawa watu hawataki kuingiza pesa yao kukarabati bandari ya Dar wanataka kujenga mpya Bwagamoyo kwanini tukatae?.

Mwisho, kama mipango yote hii ikifanikiwa basi nasisi siku moja tutajigamba na Dubai yetu ya Afrika pale Bwagamoyo! watoto wa wasukuma, wahehe, wachaga, wapare, na wakwere watafaidika kwa ajira n.k.

Wazo tu:
Msimlaumu sana Muungwana mbona kawajengea Chuo Kikuu kikubwa kabisa afrika ya mashariki pale Dodoma? kwani kaoa kule? :cool:
 
Hapa tunapigia mbuzi gitaa acheze. Tayari kama tunafahamu mapungufu ya mapendekezo haya, udhaifu wa wawakilishi wetu, ugumu wa watawala wetu kutusikiliza, n.k , Je ni kwa nini sasa tunapuliza "mavuvuzela" yetu kwenye mitandao ya internet? Kama suala hili na mengine mengi yanawagusa kuna njia nyingi sana za AMANI na zisizovunja sheria za kuonyesha kuguswa au/na kukerwa na vitu hivi, mnaweza kujikusanya na kuandamana, mnaweza pia kutowapigia kura n.k

Maneno matupu hayavunji mfupa !
 
Back
Top Bottom