Ujenzi wa Miradi hii Bagamoyo ni wa Lazima Kiasi Hiki?

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,569
19,441
HATUA ya serikali kuelekeza miradi mikubwa zaidi ya sita ikiwemo ujenzi wa bandari na uwanja wa ndege wa kimatiafa wilayani Bagamoyo, alikozaliwa Rais Jakaya Kikwete imepingwa na wapinzani wakisema uamuzi huo ni ufujaji wa fedha za walipa kodi.

Mjadala huo umeibuka wakati serikali imeshaanza mkakati wa kutekeleza azma ya kuigeuza
Bagamoyo kuwa kitovu kikuu cha biashara na uchumi nchini kwa kujenga miradi mikubwa mbalimbali wilayani humo ikiwemo bandari, uwanja wa ndege, Chuo Kikuu, Soko la Kimataifa, barabara kuu kwenda mikoa ya Kanda ya Kaskazini, kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na viwanda mbalimbali.

Juni 25, mwaka huu Rais Kikwete, alizindua eneo la uwekezaji lenye ukubwa wa ekari 300 ambapo wawekezaji wa Kampuni ya Kamal kutoka nchini India wameanza kutekeleza mradi wa kujenga viwanda na maduka wenye thamani ya Sh400 bilioni katika eneo Zinga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Kufuatia utekelezaji huo kwa nyakati tofauti wapinzani walisema mpango huo umeibuka bila kuainishwa popote ikiwemo katika Dira ya Taifa ya Maendeleo (Visioni 2020/25).

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed alikosoa mradi huo akisema: "Ni jambo baya zaidi kuanzisha miradi mipya huku ya zamani ikifa. Mpango huo wa serikali ni mbaya, 'ni missallocation' (mgawanyo mbaya) ya miradi. Huwezi kuacha uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam ukiwa haina ufanisi kwa kutosha, ukajenga uwanja mwingine mkubwa Bagamoyo".

Hamad aliongeza: "Tunachojua miradi kama hiyo ilitakiwa kuonyeshwa katika Dira ya Maendeleo ya 2020/25 na Mkakati wa Mkukuta, lakini hiyo haimo humo. Kibaya zaidi bajeti yetu inategemea wafadhili".

Hamad Rashid alidai kuwa serikali imeshindwa kutumia msaada wa fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya kuboresha utawala bora na mfumo wa mahakama badala yake ikatumia asilimia 25 tu wakati miundombimu ya Idara ya Mahakama inahitaji kuboreshwa.

"Serikali ingeweka mkazo kwa miradi iliyopo, huwezi kujenga bandari Bagamoyo wakati ya Dar utendaji wake ni mbovu na bandari za Tanga, Mtwara zinakufa. Huwezi kujenga chuo kikuu kama cha UDOM Bagamoyo na kuacha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinakufa, hili ni tatizo", alisema Hamad.

Kauli hiyo ya Hamad inakuja wakati kuna taarifa kwamba, mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege unatarajiwa kuanza wiki ijayo huku ule wa bandari ukitarajiwa kuanza mwezi mmoja ujao.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili, kuhusu miradi hiyo jumamosi iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Magessa Mulongo alisema ujenzi wa uwanja wa ndege ulitarajiwa kuanza wiki hii na bandari mwezi Julai.

"Vipo vinafanyika, kwa ujumla mambo yanakwenda vizuri. Hatua za awali za uwanja wa ndege wa kimataifa tunatarajia kuanza wiki ijayo (wiki hii), bandari mwezi ujao (Julai)," alisema Magessa.

Alisema kuwa tayari kiwanja cha kujenga Chuo Kikuu kimepatikana eneo la Msakese na kwamba ujenzi wa barabara kati ya Saadani na Tanga upo mbioni.

Naye Mwenyekiti wa NCRR-Mageuzi James Mbatia, alikosoa miradi hiyo akisema ni kupoteza fedha za walipa kodi na kuonya kuwa Watanzania wasifanywe wajinga ndani ya nchi yao.

Mbatia alifafanua kuwa kujengwa uwanja wa ndege na bandari nyingine Bagamoyo umbali wa kilometa 65 kutoka Dar es Salaam ni kuchezea akili za Watanzania na kwamba, miradi hiyo inakofanywa kwa malengo ya kisiasa ya muda mfupi bila kuangalia mbali kwa manufaa ya taifa.

"Hii ni 'wastage' (matumizi mabaya) ya fedha za walipa kodi. Hapa serikali inachezea akili za Watanzania. Kujenga bandari Bagamoyo kilometa 65 toka Dar ni akili ya wapi?" Alihoji Mbatia.

Mbatia ambaye alihitimu hivi karibuni taaluma ya bandari nchini Ujerumani, alisema serikali imepanga kufanya hayo huku ikishindwa kutumia ukanda wa bahari wenye eneo la kilometa 1,424 na kwamba, bandari ya Dar es Salaam haimo hata miongoni mwa bandari 100 bora duniani.

"Tufikiri chanya, tusifanye kienyeji na tusifanye mambo ya kitaalam kwa malengo ya kisiasa, tuache ubabaishaji," alisema.

Mwenyekiti huyo wa NCCR alisisitiza kuwa jambo muhimu kwa serikali ni kuimarisha na kuboresha utendaji wa viwanja vya ndege na bandari zilizopo, pamoja na kujenga bandari kavu eneo la Kibaha ili kusaidia ufanisi kwenye badari ya Dar es Salaam.

Uamuzi wa Rais Kikwete kujenga miraadi hiyo mikubwa katika mkoa na wilaya aliyotoka ni tofauti na ilivyokuwa kwa marais wa Tanzania waliomtangulia.

Katika uongozi wake wa awamu ya kwanza mbali na kutawala kwa miaka 25, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hakuwahi kujenga hata barabara ya lami katika wilaya aliyotoka (Musoma Vijijini).

Hata rais awamu ya tatu Benjamin Mkapa kwa miaka kumi ya madaraka yake, hakuweka mradi wowote mkubwa mkoa au katika wilaya aliyotoka.

Tunakimbiwa, Kikwete aachane na mradi wa bandari Bagamoyo!

Johnson Mbwambo
Raia Mwema

Toleo la 318
2 Oct 2013

HAKUNA shaka yoyote kwamba Uganda na Rwanda zimepania kujenga reli mpya itakayoungana na ile ya Kenya hadi bandari ya Mombasa itakayoziunganisha nchi hizo tatu – mradi ambao wakiukamilisha utakuwa ni pigo kubwa kwa bandari yetu ya Dar es Salaam hasa baada ya upanuzi wa hivi karibuni wa bandari ya Mombasa.

Naweza kuthubutu kusema ya kwamba anayeupigia chapuo la nguvu mradi huo mkubwa ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye anaiona reli hiyo ya pamoja itaharakisha nchi hizo tatu kufikia shirikisho la kisiasa. Museveni ndiye anayelitamani zaidi shirikisho hilo kuliko viongozi wenzake wote katika Afrika Mashariki.

Miaka miwili iliyopita alifanya ziara ya ghafla mjini Dar es salaam ambako alikutana na Rais Kikwete, na wawili hao, baada ya mkutano wao, wakatangaza mpango wa ujenzi wa reli mpya kutoka bandari yetu ya Tanga hadi Uganda. Waliachana kwa ahadi kwamba kila mmoja achacharike kutafuta wafadhili wa mradi huo.

Sina hakika nini kilitokea hadi mradi huo ukaota ‘mbawa', lakini nina hakika kwamba ni Museveni huyo huyo ndiye ‘aliyeuza' kwa Rais Uhuru Kenyatta na Paul Kagame wazo la kujenga reli mpya itakayoziunganisha nchi hizo hadi bandari ya Mombasa.
Hisia zangu ni kwamba Rais Museveni aliona ya kuwa Watanzania hatulichangamkii ipasavyo wazo lake la kujenga reli kutoka Tanga hadi Uganda kama ambavyo hatuchangamkii (atakavyo) wazo la kufikia haraka shirikisho la kisiasa, na ndiyo maana akahamishia wazo hilo kwa Kenya na Rwanda, na sasa reli hiyo itajengwa.

Baada ya kikao cha marais hao cha Agosti kilichofanyika Mombasa, vimeshafanyika angalau vikao vingine viwili vya mawaziri husika kujadili mradi huo. Kwa kasi ya maandalizi wanayokwenda nayo, si miaka mingi ijayo twaweza kushuhudia reli hiyo ikikamilishwa.
Wiki iliyopita Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Silas Rwekabamba, alinukuliwa na vyombo vya habari kwamba wameshaanza kufanya upembuzi yakinifu wa mradi huo.

Ndugu zangu, nilieleza mwanzoni kwamba endapo, hatimaye, reli hiyo itakamilishwa kujengwa, itakuwa ni pigo kubwa kimapato kwa bandari yetu ya Dar es Salaam ambayo chini ya uongozi mpya wa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (THA), Mhandisi Madeni Juma Kipande, imekuwa ikijitahidi kuchuana na bandari ya Mombasa.
Kwa mfano, TPA wamejitahidi, katika muda mfupi, kupunguza muda wa meli kukaa bandarini kupakua mizigo kutoka siku 21 hadi siku saba. Si hivyo tu; kwani bandari ya Dar es Salaam sasa imefikia kiwango cha kupakua magari 200 kwa saa ambacho ndicho wastani kimataifa.

Ni matumaini yangu kwamba kwa kasi hiyo ya Waziri Mwakyembe na Mhandisi Kipande, bandari ya Dar es Salaam itaingia, hivi karibuni, katika orodha ya bandari 120 bora duniani au hata katika ‘tano bora' za Afrika ambapo kwa sasa zimo bandari za Durban (Afrika Kusini), Mombasa (Kenya), Port Said na Alexandria za Misri na Tanger Med ya Morocco.

Hata hivyo, inaweza kukatisha tamaa kwamba wakati ufanisi katika bandari yetu hiyo ya Dar es Salaam umeimarika maradufu katika kipindi kifupi tu, wenzetu Uganda, Rwanda na Kenya wamefikia makubaliano ya kujenga reli mpya itakayoziunganisha nchi hizo hadi bandari ya Mombasa.
Ni dhahiri, kama nilivyoeleza mwanzo, kwamba reli hiyo mpya itakuwa pigo kubwa kiuchumi kwa bandari yetu ya Dar es Salaam kwa sababu tutapoteza wateja watatu wakubwa wa miaka mingi; yaani Rwanda, Uganda na Sudan Kusini. Kwa hakika, hata uteja wa Burundi nao utakuwa shakani.
Nikumbushe tu hapa kwamba kwa miaka mingi nguvu ya kiuchumi ya bandari yetu ya Dar es salam ilitokana na kuhudumia nchi sita zisizo na bandari; yaani Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda, Uganda na DR Congo.

Ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba, hali kwa bandari yetu hiyo itakuwa mbaya kimapato kama Uganda na Rwanda zitakamilisha mradi huo wa ujenzi wa reli mpya inayounganisha nchi hizo na ile ya Kenya hadi bandari ya Mombasa.

Hebu jiulize; kama bandari ya Mombasa inatupiku kimapato katika kipindi ambacho Dar es Salaam inahudumia mizigo ya Uganda, Burundi, Rwanda, DR Congo na hata Sudan Kusini, hali itakuaje siku reli hiyo mpya itakapokamilishwa kujengwa na nchi hizo, na hasa upanuzi wa bandari ya Mombasa utakapokamilika kabisa?

Ni dhahiri kwamba upanuzi wa bandari ya Mombasa utakapokamilika kabisa na reli hiyo mpya na ya kisasa nayo ikakamilika kujengwa, Uganda, Rwanda, Sudan Kusini na pengine Burundi zitasitisha kupitisha bidhaa zao kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Je, bandari yetu hiyo inaweza isitetereke kimapato hata kama itapoteza soko hilo kubwa la kuhudumia bidhaa za nchi hizo na hasa ikizingatiwa kwamba usafirishaji wetu bidhaa nje (export) kupitia bandari hiyo ni mdogo mno baada ya kuua kilimo na sekta ya viwanda?
Hilo ni swali ambalo ukiwatupia watawala wetu watakupa majibu ya kisiasa zaidi badala ya kiuchumi. Tayari wameshaanza kutupa matumaini ya uongo kwamba eti hatutaathirika sana kiuchumi kama tutatupwa nje ya shirikisho jipya la kisiasa la Afrika Mashariki (na dalili tunaziona). Hoja yao ni kwamba hilo likitokea, tutaelekeza nguvu zetu kwenye ushirikiano na nchi za SADC!

Mbali ya kauli hiyo tata, watawala wanatupa matumaini mengine dhaifu kwamba eti hata kama reli hiyo mpya inayounganisha Rwanda na Uganda na bandari ya Mombasa itajengwa, bado bandari yetu ya Dar es Salaam itaendelea kuimarika kimapato kwa kusafirisha mizigo ya nchi za DR Congo na Zambia.
Lakini wengi wetu tunajua kuwa huo siyo ukweli wote; maana hata Zambia nayo imeshaanza mipango ya kuitosa bandari yetu ya Dar es salaam kwa kuanza kuwekeza vya kutosha katika miundombinu ya reli kuelekea Namibia na Afrika Kusini, na pia inakarabati barabara inayoelekea Beira, Msumbiji. Lengo likiwa ni kutumia njia hizo kusafirisha bidhaa zake, na hivyo kuachana na bandari yetu ya Dar – hatua ambayo pia itaidhoofisha TAZARA.

Ni kwa kuzingatia yote hayo sioni mantiki ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kung'ang'ania kujenga bandari mpya ya Bagamoyo kwa mkopo kutoka China; hata kama tayari wameshatia saini mkataba (tata na siri) kwa ajili ya ujenzi huo. Ni busara akaachana na mpango huo kwa sasa.
Kama upanuzi wa bandari ya Mombasa na ujenzi wa reli mpya itakayounganisha Rwanda, Uganda na Kenya tayari imeiweka bandari yetu ya Dar katika hatari kubwa na ya kweli ya kupoteza soko la nchi hizo na pengine Burundi na Sudan Kusini, kuna lojiki gani kwa sasa kuendelea na mpango wa kujenga bandari mpya ya Bagamoyo?

Kama tayari Zambia nayo inaboresha miundombinu yake ili ipitishie bidhaa zake katika bandari za Beira (Msumbiji), Durban (Afrika Kusini) na Walvis Bay (Namibia), kuna lojiki gani kwa Tanzania kujenga bandari mpya ya Bagamoyo karibu mno na bandari ya Dar ambayo inaboreshwa iwe ya kisasa zaidi?

Bandari hiyo mpya ya Bagamoyo itahudumia mizigo ya nchi gani wakati tayari tunakimbiwa karibu na nchi zote za Afrika Mashariki, Kati na Kusini?

Nauliza hivyo; maana lojiki ya mwanzo ya kujenga bandari mpya Bagamoyo ilikuwa ni kuipunguzia shinikizo bandari ya Dar es Salaam, lakini sasa shinikizo hilo halitakuwepo; kwa sababu wenzetu wameshachagua bandari nyingine za kupitishia mizigo yao.
Nionavyo, serikali yetu inapaswa kuyasoma maandiko ukutani, na kuachana kwa sasa na mpango huo wa kujenga bandari mpya ya Bagamoyo ambayo itaishia tu kuwa ‘white elephant' .
Badala ya kujenga bandari mpya ya Bagamoyo, ni heri Serikali ya Kikwete ikatumia hizo dola za Kimarekani bilioni 10 za ujenzi huo, kuboresha bandari za Tanga na Mtwara kwa kiwango kikubwa zaidi, na pia kutumia sehemu nyingine ya fedha hizo kuboresha kwa kiwango kikubwa zaidi Reli ya Kati na ya TAZARA.

Wanadai kuwa bandari hiyo ya Bagamoyo itakayojengwa na Wachina kwa mkopo itakuwa ndiyo bandari kubwa Afrika kuliko zote Kusini mwa Jangwa la Sahara, lakini nionavyo mimi, ukubwa wa eneo na aina ya vifaa vya kisasa vitakavyowekwa katika bandari hiyo, si hoja kuu.

Hoja kuu ni wingi wa mizigo itakayohudumiwa na bandari hiyo au wingi wa nchi zitakazoitumia kupitisha mizigo yao. Unaweza ukawa na li-bandari likubwa lakini kwa wiki likapokea meli mbili tu! Kwa hiyo, saizi ni hoja lakini si hoja kuu. Hoja kuu ni wingi wa mizigo – wingi wa meli zitakazotia nanga bandarini hapo!

Sasa, kama tayari tunaendelea kuboresha bandari ya Dar es Salaam, na huko tuendako tutakimbiwa na wateja wetu hao wa siku nyingi - Uganda, Rwanda, Zambia nk, hiyo bandari ya Bagamoyo itapata wapi mizigo mingi kuhalalisha hadhi yake hiyo kubwa ya kimataifa?
Kwa maneno mengine, hofu yangu kubwa ni kwamba bandari hiyo itaishia tu kuwa ‘white elephant' nyingine nchini kama ilivyo TAZARA hivi sasa.

Tazara ni reli ndefu inayounganisha mataifa mawili na ilikuwa iwe mfano Afrika nzima, lakini kwa miaka mingi imebakia kuwa ‘white elephant'. Je, si kweli kwamba kung'ang'ania kujenga bandari hiyo mpya ya Bagamoyo ni sawa na kuongeza idadi ya miradi ambayo ni ‘white elephants' katika nchi yetu?

Ni kwa kuzingatia yote hayo, binafsi, naamini kuwa ni busara kwa serikali yetu kuingia katika mazungumzo mapya na Serikali ya China ili kukubaliana kuachana na mradi huo wa Bagamoyo, na badala yake mapesa ya mkopo huo yaelekezwe kwenye miradi mingine ya kuboresha miundombinu yetu mingine niliyoitaja; hususan uboreshaji zaidi wa bandari ya Dar na Reli ya Kati.
Na kwa kasi inayoonyeshwa na majirani zetu hivi sasa, hilo la serikali kuisuka upya Reli ya Kati na kuzidi kuboresha huduma katika bandari ya Dar es Salaam, lazima lifanyike kwa haraka; vinginevyo tutakimbiwa pia na DR Congo ambayo haina sababu yoyote (hata ya kisiasa) kupitishia bidhaa zake Mombasa.

Nihitimishe safu yangu kwa kusisitiza tena kwamba bandari yetu ya Dar es Salaam itapitia kipindi kigumu mno kimapato kutokana na ushindani itakaopata kutoka bandari za Mombasa na Malindi (Kenya), Beira (Msumbiji), Durban (Afrika Kusini) na hata Walvis Bay ya Namibia.

Ni dhahiri kwamba watawala wasipozinduka na kuongeza kasi ya kuiboresha zaidi bandari ya Dar, miaka si mingi ijayo inaweza ikapoteza asilimia 60 ya mapato yake, na hivyo kujisogeza katika hatari ya kupatwa na masahibu yaliyoikumba TAZARA ambayo baada ya kupigwa vita mno na matajiri nchini wenye malori makubwa yanayosafirisha mafuta na bidhaa nyingine kwenda Zambia na DR Congo, imebakia kuwa ‘white elephant'!
Tafakari.
 
Hiyo miundombinu ingekuwa inajengwa kaskazini watu wangepiga kelele????????

Ni swali tu wadau, nothing personal.
 
Ubongo mgando.

Lumbe nahisi hujauntendea haki huu ubongo, nadhani tunapaswa tuuite ubongo mgandomgando. Yaani hivi vituko vingine jamani mbona soni? Kwanini tusiborehe hii air strip ya Dar? Hili linanikumbusha zile nyumba za NHC Chalinze, nimepita juzi zimeanza kuwa magofu. Hivi ili hii nchi inendelee yote inabidi kila mtu awe rais ili aendeleze kwake? That means tunahitaji miaka milioni 40 ili tuendeleee wandugu hii mbona noma?
 
Lakini jamani tutazame upande mwingine wa Shilingi. Hii miradi yote imefanyiwa feasibility study na kuonekanaa inafaa na italeta tija. Sasa ni sawa kusema hao wataalam hawana uwezo wa kutosha?
Sidhani kama Rais akishauriwa na wataalam kwamba mradi haufai yeye akaendelea nao kwa sababu za kisiasa ama sivyo itakuwa yale ya "Alex stewwart" ya viongozi waliopita.
Mbona barabara na kiwanja cha ndege kitajengwa Serengeti?
Tujaribu kwenda ndani zaidi katika uchambuzi kabla ya kutoa hoja.
 
Kuna mada fulani tulikuwa tukijadili kipindi fulani hapa jamvini, nikajaribu kuhoji ni criteria gani zinatumika kuamua miradi ya maendeleo, hususan ile inayokula ela nyingi? Je kuna masterplan?? Kwa sababu inaonekana kama mwanasiasa mwenye nguvu ndiye anaallocate miradi na si vinginevo, (lobbying), wengi kwene mada ile (akiwemo mbunge kijana 'machachari') wakasema ohh lobbying ipo hata US na Europe, mie nikakaa kimya huku nikisema kimoyomoyo 'Eeh Kumbe TWAFWA !! '.

Walakini punde si punde kwene thread hiihii watu walewale akina Sikonge watakuja hapa kupinga huu mradi wa JK...
 
HATUA ya serikali kuelekeza miradi mikubwa zaidi ya sita ikiwemo ujenzi wa bandari na uwanja wa ndege wa kimatiafa wilayani Bagamoyo, alikozaliwa Rais Jakaya Kikwete imepingwa na wapinzani wakisema uamuzi huo ni ufujaji wa fedha za walipa kodi.

Mjadala huo umeibuka wakati serikali imeshaanza mkakati wa kutekeleza azma ya kuigeuza Bagamoyo kuwa kitovu kikuu cha biashara na uchumi nchini kwa kujenga miradi mikubwa mbalimbali wilayani humo ikiwemo bandari, uwanja wa ndege, Chuo Kikuu, Soko la Kimataifa, barabara kuu kwenda mikoa ya Kanda ya Kaskazini, kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na viwanda mbalimbali.

Juni 25, mwaka huu Rais Kikwete, alizindua eneo la uwekezaji lenye ukubwa wa ekari 300 ambapo wawekezaji wa Kampuni ya Kamal kutoka nchini India wameanza kutekeleza mradi wa kujenga viwanda na maduka wenye thamani ya Sh400 bilioni katika eneo Zinga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Kufuatia utekelezaji huo kwa nyakati tofauti wapinzani walisema mpango huo umeibuka bila kuainishwa popote ikiwemo katika Dira ya Taifa ya Maendeleo (Visioni 2020/25).

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed alikosoa mradi huo akisema: "Ni jambo baya zaidi kuanzisha miradi mipya huku ya zamani ikifa. Mpango huo wa serikali ni mbaya, 'ni missallocation' (mgawanyo mbaya) ya miradi. Huwezi kuacha uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam ukiwa haina ufanisi kwa kutosha, ukajenga uwanja mwingine mkubwa Bagamoyo".

Hamad aliongeza: "Tunachojua miradi kama hiyo ilitakiwa kuonyeshwa katika Dira ya Maendeleo ya 2020/25 na Mkakati wa Mkukuta, lakini hiyo haimo humo. Kibaya zaidi bajeti yetu inategemea wafadhili".

Hamad Rashid alidai kuwa serikali imeshindwa kutumia msaada wa fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya kuboresha utawala bora na mfumo wa mahakama badala yake ikatumia asilimia 25 tu wakati miundombimu ya Idara ya Mahakama inahitaji kuboreshwa.

"Serikali ingeweka mkazo kwa miradi iliyopo, huwezi kujenga bandari Bagamoyo wakati ya Dar utendaji wake ni mbovu na bandari za Tanga, Mtwara zinakufa. Huwezi kujenga chuo kikuu kama cha Udom Bagamoyo na kuacha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinakufa, hili ni tatizo", alisema Hamad.

Kauli hiyo ya Hamad inakuja wakati kuna taarifa kwamba, mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege unatarajiwa kuanza wiki ijayo huku ule wa bandari ukitarajiwa kuanza mwezi mmoja ujao.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili, kuhusu miradi hiyo jumamosi iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Magessa Mulongo alisema ujenzi wa uwanja wa ndege ulitarajiwa kuanza wiki hii na bandari mwezi Julai.

"Vipo vinafanyika, kwa ujumla mambo yanakwenda vizuri. Hatua za awali za uwanja wa ndege wa kimataifa tunatarajia kuanza wiki ijayo (wiki hii), bandari mwezi ujao (Julai)," alisema Magessa.

Alisema kuwa tayari kiwanja cha kujenga Chuo Kikuu kimepatikana eneo la Msakese na kwamba ujenzi wa barabara kati ya Saadani na Tanga upo mbioni.

Naye Mwenyekiti wa NCRR-Mageuzi James Mbatia, alikosoa miradi hiyo akisema ni kupoteza fedha za walipa kodi na kuonya kuwa Watanzania wasifanywe wajinga ndani ya nchi yao.

Mbatia alifafanua kuwa kujengwa uwanja wa ndege na bandari nyingine Bagamoyo umbali wa kilometa 65 kutoka Dar es Salaam ni kuchezea akili za Watanzania na kwamba, miradi hiyo inakofanywa kwa malengo ya kisiasa ya muda mfupi bila kuangalia mbali kwa manufaa ya taifa.

"Hii ni 'wastage' (matumizi mabaya) ya fedha za walipa kodi. Hapa serikali inachezea akili za Watanzania. Kujenga bandari Bagamoyo kilometa 65 toka Dar ni akili ya wapi?" Alihoji Mbatia.

Mbatia ambaye alihitimu hivi karibuni taaluma ya bandari nchini Ujerumani, alisema serikali imepanga kufanya hayo huku ikishindwa kutumia ukanda wa bahari wenye eneo la kilometa 1,424 na kwamba, bandari ya Dar es Salaam haimo hata miongoni mwa bandari 100 bora duniani.

" Tufikiri chanya, tusifanye kienyeji na tusifanye mambo ya kitaalam kwa malengo ya kisiasa, tuache ubabaishaji," alisema.

Mwenyekiti huyo wa NCCR alisisitiza kuwa jambo muhimu kwa serikali ni kuimarisha na kuboresha utendaji wa viwanja vya ndege na bandari zilizopo, pamoja na kujenga bandari kavu eneo la Kibaha ili kusaidia ufanisi kwenye badari ya Dar es Salaam.

Uamuzi wa Rais Kikwete kujenga miraadi hiyo mikubwa katika mkoa na wilaya aliyotoka ni tofauti na ilivyokuwa kwa marais wa Tanzania waliomtangulia.

Katika uongozi wake wa awamu ya kwanza mbali na kutawala kwa miaka 25, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hakuwahi kujenga hata barabara ya lami katika wilaya aliyotoka (Musoma Vijijini).

Hata rais awamu ya tatu Benjamin Mkapa kwa miaka kumi ya madaraka yake, hakuweka mradi wowote mkubwa mkoa au katika wilaya aliyotoka.

mwisho

La uwanja wa ndege halina shida.
Bandari hapa ndo penye utata mkubwa,kwani katika best ports in the world Mtwara is among them,ila tunatumia theluthi moja tu ya eneo katika bandari hiyo.
Hiivyo ningeona wamefanza la maana kama wangeenda kuiboresha ili tule vichwa kwa Malawi Zambia na hat Congo pia.
 
Mi sitoki huko Bwagamoyo lakini nadhani hii miradi ni mizuri na inastahili kujengwa. Bandari ya Mtwara imeshaanza kukua kutokana na uchimbaji wa mafuta na gesi. Bandari ya Dar iko eneo baya na sidhani kama inaweza kupanuliwa zaidi. Uwanja wa ndege wa Dar uko eneo baya sidhani kama unaweza kupanuliwa sana. Naungana na mkuu mmoja aliesema kwamba hii miradi ingejengwa kaskazini watu wengeona ni sawa...
 
Uwanja wa ndege mpya ulishatafutiwa eneo zamani kabla muungwana hajaingia madarakani. Eneo lilishatengwa wilaya ya Mkuranga, inakuwaje ahamishie Bagamoyo? kwao for that matter! sasa huu ni ulimbukeni. Jamani Nyerere angetaka kupeleka vyote Musoma nchi ingekuwaje? Muraaa, ri uwanja riko kwetu muraa... Maslahi ya taifa yaangaliwe, huo sasa ni ubinafsi...watu wataanza kuchagua kiongozi kikanda ili miradi iletwe nyumbani. Hata huo Bwagamoyo internattional Airport itahamishwa na kupelekwa BK...oooh...mmh Kamachumu International Airport.....awamu nyingine kuleee Tuykuyu.....awamu nyingine kuleee Zenj...Kibandamaiti International Airport. Watanzania tuige mwalimu alivyo allocate rersources.
 
Niliwahi kuongelea suala la Bagamoyo kupendelewa kipindi cha Muungwana baadhi ya wanajamvi walinipinga sana lakini leo wamebaini nilikuwa sahihi.

kuendeleza eneo analotoka rais au mkuu wa nchi imekuwa ni sehemu ya tabia ya watawala wengi wa nchi za Afrika.Rais wa zamani wa Zaire [Congo Kinshasa] hakubaki nyuma kufanya upuuzi wa kujenga mji alikozaliwa Gbadolite uwanja wa ndege wa kimataifa,ikulu na mambo mengi yaliyotafuana hazina ya nchi ya Zaire wakati huo,Rais wa zamani wa kenya mzee D Arap Moi alitenda dhambi ile ile ya kutumia vibaya hazina ya kenya kujenga alikozaliwa.Kufuru nyingine ilifanywa na Rais wa zamani wa Ivory Coast Bwana Felex H Boigny alitumia vibaya hazina ya taifa lake kujenge kanisa kubwa la Yamoussoukro,uwanja wa ndege,Reli,Barabara za kisasa na nk.

Inashangaza kidogo kuona Tanzania iliyopata uhuru wake mwaka 1961 bado inaongozwa na kiongozi mwenye mawazo ya akina Felex Boigny,Daniel A Moi,Omari Bongo na Mobutu Seseseko.Mbaya zaidi ni kuona mfumo wetu wa siasa unaruhusu haya kutokea.Miradi yote inayokimbizwa Bwagamoyo ina hatari ya kufa wakati rais wa sasa atakapoondoka madarakani.

Mchezo huu mchafu ukiachiwa kuendelea kushamiri ipo hatari nyingine itakayoinyemelea Tanzania siku za usoni.Tutakuwa tunachagua viongozi wataokuwa wanatazama zaidi sehemu walipo toka kwanza badala ya kuitazama Tanzania.
 
By the way itawasaidia wananchi wote wa Tanzania...!!! kama ikifanikiwa hio Miradi...!!!
 
Hii ni zawadi ya JK kwa wakwere wenzake, Mkapa yeye aliwapatia daraja la mto rufiji na barabara, hapa ndipo umuhimu wa kuwa serikali ya majimbo unapokuja. Yaani rasilimali zinatoka mikoa mingine zinaenda kuendeleza mikoa mingine. Kama mimi ningekuwa ni mpiga kura pekee wa Tanzania basi ningemwambia JK aende akaombe kura Bagamoyo, si ndiko anakotekeleza ahadi ya maisha bora kwa kila Mbagamoyo!
 
Binafsi sioni tatizo kabisa kujengwa kwa bandari Bagamoyo kwa sababu ya pale Dar imewashinda, nadhani wote tunakumbuka pia jinsi watu wanavyoteseka na foleni barabara ya Mandela kwa misemitrela kutoka au kwenda bandarini.

Na pia mizigo inayoenda sehemu kama Rwanda, Burundi na sehemu ya DRC kutumia bandari Mtwara ni mbali sana, angalieni Tanzania map. I think this is very clear.

Ila hili la uwanja wa ndege I say NO please. Waache tu ukajengwe huko mkuranga unless watoe sababu za kueleweka.

Lakini pia nahisi mikoa ya pwani siku zote huwa wanalalamika kuwa imeachwa nyuma kimaendeleo kwa makusudi kwani ndo ilikuwa ya kwanza kabisa kupata maendeleo lakini viongozi waungwana walipokuja wakaichinjilia baharini ila damu yao ilionekana labda ndo maana Muungwana aliopo madarakani ameamua angalau kuikumbuka kidogo.

Kwa wale mliofika Pwani Tanga na kadhalika nimashahidi, mfano mkoa wa Tanga umepangika vizuri sana lakini maskini watu wa hapo wamechoka ile mbaya, mida yote utaona vibaraka shehe vingi kichwani wakiendesha baiskeli huku uchumi waliokuwa wanajivunia kama vile viwanda na dandari vikiwa either vimekufa or viko taabani ICU.

ILa mikoa ya kati na magharibi ndo kabisa haijapata muungwana labda tusubiri mzee Malecela achukue ofisi 2015 labda wataweza ona mwezi na wao pia.
 
Mimi sina problem na kujengwa miradi hii bwagamoyo, my concern ni why wamewalipa na kuwahamisha watu kipawa while walikua na mpango wa kujenga kaluwanja bwagamoyo
 
1. Barabara through Bagamoyo kutokea msata ni muhimu sana kwani itapunguza fujo kwenye barabara ya Morogoro, watu wa kazkazini watapita kiurahisi badala ya kuzunguka chalinze. big up

2. Bandari ya Bagamoyo ni muhimu sana kwani bandari ya dar haiwezi kupanuliwa zaidi na si natural habour ni ya kuchimba tu. na itaserve kama inavyoserve bandari ya dar. big up

3. Kuhusu uwanja wa ndege sina la kusema

4. Chuo kikuu. big up

tatizo ninaloliona ni kuwa wale wenyeji watanufaika vipi na vitega uchumi hivi? waliowengi ni watu wa hali ya chini hasa kielimu. otherwise Bagamoyo ni eneo ambalo litawanufaisha wengi ni kama dar es salaam hainufaishi wazalamo pekee bali nchi nzima. hebu nenda pale uone profile za watu wanaofaza kazi/kufanya biashara pale utajua
 
hilo la bandari ni upuuzi mtupu, Bagamoyo hipo katikati ya bandari mbili ya Tanzga na Dar, sasa unaweka bandari nyingine ya nini katikakti, cha muhimu ilikuwa ni kuipanua na kuiboresha ile ya Tanga tu
 
Hakuna sababu yoyote ya maana bali ni ulimbukeni wa Jakaya Kikwete tu.
 
Back
Top Bottom