Ujasusi - Umoja namba 97

singanojr

JF-Expert Member
Sep 24, 2020
1,454
8,120
UMOJA NAMBA TISINI NA SABA
KAULI YA MWISHO YA RAISI
KABLA YA KIFO CHAKE
MWANDISHI: SINGANOJR
GENRE: FICTION (KUBUNI )

........................….........................................

UTANGULIZI
.....................................................
Damiani mhitimu wa chuo kikuu cha uhasibu , anahitimu masomo yake na kurudi kijijini kwao kwa ajili ya kusubiria upepo wa ajira lakini katika hali ya kutokutegemea mama yake kipenzi anapigwa risasi mbili za kifuani na kufa hapo hapo na hio inatokana na kumpatia msaada mwanaume ambae hamfahamu mwenye asili ya ulaya (mzungu ) ambae na yeye alikuwa kwenye hatua ya mwisho ya kupoteza uhai wake kwani alikuwa na jeraha la risasi tumboni ,lakini mzungu huyo kabla ya kupoteza maisha anamkabidhi damiani nyaraka bila kumpa maelekezo ya aina yoyote ile .

Damiani anajikuta anajenga chuki na kisasi kwa watu waliohusika na mauaji ya mama yake , anajiapiza kuwatafuta mahali popote pale na kulipiza kisasi , katika harakati za kuwatafuta wabaya wake anajikuta akifahamu siri nzito iliokuwa nyuma ya kifo cha ghafla cha raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania , anapata waraka ulioachwa na raisi huyo uliopewa jina la KAULI YA MWISHO YA RAIS KABLA YA KIFO CHAKE .
JE UNAFIKIRI ATAFANIKIWA KULIPIZA KISASI CHAKE ?
JE NI KAULI GANI YA MWISHO ALIO ACHA MHESHIMIWA RAISII KABLA YA KIFO CHAKE ?.
.
>>≥>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
SEHEMU YA KWANZA
Damiani ni kijana wa miaka ishirini na mbili mhitimu wa chuo kikuu cha TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA) akiwa amechukua kozi ya Finance and accounting in public sector(kozi inayohusu maswala ya uhasibu) , mara baada ya damiani kumaliza masomo yake hakutaka kubaki ndani ya jiji la dar es salaam , kwani hakuwa na kazi maalumu ambayo ingemuwezesha kujiingizia kipato ndani ya jiji hilo , pia maisha ndani ya jiji hilo yalikuwa ni ghali sana na yalikuwa yakihitaji pesa ili kuweza kuishi .

Hivyo mara baada tu ya kumaliza masomo yake aliamua kurudi nyumbni kwao kijijini mkoani Tanga kwa ajili ya kusikilizia upepo wa ajira kwani mwaka ambao alikuwa amemaliza haikuwa kama miaka ya nyuma kwamba ukimaliza tu unasubiria matokeo na kupata ajira , kinyume chake ni kwamba utasubiria matokeo yatoke na kuomba ajira kwa makampuni ambayo yatakuwa na uhitaji ama serikari pale itakapo tangaza nafasi za ajira na kuomba , na kwakuwa kipindi hicho kulikuwa na wimbi kubwa la vijana ambao walikuwa ni wahitimu na hawakuwa na ajira mtaani hivyo ilikuwa ni ngumu sana kupata ajira , ilikuwa ni kama kubahatisha tu pale nafasi zinapo toka kwani wengi waombaji wana sifa zinazofanana .

Mkuzi ndio kijijini kwa kijana damiani , kijiji hiki kilikuwa ndani ya wilaya lushoto kilomita kadhaa kutoka lushoto mjini , yaani kama utasafiri kwa gari ni muda wa dakika therathini mpaka arobaimi kufika ndani ya kijiji hichi , ni moja ya vijiji ambavyo vilikuwa vimezungukwa na misitu na kuwa na mazingira ya kuvutia sana , na yalikuwa ni moja ya mazingira ambayo watalii wengi wa mataifa ya nje na hata watalii wa ndani pia walikuwa wakipenda kutembelea na hio yote ni kutokana na hali yake ya hewa ilivyokuwa safi na ya kuvutia .

Basi kijana damiani ndani ya kijiji cha mkuzi ndio alikulia na kujipatia elimu yake ya msingi na sekondary .

Damiani alikuwa ni kijana mpole mcheshi mrefu maji ya kunde mwenye sura yake ya kuchongoka lakini ilioumbwa vizuri , alikuwa ni moja ya vijana walio kuwa na miili mikubwa ya wastani , Damiani alikuwa akiishi na mama yake tu kwani baba yake alikuwa amekwisha kufariki miaka mingi nyuma kipindi akiwa tu na umri wa miaka kumi .
Kurudi kwa damiani kijijini baada ya kumaliza masomo ilikuwa ni moja ya furaha kubwa sana kwa mama yake kumuona mwanae kurudi ndani ya kijiji hicho , kwani mama huyo alikuwa akimpenda sana mwanae .

" karibu sana mwanangu " mama alifurahia sana kwa mwanae kumaliza masomo yake ya ngazi ya juu , na kujihisi kuwa mwanamke aliefanikiwa kulea kwani watoto wengi ndani ya kijiji hicho hawakufanikiwa kufika ngazi ya juu ya kielimu kama ilivyokuwa kwa damiani .

" Asante mama , hatimae nimemaliza chuo na nimerudi rasmi " aliongea damiani huku akiachia tabasamu huku nje watoto wengi walikuwa wakimwangalia na kumshangaa , hio ilikuwa ni kawaida sana kwa vijiji kushangaa watu walio tokea mjini na hata kwa wageni pia .

Basi damiani alikaribishwa vizuri na mama yake katika nyumba yao hio ya vyumba vitatu ilio ezekwa kwa samora , na kwakuwa damiani alikuwa na chumba chake tokea akiwa shuleni ndiko mama yake alipeleka begi lake na kukifanyia usafi .

Maisha ya kijana damiani yanaanza rasmi ndani ya kijiji cha mkuzi , licha ya damiani kuwepo ndani ya kijiji hicho lakini alikuwa na mipango mikubwa sana ya maisha yake hapo mbeleni , kwani alihitaji kuja kuwa mfanya biashara mkubwa sana katika maisha yake na hio ilikuwa ndio moja ya ndoto yake kubwa, japo alikuwa amesoma na alikuwa akitarajia kuwajiriwa lakini ajira kwake haikuwa kipaumbele , ila kipaumbele kwake ikikuwa nikupata mtaji utakoa mwezesha kuanzisha biashara , hakika alikuwa na safari ndefu sana na hata kwa yeye pia alilijua hilo na hivyo kwa umri aliokuwa nao hakuwa na sababu ya kukatishwa tamaa na mazingira aliokuwemo na aliokulia , kwani alichokuwa akikiamiani katika maisha yake ni juu ya uchapaji kazi kwa bidiii na kutokukata tamaa na kuwa na malengo ndio nguzo kubwa sana ya kuja kufanikiwa , hakutaka kabisa kukatishwa tamaa na hali ya maisha yao ya umasikini yaliopo hapo nyumbani , ila aliamini katika mawazo chanya tu .
Basi hatimae wiki ,mwezi na hata miezi ilikatika na matokeo yake yalikuwa yamekwisha kutoka na akiwa amefaulu kwa ufaulu wa daraja la kwanza , kwake na kwa mama yake ilikuwa ni furaha na faraja kubwa sana , kwani aliamini kupitia ufaululu mkubwa basi angeweza kumrahisishia kupata kazi kwa wepesi zaidi .
Hakutaka kusafiri mpaka dar es salaam kwa ajili ya kuomba kazi ilihali kulikuwa na njia rahisi , alichokifanya yeye ni kutuma maombi kwa kila kampuni ambayo iljkuwa ikitangaza nafasi za ajira kwa njia ya mtandao .

Mwezi wa kwanza uliisha kijana damiani akiwa amekosa kabisa uelekeo wa ajira kwani ni makampuni zaidi ya matatu ambayo alikuwa ameomba kwa ajili ya kupata ajira lakini amekosa hata wito wa interview( mahojiano ya kiufanisi ) , zikiwa zimepita siku kadhaa za kijana damiani kukata tamaa hatimae kwenye moja ya kampuni ambayo haikuwa imetoa majibu ilirudisha jibu kwa kijana damiani kwa ajili ya kuhudhuria interview .
ilikuwa ji moja ya kampuni ilio kuwa ikipatikana ndani ya jiji la dar es salaam ,kampuni moja ya usafirishaji iliokuwa na makao yake makuu ndani ya posta , kwake damiani alifurahia kwani aliona tumaini la kupata ajira linaridhisha zaidi , alimwambia mama yake juu ya taarifa hio na mama yake pia alifurahia na kumpa baraka zote mwanae kwa ajili ya kuhudhuria interview hio.

Ilikuwa ni siku ya jumatatu ndio siku ambayo kijana damiani alikuwa ndani ya basi akielekea jijini dar kwa ajili ya kuhudhiria interview ,alifanya maombi juu ya safari yake hio na kusudio lake analoliendea kulifanyia kazi.
Kutoka lushoto mpaka ndani ya jiji la dar ni umbali wa masaa sita mpaka saba , hivyo damiani alikuja kufika ndani ya jiji hilo kwenye muda wa saa nane kamili mchana ,siku hio alipanga akifika ndani ya jiji hilo kwakuwa hakuwa na ndugu wa kufikia , alipanga kwenda kwa rafiki yake mmoja aliekuwa amemuacha ndani ya chuo akiendelea na masomo kwa ajili ya kumuhifadhi mpaka siku inayofuata afanye interview na kisha ageuze kurudi nyumbani .
Basi baada tu ya kushuka ndani ya basi akijisogeza mpaka kwenye daladala zinazoelekea mbagala na kisha alipanda huku malengo yake aje ashukie mtongani kwa azizi ally kwani hapo ndio rafiki yake huyo alipokuwa akipatikana kwa kuishi , barabara haikuwa na foleni sana hivyo hawakuchukua masaa mengi kufika sehemu aliokuwa amekusudia .

Mara baada tu ya kushushwa hatimae alinyoosha moja kwa moja upande wa kushoto wa barabara , huku akipita vichochoro viwili vitatu na kuja kutokelezea mbele ya nyumba moja kubwa iliokuwa na ukuta, Hatimae alisimama nje ya geti la nyumba hio huku nikama ni mtu aliekuwa akijishauri agonge ama asigonge , ila kwakuwa kilichomleta hapo ni kuonana na rafiki yake na rafiki yake alikuwa akiishi ndani ya nyumba hio basi hakuwa na budi ya kugonga geti hilo.

Haikuchukua muda mrefu hatimae alikuwa amefunguliwa na msichana mmoja aliekuwa amejifunga khanga moja , na alionekana alikuwa akifua kwani alikuwa na mapovu mikononi .

" Karibu " sauti hio nyororo ilimkaribisha ndani huku.dada huyo akitangulia mbele na kumuacha kijana damiani kumsanifu mdada huyo kwa nyuma , alikuwa ni mlimbwende kweli aliekuwa amejaliwa umbo zuri haswa la kumvutia kila mwanaume atakae mtia machoni , alikuwa mrefu wa wastani mwenye rangi yake ya chocolate , alibarikiwa uso wa duara na kwa tathimini za haraka haraka mdada huyo alionekana umri wake haukuwa si chini ya miaka ishirini kwenda juu.
" nimemkuta elvisi ??"
" katoka sema anakuja muda si mrefu , wewe ndio Damiani ??"
" Ndio ni mimi "
" " Okey ! Alinipa maelekezo yako kwamba ukifika nikukaribishe ndani " aliongea msichana huyo huku akimkaribisha damiani ndani kwani muda wote huo alikuwa amesimama , Damiani alijua lazima huyo bidada atakuwa hawara(mwanamke anaeishi na mwanaume pasipo kuolewa au mpenzi ) wake elvis maana alimjua mngoni huyo songea kwa kupenda warembo hakuwa nyuma na ndio maana kabla ya kutoka nyumbani alimtaarifu kuwa atakuja kulala kwake .

Basi bidada huyo alimuongoza damiani ndani ya nyumba hio iliokuwa imepakwa rangi nyeupe mpaka kwenye chumba cha katikati upande kushoto na kisha alimkaribisha ndani , kilikuwa ni chumba kimoja kikubwa saizi ya kati kilichokuwa kimejaa makorokocho mengi , Damiani alikuwa akikijua chumba hichi sana kwani hata kwa baadhi ya vitu hivyo villkuwa vyake na ni baada ya yeye kumaliza masomo alimuuzia rafiki yake huyo .
Basi baada ya kukaribishwa dada yule alitoka nje na kuendelea na shughuri yake ya ufuaji huku akimwacha damiani akimsubiri rafiki yake , na haikuchukuwa hata dakika isbirini rafiki yake elvisi aliingia ndani ya nyumba hio , elvisi alifurahia sana kumuona damiani na hata kwa damiani ilikuwa ni hivyo hivyo , wote walifurahia kuonana kwa mara nyingine .

" karibu sana HB asietaka warembo " aliongea elvis akionesha kumtania mwenzie na kwa damiani kwakuwa alikuwa ashamzoea rafiki yake huyo kwa matani basi na yeye alicheka .

" mzee wa totozi , naona shemeji yangu wa awamu hii ni shida "
" Yaani acha tu mzee toto la toto na isitoshe limedata na ndio limenifanya nihangaike siku ya leo "
" Unahangaishwa na nini sasa?? "
" hahaha lazima kuhangaika , unajua jana ulivyonicheki unakuja ilikuwa ghafra sana na sikutaka kukwambia naishi na mtoto wa kike, kwa hio unavyoniona hapa kuna msela nimetoka kumpanga ili ukale mbonji kwake ukamilishe mambo yako maana hapa sikuwa na jinsi "
" Daah ! hapo ndio maana nakukubali mshikaji wangu "
" hahaha .. usijali mzee si unajua hata wewe umenisaidia mara kibao , hata mavitu haya ni kama ulinipa tu kutokana na bei ile "
Basi damiani walichukuana na rafiki yake na kutoka eneo hilo kuelekea barabarani na kupanda magari ya kuelekea Rangi tatu , walivyo fika mbagala zakhemu walishuka na kuchukua upande wa kushoto barabara , umbali wa mita kadhaa hatimae waliingia chochoro ambayo walikuja kuibukia mbele mtaa mwingine , na wakaja kutokea mbele ya kanisa la KKKT na hapo walipinda kushoto tena na kukuta nyumba moja kubwa iliokuwa na geti na kwa nje ilisomeka kwa maandishi ya lodge , elvis alisukuma mlango na kisha aliingia ndani , kwa damiani yeye alikuwa akifatisha tu kuona mwisho wake kwani kuna hisia zilizokuwa zikimwambia kaletwa lodge

" Oya mshikaji anakaa hapa , sio lodge hapa tena japo ilikuwa lodge , mwenye nyumba kaamua kuifanya nyumba ya kupangisha " aliongea elvis na kumfanya Damiani aelewe , walipita kwenye vyumba kadhaa na hatimae walisimama nje ya mlango na elvisi aligonga na nusu dakika mlango ilifunguliwa na jamaa mmoja wa makamo mfupi mwenye mwili mkubwa wa kibonge .

" Karibuni "
Waliingia ndani ya chumba hicho , kilikuwa ni chumba kikubwa na kizuri sana , na pia hata kitanda na samani(furniture) zilizokuwemo humo ndani zilionesha jamaa anaeishi humo ndani hakuwa mnyonge kipesa .

" oyaa huyu ni joshua rafiki yangu sana mwaka wa kwanza hivyo ndio utachili hapa kwake mpaka utakapo kamilisha mambo yako " aliongea elvis na joshua alimkaribisha Damiani na elvisi aliaga akaondoka .

Basi siku nyingine iliingia ambayo ni siku Damiani alikuwa akielekea mtaa wa posta kwa ajili ya kufanya interview , alikuwa amevaa akapendeza maana kwenye nguo alikuwa nazo na mkopo ulimsaidia sana kipindi akiwa chuo .

Alijisogeza mpaka barabarani ili kusubiria gari ya kwenda stesheni posta apande , ila mara baada ya kufika tu kwenye barabara nje kabisa ya supermarkert iliosomeka kwa jina la Kivoni , ilisimama gari moja aina ya vanguard nyeusi na kioo kilishushwa na akaonekana bwana mmoja wa makamo , makadirio ya miaka 30 kuendelea mweusi alivalia shati jeupe na koti akiwa na miwani , Damiani wakati huo gari hio ikisimama alikuwa akiiangalia na hata jamaa huyo alivyoshusha kioo alikuwa pia akimwangalia , Damiani alijikuta akijishtukia na hio ni mara baada ya jamaa huyo kumuonesha ishara ya kumuita , alijihakikishia kama ndio yeye aliekuwa akiitwa na hapo ndipo alipo piga hatua kulisogelea gari hilo

INAENDELEA HIVI PUNDE ........


SEHEMU YA 02.

INAENDELEA
“Vipi wapi unaelekea ?”. aliuliza mwanaume yule
" Naelekea posta "
" Okey ingia twende , naelekea upande huo , nina baadhi ya maswal nataka nikuulize " aliongea jamaa yule na kumfanya hata damiani ashangae inakuwaje mtu asie mjua awe na maswali ya kuulizwa na yeye ,jambo hilo lilimpa mashaka mengi juu ya mtu huyo .
" fanya haraka , ingia acha uoga asubuhi yote hii unawaza mambo mabaya " aliongea yule jamaa na ni kama alijua ni kitu gani alikuwa akimaanisha na Damiani kwa mashaka mengi alijiingiza kwenye gari hilo na kisha likawashwa na kuondoshwa eneo hilo .
" Unaenda kufanya interview ?" aliuliza yule bwana na kumfanya damiani ashangae Zaidi ni kivipi kajua anaenda kufanya interview .
" usiwe na wasiwasi mimi nimeishi miaka mingi na najua hulka ya vijana wengi hasa wanaoenda kuomba kazi na wewe kwa uvaaji wako unaonekana kabisa unaenda kufanya interview kama sio kuomba kazi .”
" Yeah! naenda kufanya interview " alijibu
" umesomea kozi gani na elimu yako ni kiwango gani ?? "
" Degree of finance and accounting in public sector"
" okey safi na hongera , unapaswa kujiamini tu na maswali ya kawaida sana wanauliza , unaweza ulizwa elfu kumi ina mnyama gani na ukakuta swali lina maksi nyingi "
Aliongea yule bwana huku akiongeza umakini katika barabara hio iliokuwa na magari mengi asubuhi hio .

Hawakuchukua muda mrefu walikuwa posta , na gari ilisimamishwa kwenye jengo la waterfront na Damiani akashuka , huku bado akiwa na dukuduku la maswali mengi kichwani mwake kwa jamaa yule kwa jinsi alivyomwambia wakati wa kumpandisha kwenye gari kwamba alikuwa na maswali ya kumuuliza , lakini cha kushangaza hata hayo maswali yenyewe hakuulizwa , ila hakutaka kufikiria sana na aliona ni labda jamaa huyo hakuwa na nia ya kumuuliza maswali ila alikuwa akitaka tu kumsaidia kwa kumpa lift na kama alivyosema alijua kuwa alikuwa akielekea kwenye interview .

Basi wakati akiwa anatembnea kuelekea upande wa samora alijikuta akikumbuka yale maneno ya kwamba anaweza kuulizwa maswali ya kawaida sana hata elfu kumi ina mnyama gani , na hapo ni kama amekumbuka kitu , alianza kujiuliza elfu kumi ina mnyama gani lakini hakuweza kabisa kupatia alijaribu kuchekescha akili yake ili kupata jibu la elfu kumi ina mnyama gani lakini alijikuta akikosa jibu kabisa , aliinua mkono wake wenye saa na kuona bado alikuwa na muda wa kutosha kabla ya interview kuanza .

Basi kijana damiani alijiamulia kusogelea duka moja lililokuwa na tigo pesa kwa ajili ya kutoa kiasi kidogo cha pesa ambacho kitamsaidia katika mahitaji yake ya siku hio na pia kilichokuwa kingebaki angefanya nauli ya kurudi nyumbani kwao lushoto.
“ kumbe tembo daah ! upuuzi kabisa yaani siku zote naishika hii hela nimeshindwa kujua kuwa mnyama ni tembo haha .. “ aliongea huku akivuka barabara na kutembea hatua chache tu aliona jengo alilokuwa akilitafuta mita kadhaa kwani ndipo kampuni ya usafirishaji aliokuwa akiitafuta na kwenda kufanya interview ndio ilikuwa ikipatikana katika eneo hilo .
Alijikuta akipigwa na mshangao mara baada ya kufika ndani ya eneo hilo maana kulikuwa na watu kibao waliokuwepo ndani ya eneo hilo na wote hao walionekana walikuwa wameitwa kwa jili ya kufanya interview .
“ hapa kweli kuna kupata ajira kweli?? “ alijiongelesha huku akiingia ndani kabisa ya jengo hilo na kwenda mpaka eneo la mapokezi na aliambiwa kuwa utaratibu ni kusubiri kwani interview itaanza muda sio mrefu .

Basi alijiunga na wenzie kwa ajili ya kusubiri na hakutaka kukata tamaa kirahisi kwani alikuwa amejiandaa vya kutosha na siku zote aliamini kwamba kwenye nafasi ya watu kuchaguliwa na wakawa na nafasi sawa basi hakuna kukata tamaa na hata yeye anayo nafassi ya kushinda na kupata ajira hivyo alizidi kujipa moyo na kujiandaa na interview , ni baada ya kama dakika arobaini hivi ndio watu wote waliitwa kwa kuanza interview, ilikuwa ni written interview(mahojiano ya kuandika ) katika nafasi ya finance manager( msimamizi wa fedha ) .


Basi mameneja rasilimali watu waliokuwa wakisimamia interview hio walitoa taratibu na maelekzo ya kila namna na hatimae interview ilianza , ajabu kwa damiani ni kwamba jambo lile aliloambiwa kule na yule mtu aliempa lift likuwa ni vile vile na hata yeye alijikuta akishangaa sana ilikuwaje jamaa yule akajua kwamba ataulizwa swali la kwamba elfu kumi ilikuwa na mnyama gani ilikuwa ajabu ilio jaa bahati .

Basi interview ile ilienda vizuri kwa upande wake huku akiamini kabisa amefanya vizuri na kilichofata hapo ilikuwa ni matokeo tu ya interview hio , japo mtu yule wa asubuhi alikuwa na mashaka nae ila alijikuta akiona kwamba mtu yuke alikuwa kama malaika kwake alietumwa na mungu . .

*****
Upande mwingine ndani ya jengo la LPPF tower lililokuwa likipatioana ndani ya mikocheni sayansi kuna gari moja nyeusi aina ya range rover sport ilisimama asubuhi hio ndani ya eneo la kupark magari na alishuka mwanaume mmoja mwenye umri kati ya miaka hamsini hivi aliekuwa amevalia suti yake nadhifu kabisa iliomkaa vizuri , alikuwa na mwili mkubwa kidogo na alionesha hali yake ya kiafya sio mbaya , alikuwa ametangulizana na bwana mmoja hivi aliekuwa amevalia miwani na bila shaka alikuwa ni mlinzi wake kama sio msaidizi .

Basi alitembea kuingia ndani ya jengo hilo huku mkononi alikiwa ameshikilia miwani yake ya jua na yule msaidizi wake akiwa ameshikilia briefcase nyeusi ,walifatana mpaka kwenye lift na kisha walibofya kitufe cha namba kumi na sita kuashiria ndio floor waliokuwa wakielekea , haikuwachukua muda mrefu walikuwa ndani ya korido ndefu kidogo iliokuwa na mandhari ya kuvutia huku kwa mbele kabisa kulikuwa na maandishi yameandikwa KIMBONA INTERNATIONAL LINK AND COMPANY (KILAC)

Mzee huyo alitembea kwa mwendo wake wa taratibu lakini wenye afya na kufika eneo la mapokezi na alikutana na dada .mmoja alievalia nadhifu kabisa eneo la mapokezi na baada ya kumuona mzee huyo alisimama haraka na kusalimia, alikuwa ni secretary .
" shikamoo boss ,karibu kazini " aliongea dada huyo kwa heshima kubwa sana na mzee huyo aliitika huku akiwa sio mwenye kujali sana na akapita kuelekea ofisi moja iliokuwa ikisomeka jina la mkurugenzi , aliingia ofisini humo na kisha yule mlinzi aliweka ile briefcase juu ya meza

Ni moja ya ofisi iliokuwa ikivutia sana iliokuwa imenakishiwa vyema huku samani zilizokuwemo humo ndani zilionesha kuwa zillikuwa ni za bei ya juu sana lakini bei hio iliendana na ofisi kwani ziliipendezesha kwa ujumla wake .
"okey derick tutaonana baadae na hakikisha unafatilia lile.swala kwa umakini mkubwa maana baadae nina kikao na nataka kuwa kwenye nafasi nzuri kwemye kikao hicho "
" Sawa boss " aliongea kijana huyo kwa sauti ya kikakamavu kabisa na kisha aligeuka na kutoka ndani ya ofisi hio .
Hazikupita dakika kumi simu ilipigwa na ilitoka kwa sekretary na alimjulisha bossi wake huyo kuwa kuna mgeni wake na bwana huyo aliruhusu mgeni huyo kuingia .
" mister kimbona!. "
" Samueli! hahha ..Umefika lini Tanzania? " aliongea mister kimbona kwa bashasha sana huku akimlaki mwanaume huyo aliekuwepo mbele yake , alikuwa ni mwanaume wa saizi yake sio mrefu sana umri ulikuwa ni miaka arobaini hivi kupanda kimakadirio, akiwa amevalia suti yake ya gharama ya rangi ya blue .
" Nimefika juzi mara baada tu ya kupata taarifa za kunifurahisha moyo wangu ".
" hahaha karibu sana , unipe hizo taarifa , huenda na kwangu pia zikawa zakufurahisha .
" wewe ushazisikia sana na kama ni zakufurahisha basi zishakufurahisha mpaka zikachuja .
" hahahahaha... hahahaha... ni kweli kabisa usemayo na najua ni kipi una maanisha hahhaha.. , karibu sana Tanzania kwa mara nyingine kwenye nchi yako .
Basi walionekana kuwa maswahiba wakubwa sana hawa watu kwani walionesha furaha sana kwenye nyuso zao na walionekana kufurahia jambo .
" Nimekuja Tanzania kwa kazi maalumu , naamini unaelewa biashara zetu hizi zilivyoyumba ndani ya utawala wa mwendazake , sasa baada ya kusikia taarifa ya kwamba keshatutangulia mbele za haki , kwangu ilikuwa njema sana na niliona ni wakati mwingine tena wa kufufua biashara zetu .
" ni kweli usemayo , lakini sidhani kama itakuwa ni rahisi na jambo la kufanyika haraka haraka maana linahitaji connection na unajua nchi yetu imeimarika ki ulinzi kwa sasa .
" Ndio hilo nalifahamu fika , na ndio maana nikasema nimekuja kwa kazi hio na mtu ambae naamini atanisaidia kwenye mpango huo ni wewe , we have to establish our destroyed system once again."
"Nimekusikia na ninaelewa shauku na mipango yako , lakini mimi nakusaidiaje katika hilo ?."
" Nafikiri unaelewa mister bruno ndio alikuwa chanzo kwa sysytrm yetu kufa hapa nchini mara baada ya mwendazake kuchukua madaraka "
" Ndio nalielewa fika swala hilo "
"Sasa hapo ndio pa kuanzia "
" Kivipi sam??? "
" come on! Kimbona usiniambie siku hizi umekuwa mlokole kiasi cha kupelekea akili yako kushindwa kung'amua swala dogo kama hilo ."
" haha….you meaan to kill him?? "
" correct , na naamini hilo ni swala unalo liweza sana na lipo ndani ya uwezo wako , naujua upande wako mwingine , na ukiutumia vyema tutafanikiwa katika hili , na nakwambia mtu wa kwanza kupata faida sio mimi tu ni wewe pia maana utakuwa pia kwenye system " aliongea mwanaume huyu anaejulikana kwa jina la samueli kwa lugha yake iliojaa tamathali za nchi za nje .
Bwana kimbona alijikuta akiwaza na kukuna kichwa na akainua uso wake akamwangalia sam usoni na kisha aliachia tabasamu .
"Assume its dome from now on , We are back my friend " aliongea huku akimfanya sam kufurahia sana na kisha walipeana mikono na kutakiana siku njema na kisha wkaagana huku sam akimsisitizia kuwa swala hilo lifanyike mapema .

*******
Katika watu waliotoka na sura zilizojaa tabasamu alikuwa ni kijana Damiani , huku wenzake wengi wakitoka na nyuso za kuonesha kukata tamaa kwa kile walichokutana nacho .
" Daah ! nakutumia kwangu kote pesa eti leo nimeshindwa kung'amua elfu kumi ina mnyama gani , hata hawa HR wenyewe wanazingua " aliongea kijana mmoja aliekuwa na marafiki zake hapo akionesha kulalamika kwa kukutana na swali kama lile kwani lilikuwa ni swali ambalo halikuwa la kawaida na la kutegemea hasa kwa nafasi kama hio ya finance manager (usimamizi wa pesa ).,hakuwa kijana mmoja tu aliekuwa akilalamika ila wengi walionyesha kuchukizwa na aina hio ya swali na kilichowakasirisha ni kwamba maswali yale magumu yaliwekewa maksi chache . .
" Mambo ! " Ilisikika sauti moja nyororo sana ya kuamsha hisia kwenye ngoma za masikio ya Damiani na kumfanya ainuke kwani wakati huo alikuwa ameegamia uzio kuangalia upande wa barabarani magari yaliokuwa yakipita na watu waliokuwa kwenye hekaheka za siku hio .

Alikuwa ni msichana mrembo kweli kweli , alikuwa mrefu saizi ya kati , aliekuwa na rangi flani hivi ambayo kwa haraka haraka ungejua kabisa mlimbwende huyu alikuwa ni mchanganyiko wa mataifa mawili ,kama sio wa muhindi basi ni mzungu na mwafrika , huku baba yake akiwa ni mzungu kamili ama mhindi , alikuwa anavutia kwakweli na hasa tabasamu alilokuwa ameachia usoni mwake lilimfanya vishimo vyake kwenye mashavu vizidi kuupamba uso wake na kumfanya kijana damiani abung'ae .
" poa mambo " alijikuta akiitikia ki uoga uoga
" Naitwa merina wewe je ??"
" Damiani " .
" Ohoo ! Na wewe upo kwenye interview?! "
" Ndio " .
" Hata mimi pia , nafrah kukufahamu Damiani " Aliongea msichana huyo na alionekana kuwa mchangamfu kwani ndio aliekuwa ametawala maongezi hayo .
" by the way how is written ?" aliongea mwanadada huyo kumuuliza swali hilo na kumfanya Damiani atabasamu kidogo na kisha alijibu .
" Nashukuru mungu , ilikuwa safi , and you ??? "
" Me pia " jibu hilo lilimfanya Damiani awaze na kuona kati ya watu waliokuwa wamefanikiwa kujua elfu kumi ina mnyama gani basi hata huyo mlimbwende atakuwa amepatia , sasa swala hilo kidogo lilimnyima raha maana aliona kuwa nafasi yake inakuwa ndogo ya kuchaguliwa ila hakutaka kuonyesha hilo na kukata tamaa ,
" Umetokea chuo gani?"
" Harvard " jibu hilo lilimfanya Damiani ashangae kwani alijua duniani chuo kinachotamkika kwa jina hilo kilikuwa ni chuo kikubwa duniani na kilikuwa hakipo tanzania bali kilikuwepo ndani ya nchi kubwa duniani yaani Marekani .
" You mean USA ??"
" Yeah !." Hapo Damiani ndio alipochoka maana alijua kama mwanadada huyo alikuwa amepatia maswali yote ya written basi hata kama yeye atapita na kwenda oral interview basi asingefua dafu mbele ya bidada huyo man a kwanza chuo tu kingembeba .
" congratulation (hongera ) "
"Thanks!, And you? "
" TIA "
" ooh! Kipo wapi? "
" Tanzania institute of accountancy kipo njia ya mbagala " aliongea Damiani huku akionekana hata mood ya kuongea na mwanamke huyo ikipotea ghafra kwani aliamini kwa nafasi hio moja iliokuwa ikipiganiwa na mamia ya wahitimu asingepata kitu kabisa , kiufupi alinyong'onyea .

Basi damiani aliachana na mlimbwende yule na hio ni mara baada ya kutangaziwa kuwa majibu yatatoka kesho na kwa wale ambao wamepita kwa hatua inayofata basi watajulishwa na ukiona wewe mpaka saa nne asubuhi hujapata ujumbe wowote ama simu kutoka kwetu basi jua hujapita na tunakushukuru sana kwa kushiriki .
Kwa damiani alikosa Tumaini kabisa na aliona ni kama alipoteza hela zake tu za kuja jijini dar ,alitamani kuondoka siku hio hio kurudi lushoto kwao lakini hakutaka kuondoka siku hio hio , aliona ngoja asubiri akapambane na mwanadada yule , kwani aliamini pia kumaliza kwenye chuo kikubwa sio tija, tija ni kuwa competent(uwezo) kwa kile unachokijua .

Alirudi zake mbagala huku akiwasiliana na mama yake juu ya siku yake ilivyo enda , huku mama yake akiendelea kumpa nguvu ya kutokata tamaa bali azidi kujipanga , alirudi mpaka zakhem mbagala bahati nzuri au mbaya hakumkuta yule joshua ila kwakua alikuwa amepewa ufunguo aliingia na kujipumzisha huku akianza kufikiria matukio yote ya siku hio ,kuanzia asubuhi mpaka muda huo , alijikuta akitabasamu na kuna jambo lilimpa nguvu zaidi na kuona kama mungu alikuwa na makusudi ya kupata ajira kwa wiki hio atapata kwa hio hakutaka kukata tamaa , kwani alivyokumbuka mtu yule wa asubuhi alivyomuambia kuhusu elfu kumi ina mnyama gani na kweli swali hilo likawepo kwenye interview basi aliona ni mungu ndie aliemua kujidhihilisha kwake kupitia mtu yule , kwa hio hakuona kuna haja ya kukata tamaa .

Siku nyingine iliwadia na kwa damiani alikuwa na furaha sana kwani alikuwa tayari amekwisha kupokea ujumbe kuwa amepita kwenda kwenye oral interview , kwake ilikuwa jambo la baraka sana na alimshukuru mungu na alijipanga haswa kwa ajili ya lililoko mbele yake .

Aliagana na joshua huku akimtakia mafanikio mema na pia alimpigia mama yake kipenzi kwa hatua alio fikia na mama yake alimuambia anamuombea , alifika barabarani na alibahatika kupata gari baada ya kufika tu lililokuwa likielekea stesheni na alipanda , ndani ya madakika machache alikuwa chini ya jengo la kampuni hio .
Alitembea kwenye ukingo wa barabara na kisha alikunja kushoto na kuingia eneo hilo na wakati huo huo anaingia gari aina ya Audi new model rangi nyeupe ilisimama na alishuka yule dada wajana Merina na alionyesha alikuwa akiendesha yeye mwenyewe , alimuoa a Damiani na mdada ndio wa kwanza kuita jina la damiani kwani Damiani wala hakuwa hata na habari nae .
" Mambo "
" Poa , za toka jana?. "
" Safi , hongera " aliongea merina na kutabasamu huku akionekana hakuwa na wasiwasi wowote kabisa hali iliomfanya Damiani kuamini kwamba mdada huyo alikiwa na uhakika wa kupata nafasi hio .
Waliongozana na kupewa utaratibu na muda kidogo alianza merina ,siku hio walikuwa wa nne ndani hapo , aliingia merina na ndani ya dakika kumi na tano alitoka , na aliingia mwingine na kisha aliingja Damiani , aliulizwa maswali kadhaa na akajibu ki ufasaha kwa kadri anavyojua na kisha alimaliza interview yake.
UNAFIKIRI NI BIASHARA GANI ,



.................SEHEMU YA TATU..............

.

ILIPOISHIA
Siku nyingine iliwadia na kwa damiani alikuwa na furaha sana kwani alikuwa tayari amekwisha kupokea ujumbe kuwa amepita kwenda kwenye oral interview , kwake ilikuwa jambo la baraka sana na alimshukuru mungu na alijipanga haswa kwa ajili ya lililoko mbele yake .

Aliagana na joshua huku akimtakia mafanikio mema na pia alimpigia mama yake kipenzi kwa hatua alio fikia na mama yake alimuambia anamuombea , alifika barabarani na alibahatika kupata gari baada ya kufika tu lililokuwa likielekea stesheni na alipanda , ndani ya madakika machache alikuwa chini ya jengo la kampuni hio .

Alitembea kwenye ukingo wa barabara na kisha alikunja kushoto na kuingia eneo hilo na wakati huo huo anaingia gari aina ya Audi new model rangi nyeupe ilisimama na alishuka yule dada wajana Merina na alionyesha alikuwa akiendesha yeye mwenyewe , alimuoa a Damiani na mdada ndio wa kwanza kuita jina la damiani kwani Damiani wala hakuwa hata na habari nae .
" Mambo "
" Poa , za toka jana?. "
" Safi , hongera " aliongea merina na kutabasamu huku akionekana hakuwa na wasiwasi wowote kabisa hali iliomfanya Damiani kuamini kwamba mdada huyo alikiwa na uhakika wa kupata nafasi hio .
Waliongozana na kupewa utaratibu na muda kidogo alianza merina ,siku hio walikuwa wa nne ndani hapo , aliingia merina na ndani ya dakika kumi na tano alitoka , na aliingia mwingine na kisha aliingja Damiani , aliulizwa maswali kadhaa na akajibu ki ufasaha kwa kadri anavyojua na kisha alimaliza interview yake

INAENDELEA ……….
Basi baada ya damiani kumaliza interview ,alitoka huku akiwa amepewa maelekezo kwamba majibu yatatoka siku kumi zijazo kama amepata kazi au hajapata . .

Alitoka na moja kwa moja na kuondoka eneo hilo na alipanga siku hio hio kuondoka kuelekea Tanga maana muda ulikuwa ukirihusu .

Saa sita kamili alikuwa ndani ya basi la mining nice akielekea lushoto , alikuwa na nusu tumaini la kupata ajira , kwani kila akikumbuka bidada yule aliona kabisa kumshinda mtu alietoka katika moja ya chuo kikubwa duniani ni vigumu na ndio maana alikuwa na nusu tumaini na hilo lilikuwa ni kutokana na kwamba alikuwa amejibu vyema maswali alioulizwa , lakini alijua mfumo wa Tanzania ulikuwa ukiangalia sana nani katoka chuo gani .

Basi saa moja kamili ndio muda aliokuwa akiingia lushoto mjini , alishuka na nakisha alisogelea mpaka moja ya noah zilizokuwa zikielekea kijijini kwao na kisha bahati nzuri zilikuwepo , alipanda na kisha alisubiria baadhi ya abiria wajae na hatimae walifanikiwa kuondoka eneo hilo kuelekea kijijini kwao mkuzi .
Japo alikuwa na mawazo ila picha ya yule mwanadada ilikuwa muda mwingine ilikuwa ikimjia , kuna muda alijisema kama ingekuwa ni rafiki yake elvis mpenda warembo basi hata interview asingejali na angejali kumtongoza yule mwanamke , maana kila akimkumbuka aliishia kutabsamu na kukiri kwamba alikuwa mrembo haswa ambae hakuwa level yake .

Alikuja kushituka kwenye mawazo mara baada ya kufika mkuzi na konda kumshitua, aliangalia nje kama ndio sehemu aliokuwa akishukia , ila aliona anashukia kituo cha mbele yake kwa hio alimtaaarfiu kabisa konda na mara baada ya kufika eneo husika alishushwa na kuanza kuporomoka kwenye kijimlima kuelekea kijijini kwao , kijiji cha mkuzi kilikuwa na umeme kila kona , na pia kilikuwa kimechangamka na hata baada tu ya yeye kushuka alionekana na baadhi ya watu waliuokuwa wakimfahamu na walimsalimia na watoto walimpokea na kupeleka mizigo kwao .

********
Ilikuwa ni siku kadhaa tokea raisi wa tanzania apoteze maisha , raia wengi wa tanziania walikuwa kwenye maombolezo ya siku ishirini na moja , japo kiongozi huyo alikuwa amezikwa lakini watanziania wengi waliokuwa wakimpenda walikuwa wakimlilia na hio ni kutokana na raisi huyo kupendwa sana , .

Naam ! bendera onyango ni raisi wa awamu ya nane ndani ya taifa la Tanzania , ni moja ya maraisi waliokuwa na msimamo sana katika uongozi wake , na kupita hilo alitokea kupendwa sana na kundi kubwa la watanzania huku kundi lingine likuwa halimpendi na hio nikawaida sana katika siasa , licha ya raisi huyu kutopendwa na kundi dogo la watu ni raisi aliekuwa akijitahidi sana kutekeleza majukumu yake ya kazi , hususani yale ambayo alikuwa ameyaahidi katika kampeni zake , huku chini yake akiwa na makamu wake bwana henri mushi .

Hakika bwana onyango alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana katika kuhakikisha yale yote aliyo yaahidi kuyatimiza na hayo ni hususani katika maswala ya miundombinu , msimamo wake katika kusimamia kodi za raia ulimpa wafuasi wengi sana , lakini hata hivyo kuna waliokuwa hawampendi kwasababu zao ama ziwe za msingi ama sio za kimsingi ilihali binadamu hakuwa amekamilika na alikuwa na madhaifu yake basi hawezi kuwa sawa katika kila Nyanja za kiuongozi na hivyo hata bwana bendera alikuwa moja ya binadamu hao ambao hawakuwa wamekamilika .

Katika mambo ambayo bwana onyango alifanikiwa kuyakomesha ndani ya utawala wake moja wapo lilikuwa ni swala la madawa ya kulevya nchini , kwani alijitahidi kwa kushirikiana na wasaidizi wake na polisi kuhakikisha anaziba njia zote za uingizwaji wa madawa ya kulevya hapa nchini, na vile vile madawa kupitishwa nchini, na kwa asilimia kubwa hilo lilifanikiwa , lakini mwanzo wa kufanikiwa kwa jambo hilo ndio mwanzo wa kutengeneza maadui na wafanya biashara hao wa madawa , lakini kwakuwa kazi hio hakuwa akifanya mwenyewe, bali alikuwa akishirikiana na watu wengine na hao walikuwa ni mawaziri na wafanya biashara hao hao wa madawa ya kulevya , na moja ya wafanya biashara hao alikuwa ni bwana Bruno lamberk , huyu bwana alikuwa ni mzungu na alikuwa ndani ya nchi ya Tanzania kwa muda wa miaka ishirini na alikuwa ni moja ya wawekezaji wakongwe ndani ya tafia la Tanzania , bwana huyu alikuwa ni nmoja ya matajiri wakubwa sana waliotajirika wakiwa ndani ya taifa hili , lakini licha ya biashara zake za halali , pia alikuwa ni muuza ngada ndani ya ukanda wa afrika mashariki na kwa kifupi yeye ndie aliekuwa doni ndani ya ukanda wa afrika mashariki yote ,.

Bwana huyu haikujulikana kama alikuwa na familia au lah , kwani kwenye maisha yake hakuwahi kuishi na mwanamke zaidi ya wale wanawake wa kuja kufanya starehe na kuondoka , basi bwana huyu mara baada ya raisi bendera kuingia madarakani , haikujulikana raisi huyo alitumia mbinu gani kumnasa bwana huyo mpaka kupelekea bwana Bruno kutoa ushirikiano na kuwasaliti wauza madawa wenzake, na kupelekea biashara hio kwa Tanzania kufungiwa kabisa na haikuweza kufanyika ,na wauza madawa maarufu kukimbilia nje ya nchi , na moja ya watu waliokuwa wamekimbilia nje ya nchi alikuwa ni bwana Samuel saitoto(rich sam) , huyu alikuwa ni muuza madawa mkubwa sana ndani ya mtandao wa bwana bruno na baada ya kusalitiwa na rafiki yake ndipo alipo amua kukimbilia mexico pamoja na familia yake

Basi habari ya kifo cha raisi bendera kwa bwana Bruno ilikuwa ni pigo kubwa sana , kwani raisi huyo ndie aliekuwa akimpa ulinzi mkubwa sana zidi ya maadui zake , ni siku ya ishirini sasa tokea kuzikwa kwa raisi bendera ndani ya nchi ya Tanzania, bwana Bruno alikuwa amejificha ndani ya jiji la Tanga wilayani lushoto.
“ mkuu nimefanikiwa kuongea nae , anaoneakna ni kijana shupavu kama atakuwa na mafunzo maalumu atafaa kabisa “ aliongea bwana mmoja ambae tulimuona ndani ya jiji la dar es salaam , aliempa lift kijana Damiani . na siku hio bwana huyo alikuwa ndani ya wilaya hio na walioneakana walikuwa na mambo kadha wa kadha walikuwa wakiuongea .
“ Good nimempenda yule kijana na piga ua piga chini lazima tumuingize kwenye system , kwa hio endelea kumwangalia , maana muda si mrefu tutaexcute the plan , my enemies are looking for me , bendera is dead , no one can protect me now “ aliongea huku akiamaanisha kwamba muda mchache ujao wataendelea na mpango wao kwani bendera amekufa na hakuna mtu yoyte anaeweza kumlinda .
“Inabidi uondoke ndani ya nchi hii “
“ siwezi danny nitafia hapa hapa Tanzania “
“ but its too dangerous “{ lakini ni hatari sana )
“ najua na ndio maana nakwambia endelea kumtrack Damiani we need to prepare him ( akimaanisha aendelee kumchunguza damiani kwani wanatakiwa kumuandaa mapema .

*******
Kimbona kama alivyokuwa ameahidiana na samu juu ya kumtafuta bruno na kumpotezea mbali mzungu huyo , hakutaka kabisa swala hilo lifeli , na alikuwa na mood kweli ya kulifanya swala hilo , hasa kila alipokuwa akikumbuka ni kiasi gani alikipoteza mara baada ya Bruno lamberk kuwasaliti kwenye mtandao wao , kilimuuma sana , hela zake zilimpa nguvu ya kukamilisha mauaji hayo .
Haikumuia vigumu ,kwani ni kama alikuwa amepumzika katika biashara hio, kwani watu wake (gang) walikuwepo ndani ya nchi hio na alikuwa akiwalipa kisiri siri kwani alikuwa akiamini siku moja atarudi ulingoni na kuendelea na biashara hio, kwake baada ya kifo cha ghafra cha raisi bendera aliiona hio kama fursa nyingine ya kurudi kwa kishindo katika biashara hio ya uuzaji wa madawa ya kulevya .
“ Derick hakikisha unawapanga vijana mkao wa kazi , taarifa zilizopo kwa sasa kutoka kwa shushu wetu ndani ya TISS ni kwamba bwana Bruno kajificha ndani ya wilaya ya lushoto mambo view hotel.
“sawa mkuu vijana kwa sasa wako tayari na wanasubiria maelekezo yako tu “
“ basi safi , pumzika kwa leo na kesho nitakuambia nini cha kufanya , hakikisha swala hili linafanyika kwa weledi mkubwa , hakuna kufeli “
“ sawa boss “ huku akitoka
“ hahahahaha… hahaha… hii ni fursa nyingine kabisa kwangu naenda kurudi ulingoni muda si mrefu , Bruno …. Brunooooo …. Ama zako ama zangu “ aliongea tajiri kimbona kwa kicheko cha kifedhuli huku akigugumia wine yake aina ya black and white .

Siku ilio fuata derick alipokea simu kutoka kwa boss wake na kumtaarifu kufika kwenye kampuni yake ndani ya jengo la LAPF tower , kampuni iliokuwa ikjjulikna kwa jina la KILAC (KIMBONA INTERNATIONAL LINK AND COMPANIES }.
Derick haikumchukua muda mrefu kufika ndani ya jengo hilo la LAPF, alifika moja kwa moja na aliripoti kwa secretary na aliruhusiwa kuingia moja kwa moja na alisalimiana na boss wake huyo na kisha alipewa ramani nzima ya kufanya tukio hilo .
“ kuweni makini na Danny huyu ni jasusi wa kimataifa na ana mbinu nyingi za kuwazidi , lakini na nyie pia mna mbinu nyingi za kumzidi akili , narudia swala hili halina kufeli hakikisheni mnalimaliza baada ya siku kumi zijazo.
“ sawa boss “
Derick alitoka ofisini hapo na kisha hakutaka kuchelewa aliwashitua genge lake la kimafia na kuwapa ramani wapi wakutane kuelekea lushoto .

********
Ni baada ya siku kumi kupita kijana damiani bila kupokea ujumbe wowote kutoka kwa kampuni ambayo amekwisha kufanya interview , japo mama yake alimtia moyo wa kutokata tamaa ila kwake yeye ukiunganisha na yale anayo yajua mwenyewe hakuona nafasi kabisa ya kushinda kazi ile , alimwangalia mama yake aliekuwa amevaa nguo zilizoochanika na zisizokuwa zikivutia , alimuonea hruma sana , alitamani amtoe mama yake katika lindi hilo la umasikini kadri ya uwezo wake , kiufupi alikuwa akimpenda mama yake sana , kila akikumbuka misoto mama yake aliopitia kwa ajili ya kuhakikisha anasoma ,ilizidi kuumia mno aliilaumu serikali sana kwa kutokuwa na mfumo mzuri wa kutoa ajira kwa wanafunzi , kwani wahitimu walikuwa wakijitahidi kusoma sana kwa bidiii na pia wazazi wanawasomesha watoto wao kwa juhudi zote, lakini mwisho wa siku wanamaliza hakuna ajira , ilikuwa ni swala la kukatisha tamaa sana wazazi pia na wahtimu wenyewe .

Siku hio damiani aliamua kushinda na mama yake tu nyumbani hawakwenda popote , maana hata mama yake siku hio alikuwa kichwa kinamsumbua hivyo hakuweza kabisa kwenda kwenye vibarua vyake ambavyo vilikuwa vikimuwezesha kuleta nyumbani na kupata chochote tumboni .

Basi siku hio damiani alikuwa akitengeneza banda lao la mbuzi hapo uwani huku muda mwingi aliangalia emaili yake ama simu ikiita , kwani alikuwa na shauku kubwa ya kujua kama amepita ama hajapita , lisaa la kwanza likapita , la pili nalo likapita , la tatu hatimae la nne , mpaka saa kumi na moja hakukuwa na jumbe wala simu yoyote , aliweka simu chini huku akiona kabisa hakukuwa na tumaini lingine lililobaki la kupata ajira , hakuona sababu ya kukaa nyumbani hapo alimuaga mama yake kwa kumwabia anarudi muda si mrefu anaenda kwenye shanba lao la miti kwa ajili ya kuchukua miti kidogo aje amalizie banda lao la mbuzi , maana hakupenda kabisa kulala na mbuzi hao nyumba moja kwani mikojo yao ilikuwa na harufu kali .

Alitembea kwa muda wa kama nusu saa na hatimae alipita kijijini kwao , siku hio watu wengi walionekana kuwa barabarani kwani siku hio kulikuwa na sherehe iliokuwa ikifanyika kwenye kanisa moja la roman kwa hio watoto watoto alikuwepo huko na hata baadhi ya wamama pia , ni mama yake pekeee na baadhi ya wanakijiji waliokuwa wapo majumbani hasa wale wazee waliokuwa hawawezi kutembea , alitembea huku akiwa anakula apple kwani kijiji chao hicho kilikuwa na kilimo cha matunda aina ya apple , matunda damu na peasi na hata mananasi.

Basi baada ya dakika kama arobaini na tano hivi ndio muda alioingia kwenye shamba lao kubwa la miti ya biashara , hakutaka kuchelewa maana baada ya kufika tu alianza kazi ya kutafuta mikalitusi ilio nyooka na kisha kuikata , lakini wakati akiendelea na kazi hio simu yake ilitoa mlio kwamba kuna ujumbe umeingia , aliendelea kukata miti kwanza kama ishirini na aliridhika kwamba hio inatosha , ndipo alipo toa simu yake kuangalia ni ujumbe gani umeingia .

“ HONGERA BWANA DAMIANI RABANI UMEFANIKIWA KUPITA KWENYE INTERVIEW YAKO ULIO FANYA TAHEHE HIO , UNAPASWA KURIPOTI KAZINI MAPEMA KABLA YA TAREHE HIO”

Ulikuwa ni ujumbe uliomtoa machozi bwana damiani , yes yalikuwa ni machozi ya furaha alijikjuta akiruka ruka kwa furaha sana , hata ile kazi ya kukata miti iliishia hapo na jambo alilolifikiria kwa kwakati huo ni kurudi nyumbani na kwenda kumuonesha mama yake ili wafurahie pamoja , muda ulikuwa umeenda na kagiza kameanza kuingia alifunga miti yake haraka haraka huku akipiga mluzi wa furaha hata haikueleweka ni wimbo gani ulikuwa ukiimbwa .

Lakini wakati hayo yakiendelea mara alisikia kitu kilicho mfanya kunyanyuka haraka na kuangalia upande wa kushoto kwani kilikuwa ni kishindo kikubwa cha kitu kudondoka , lahaula ! ilikuwa mtu bwana kadondoka tena mwenye ngozi nyeupe huku akioneakana kuvuja damu nyingi usoni na ubavuni , damiani alipatwa na woga na akili yake yote iliwaza kukimbia kwa wakti huo , lakini alishuhudia mtu yule akimpungia mkono kwa shida kama anaomba msaada , ilibidi damiani aangalie kulia na kushoto kuona kama kuna mtu anakuja , maana akili yake ilicheza na kufanya kazi kama mashine kwa wakati huo na alijua mtu yule lazima atakuwa anawindwa kama sio kukimbizwa , alimsogelea kwa tahadhari .
“ help me to get out here wataniuu ..wa tafadhari nisaidie “ aliongea na kweli alikuwa mzungu kama damiani hisia zake zilivyokuwa zikimwambia , hakutaka sana kujishauri maana kweli aliona mtu huyo alikuwa akihitaji msaada , lakini alifikiria ni msaada gani anatakiwa kumpa , alichokifanya ni kurudi pale alpoacha miti yake na kisha aliichukua na kuisukumizia kichakani na haikueleka alikuwa na maana gani , kisha alimrudia yule mtu na kumuweka begani huku mzungu yule akiinua uso wake.
“shika hii just in case tusipofanikiwa , kimbia uniache.” Ilikuwa ni bahasha iliojaradiwa kwa mfuko wa plastic.

Damiani alivipokea huku akiwa hajui mzee yule alikuwa akimaanisha nini , ila kwakuwa wakati huo alichokuwa akiamini ni kumuokoa tu basi alijitahidi kadri ya uwezo wake kumtoa msituni hapo na kumfikisha nyumbani kwao kwani aliamini ndio ingekuwa sehemu salama , na angejua angefanya nini baada ya hapo
Uzuri ni kwamba giza lilikuwa limetamalaki hivyo kwa kupitia njia za vichaka aliweza kupita bila kuonekana kwa urahisi lakini pia kwakuwa watu walikuwa kwenye sherehe , alitembea na kufanikiwa kutoka kwenye msitu na hatimae aliingia ndani ya kijiji chao, alionekana na mbibi mmoja tu aliekuewa hawezi kutembea vizuri na kuongea pia kwani alikuwa amepinda mdomo , na kwa fununu ni kwamba ni adhabu alio pata katika shughuli ya ulozi wake .

Alimpitisha mpaka kwao na mama yake alipigwa na mshangao nusu apige kelele, lakini damiani alimzuia na kumwambia huyo mtu anataka msaada kamuokota huko msituni , mama yake alifungua mlango na walimpitisha kisha walimlaza kwenye kipande cha mketa , na wakati huo mzungu huyo hakuwa na fahamu , nadhani ni kutokana na kupoteza damu nyingi .
“ mama inabidi tumuite mzee kivinje anaweza kumsaidia nikifanya taratibu za kupata usafiri wa kumpeka hospitalini “( mzee kivinje alikuwa ni mganga kutumia mitishamba )
“ kwanini usimpeleke moja kwa moja akitufia hapa si itakuwa kesi “
“ hapana mama hali yake hio inaonesha anawindwa na inatupasa kumsaidia kwanza na kufanya mambo kwa umakini “ aliongea damiani kwa ujasiri mkubwa sana na kisha alitoka na kwenda kwa kivinje daktri wa mitishanmba lakini pia alikuwa mganga wa kienyeji .

Hapakuwa mbali sana , kutokana na mwendo wake alifanikiwa na bahati nzuri aliweza kumkuta bwana kivinje akiwa nje kashikiria kikombe na alionekana alikuwa akinywa maziwa ya mbuzi , damiani alieleza shida yake na kumstua sana kivinje na hakutaka kupoteza muda aliingia ndani na kutoka na dhana zake za kazi na kuongozana na damiani .

Haikuwchukua muda , walifika na kivinje alihitaji damiani amuoneshe mgonjwa alipo lakini hapo ndipo damiani aliposhuhudia kitu ambacho hakukitarajia kabisa .

Alimuona mama yake akiwa kwenye dimbwi la damu , huku mwili wa yule mzungu na wenyewe ukiwa kwenye dimbwi la damu , aliishia kutamka neno mama lakini sauti haikutoka.

INAENDELEA


INAENDELEA SEHEMU YA NNE

Damiani alijikuta akijikaza na kumkimbilia mama yake pale alipo na wala hakujali zile damu maana alimuinua mama yake huku akilia
“ mamaaa, mamama , amka mama nini kimetokea mama yangu … mamaaaa… mama amka “ mama yake damiani alikuwa akitapatapa na aliishia kunyosha mkono kuelekea mlangoni na hapo hapo akakata roho , ilikuwa ni huzuni kwake kwani alilia na kuutingisha mwili wa mama yake japo aamke , lakini haikuwezekana kabisa na kivinje ndio alimsogelea na kumshikilia asiendelee kufanya anacho kifanya
“ mama mama wee ,, mama amka mimi mwanao unaniacha na nani , mama yangu , bado sijapata nafasi ya kukutoa kwenye umasikini mama yangu wee …. Amka mamama nimefanikiwa kupata ajira sijakuambia bado mma amka mama weeee…..” ilikuwa ni huzuni na kama haukuwa na moyo basi ungelia ,maana mama yake alikuwa ameuwawa kikatili sana , watu tayari walikuw wamejaa kwani walisikia vilio hivyo , kila alieambiwa na kivinje kwamba mama damiani kafariki ilikuwa ni kilio kikubwa mno kwa kila aliekuwa akimjua mama huyo .

Watu waliendelea kulia ,damiani alikuwa amezimia wakati huo ,chopa ilisikika ikitua eneo la karibu ndani ya kijiji hicho na mwili wa yule Bruno ukichukuliwa na kupelekwa upande chopa ilipokuwepo , huku polisi nao wakiwa eneo la tukio , ilikuwa ni tukio la kusikitisha na kila mtu alikuwa akiongea lake , na wakati huo hayo yanaendelea vijana wa kimbona walionekana hapo na derick mwenyewe akiwa wamesimama upande wa juu hivi kuepuka watu kuwaona na mara baada ya kuona mwili wa Bruno ukitolewa na wao waliondoka eneo hilo .
*******
“Hahaha… hahahah…. Safi sana derick , kazi nzuri vijana wangu “ aliongea kimbona huku akionekana kuwa katika uso uliojawa na furaha ya ushindi baada ya kusikia kuwa bruno kazichapwa risasi na amekwisha kufa.
Hakutaka kuchelewa aliinua mkonga wake na kumpigia sam na kumpa tarifa hizo ambazo kwa sam alizipokea kwa furaha kubwa mno , na kumshukuru sana kimbona huku akimualika kuwa siku hio aende serena hoteli kuna watu anataka kuwakutanisha nao muda was aa nne usiku .

Na bila hiyana mzee huyo aliitikia wito huo kama atakuwepo eneo hilo bila kukosa , ilikuwa ni furaha sana kwa kimbona katika moja ya hatua ya kurudi kwenye biashara yake aliiona kabisa kwa mafanikio makubwa inakwenda kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana .
Ilivyofika muda wa saa nne usiku kimbona alimuaga mkewe na familia yake kwa ujumla na kisha alitoka na mlinzi wake kuelekea kwenye miadi yake kama alivyokuwa ameelekezwa na Samuel , kwakuwa ni usiku gari haikukawia kufika ndani ya hoteli hio ya hadhi ya juu sana ndani ya jiji la dar es salaam .

Alifika mpaka mapokezi na kujitambulisha hapo na kisha ni kama ujio wake ulikuwa umetegemewa kwani aliongozwa mpaka kwenye lift na mdada mmoja mrembo sana aliefika eneo hilo kumchukua , lift ilipanda mpaka kwenye floor ambayo ilikuwa na vyumba vya VVIP yaani kwamba hapo walikuwa wakiingia watu wa hadhi ya juu sana ndani ya jiji hilo , alitabasamu maana ilikuwa ni muda kidogo kuingia sehemu zilizokuwa zina ulinzi mkali kama aliouona ndani hapo .

Mdada yule mrefu mrembo alievalia suti yake ya zambarau na viatu vya high heels alitembea mpaka kufika kwenye moja ya chumba na kisha alifungua mlango na kumkaribisha bwana kimbona , kimbona alijikuta akiwa kwenye mshangao kwani watu waliokuwepo hapo ndani hakuwatarajia kabisa .
“ mheshimiwa , alijikuta kimbona akiongea kwa kupaniki kwani aliekuwa mbele yake alikuwa ni rais mstaafu wa awamu ya saba bwana Athumani ndalu , upande wa kulia alikuwepo waziri wa mambo ya ndani bwana musiba , mbele yake alikuwepo samueli , kulikuwa na jumla ya watu wanne ukimjulisha na yeye pia lakini kuna kiti kilionekana hakikuwa na mtu ..
“ hongeera sana bwana kimbona kwa ushindi wa leo “ aliongea raisi mstaafu .
“ asante sana mheshimiwa , unajua ni mara yangu ya kwanza kuonana na wewe laivu , ni heshima kubwa sana “
“ hahahaha.. kimbona huu ni mwanzo tu , na sasa unakwenda kukutana na mtu mkubwa Zaidi na penginepo wakubwa Zaidi karibu kwenye U-97( UNITY 97) aliongea sam kwa sauti ya majisifu
“U-97?” aliongea kimbona akimwangalia sam lakini hapo hapo mlango ulifunguliwa na hapo ndipo bwana kimbona aliposhangaa zidi kwani mtu aliekuwepo mahali hapo hakumtegemea kabisa.
“ Mheshimiwa raisi!!!”””” alijikuta akijisemea moyoni kwa mshangao

*******
Watu walikuwa wakizungumza hili na lile ndani ya kijiji hicho na habari zilitapakaa kila kona , kila mtu alikuwa akiongelea swala la mama damiani kupigwa risasi na watu wasiojulikana , pia mzungu kupigwa risasi ndani ya nyumba hio hio ya mama daniani na hata chopa kuja kumchukua mzungu huyo , watu hawakulala kila mtu alikuwa akiongea hili na lile ilimradi tu ni jambo la kuongea , lakini pia kuna baadhi ya watu walikuwa kwenye majonzi makubwa ya kupoteza uhai kwa mama damiani tena kwa kifo cha kikatiri sana , watu walilaani vikali kwa kilicho tokea .

Damini alikuja kupata fahamu lisaa limoja mbeleni akijikuta yupo ndani ya zahanati akiwa amelazwa , ni kama akili zake hazikiwa sawa wakati wa kuzinduka na hata nesi na daktari walimuona wakati wa kuzinduka huku kila mtu akiwa kwenye uso wa majonzi na kumuonea huruma kijana huyo , kwani waliona ni mambo makubwa na magumu ambayo anakwenda kupambana nayo katika maisha yake .

Ni kama mkanda wa filmu ulikuwa ukipita ndani ya kichwa cha kijana damiani , picha ya kumuona mama yake akiwa amelala kwenye dimbwi la damu zilianza kupita .
Alijikuta akitoa ukulele uliowafanya dokta amsogeleee haraka haraka na kumtuliza, hawakua na jinsi ilibidi wamchome tena sindano ya usingizi ambayo ilikuwa makali ya kuisha siku nyingine .
Ilikuwa muda wa asubuhi ambao habari za majambazi kumuaa mama damiani na mzungu zilisambaa lushoto nzima na kwenye vyombo vya habari.

Jeshi la polisi lilithibtisha kuwa wahusika wa mauaji hayo walikuwaa ni majambazi yaliokuwa na makazi yao katika msitu wa mlola huku wakihusisha swala hilo na tukio lililotokea miaka ya nyuma la kuvamiwa kwa chuo kikuu cha SEBATIANI KOROA MEMORIAL UNIVERSITY (SEKOMU) miaka iliopita huku wakiahidi uchunguzi unaendelea mpaka kuwatia hatiani majambazi hayo .

Upande wa damiani alifumbua macho asubuhi akiwa na akili zake zote , roho yake ilimuuma mno pale alipokumbuka duniani amebaki kuwa yatima , alijilaumu kwa kumsaidia mzungu yule kwani aliona kama angemuacha tu kule kule huenda yote hayo yasingemkuta mama yake , alijilaumu sana na kuhuzunika na moyo wake , lakini hakuwa na lakufanya kwa wakati huo , ilibidi aruhusiwe ili akashuhudie maziko ya mama yake , watu walimuonea huruma sana na kumpa pole , alizipokea huku akijitahidi kujikaza kiume .

Taratibu zote mazishi zilikuwa zimekwisha kufanywa na serikali , akiwemu mkuu wa wilaya aliehudhuria mazishi hayo.
Basi padri alifanya sala fupi na kuruhusu watu waage mwili akiwemo damiani alielia sana baada ya kumuona mama yake akiwa kwenye jeneza , alitolewa na watu wengine walipewa nafasi na hatimae mwili ulipelekwa makaburini
“SARAH RABAN AMEZALIWA MWAKA 1979 AKAFARIKI MWAKA 2019 AKIWA NA MIAKA 40 AMEACHA MTOTO MMOJA “ wosia mfupi ulisomwa na hapo mwili ukapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.
Damini hakuamini kama mama yake hakuwa nae tena duniani , watu walimhurumia sana , lakini ndio la kutokea lishatokea
*******
Maisha mapya ya kijana damiani yalianza , yalikuwa ni maisha ya huzuni kwani alikuwa amemzoea mama yake sana na sasa hakuwa nae tena duniani , kwake aliona kama ndoto na asubuhi ataamka na kumkuta mama yake , lakini haikuwa ndoto tena ulikuwa uhalisia na mama yake hakuwpo tena duniani , kila akikumbuka ahadi alizojiwekea juu ya kumtoa mama yake katika umasikini alijikuta akihuzunika sana .

Wiki moja ilipita na siku hio ilikuwa ni asubuhi ni siku ambayo aliamka na mawazo mapya na aliona kabisa yakutokea yamekwisha kutokea na sasa anatakiwa kujikaza kama mwanaume na kuruhusu mambo megnine yaendelee . lakini siku hio pia alikumbuka tukio la yule mzungu kumpa bahasha flani iliojaradiwa na plastic alifikicha kichwa chake na hapo hapo alikumbuka sehemu aliokuwa ameificha , ilikuwa ni nje kwenye banda la mbuzi kwenye paa la nyasi kwani anakumbuka ndipo sehemu alio ichomeka siku ile kabla ya kwenda kumuita mzee kivinje , alitoka nje na kisha alisogelea banda lile na kisha aliingiza mkono sehemu alipo amini ndio alipoweka , lakini hakuiona alijaribu tena lakini hakuona , alijikuta akitafuta mpaka akikata tamaa , alilalia kibanda hicho akiwa anaangalia chini na kujiona kuwa na mkosi lakini ni kama kuna kitu alikuwa amekiona kwenye kinyesi cha mbuzi wale aliona plastc kama ile ile , alikurupuka na kukimbilia upande wa nyuma ya banda lile na kushika ile plastic na kuivuta na kweli ilikuwa ni yenyewe alijikuta akitabasamu na kuifuta uchafu ule na bahati nzuri ni kwamba ilikuwa imehifadhiwa kwenye plastic bag kwa hio ilichafuka juu tu .

Alisogea mpaka ndani kwao na kisha aliitoa kwa utaratibu bahasha ile na kutoa karatasi nne alizitoa haraka haraka na kuanza kupitia moja “: BRUNO LAMBERK BORN 1947 hapo alitambua kuwa mzungu yule alikuwa akiitwa kwa jina la bruno lamberk
“ owned properties ( mali anazomiliki )

Chini ilikuwa ni orodha mjumuisho iliokuwa na maelezo ya mali anazomiliki bwana Bruno ilikuwa ni mali nyingi bwana huyu ambazo alikuwa akimiliki kulikuwa n mashamba nyumba na namba account ya bank ya uswisi na card yake benki ambayo damiani hakuitambua “
Alipitia karatasi nyingine ilikuwa ni ramani ya Tanzania lakini ndani yake kulikuwa na sehemu zimechorwa kwa alama nyekundu ni kama zilikuwa zikionesha eneo husika hakutaka kuangalia sana hio karatasi alipitia ya pili yake ilikuwa na akaunti za benki ya CRDB na card yake lakini jina halikuwa la Bruno bali limeandika seline amber aliweka pembeni na ya mwisho ilikuwa na majina mengi karibia tisini , ila hakutaka kujihaingaisha nayo , alifungua kimkebe kilichokuwa ndani ya hio bahasha na ndani yake kulikuwa na vitu viwili moja ilikuwa ni flash disk , pili ilikuwa cheni yenye kidani kilichokaa kwa muundo wa msalaba lakini kina utofuti kidogo , aliachana na ile cheni na kisha akahamia kwenye ile flash , alijua kuna kitu kilikuwa ndani ya hio flash , alikumbuka alikuwa na laptop , alifuata kwenye begi lake na kisha aliitoa na ikawaka alisubiria window iload na ikakubali na hapo hapo hakutaka kuchelewa aliingiza password na kisha akchomeka ile flash.

CONTINUARA......
 
SEHEMU YA TANO


INAENDELEA HAPA SEHEMU YA TANO

Bwana kimbona hakuamini kwamba mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alieapishwa juzi kuwa raisi .

“ karibu sana mheshimiwa “ aliongea sam na kumkaribisha bwana henry mushi ndani ya eneo hilo na bwana huyo mwenye mwili mkubwa kidogo wa wastani huku kitambi kwa mbali kikionekana alisogea mpaka kwenye nafasi yake na kukaa .

“asanteni mnaweza kukaa “ aliongea

“ Jamani kwanza niwashukuru wote kwa kuitika wito wa kufika kwenye kikao chetu , wapo wengi ambao walipaswa kuwepo katika kikao hichi lakini ambao mpo mahali hapa tambueni kwamba nyie ndio mpo ngazi za juu “ aliongea samueli .

“ dhumuni la kikao hichi kwanza ni kufurahia swala la bendera kupoteza maisha huu ni Zaidi ya ushindi kwani katika mfumo wetu hakuna aliewahi kumpenda huyu bwana na sasa ameondoka ni swala la kujipongeza na kushukuru walio juu yetu , pia swala la pili ni juu ya kifo cha bwana Bruno ambae naamini wote tuliokuwepo hapa tunajua ashapoteza maisha , jambo ambalo ni haki yake kwa dhambi yke ya kutusaliti . na hili ni mpongeze kimbona , na kupitia hili amepanda nafasi nne katika umoja wetu na hayo ni maagizo ya mkuu wetu ukanda wa afrika .” aliongea kimbona na hapo kila mmoja aliinua glasss yake ya wine na kugonga cheers kufurahia jambo lao .

“ jambo kubwa Zaidi ya yote ni juu ya biashara yetu , nadhani kila mmoja anaelewa ni kwa jinsi gani tumekwama katika biashara hii katika miaka mitano iliopita ya mwenda zake , hivyo kwakuwa neema ipo mikononi mwetu , basi ni muda wa kufufua mtandao wetu ndani ya nchi hii .”

“ ni kweli kabisa bwana sam swala hilo , lakini sio kirahisi kama unavyo ona “ aliongea mheshimiwa raisi .

“ naelewa bwana henry na ndio maana leo hii wewe ni raisi na kupitia wewe kila kitu hakitakuwa na ugumu wa aina yoyote ni swala la kimkakati tu , na isitoshe sio wewe tu utakae nufaika lakini pia na wananchi wanakwenda kunufaika kwani miradi yote ilioanzisha na mwenda zake tutaikamilisha na biashara yetu itaendelea na wewe utaimarika kisiasa “

“Ni sawa uzungumzalo bwana sam balozi , lakini swala hili ili kufanikiwa na biashara yetu kuneemeka na hatimae kutuingizia faida lazima tuwe na mpango imara na wa kuaminika “ aliongea mstaafu raisi bwana ndalu .

“ swala hili lipo kwenye mpango na kila jambo linaloendeea ndani ya nchi hii limeratibiwa na wakubwa kwa hio hata kifo cha mwendazake huwezi jua likawa ni mpango pia wa U-97 . wote walishituka lakini sam alitabasamu .

“mpango uliopo kwa sasa ni kutakiwa kufumua mfumo wa kiuongozi , hii namaanisha kuanzia mkuu wa TISS, waziri mkuu , waziri wa fedha , waziri wa mambo ya nje na waziri wa katiba na sheria , na hao watu wote watakao kaimu hizo nafasi faili hilo litakuja ofisini kwako mheshimiwa raisi , swala la pili ni kuhakikisha vibaraka wote wa mwenda zake wanakuwa neutralized kwenye mfumo wa kiserikali , tatu ni kuhakikisha biashara za bwana bruno zote zinaingia kwenye mikono ya U -97.”

“hizi bishara za bwana Bruno swala hili tutafanikiwa vipi ,tunaweza kupata baadhi ya asset zake , lakini sio pesa zake ,kwani mpaka sasa haijaeleweka bwana huyu ni wapi pesa zake anahifadhi , na hata nyaraka zake ni kwamba mpaka sasa hazijapatikana .

“kimbona hili lipo juu yako , utafatilia watu wote wa karibu wa bwana bruno , na hakikisha unapata nyaraka hizo “

“ sawa sam nitalifanyia kazi “

“ well mwisho kabisa natangaza nafasi kama nilivypewa magizo na level 01 “

“ bwana kimbona umepanda kutoka level 73 uliokuwepo mpaka level unity 45 , bwan henry mheshimiwa umepanda mpake level unity 33 , mheshimiwa mstaafu umepanda mpaka level 32 , mheshimiwa wa mambo ya ndani umepanda mpaka level 34 ni hayo tu “ aliongea sam na kisha kikaao kikafungwa.

*****

Upande wa masaki alionekana mwanadada merina akiwa juu kabisa ya balcon akifurahia upepo wa bahari , wakati huo alikuwa amevalia shati kuu kuu la mikono mirefu la rangi nyeupe , alionekana kabisa hakuwa amevaa kitu kingine ndani , mkononi alikuwa ameshikilia cocktail(mvinyo),alionekna kuwaza jambo .

“ Damiani , where are you am going crazy thinking of you ( akimaanisha kwamba damiani uko wapi najikuta chizi kukuwaza ).

Mrembo huyu hakuwa muombaji wa kazi katika kampuni ya damiani aliofanya interview ila alikuwa ni chief exucutiv officer (CEO) wa kampuni hio , na siku ya kwanza aliomuona kijana damiani ni siku ya written interview , na hapo ndio mrembo huyu alivutika sana na kumpenda kijana damiani na hata wakati wanamaliza kufanya interview alitamani sana kuongea japo kidogo na kijana huyo .

Kwa hio ile yote kumwambia kwamba alikuwa na yeye mahali hapo kaja kwa ajili ya kufanya interview ilikuwa ni geresha tu ya kumpumbaza damiani aamini kwamba na mrembo huyo alikuwa akiomba kazi kama yeye .

Lakini ajabu alio iona merina kwa damiani ni kwamba hakuwa hata na dalili za kumchangamkia tofauti na wanaume aliowahi kukutana nao na anao endelea kukutana nao kila siku , kwani alitarajia kama ni mwanaume anaependa warembo basi siku hio hio angeombwa namba , lakini ilikuwa tofauti kabisa kwa damiani kwani hakujiahangaisha na mrembo huyo na jambo hilo lilimfanya ampende zaidi.

Kilichomshangaza Zaidi ni kutoonekana kwa kijana damiani hata pale ambapo walipompa taarifa ya kupata ajira ndani ya kampuni hio kama finance manager ( msimamizi wa fedha ), jambo hilo lilimfanya mlimbwende huyu kwa kuishi kwa kumsubiria damiani lakini hakuweza kumtia machoni mpaka siku ya mwisho ya tarehe ya kuripoti kazini bado hakumuona , aliongeza wiki moja mbele kwa damiani kusubiriwa , lakini bado kijana huyo hakuonekana , mwishowe alijikatia tamaa kabisa na kuona kwamba hakukuwa na uwezekano wa kijana huyo kuja kufanya kazi katika kampuni hio ,hivyo walifanya maamuzi ya kumuajiri mtu mwingine , lakini hilo halikuwa mwisho kwa mrembo merina kumuwaza damiani , sio usiku sio mchana akiwa kazini alikuwa akimuwaza kijana huyo alitamani muujiza utokee amuone kijana huyo tena .

Mpenzi wake patrick alishangaa hali aliokuwa nayo merina kwani alikuwa amebadilika sana na hakuwa yule ambae alikuwa akimjua, kwani alikuwa na uhakika merina alikuwa akimpenda sana yeye , sasa kubadilika kwa merina kulimchanganya na aliamini kabisa kuna jambo halikuwa sawa

“ merina kuna tatizo gani mpenzi wengu , mbona siku hizi umebadilika sana , what is going on my love “

“ nothing pat , i am okey , everything is right with me its just.. I need time”(hakuna kitu pat niko sawa ni kwamba tu nahitaji muda kidogo kuweka mambo yangu sawa )

“ lakini merina mpenzi napaswa kujua kile kinacho endelea kwenye maisha yako kumbuka wewe ni mpenzi wangu “.

“ naelewa Patrick , ila kwa sasa unapaswa kunielewa siko sawa emotionally nahitaji muda and soon i will be fine “

******

Patrick henry mushi , alikuwa ni mtoto wa raisi ya jamhuri ya muungano wa Tanzania bwana henry mushi , alikuwa na miaka ishirini na saba. .

Alikuwa ni kijana mtanashati sana , mrefu wa maji ya kunde ni wale wanaume ambao wanapendwa sana na wadada kutokana na muonekano wao yaani mahandsome .

Licha ya yote pia Patrick alikuwa ni moja msomi kutoka chuo cha Georgetown university kilichokuwepo ndani ya jiji la marekani washington DC , ni moja ya vijana ambao wanamafanikio makubwa ndani ya taifa la Tanzania , kwani alikuwa ndio msimamizi mkuu wa mali zote za baba yake .

Mwaka 2019 ndio mwaka aliokutana na mrembo merina , ndani ya hoteli ya the hay -adams iliokuwa ndani ya jiji la Washington DC, downtown , siku hio japo bwana Patrick alikuwa na mwanamke lakini ,macho yake hayakuweza kutoka kwa mrembo huyo aliekuwa mapokezi na alionekana kuna mtu alikuwa akimsubiria .

“mary go ahead am coming in minutes “ aliongea akimwambia mchumba wake wa kizungu alieingia nae eneo hilo atangulie kwani alikuwa anakuja ndani ya dakika moja .

Baada ya mrembo aliekuwa na Patrick kutangulia , Patrick alisogea kwenye masofa sehemu aliokalia mrembo merina eneo hilo la mapokezi , lakini ile anamkaribia mrembo yule alitoa simu yake na kuongea kwa lugha ya Kiswahili , na hapo ndipo Patrick alipo mjua mrembo huyo kuwa kama siio mtanzania basi ni mkenya , lakini lafudhi yake ilimjulisha kuwa ni mtanzania japo hakuwa na uhakika .

“ mambo “ Patrick alimsalimia mrembo huyo kwa lugh ya Kiswahili , jambo lililomfanya merina atabasamu na hapo ndipo Patrick alizidi kuvutiwa na mwanadada huyo , kwani dimples zake zilizidi kuupendezesha uso wake .

“ safi “ alijibu merina huku akiwa bado na tabasamu na yote hayo ni kutokana na kusalimiwa kwa Kiswahili na alijua kabisa mwanaume huyo alikuwa mtanzania .
“ wewe ni mtanzania ?” aliuliza Patrick .
“ yeah and you ?”
“ mimi pia ni mtanzania , nafurahi kukutana na mtanzania mwenzangu ndani ya jiji hili “.
“ mimi pia “
“ naitwa Patrick “
“ naitwa merina “
“ nashukutu kukufahamu merina “

Basi kuanzia siku hio ndio Patrick alijuana na mrembo huyo , na kuvutiwa nae sana alifanikiwa kuchukua namba ya simu ya mrembo huyo ya Tanzania .

Baada ya Patrick kurudi Tanzania ndio alianza mchakato wa kumpata mrembo huyo kwani alikuwa akimuota kila siku na hakutaka kuumia Zaidi ili hali dawa ilikuwepo , alijaribu kuomba kukutana na mrembo huyo japo mwanzoni ilikuwa ngumu lakini siku moja alifanikiwa , ukaanza urafiki uliodumu kwa wiki mbili hatimae Patrick alirusha ndoano lakini mrembo huyo alichomoa kwa mara ya kwanza , lakini kwa patrick hakutaka kabisa kukata tamaa , aliendelea kubembeleza na mwishowe alikuja kukubaliwa rasmi , kwa masharti ya kutoshiriki mapenzi mpaka pale watakapo oana , na kwakuwa Patrick alikuwa amempenda kweli mrembo huyo na pia umri wake ulikuwa ukiruhusu kuoa alikubaliana nae .

Mapenzi yalinoga kwa pende zote , merina alimzoea sana Patrick , na Patrick nae alitokea kumpenda sana merina , tabia ya Patrick kuwa na wanawake wengi aliacha rasmi kitendo ambacho kwa marafiki zake kiliwashangaza tena , lakini Patrick alivyowaambia msimamo wake juu ya merina kila mtu alimuelewa .

Mwezi wa kumi na moja mwishoni penzi likuwa na miezi mitano ndio lilianza kuwa chungu kwa upande wa Patrick , kwani merina alibadilika sana , mawasilano kutoka kwa mrembo huyo yalipungua ghafra .

Kubadilika kwa merina kunatokea kumtesa sana na kumkosesha furaha , anajaribu kulipigania penzi lake kwa mrembo huyo lakini hakuna kinacho saidia , lakini anaapa kutomkatia tamaa mrembo huyo na kuamini lazima atakubali na kuingia kwenye laini siku moja , pasipo kujua kuwa mrembo huyo alikuwa akimuwazia mwanaume mwingine kabisa .

“ come on Patrick unateswaje na demu hivyo rafiki yangu , mbona umebadilika sana , yule demu hakupendi achana nae rudi kwenye maisha yako ya zamani tule bata bhana unaboa “

“Ahmed niache nampenda nampenda nampenda merina kuliko kitu chochote kile , ndio mwanamke niliekuwa nikimuota usiku na mchana na kumuacha sio kirahisi kama unavyo ongea “

“ najua unampenda lakini yeye hakupendi unajihangaisha bure tu rafiki yangu na kujitafutia matatizo “

“ bhna wee hebu niache na maisha yangu , ananipenda hanipendi mimi atakuwa wangu tu milele na atakae ingilia penzi letu nikimgundua ama zangu ama zake nitamtoa ubongo .”
Hayo yalikuwa ni ulevi wa patrick siku hio alikuwa amelewa na alichokuwa akiongea alikuwa akimaanisha kweli hakutaka kuamini kabisa kuwa merina hakuwa akimpenda .

****
Basi tukirudi kwa damiani Laptop ile ilizimika ghafra kuashiria kuwa haikuwa na moto , na hapo ndipo alipokumbuka kuwa siku zilizopita alizima ikiwa imeisha chaji na hakupeleka kwa jirani yake kuchaji , alitoka na kuelekea nyumba ya jirani yao hapo hapo kijijini iliokuwa na umeme na kisha aliomba kubustiwa kwa dakika kama tano huku akikaa kwenye masofa yaliokuwa sebleni hapo kusubiria na zilivyopita dakika tano tu aliichukua na kurudi nayo nyumbani kwao ,huku akiahidi kuileta kuijaza kabisa chaji

Alirudi nyumbani kwao na kisha aliwasha na kuchukua ile flash na kuichomeka na ilifunguka na haikuwa na mafaili mengi , ilikuwa na faili la video , aliplay na kuisikiliza.

“ NADHANI UNAANGALIA VIDIEO HII HUKU NIKIWA SIPO TENA DUNIANI , INAWEZEKANA SIKUJUI NA TUMEKUTANA MUDA MFUPI , HILO HALIJALISHI ILIMRADI ULICHONACHO MIKONONI MWAKO KIPO SALAMA , DHUMUNI YA KUREKODI VIDIO HII NI KUKUAMBIA KWAMBA NAFURAHI KUKUAMBIA KUWA WEWE NDIO MRITHI HALALI WA MALI ZANGU ZOTE NINAZO MILIKI , LAKINI ILI KUMILIKI MALI ZANGU HIZO KUNA HATUA ZA KUPITIA NA ILI KUJUA HATUA HIZO NI LAZIMA UWE JASIRI , MTAFUTE MTU MWENYE NAMBA O713**** ATAKUPA MAELEKEZO YA KILE UNACHOTAKIWA KUFANYA UTAJITAMBULISHA KWA NAMBA NILIZOAMBATANISHA KWENYE KARATASI ZILIZOPO KWENYE BAHASHA ULIOTOLEA HII FLASH , MWISHO MTAFUTE MTU MWENYE HIKI KIDANI ( ALIKIONYESHA ) KISHA MUONYESHE KIDANI KILICHOKUWA KWENYE MKEBE HUYO ATAKUWA NI MWANANGU NA NAOMBA UKIFANIKISHA HILO CHUKUA KIDANI HICHO NA KITAKUWA UFUNGUO NA KINAELEKEZA ENEO NILILOACHA HAZINA YANGU NA HATI INAYOKURUHUSU KUMILIKI MALI ZANGU ZOTE.” na video iliishia hapo .

Damiani alielewa lakini ni kama mtu ambae hakutaka kuelewa Bruno alichokuwa akimaanisha , hakujua ni lipi alifanye kwa wakati huo , alikumbuka siku bwna huyo alipo mkabidhi bahasha hio na ni kweli kama alivyo ongea ni kwamba hawafahamiani , lakini pia kijana damiani alikuwa na hasira sana na mzungu huyo aliona yeye ndio chanzo kikubwa cha mama yake kuuwawa kikatili .

Aliwaza na kuwazua maisha yake kwanzia siku hio anakwenda kuishije , hakuona namna , lakini wakati akiwa anawaza kuna jambo lilimjia akilini , na lilikuwa ni kama picha , na ni kama ni jambo alilokuwa amelisahau , alikumbuka mama yake kuna kitu alitaka kutamka na alionekana kuna kitu alichokuwa akinyooshea kidole , hakuelewa ni kitu gani alikuwa amenyooshea kidole lakini aliamini kulikuwa na sababu . alijikuta akikurupuka na kukaa kwenye kitanda huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio na jasho liianza kumtoka , alifumba macho kama mtu aliekuwa akivuta kumbukumbu , na alifanikiwa kukumbuka kuwa siku ile alikuwa na kivinje , lakini aliendelea kujiuliza ilikuwaje mama ake likuwa akinyoosha mkono . alijjikuta akiamka na kwenda mahali mama yake alipomkuta na staili aliokuwa amekaa , kwa jinsi alivyokuwa anafanya kama mtu wa nje angemuona angesema kijana sasa alikuwa akichangayikiwa .

Alijaribu kumuigiza mama yake alivyovyokuwa amenyoosha mkono na hapo ndipo alipo ona uelekeo , ilikuwaa ni nyuma ya mlango sehemu ambayo ilikuwa na majembe na kuni zilizosimamishwa na hapo hisia zake zilicheza na kuanza kuvuta picha na kugundua kuwa kuna mtu aliekuwa amejificha nyuma ya mlango .

“ inamaana siku ile muuaji alikuwa amejificha nyuma ya mlango ?” alijikuta akijiuliza hilo swali na hapo aliona hisia zake ziko sawa kabisa .

“ ngoja niende kwa mzee kivinje “ aliongea huku akinyanyuka na kuelekea nyumbani kwa kivinje , alitembea haraka haraka na kufika ndani ya mji wake na kuuliza kama alimkuta , aliambiwa yupo ila anmtu anamuagua , aliamua kusubiri na baada ya kama lisaa hivi , kivinje alitoka .

“ karibu bwana damiani “ aliongea kivinje na damiani hakutaka kupoteza muda ndani ya eneo hilo alimueleza kwa ufasaha na kivinje alielewa na alikuwa sasa anatakiwa kujibu .

“ uko sahihi bwana damiani , na siku taka kulizungumza hili , lakini kwakuwa umekuja ngoja nikuambie nilichoshuhudia “

“ siku ile pale nyumbani kwenu kulikuwa na watu wawili mmoja alikuwa amejeruhiwa kwa risasi na wakati tunafika haukuwa makini lakini niliona akitokomea lakini alikuwa ameshika siraha na mimi pale nilishikwa na kiwewe .”

“ wa pili alikuwa mule ndani nyuma ya mlango ila alikuwa amejiziba uso sikuweza kuiona sura yake ,na wa nje pia sikuweza kuona sura yake ila naweza kuwaelezea tu maumbo yao “ aliongea kivinje na hapo damiani alijikuta chozi likimtoka , alikumbuka jinsi mama yake alivyokuwa akinyoosha mkono nyuma ya mlango kumbe alikuwa akimuonesha muuaji alipo .

“polisi umewaambia kuhusu swala hilo ?”

“ ndio nishatoa ushahidi wangu na walisema watanitafuta lakini hawakunitafuta mpaka leo “.

Hapo ndipo damiani alichoka hakujua ni kitu gani akifanye kwa wakti huo , roho ilimuuma sana , aliamua kuagana na mzee kivinje na kuelekea nyumbani kwao , muda huo ilikuwa ni asubuhi karibia wanakijiji wote walikuwa hawapo washaenda mashambani na wanaosoma washaenda shule .

Alirudi na kujilaza kitandani huku akianza kuwazua , kuna wazo lilimjia na wazo hilo aliona alifanyie kazi wakati huo huo , alichukua vile vitu vilivyokuwa katika bahasha na kuvirudisha kama vilivyo na kisha alitoka mpaka nyuma ya choo na kuchimba shimo na kisha alifukia vile vitu vyote na kuweka mazingira kama yalivyokuwa na alirudi .

Lakini sasa baada ya kufika mlangoni kuna jambo alilihisi sio la kawaida , mlango ulikuwa wazi na aliufunga , na muda huo machale yalikuwa yashaanza kumcheza tayari , alisubiria kwa dakika hivi , lakini alipuuzia na kuingia ila hilo ndio lilikuwa kosa kwani ile anaingia tu alikamatwa na kuwekewa kitambaa puani na hapo hapo aliona nyota na kuzima

Alibebwa mzobe mzobe mchana kweupe na kupitisha kwenye vichaka tu na mtu yule aliekuwa amevalia kitambaa usoni lakini alivyofika mbele alikivua na hapo ndio sura yake ilionekana alikuwa ni DERICK kijana wa kimbona .
ITAENDELEA USIKOSE KESHO MUDA WA
 
Write your reply...inaonekanza nzur tatzo itafika mwisho ndo watu tutabaki na alosto tu.
Alaf itaendelea lini na mda gani?
 
MAWASILIANO : 0687151346
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA
Iliishia ndani ya miaka mitano nyuma kipindi ambacho raisi bendera anapewa madaraka rasmi na kutangaza vita zidi ya wauzaji wa madawa ya kulevya
“mimi nafikiri kwa sasa hakuna swala la kuogopa kwani mtandao wetu una mizizi mirefu sana na hata kwa washirika wake pia ni waaminifu , kinachotakiwa kwasasa ni kuangalia upepo kwanza na kuzuia mzigo wowote kuingia nchini kwa muda huku tukitafuta ni mbinu gani raisi anaipanga “ aliongea Bruno kwani ndie aliekuwa kiongozi mkuu wa umoja wa wauza madawa nchini..
“ mkuu ulichosema ni sahihi kabisa lakini swala hili ili lifanikiwe lazima tuwe na mtandao wetu pale ikulu ambao utakuwa unatupatia taarifa “ wakati wakiendelea na kikao mlango ulifunguliwa na aliingia mwanadada aliekuwa amevalia suti ya zambarau mwenye rangi nyeupe mrefu mrembo. Alimsogelea bwana Bruno na akamuinamia na alionekana kuna jambo alilokuwa akimwambia na hapo Bruno alijikuta akitoa macho .

SEHEMU YA SABA
“ kuna nini mkuu ?” aliuliza mkuu wa majeshi .
“washa televisheni hio “ aliongea Bruno .

Ilikuwa ni taarifa ya mkuu wa police akitangaza rasmi kuvunjwa kwa kamati ya ulinzi wa kamati ya maswala ya upambanaji ya madawa ya kulevya (DCEA).
“ hili ni swala ambalo tulilitegemea raisi kulifanya “ aliongea athumani .
“ sio hilo tu kuna kubwa Zaidi “
“ lipi hilo Bruno? “
“ mheshimiwa raisi kavunja kamati zote za ulinzi , chakula , mpaka usafi ikulu “ aliongea Bruno na hapo kila mmoja alitoa leso yake na kufut jasho .
“ naona mambo yanazidi kuwa magumu na tunahitaji kulifaanyia kazi hili haraka iwezekanavyo maana mpaka sasa hatuna mtandao wa kutupatia taarifa kwa kile kinachoendelea ikulu “ aliongea sam.
“ mkuu tunafanyaje? “
“ hapa hakuna cha kufanya inabidi tuhold biashara kwa sasa , nitaandaa ripoti na nitaituma makao makuu ya U-97 , nyie wengine inabidi muwaambie washirika wenu kusimamisha biashara na kufuta ushahidi .”

Na kikao kilifungwa huku kila mmoj akitoka , hakuna hata mmoja kati yao aliekuwa kwenye hali nzuri kiumunekano kwani wote walionekna walikuwa kwenye frustration ( waswasi ).

****

Zikiwa zimepita siku mbili mbele , raisi bendera alisaini sheria mpya ya ubadilishaji fedha za kigeni , uliowasilishwa na gavana wa benki , sheria hio ilikuwa ikizuia taasisi zote na maduka yaliokuwa yakibadilisha fedha kutokubali au kufanya mabadilishano ya pesa za kigeni juu ya kiwango cha dollar elfu kumi yaani milioni ishirini na Zaidi , pili sheria ya kuzuia wasafiri kuingia nchini na kiasi cha pesa juu ya dollar elfu kumi bila kutolewa maelezo TRA .

Sheria hio mpya ilikuwa ni mwiba kwa wafanya biashara wa madawa ya kulevya nchini , na hilo walilipokea kama pigo lingine .

Baada ya mswada huo wa sheria raisi aliendelea na pangua pangua yake kwanzia ngazi za juu bandarini mpaka ngazi za chini alimteua mkuu wa mkoa mpya wa dar es salaam , mtwara , mwanza , tanga , katavi , na kigoma , lakini hakuishia hapo tu aliunda baraza jipya la mawaziri huku pia akimteua waziri mkuu mpya , jamnbo ambalo liliacha wananchi mdomo wazi pamoja na washirika wake kwani mtu alieteuliwa hakutegemewa .

Bwna hamduni saidi rajabu ndie aliekuwa waziri mkuu mpya , mwanzoni akiwa ni katibu ofisi ya waziri mkuu .

Baada ya teuzi hizo raisi aliitisha kikao kingine huku kikao hiki kikiwa na watu wengi Zaidi , alikuwemo waziri mkuu wakuu wote wa idara ya usalama , mkuu wa DCEA mpya alieteuliwa , waziri wa mambo ya ndani bwana rajabu ngasu , waziri wa katiba na sheria alfred peter na waziri wa fedha bwna innocent mushi .

“ hongereni waheshimiwa kwa kuteuliwa kwa kila mtu na nafasi yake , lakini niseme kwamba pia niwapongeze kwa uzalendo wenu kwa nchi hii , kwani kupitia hilo ndio leo hii linatufanya tuwepo mahali hap kwenye hiki kikao , simaanishi kwamba sisi ndio wazalendo tu wa nchii hii , wapo wazalendo wengine lakini sisi ndio wawakilishi wao , na naamini huko nje kwa sasa wanamatumaini makubwa sana juu yetu katika ufanyaji maamjuzi yenye maslahi mapana ya nchi hii .” alitulia kidogo kisha akaendelea

“ nafasi mlizopo zinasababu kubwa sana , na niseme kwamba ni nafasi ngumu sana kwani zina majukumu makubwa sana ambayo mnakwenda kuyatimiza kwa maslahi mapana ya nchi hii nyie kama wazalendo , kama mnavyo jua taifa hili lipo kwenye wakati mgumu sana na kipinid tulichopo sasa ni kibaya sana kwani vijana wanadhidi kuangamia kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya , hivyo basi nimewaita ndugu zangu hapa kwa nia kuu moja ya kuwaapa muelekeo wa serikali yangu , pili kuweka na kuwapa mpango wa hatua za mapambno ya madawa ya kulevya .

“ bwana lazaro kitwana “ (huyu alikuwa ndio mkuu wa DCEA mpya ) kazi yako kuanzia sasa ni kuunda timu ambayo itakuwa na polisi watakao kuwa na kazi moja maalumu ya kukamata kila mshukiwa yoyote wa biashara ya madawa ya kulevya hapa nchini .” aliendelea
“ mkuu wa TISS , mkuu wa majeshi na IGP nadhani faili langu lipo tayari “
“ ndio mkuu “
“ good nikitoka hapa nitalihitaji “.
“hivyo basi kwa umoja wetu hapa ndani nataka nitangaze kwamba kuanzia sasa nyie ni wajumbe wa mamlaka ya kupambana na madawa ya kulevya nchini , mamlaka hii itaongozwa na makamu wa raisi na mwenendo mzima wa maswala haya mtahusika , niwaamnbie tu kuwa vita imeanza na ndani ya mwezi ujao sihitaji kunusa harufu ya aina yoyote ya madawa ya kulevya .” aliongea muheshimiwa na kisha kikao kiliisha lakini mkuu wa majeshi , mkuu wa usalama wa taifa na IGP walibaki .

“ waheshimiwa nadhani kazi mmeimaliza , hivyo nahitaji orodha ya vijana wa kazi .

“Danieli mtalemwa mwenye namba ya utambulisho N00D)( huyu ni komandoo daraja la kwanza amepata mafunzo yake nchini CUBA , china na Thailand , huku elimu yake ya kipelelezi na ujasusi akiichukua nchini Israeli , mafanikio yake ni makubwa sana katika operesheni alizo fanya hapa nchini ikiwemo ya ambone tanga , kibiti na rusumo ni mhitimu wa chuo kikuu UDSM ngazi ya shahada , monash nchni Australia akisomea maswala ya uinjinia .

Suzzane rashidi ( aka miss k) namba za utambulisho N02S huyu ni komandoo daraja la kwanza , lakini pia amefudhu mafunzo ya kipelezi kwasasa yuko nchini urusi kama undercover agent katika misheni ya umoja wa taifa , mafunzo yake kachukua CUBA na thailland huyu ni hatari Zaidi katika udunguaji , lakini pia ni mbobezi katika maswala ya computer (IT).

Zakayo yakobo( agent z ) mwenye namba za utambulisho N01Z huyu ni pia ni komandoo , lakini pia ni mhitimu wa maswala ya kipelelezi ni mhitimu wa chuo cha uigizaji nchini marekani elimu yake ya kimapigano kamalizia nchini china ,, kwasasa yupo chini Indonesia kwenye mashindano ya mitindo .

Wengine ni Irene joseph , martine sheiza na abasi ndumbalo hawa wote ni wana usalama chini ya kitengo cha TISS .”

Alimaliza mkuu wa TISS na kisha alimkabishi mheshimiwa faili hilo .

“ kazi nzuri naamini upembuzi wenu ni yakinifu mkuu wa idara kazi ya kwanza anayotakiwa kufanya agent Z ni ya abduction(utekaji) .

“ unamaanisha nini mheshimiwa kuhusu utekaji , ni nani anapaswa kutekwa?? “

“hio ndio kazi ya kwanza itakayotuingiza katika mtandao wa madawa ya kulevya nikimaanisha mtu anayetakiwa kutekwa ni weak point(sehemu yenye udhaifu ) na tunatakiwa kuitumia kikamilifu , target yetu kwa sasa ni bwana Bruno lamberk” akanyamaza kisha akaendelea .

“ kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba huyu ndio mkuu wa usambazaji wa madawa ya kulevya hapa nchini na afrika mashariki kwa ujumla , chini yake anawashirika wengi ambao hawajulikani na wapo hapa nchini , tukifanikiwa kumpata Bruno basi na washirika wake tunaweza kuwapata , lakini kazi hio sio rahisi kwani hakuna ushahidi wa moja kwa moja , na ili kufanikiwa katika hilo inatupasa kumgeuza mshirika wetu .

wazee walichoka maana walikuwa wakimjua huyo mzungu alikuwa ni mwekezaji mkubwa hapa nchini , na ukiachana na uwekezaji wake alikuwa pia ni moja ya watu waliokuwa wakisaidia jamii sana , sasa kutajwa kwake kama muuza ngada mkubwa nchini jambo hilo lilikuwa ni kubwa na la kuogopesha, na kustajabisha kwa wakati mmoja , lakini ndio hivyo bwana huyu alikuwa akijizificha biashara zake haramu kwa kujivika ngozi ya chui .

“mheshimiwa kama uzungumzalo ni kweli , swala hilo linahusiana vipi na misheni unayotaka aifanye agent Z “

“safi iko hivi , Bruno ana mtoto wake wa siri sana kwa taarifa nilizo nazo na mtoto huyo inasemakana bwana huyu anampenda sana huyo mtoto na anaweza kufanya kitu chochote kile ilimradi mtoto huyo asidhurike kwani ndio anatarajia kuwa mrithi wake , nadhani mpaka hapo mnaelewa kwamba udhaifu mkubwa wa Bruno ni huyo mtoto, lakini jambo la kushangaza mpaka sasa ni kwamba bwana Bruno hamfahamu huyo mtoto kwani mwanamke aliezaa nae kaamua kumficha , na anachojua bruno ni kitu kimoja tu kuwa ana mtoto wa kike .

“ sasa kama hamjui mtoto wake sisi tutafanikiwa vipi kumshawishi aamini kwamba huyo ni mtoto wake? “

“hio kazi niachieni mimi mpango huu haujaanza kusukwa leo tu umeanza muda mrefu mimi ni mtekelezaji tu na nyie pia mnatakiwa kutekeleza swala hilo “

Baada ya msheshimiwa kutoa maagizo hayo zakayo alitumiwa ujumbe wa misheni ambayo alitakiuwa kuifanya nchini marekani, huku akipokea maagizo ya moja kwa moja kutoka ofisi ya raisi .

“ unapaswa kupiga picha baada ya kumteka cheni alio vaa hakikisha sura haionekani mtoto huyo yuko chuo x na picha yake ni hio .

******
Tajiri lamberk alikuwa kwenye wakati mgumu sana wakati huo wa kiuongozi katika umoja wao walio upa jina la UNITY 97(U-97) , aliandaa ripoti na kuikamilisha kisha aliituma makao makuu ya umoja huo yaliokuwa nchini mexico , ripoti hio ilikuwa imejumuisha mwenendo wa maswala ya kibiashara kwa ujumla nchini Tanzania .

Baada ya kutuma ripoti hio masaa machache alipokea ujumbe kutoka makao makuu .

“ we received your report and level 01 unity leader conceded with your recommendations until further notice. “ akimaanisha kwamba kiongozi wa juu kabisa wa U-97 amepokea na kukubaliana na mapendekezo yake mpaka pale taarifa nyingine Zaidi itakapo tolewa .

Baada ya kupokea feedback alisambaza kwa wakubwa walio chini yake huku akitoa onyo la kuchukua tahadhari mapema kwani muda wowote hali inaweza kubadilika.

Siku mbili mbele baada ya kutoa ripoti hio , ilikuwa muda wa saa mbili usiku akiwa kwenye jumba lake la kifahari eneo la mbezi beach , alipokea simu kutoka kwa mtu asiemfahamu , simu hio ilimtaka kuingia upande wa watsapp kwani kuna zawaid yake .

Bruno hakuamini macho yake , mapigo ya moyo yalipiga kite kitu alichokiona na taarifa alio iona ilikuwa ni mwiba kwake .
Kilikuwa ni kidani flani ambacho kilitengenezwa kwa madini ya almasi na kidani hicho kumbukumbu zake zilimpeleka miaka ishirini nyuma , ndani ya miaka miwili tu tokea aanzishe makazi yake nchini Tanzania , miaka hio mara baada ya kuanzisha makazi yake nchini Tanzania akiwa kwenye mawazo sana ya familia yake aliokuwa akiishi nayo katika jiji la new York kuuwawa kikatili sana na hio ilitokana na ugomvi mkubwa aliokuwa nao na wauza madawa ya kulevya wenzake , huku akituhumiwa kuwasaliti, ndipo mkuu wa kikundi hicho alipotuma watu wake na kuiteketeza familia yake na yeye baada ya tukio hilo la kusikitisha katika maisha yake alikimbilia nchini Tanzania , na kwanzia siku hio aliishi akiwa na kisasi moyoni , na kupitia tukio hilo alikuja kujiapia hata kuja kutengeneza familia katika maisha yake yote , lakini baada ya kupita miaka miwili ndipo alipo kutana na mwanamke wa kitanzania kabila la kinyaturu , mwanamke huyu alikuwa ni mfanya kazi wa hoteli ya singita grumet iliokuwa ndani ya mbuga ya wanyama serengeti , ulianza urafiki ndani ya hoteli hio na mwishowe ukazaa mapenzi , kutokana na hali ya kulewa ya bwana Bruno siku hio alijikuta akifanya mapenzi na mwanamke huyo aliejitambulisha kwake kwa jina la wema sufiani , kulivyokucha ndipo alipokuja kushituka akiwa kalaliwa na mrembo huyo , kuanzia siku hio bwana Bruno kila akifika kwenye hoteli hio lazima afanye mapenzi na wema , baada ya mwaka mmoja kupita wa mahusiano yake na wema ndipo siku alipo fika ndani ya hoteli hio kukutana na habari za wema kuwa mjamzito .
Ilikuw ni habari mbaya sana kwake kwani alikuwa ashaweka nadhiri ya kutokuja kutengeneza familia katika maisha yake yote lakini pia aliogopa jambo lililomtokea miaka ya nyuma kujirudia kwa mwanamke wema na mtoto atakaezaliwa , hakutaka kumuonesha wema ni jinsi gani habari hio ilikuwa mbaya kwake , alichokifanya yeye ni kumuonesha kuwa kafurahia habari hio huku kichwani akipanga yake .

Baada ya miezi tisa hatimae wema alijifungua na wakati huo alikuwa ashaacha kazi yake ya uhudumu wa hoteli na alikuwa nyumbani kwao singida , Bruno alipata taarifa ya wema kujifungua mtoto wa kike , iilikuwa habari ya kufurahisha kwake , lakini ya kuogopesha siku mbili mbele ndio siku alio fika singida kwa siri sana na akakutana na wema na hapo ndipo alipo fanya jambo ambalo kwa wema lilikuwa na majonzi sana na kuhudhunisha , kwani alimpa kadi ya benki huku akimwambia hela iliokuwemo humo ilikuwa ni kwa ajili ya matunzo ya mtoto na yake lakini pia alimpa kidani cha almasi kikiwa na cheni , kilikuwa kimetengeneza kwa muundo wake wa kipekee sana .

“ wema consider me I am dead from now on , I have family and I don’t need trouble with your baby , my family will not accept her , and I cant do anything about it, for child safety and yours don’t ever ever look for me .( akimaanisha kwamba kwanzia siku hio amchukulie kama amekufa kwani familia yake haingeweza kumkubali huyo mtoto , na akimwambia kuwa asije akamtafuta tena “

“ kwa wema ilikuwa ni kilio lakini baada ya siku alikubaliana na swala hilo , alikiangalia ile cheni na kisha akamvalisha mwanae , huku akienda benki na kuangalia kiasi cha pesa alichoachiwa na mzungu huyo , zilikuwa ni pesa nyingi sana kwa wakati huo , na kwakuwa mwanamke huyo alikuwa na akili ya maisha basi aliweza kufanya biashara , na biashara hio ikamtambulisha rasmi na kuwa mwanamke mashuru ndani ya nchi , na hio ilikuwa ni baada ya miaka kumi mbeleni , katika wakati wote huo alikuwa akisikia habari za Bruno na kwa Bruno pia alikuwa akisikia habari za wema , baadae wema alikuja kuolewa na henry mushi , kipindi hicho bwana huyo akiwa ni waziri wa maliasili na utalii, lakini jambo ambalo lilimshangza bwana Bruno ni kwamba hakuwahi kumuona mtoto wake kabisa , na hata kwenye familia ya henry na wema hakukuwa na jina la mtoto wake swala hilo lilikuwa likimuumiza kichwa sana na kutaka kujua ni wapi mtoto wake alipo lakini liligonga mwamba , kwani japo alijaribu kuongea na mwanamke huyo hakupata ushirikiano kabisa kwani jibu lake lilikuwa moja kuwa asahau kuwa ana mtoto kwenye maisha yake yote na akiendelea kumfatilia atampoteza , na kwakuwa Bruno hakutaka ugomvi na mwanamke huyo ukizingatia kipindi hicho mwanamama huyo alikuwa na nguvu sana nchini , na mume wake walikuwa ni watu wenye msimamo ndani y serikali hakutaka kabisa purukushani .

Upande pia wa henry hakuwahi kujua kuwa mke wake wema ashawahi kuwa na mtoto , kwani wema hakuwahi kumtambulisha mtoto wake kwake, miaka kadha mbele walifanikiwa kupata watoto pia . kwa hio hio ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka ishirini iliopita .

Basi turudi kwenye mika mitano nyuma siku hio ndio siku ambayo bwana Bruno anatumiwa picha na mtu asiemjua ikionesha kidani hicho ,huku chini ikiambatana na maelezo

“ ukitaka ukweli juu ya mahali alipo mtoto wako fika new Africa hoteli chumba namba 108 siku ya ijumaa saa nne kamili usiku hakikisha jambo hili linakuwa siri yako kosa moja tu utampoteza mtoto wako” huku video ya mtoto wake ikimuonesha katekwa .
inaendelea,...... ..
 
ILIPOISHIA
Basi turudi kwenye mika mitano nyuma siku hio ndio siku ambayo bwana Bruno anatumiwa picha na mtu asiemjua ikionesha kidani hicho ,huku chini ikiambatana na maelezo
“ ukitaka ukweli juu ya mahali alipo mtoto wako fika new Africa hoteli chumba namba 108 siku ya ijumaa saa nne kamili usiku hakikisha jambo hili linakuwa siri yako kosa moja tu utampoteza mtoto wako” huku video ya mtoto wake ikimuonesha katekwa .

UNAENDELEA SEHEMU YA NANE .
Siku hio bwana Bruno aliopokea ujumbe ilikuwa ni siku ya jumanne usiku kwenda jumatano , kwa hio alikuwa na siku mbili za kujiandaa , hakujua watu hao walikuwa ni watu gani na walikuwa wakihitaji nini.

Alitamani kumtafuta wema japo amuulize juu ya swala hilo lakini aliogopa kwani aliona watu hao ni watu waliokuwa wakimjua nje ndani , lakini alijiuliza inakuwaje watu hao wakajua kuhusu mtoto wake , je ni wema anamchezea mchezo , au ni mtu gani , hayo yalikuwa ni maswali mengi ambayo yalieongeza shauku ya kutaka kujua na siku hio ifike .

Hatimae siku iliwadia siku ambayo kwa Bruno aliisubiri sana kwa hamu , ilikuwa muda wa saa tatu kama na nusu hivi ndio aliokuwa akiingia ndani ya hoteli ya new Africa .

Aliingia ndani ya hoteli hio huku akiangalia saa yake , moja kwa moja alielekea kwenye bar ilokuwemo humo ndani na kuagiza kinywaji ,, kilichomshangaza ni kwamba siku hio ndani ya bar hio kulikuwa na ulinzi mkubwa sana ambao mpaka yeye ulishangaza ila hakutaka kujali sana .

Alivuta muda mpaka ilipofika saa nne kamili ndipo alienda mpaka kwenye lift na kuelekea sehemu alipoambiwa sekunde kadhaa tu alikuwa nje ya chumba namba 108 , aligonga mlango na ulifunguliwa na mwanadada mmoja mrembo hivi mrefu alievalia suti nyeusi , aliingia na kisha alikaguliwa na mashine kisha alionyeswa kukaa kwenye moja ya sofa lililopo humo ndani huku akiambiwa subiri na muda mfupi baadae ndipo alipopigwa na mshituko baada ya kumuona mtu alieoko mbele yake .
“ mheshimiwa raisi “
“ ndio bwana Bruno karibu sana “ aliongea raisi na kwenda kukaa na baada ya hapo kuliletwa vinywaji aina ya cocktail(mvinyo) na akakaribishwa huku wengine wakiwapisha kwa maongezi
“nadhani upo kwenye mshituko bwana Bruno mkubwa sana , lakini nitangulie kwa kusema kuwa nakujua nje ndani , najua historia yako nzima ya maisha yako kwa ujumla , na hata simu na ujumbe uliopokea juzi unatoka kwangu”
“nimekusikia muheshimiwa , lakini ni nini dhumuni ya haya yote na unamjuaje mwanangu ?”
“safi sana Bruno najua mahusiano yako ya nyuma na wema , lakini pia namjua mtoto uliezaa na wema , nadhani uthibitisho niliokutumia umeuona , hapa nizungumzapo , mtoto wako yupo mikononi mwangu “
“Bruno lamberk alijikuta akipandwa na hasira na uchungu wa ajabu maana kila akimkumbuka mtoto wake huyo na jinsi alivyohangaika japo kuijua sura yake, jambo hilo lilimuuma lakini pia lilimpa shauku na furaha ya kujua kuwa mtoto wake yupo hai “
“ ni kweli mheshimiwa unachozungumza , lakini sijajua sababu ya haya yote “
“ kama nilivyotangulia kusema nakujua nje ndani , ndio kitu kinachonipa sababu ya kuwepo mahali hapa kuzungumza , najua kwamba wewe ndio kiongozi wa genge la uuzaji wa madawa ya kulevya afrika mashariki yote huku ukijificha kwa kujifnya kutoa misaada huku ukiharibu vijana wataifa hili ambao ndio nguzo ya nchi hii” aliongea raisi na wakati huo alikuwa siriasi kweli na alimfanya Bruno ashituke .
“unataka nini kwangu muheshimiwa ?”
“ nadhani mpaka sasa ushajua ninacho hitaji , nataka kuondoa biashara yote ya madawa ya kulevya nchini na wewe utanisaidia katika hilo “.
“hahahha.. mheshimiwa hilo ni jambo ambalo haliwezekani kabisa , na ni bora ukaendelea kuongoza kwa utulivu huku ukichana na swala hili kabisa litakuletea matatizo mbeleni “
“ nadhani bwana Bruno unanichukulia kirahisi , nimetoka mbali na kuyaweka rehani maisha yangu mpaka kufikia hatua hii na usitake kunitishia kwamba haliwezekani , linawezekana kabisa na wewe utakuwa mmoja ya watu ambao utasaidia katika hilo vinginevyo utaletewa zawadi ya mtoto wako akiwa maiti “.
“ huna huo ujasiri bendera wa kuuwa watu , na nikutahadharishe tu kwamba usije ukathubutu kumgusa mtoto wangu , utakiona kiti chako cha uraisi cha moto sana “
“kwa hio unataka kusema kwamba humtaki tena mtoto wako , au unanipima kama naweza kuua au siwezi sasa subiri uone “ aliongea na kisha alibofya simu akaongea kwa lugha ya kifaransa ambayo kwa Bruno ilisikika vyema baada ya sekunde bwana Bruno alipewa simu na hapo ndipo alipo sikia sauti mwanadada akilalamika kwa maumivu ya mateso .

Raisi aliichukua kisha akaiweka sikioni “ you can kill her now “ aliongea na kisha alimpa bodigdi wake simu huku akinyanyuka akiondoka .
“ wait bendera “
“ unataka nini kutoka kwangu “
“ are you ready to talk?? “ aliuliza raisi akimwangalia Bruno alietingisha kichwa kuwa yuko tayari na raisi alirudi na kukaa .
“ nahitaji kujua mtandao wa madawa ya kulevya unavyofanyika hapa nchini ,watu wote waliopo chini yako majina yao na mahali wanapo patikana “
“ unaloongea ni gumu kutendeka maana nitakuwa na wasaliti wenzangu na nitakapo sema tu jua na mimi nitakuwa mfu “
“ unamaanisha nini kuwa mfu ?”
“ kwasababu mimi sio mwanzilishi wa mtandao huo hapa Tanzania kuna waanzilishi , mimi nilipewa uongozi tu “
“tutakupa ulinzi na hakuna baya lolote litakalokukuta “
“ huna ulinzi wa kunipa mimi , mtandao una mizizi mirefu mno kuanzia ikulu mpaka idara za usalama kote huko kuna washirika na inawezekana hata huyo utakae nipa anilinde akawa mshirika , sasa niambie ni ulinzi gani ambao unataka kunipa ?”
“Bruno I am not asking you here , mtoto wako maisha yake umeyabeba wewe , na hapa huna choice ni wewe kukubaliana na mimi au mtoto wako afe , pili nakuambia nitakupa ulinzi so you have nothing to fear “
“ okey let do it , lakini nayafanya haya kwa ajili ya mtoto wangu sio vinginevyo na nataka unihakikishie ulinzi wa mtoto wangu “ aliongea Bruno na raisi alikubali hilo na muda mfupi baadae mwanadada mmoja aliingia akiwa na karatasi mkononi ulikuwa ni mkataba ambao ulipaswa Bruno asaini , ulikuwa na vipengele ambavyo bruno baada ya kumaliza kusoma alijikuta akitoa jasho .
“ alishika karamu huku akitetemeka na kumfanya raisi atabasamu , lakini Bruno aliishia kusaidi mkataba huo .
“ hongera sana na nikuambie hakuna baya lolote litakalo kukuta na kwanzia sasa na nataka nikutambulishe kwa walinzi wako wapya .” alitoa ishara na kisha waliingia watu wawili ,waliovalia suti alikuwa ni msichana mdada mrembo kweli mrefu wa rangi ya chocholate , mwingine alikuwa ni mwanaume kwa haraka haraka umri wakeulioonesha sio chini ya miaka 25.
“ huyu ni danieli na huyu ni suzzane . ni wana usalama , kuwanzia sasa ndio watakuwa walinzi wako ni makomandoo wako vizuri , na kesho suzzane utaniletea ripoti kutoka kwa Bruno . aliongea raisi na kisha aliagana na Bruno na kisha kuondoka .
*****
Wakati hayo yanaendelea ndani ya jumba la kifahari la mheshimiwa raisi mstaafu ndani ya sable hio kubwa , alionekana mheshimiwa mwenyewe akiwa sebleni na mvinyo wake akiangalia runinga , muda huo ilikuwa ni saa nne na nusu hivi usiku , alionekna kunogewa na kipindi kilichokuwa kikioneshwa kiasi kwamba hata simu yake ilivyo ingia uumbe wa maandishi alijikuta akihituka .
“mheshimiwa kakutana na Bruno saa nne kamili new Africa hoteli “ ulikuwa ni ujumbe mfupi lakini uliobeba taarifa iliomshitua sana mstaafu .
“ kwanini Bruno akutane na bendera ?”” ni swali la kwanza alilojiuliza huku akisimama akizunguka zunguka hapo sebleni .
“ lazima kuna kitu kinacho endelea sio bure , na kama itakuwa ni jinsi ninavyo hisi basi tumekwisha “ aliongea huku akichukua simu yake na kutafuta namba Fulani kwenye simu yake , na baada ya sekunde kadhaa alikuwa amekwisha kuipata na alipiga na ikapokelewa upande wa pili .
“sam Bruno kakutana na bendera “ aliongea mstaafu na kusababisha kimya kifupi .
“ ni kweli muheshimiwa ??“
“ ndio ni kweli nimepokea ujumbe mfupi kutoka ikulu sasa hivi “
‘ unahisi ni kipi wameongea ?”
“ siwezi kujua , lakini nina hisia mbaya juu ya hili na kama hisia zangu zinanimbia kweli basi itakuwa hatari kwetu .”
“ naelewa lakini Bruno hawezi kufanya hivyo kabisa , naelewa msimammo wake na anakotoka yule ila inabidi kesho tukutane tulijadili hili kwa mapana ili tujue ni kipi Bruno aliongea na muheshimiwa “ aliongea sam na mstaafu alikubali .
Siku ya pili yake asubuhi matajiri hawa walifika ndani ya hoteli ya serena walipo kubaliana , kila mmoja alionakena kuwa na dukuduku la kujua ni kipi Bruno aliongea na raisi.
“ jamani nina hisia mbaya sana juu ya hili , tunaitaji kulitafutia ufumbuzi mapema kabla hata bruno hajajua tulichokifahamu “
“ ni kweli sam na hili tokea jana nalifatilia kwa umakini mkubwa sana , lakini mpaka sasa sijajua wameongea nini , kwani muheshimiwa inaonekana anafanya mambo yake kwa siri sana “
“ sasa tunafanyaje ?”
“ mimi naona tusubiri , ila inabidi Bruno awe kwenye uchunguzi “
“ nina shushu wangu kwenye moja ya walinzi wa Bruno nadhani anaweza kufatilia hilo na akatupa majawabu , nishampa kazi hio tokea jana “ aliongea sam lakini kabla hajamaliza sentesi yake alipokea simu kutoka kwa mtu aliempa kazi .
“ ingia watsapp mkuu “ ilikuwa ni kauli moja tu . na sam aliingia watsapp , zilikuwa ni picha za danny na suzzane walinzi wapya wa Bruno . kwani caption ilisomeka hivyo .
“ Bruno kaongeza walinzi wapya picha zao hizi hapa “ aliongea sam na kisha zilipitiswa kwa kila mmoja ,
“ wanaonekana kama wanausalama “ aliongea mstaafu huku mkuu wa TISS mstaafu akichukua simu ile .
“ unawajua ??”
“hapana , ila kama sura zao zinakuja kuja nitumie hizo picha kuna mtu anisaidie kuzitambua , aliongea mkuu wa mstaafu TISS huku akimkabidhi simu rich sam , na alimfowadia , huku mkuu wa TISS akipiga simu .
“ Michael upo ofisini ?”” ilikuw swali la kwanza
“ ndio mkuu “
“ kuna picha nahitaji kuzitambua nakutumia sasa hivi “
“ sawa “ aliongea na kuzituma huku wote wakisubiria kwa hamu jibu na baada ya dakika kadhaa kulitumwa faili kwa njia ya watsapp .
““Danieli mtalemwa mwenye namba ya utambulisho N00D)( huyu ni komandoo daraja la kwanza amepata mafunzo yake nchini CUBA , china na Thailand , huku elimu yake ya kipelelezi na ujasusi akiichukua nchini Israeli , mafanikio yake ni makubwa sana katika operesheni alizo fanya hapa nchini ikiwemo ya amboni tanga , kibiti na rusumo ni mhitimu wa chuo kikuu UDSM ngazi ya shahada ,na uzamivu monash nchni Australia akisomea maswala ya uinjinia .
Suzzane rashidi ( aka miss k) namba za utambulisho N02S huyu ni komandoo daraja la kwanza , lakini pia amafudhu mafunzo ya kipelezi alikuwa nchini urusi kama undercover agent katika misheni ya umoja wa taifa , mafunzo yake kachukua CUBA na thailland huyu ni hatari Zaidi katika udunguaji , lakini pia ni mbobezi katika maswala ya computer (IT).”

Mkuu wa TISS alitoa jasho , hakutaka hata kuongea kitu aliwapa wenzake taarifa ile na kila mtu alishangaa.
“ nadhani sasa tunapata picha ya kinacho endelea kwasasa , nanusa harufu ya usaliti “. Aliongea sam .
“ sio harufu , Bruno keshatusaliti mpaka sasa na adhabu ya Bruno ni kifo kama sheria ya kundi inavyosema “ aliongea mstaafu raisi .
“ nadhani kwa upande wetu ni swala la kuchukua tahadhari kwa sasa , japo nashindwa kuelewa ni kwa jinsi gani Bruno kahadaika mpaka kukubali kushirikiana na raisi “ aliongea mkuu wa majeshi .
“ mimi naitoa familia yangu mapema bongo huku tukiendelea , ila mheshimmiwa inabidi uandae ripoti ili iende makao makuu tuone wanatoa majibu gani “ aliongea rich sam.
“ ni kweli ila haina haja ya kupaniki kwa sasa , swala hili nitalishughulikia mwenyewe na nawahakikishia hakuna atakaepata madhara .’”
“ ni sawa lakini mimi familia yangu ni muhimu Zaidi “ aliongea sam na kisha kila mtu akinyanyuka . lakini hapo hapo kuliingia msaidizi wa raisi na kumpa kimemo .
“Mheshimiwa raisi bendera yupo mlangoni anataka kuingia “ .
 
SIMULIZI YA KIJASUSI
UMOJA NAMBA 97 (U-97)
UNITY 97 (U-97).
LAST STATEMENT FROM PRESIDENT.

BY SINGANOJR

SEHEMU YA TISA .
UKIMALIZA KUSOMA SEHEMU YA KUMI INAENDELEA HAPA like isikupite
Hadithi na simulizi Media

MASAA KADHAA NYUMA
Bruno mara baada ya kuonana na mheshimiwa raisi ndani ya gari alikuwa na mawazo mengi mno , hali yake haikuwa sawa kabisa kwa wakati huo alikuwa akiwazia maisha yake ya nyuma , picha ya familia yake miaka iliopita kuuliwa kikatili haijawahi kumfutika kirahisi kabisa , familia yake alioipenda kwa moyo wake wote , alijikuta akitoa chozi la kiume , mawazo yalikuwa ni mengi alikumbuka maisha yake yalikuwa ni kama jehenamu kwa maumivu alioishi nayo moyoni , aliapia siku moja lazima aje kulipiza kisasi kwa wale wote waliomsababishia maumivu .

Alijikuta mawazo aliyahamishia kwa mtoto aliezaa na wema , kukumbuka swala hilo alijikuta akifikiria maneno ya miaka kumi nyuma akiwa ndani ya hospitali ya aghakhani .

“ pole sana Bruno kwa sasa unasumbuliwa na prostate cancer na nikwambie tu kwamba huna uwezo tena wa kupata mtoto” ni kauli ambayo ilimuumiza sana , japo wakati anakuja Tanzania alikuwa hana wazo la kutengeneza familia , lakini kadri utajiri wake ulivyokuwa unakuwa ndio hamu ya kuwa na mrithi iliongezeka siku hadi siku na kuanzia siku hio anapewa kauli na dokta mapenzi yake yote akayahamishia kwa mtoto aliezaa na wema , alihitaji kumjua mtoto huyo kwa hali na mali , lakini njia zake zote zilikwama , alijiapia kuja kumrithisha mtoto wake huyo biashara zake zote zilizozahalali , kwanzia siku hio aliishi kwa matumaini huku akiamini siku moja atakutana na mwane na mishowe atamrithisha mali .

“ boss tumefika “ ilikuwa sauti ya dereva iliomshitua bwana Bruno kutoka kwenye mawazo .

Alishuka kwenye gari na kuingia ndani na kujibwaga kwenye masofa ya humo ndani , alikaa kidogo na kisha alinyanyuka na kufuata friji kisha alitoa vodka na kuweka kwenye glass iliojaa barafu kisha alikunywa .

“ I think its time to withdrawal , but my revenge must be done “ aliongea huku akimaanisha anafikiria ni muda wa kuachana na biashara ya uuzaji ngada au madwa ya kulevya .

Alikaa hapo sebleni kwa muda kisha ni kama mtu alieshituka kwani aliinuka na kufata tarakishi yake ya mapakato aina ya mackbook na kuja nayo sebleni na kuanza kuchapa , ilikuwa ni barua ya kujiudhuru uongozi wa U-97 kwa Africa mshariki .

Alimaliza kuchapa na kisha aliingia kwenye mtandao huo na kutuma barua ile .
“its received please wait for feedback ‘’ vilikuwa ni vijimaandishi vilivyosemaka mara baada ya kutuma barua hio ., dakika kumi mbele majibu yalirudishwa .

“mister Bruno lamberk we received your request and reviewed it but according to U-97 rules there is no withdrawal, unless you are ready to die as per rules ,application stutus: “ rejected “”. Akimaanisha kwamba wamepokea ombi lake na wamelipitia lakini limekataliwa na kama sheria zao zinavyosema kwamba hakuna kujitoa labda tu kama uko tayari kwa kifo .

“I am not ready to die until my revenge is taken “ alijiongelesha mwenyewe kwa hasira akimaanisha kwamba hayuko tayari kufa mpaka pale kisasi chake kitakapo kamilika

Aliinuka hapo sebleni akiwa na glass yake ya pombe mkononi na kuelekea ndani chumbani , alifika na kisha alivuta picha ya mlima Kilimanjaro iliochorwa kwa usanifu wa hali ya juu na mara baada ya kuvuta picha hio zilitokea namba flani ukutani kama kijisimu , alibonyeza namba flani na kisha hapo hapo kidroo kilitoka nje kama vile unavyota CD kwenye deki .

Alivuta kijimkebe kimoja na kutoa flashdisk iliokuwa na nembo ya U-97 alitoa flash ile na kisha alifunga kile kijidroo na akaingiza namba zingine tofauti na hapo hapo ukuta ulitengeneza mlango ( yani ulifunguka kama lift inavyofunguka , alingia ndani ya kijichumba na mlango ulijifunga, ilikuwa ni lift maana ilimshusha mpaka chini na mara baada ya kufunguka .

“WELCOME AGAIN MISTER BRUNO IN LEGACY ROOM “ilikuwa ni sauti ya mwanadada ikisikika mara baada ya bwana Bruno kuingia , kilikuwa ni chumba kikubwa kama darasa , kilichokuwa na tarakishi zilizopangiliwa kwa mtindo wa kupendeza kabisa , huku chumba hicho kikinakishiwa na rangi ya blue , kwa mbele kabisa kulikuwa na noteboard , iliokuwa na michoro .

“ I will find you soon “ aliongea Bruno huku akiangalia michoro aliochora huku kukiwa na majina ya uongozi wa U-97

“nani ni level 20 mpaka 1 kwenye U-97?” alionekna kama mtu aliekuwa akijiuliza hilo kuonesha kwamba hakuwa akimjua ni nani kiongozi kuanzia level 1 mpaka 20 .

“aliangalia ile flash na kisha aliamua kutoka humo ndani huku akipiga simu

Ndani ya dakika chache miss k(suzzane) aliingia hapo ndani .
“ nimeitika wito “ aliongea kikakamavu .
“ take this , mkabidhi muheshimiwa nitampigia simu saivi “ alionge

Bruno na wakati huo ilikuwa ni saa saba usiku .
Miss k aliichukua huku akipigiwa simu na mhesimiwa raisi kuwa apeleke moja kwa moja huo mzigo ikulu na alitii .

****
Ni saa moja kamili ndani ya ukumbi wa mikutano alionekana mkuu wa majeshi, waziri mkuu , mkuu wa usalama wa taifa , IGP , makamu wa raisi na waziri wa mambo ya ndani .
“ waheshimiwa sina muda wa kupoteza na nimewaita hapa asubuhi ya leo kwani nahitaji ushauri wenu , mpaka sasa nina faili la mtandao wote wa madawa ya kulevya hapa nchini na kiukweli ni swala la kusikitisha sana kwa kila atakaesoma ripoti hii “ aliongea raisi na kuwafanya walio ndani kushangaaa.

“naomba nisome .

“unity 97 ni umoja ulionzishwa mwaka 1988 nchini mexico , mwanzilishi wake ni marehemu paul alexander marehemu , ulianzishwa kwa jina la U- 01 lakini jin hili lilibadilika siku hadi siku kadri umoja huu ulivyokuwa ukipanuka , dhumuni la umoja huu ni kusimamia biashara zote za mihadarati zilizokuwa zikiendeswa chini ya umoja huu , pamoja na kutoa adhabu , kuimarisha bishara , kulinda wafanya biashara na maslahi yao na kuibua masoko mapya ya mihadarati duniani . kwanini zamani ulikuwa ukiitwa U 01 ?, jibu ni kwamba umoja huu kuanzia kuanzishwa kwake mpaka mwaka huu umejipanua katika mataifa 97 na taifa hilo likiwemo Tanzania “ aliongea raisi na kuwafanya viongozi wshangae .

“ hio ni historia fupi ya umoja huu , kuhusu viongozi wa umoja huu unatolewa kwa mtindo wa level yaani kuna level one na kuendelea , wanaojulikana ni kuanzia level 21 mpaka 97 pekee kama jinsi wanavyotoa uongozi wao huku level 20 mpaka level 01 hawajulikani , kiongozi mkubwa Zaidi ni level 01 .

“taarifa nilio nayo hapa ni umoja huu ndani ya taifa letu pekee na viongozi waliopo katika uongozi na mtandao mzima wa ufanyaji wa madawa ya kulevya kuanzia yanavyo ingia nchini na yanavyowafikiwa watumiaji , list ya juu kabisa yupo mheshimiwa athumani ndalu , yupo mkuu wa majeshi , yupo mkuu wa TISS , yupo mkuu wa mkoa mstaafu wa dar es salaam , yupo tajiri Samuel , yupo bruno lamberk “akanyamaza akameza mate kisha akaendelea

“ sasa kwa list hio fupi , ukijumlisha na nia yetu ya kutokomeza dawa za kulevya hapa nchini nahitaji mawazo yenu juu ya hili maana limekuwa ni swala zito “

“ mheshimiwa kama ulivyosema ni swala zito , na mimi niseme ni swala zito kweli kweli na linahitaji busara Zaidi katika kulifanyia maamuzi “ aliongea waziri mkuu .

“ ni kweli kabisa anayo ongea mheshimiwa waziri mkuu , swala hili ni zito ushauri wangu mimi ni kwamba maamuzi tutakayotoa hapa yasikinzane na msimamo wetu wa kutokomeza madawa ya kulevya nchini .

“ ni kweli kabisa IGP lakini ni kipi kifanyike kwa sasa , nadhani hilo ndio la muhimu na kama ulivyosema kwamba hatuhitaji kuwa nje ya msimamo wetu “ aliongea mkuu wa usalama bwana matinde .

“ mimi ushauri wangu kwa sasa naona swal hili kabla ya kulichukulia maumuzi na kwakuwa linagusa viongozi wa juu kabisa , kwanini tusitafute maridhiano na hawa viongozi wa juu kabisa kuondoa bishara zao kwenye nchi hii , na kama wakishindwa kuondoa biashara zao hatua zingine zichukuliewe “ aliongea waziri wa mambo ya ndani .

“ naunga hoja waziri , nadhani itakuwa busara Zaidi,na kama kweli muheshimiwa mstaafu yupo kwenye hili itahitajika ushahidi wa kuaminika kwa wananchi kabla ya kumkamta , na sidhani ushahidi huo kwasasa tunao na hata kama upo kutakuwa na mvutano mkubwa , hivyo kabla ya kulifanyia maamuzi swala hilo lazima tukae nao chini tuongee kama watakubaliana na msimamo wetu kama serikali “ aliongea makamu wa raisi bwana henry mushi .

“ waheshimiwa nashukuru kwa mchango wenu na niseme hilo pia kwangu lilikuwa ni wazo namba moja na nilichokuwa nikihitaji hapa ni mchango wenu juu ya swala hili , lakini kama mlivyosema juu ya kukaa nao meza moja na kuona ni kwa namna gani tunapaswa kukaa na kulitatua swala hili basi sina budi ya kufanya hivyo , na swala hilo ninalifanya sasa hivi kwani najua niwapi walipo “ aliongea mheshimiwa na kisha aliinuka na kuondoka .

“ nassani tunaelekea serena hoteli “ aliongea mheshimiwa na ulinzi uliandaliwa na akaondoka eneo la ikulu .

******
“Mheshimiwa raisi bendera yupo mlangoni anataka kuingia “ . kilisomeka kile kimemo

Raisi mstaafu alishituka kwa ujio huo wa ghafra wa raisi bendera kwenye kikao chao , alijiuliza ni kwa vipi raisi huyo kajua uwepo wao mahali hapo .

Aliwajulisha wenzake ambao na wao walipatwa na mshangao , waliangaliana kwa sekunde kadhaa na kisha athumani mstaafu alitoa ishara kwa bidada huyo kuwa amruhusu aingie .

Baada ya maongezi na wauza madawa hao , maongezi yaliochukua takribani nusu saa nzima raisi bendera alitoka na kurudi ikulu .

Siku chache baadae msako na kamata kamaa ya baadhi ya matajiri watuamiaji madawa ukiongozwa na mkuu wa mkoa wa dar es salaam ulianza , ulikuwa ni msako ambao ulihusisha mpaka baadhi ya viongozi wa dini , ulikuwa ni mvutano wa aina yake , ulioibua hisia za wananchi , huku wengi wakimpongeza mkuu wa mkoa wa dar es salaam kwa hatua hio ya kupambana na wauza madawa hayo , lakini kuna waliokuwa wakisema kuwa alikuwa akifanya mambo ambayo yalikuwa nje ya madaraka yake .

Hatimae hali ya madawa ya kulevya nchini ilipungua sana , kwani mheshimiwa bendeera alibana pande zote , wafanya biashara wengi walihamia nchi za jirani huku kisingizio kikubwa kikiwa ni kwamba masharti ya uwekezaji nchini yamekuwa magumu , lakini hata hivyo raisi hakuteteleka nchi ikatulia ikawa na Amani yapo mataifa ya nje yaliomuona kama kichaa lakini hakutetereka , wapo pia wana siasa waliokuwa wakimsema vibaya kuwa ni mtu wa kukurupuka , lakini hakusikiliza yote hayo , aliendelea kuchapa kazi huku akijizolea umaarufu mkubwa sana katika maswala mbali mbali ya uongozi wake .

Raisi bendera akamaliza muhula wake wa kwanza , akapigiwa tena kura kwa muhula wa pili na akashinda kwa kura nyingi sana tofauti na ilivyokuwa kwenye kipindi cha uchaguzi uliopita , mwaka wa kwanza wa muhula wake ndipo mheshimiwa raisi bendera kupitia makamu wake henry alitangaza kifo chake , huku sababu ikiwa ni mshituko wa moyo . jambo ambalo liliibua sintofahamu kubwa sana kuanzia kwa wanasiasa mpaka kwa wananchi .

Upande wa bruno na yeye aliingia kwenye vita rasmi na umoja wa madawa ya kulevya wa U 97 , lakini mheshimiwa bendera alijitahidi kwa nguvu zake kumlinda bwana huyo kama ilivyokuwa katika mkataba wake ulivyokuwa ukisema katika baadhi ya vipengele .
Mtoto wake aliachiwa na bendera alimhakikishia kuwa mtoto huyo atakuwa salama kabisa , lakini pia kwa busara za raisi alimuambia kuwa hatakuwa jambo jemba kwa bruno kukutana na mtoto huyo kwani alikuwa katika vita hivyo mtoto huyo angeingia kwenye matatizo .

Lakini kifo cha bendera kinakuwa pigo kwake .
Je unafikiri bendera alikubaliana nini na wauza madawa wakubwa nchini
makamu wa raisi alijounga vipi na U-97 ?
Haya sasa ngoma ndio kwanza mbichi , simulizi ni ndefu sana ina visa vingi vingi mno .

ITAENDELEA USIKOSE
 
SIMULIZI YA KIJASUSI
UMOJA NAMBA TISINI NA SABA
UNITY 97
KAULI YA MWISHO YA RAISI
KABLA YA KIFO
MWANDISHI : SINGANOJR
MAWASILIANO : 0687151346 WATSAPP/SMS

SEHEMU YA KUMI

UMRI JUU YA MIAKA 18
inaendelea hapa >>>>>>>, Hadithi na simulizi Media

TULIPOTOKA
Ni katika kumbukumbu ya miaka mitano nyuma miaka ambayo raisi wa awamu ya nane wa Tanzania mheshimiwa bendera baada ya kuingia madarakani alivyo onesha nia yake ya kutokomeza biashara ya madawa ya kulevya nchini , swala hilo linafanikiwa kwa asilimia kubwa kwa kuingia maridhiano na wafanya biashara wakubwa nchini kwa ajili ya kuondoa biashara hizo nchini .

Baada ya hali ya madawa kutulia nchini hatimae raisi bendera anapata mshituko wa moyo na kupoteza maisha baada tu ya kuingia muhula wa pili wa uongozi wake , henry mushi aliekuwa makamu anakaimu nafasi ya raisi bendera na kuendeleza gurudumu , lakini wakati huo huo raisi henry akiwa ni mwanachama wa kikundi cha umoja namba tisini na saba ( unity 97) umoja ambao kwa taarifa za awali unahusika na kusimamia biashara ya madawa ya kulevya .

Bruno lamberk mfanyabiashara mkubwa nchini ambae alikuwa pia mfanya biashara wa madawa ya kulevya nchini , pia akiwa kiongozi mkubwa wa umoja tisini na saba anawasaliti wenzake kipindi cha uongozi raisi bendera na kumsaidia kutokomeza biashara madawa ya kulevya nchini , lakini kifo cha raisi bendera kinamuweka katika wakati mgumu katika swala la kujilinda kwani alikuwa na maadui wengi ambao aliwasaliti na kuwapelekea kupoteza pesa nyingi na anakuwa adui mkubwa wa umoja namba tisini na saba (unity 97), hatimae maadui zake wanampaata na kumpiga risasi lakini anafanikiwa kuchoropoka na kukimbia anaomba msaada kwa kijana damini mhitimu wa uhasibu chuo cha TIA , kijana damiani anampa msaada matokeo yake anasababisha mama yake kuuwawa na maaudi wa bruno na brunoo kupoteza maisha hapo hapo , damiani anaapia kuwatafuta watu hao waliohusika na kifo cha mama yake na kulipiza kisasi .

TUNAENDELEA HAPA BAADA YA KUMBUKUMBU
Sasa baada ya kumbukumbu hio ya miaka mitano ya uongozi wa bendera huku kifo chake kikiwa cha mashaka turudi sasa kwa damiani , derick aliendelea kumfungia damiani kwenye chumba kile huku kila siku wakijaribu kumhoji juu ya mzigo aliopewa na tajiri bruno lamberk , lakini damiani japo mateso yalikuwa makali sana lakini hakuthubutu hata kuinua mdomo wake kusema ukweli ,alikuwa yupo radhi na amejiapia ndani ya moyo wake kuliko kuwaambia mafedhuli walikuwepio mbele yake ukweli , kila alipokuwa akifikiria kifo cha mama yake , picha ya mama yake kulala kwenye dimbwi la damu alizidi kusisimka mwili na chuki na kisasi vyote kwa wakati mmoja vilimjaa ndani ya moyo wake .

Derick na ujanja wake wote wa kutesa watu ili kupata ukweli kwa damiani aliinua mikono juu , hakujua damiani ana roho ya aina gani , kwa mateso aliompa hakuamini macho yake na masikio yake kwamba kijana huyo hakuwa tayari , mwisho wa siku alijua kabisa kwamba walikuwa wakipoteza muda na kijana huyo na hakuwa akijua lolote .

Derick alitoka hadi nje ya jumba hilo kisha alizunguka nyuma kabisa na kuwaona vijana wake anao waongoza katika ngome hio wakiwa bize kucheza karata , alipiga mluzi na wote waligeuka na kumwangalia , huku akionesha ishara kwa mmoja ya vijana hao wapatao wa nne walioonekana kuwa na miili ya kimazoezi , aliita kiijana mmoja ambae alikuwa ni kiongozi wa wenzake .

Kijana aliemuita alikuwa na mwili mkubwa kidogo na walikuwa wamesimama nje kabisa ya ua , lakini katika hali ambayo haikutegemewa mara yule kijana alimtemea damu derick usoni na hapo hapo akaanguka chini na kupoteza maisha hali iliomfanya derick ageuze shingo haraka haraka lakini alikuwa amechelewa kwani alijikuta akipigwa risasi ya bega huku aliempiga hamuoni , alikimbilia ndani kuchukua siraha yake huku wale vijana akiwapa ishara lakini kufumba na kufumbua vijana wote walikuwa chini wakiuguliia maumivu kwani walikuwa tayari washapigwa risasi.

Damiani akiwa ndanii ya chumba alichofungiwa akiwa hana nguvu kabisa , alisikia mlango ukifunguliwa na mawazo yake alijua mateso yalikuwa yanaendelea , lakini mtu alieingia hapo ndani kidogo alimshangaza , kwanza kwa haraka haraka alivyomwangalia utembeaji wake alijua kabisa mtu huyo alikuwa ni mwanamke .

“ unaweza kwenda “ aliongea kwa sauti ya ukali yule mwanadada ambae kwa damiani alishindwa kuona sura yake kwani alikuwa amejiziba uso na hio ni baada ya kumfungulia .

Damiani hakutaka kuzubaa , japo alikuwa na maumivu makali aliokuwa akihisi katika mwili wake , hakutaka kuendelea kukaa hapo ndani , alijiinua na kisha kwa mwendo wa maumivu sana alijitoa nje huku akishangaa damu iliotapakaa kila mahali ndani ya jumba hilo ,alitoka hadi nje ya uzio huku akishindwa kujua ni sehemu gani aliopo , , alitembea haraka haraka kwa kujikongoja kwa kuchchemea , mpaka nje kabisa ya uzio wa nyumba hio na kufika barabarani ,, ilikuwa ni barabara ya vumbi lakini iliotengenezwa vizuri kwa changarawe .

Alichukua upande wa kushoto wa barabara hio na kuanza kujiburuza kwa mwendo wa tahadhari , huku akipita katikati ya baadhi ya vichaka , baada ya dakika tano za kutembea alisikia sauti ya gari ikija kutoka mbele yake , na hakutaka yalio mtokea kumtokea tena kwani alikimbilia kichaka na kujificha , na sekunde kadhaa gari ile ilipita , ilikuwa ni gari aina ya land cruser , iliokuwa ipo kwenye spidi kali .

Kwake kuona gari ya aina hio ilikuwa ni hatari kubwa na aliona bado hakuwa ametoka kwenye mikono ya maharamia waliokuwa wamemteka , alitembea kando ya barabara kwa tahadhari kubwa mpaka alipotekelezea kwenye mji mdogo uliokuwa kimya , alijivuta mpaka kwenye moja ya nyumba iliokuwa karibu yake ilio ezekwa kwa nyasi na kujengwa kwa udongo na miti na kisha aligonga mlango lakini hakuna aliekuwa akiitika lakini muda kidogo alisikia suti ya karibu nyuma yake .

Alikuwa ni mama mmoja alievalia nguo zake zilizochakaa huku mama huyo akionekana kudhoofu , huku mkononi akiwa ameshikilia majani ya maboga na alionekana alikuwa akiandaa chakula cha usiku .
“ karibu “ mama huyo aliongea huku akimshangaa damiani kwani nguo zake zilikuwa zimechafuka na kugandiwa na damu “.
“ asante mama yangu , nina kiu ya maji “ aliongea damiani na mama huyo aliingia ndani kwa wasiwasi na kutoka na jagi la maji , na kumpa .
“ mama samahani hapa kunaitwaje ?”
“ hapa ni kijiji cha makumbara “
“ ni mbali na mkuzi ?”
“ ndio ni mbali sana kutoka hapa mpaka upande hiece au noah zinazoenda huko au bodaboda “ aliongea mama huyo.
“ sawa asante mama yangu “ aliongea huku akiendelea kutembea mbele ya barabara hio muda huo ilikuwa yapata saa kumi na moja jioni kwenda saa kumi na mbili na hata kijua kilikuwa kikielekea kuzama , damiani alikuwa akihisi maumivu makali kwenye mwili wake lakini hakutaka kupumzika , alipanga atembee umbali mrefu kidogo huku akitumainia kupata lift itakayo mfikisha nyumbani , hilo lilikuwa kwake wazo la kwanza , na wazo la pili lilikuwa ni kutembea na akiona amechoka aombe hifadhi kwa wasamaria wema.
Kadri alivyokuwa akitembea nguvu zilikuwa zikimuishia kabisa , alikuwa akihisi njaa kali ndani ya tumbo lake huku magoti yakizidi kumsumbua kwa maumivu , alitembea umbali mrefu , alipita kijiji cha kwanza na watu wake wala hawakuwa na habari nae Zaidi ya kumshangaa , huku akitegemea kijiji kingine atakachokuta mbele yake ndio apumzike na aombe hifadhi , lakini kadri alivyokuwa akitembea ndio nguvu zilivyokuwa zikimuishia kabisa na hata macho yalikuwa yakikosa nguvu , bodaboda zilimpita bila kumjali japo kuna muda aliaribu kupungia mkono lakini hakuna aliweza kusimamisha .

Lakini wakati huo giza lishatanda kila kona akipita kwenye moja ya kona ndipo aliposikia sauti ya gari kwa mbali ikiwa inakuja kutoka nyuma yake , akili yake ilifanya kazi huku akiamua kujitoa muhanga tu , alijishauri akae katikati ya barabara , na hakujali tena kwamba alikuwa na maadui eneo hilo na wanaweza wakawa ndio hao wanakuja upande wake , lakini kwa hali yake aliamua kuweka maisha yake rehani na kusimama katikati ya barabara , na dakika kama mbili hivi ndipo alipo mulikwa na mwanga wa gari aina ya rangerover sport nyeupe , aliishia kupunga mkono huku akiwa amesimama katikati ya barabara huku macho yakikosa nguvu na hapo hapo alidondoka chini na giza lilitanda kwenye macho yake na hakujua kilicho endelea .

Harufu ya manukato na ubaridi ndio kitu alichoanza kukihisi kwenye
pua za masikio yake japo alikuwa akihisi uvivu wa hali ya juu kufumbua macho yake lakini alijikuta akijitahidi , kwa mbali alianza kuona mwanga wa taa uliomulika kwenye macho yake na kumfanya arudie kufumba macho huku akianza kuyafungua taratibu , ili kuzoea mwanga , alihisi maumivu kwa mbali lakini hayakuwa makali sana .

Alifanikiwa kufumbua macho yake kabisa na kushuhudia akiwa ndani ya chumba ambacho juu yake kulikuwa na feni inayo zunguka , kitu cha kwanza kilichomjulisha eneo alilokuwepo ni madirisha na rangi ya mapazia yaliokuwemo humo ndani na moja kwa moja akili zake zilimwambia kuwa eneo alilokuwepo ni hospitali , alijaribu kugeuza shingo yake upande mwingine ili kusanifu Zaidi mazingira , japo shingo ilikuwa ikimletea maumivu lakini alifanikiwa kuizungusha na hapo ndipo alipo kutana na mtu aliekuwa amelala pembeni yake huku nywele za kichwa zikiwa zimemfunika uso , hakujua mtu huyo ni nani lakini fahamu zake za utambuzi zilimwambia kuwa mtu huyo alikuwa ni mwanamke . alijaribu kutingisha mguu wake na hapo ndipo alipo mfanya mwanamke huyo kunyanyua kichwa chake .
“ Damian !!!..” ilikuwa ni sauti ya kike tena ile nyororo ya kumtoa nyoka pangoni , sauti ambayo haikuwa hata na aina moja ya mkwaruzo .
Damiani alijikuta akiachia tabasamu hafifu lililofanya mrembo huyo kutoa machozi ya furaha , alijikuta akimuinamia na kisha alimbusu kwenye paji la uso kwa hisia kali sana .

*******
Ni jambo la kawaida sana kwa binadamu pale wanapofanya vizuri na kusifiwa hata kupewa zawadi , ama kupandishwa cheo kazini , watataka kufanya bidii zaidi katika kazi zao ili waendelee kuwa na sifa zote zile za uchapaji kazi , hii ni moja ya mbinu kubwa sana kwa wale waendesha taasisi ambao wameajiri wafanyakazi , na hata pia kwa serikali kwa ujumla hutumia ili kiluhakikisha wafanyakazi wao wanaongeza juhudi na ufanisi katika kutekeleza majukumu yao .

Kama ilivyokuwa kawaida basi pia kwa bwana kimbona ilikuwa hivyo hivyo , kimbona mara baada ya kuwekwa katika kikao cha wakuu wa wa mtandao wa uuzaji wa madawa ya kulevya nchini jambo lililotokea kwa ufanisi wa kazi yake ya kumua Bruno lamberk , kwake swala hilo alilichukulia kqma moja ya mafanikio makubwa sana na hatua kubwa ya kufikia malengo yake , mzee huyu ambae umri ulikuwa umeenda kidogo kwa kuvuka daraja la vijana na kuingia la wazee alikuwa na malengo makubwa ya kujipanua kibiashara zaidi , kwani hela aliokuwa nayo hakuona kama ilikuwa ikimtosha ila zaidi sana alitaka kurudisha kiasi cha pesa alichokipoteza wakati wa uongozi wa marehemu raisi bendera .

Akiwa ndani ya ofisi yake ya makao makuu ya kampuni yake , alikuwa akiwaza hili na lile lakini wazo kuu lililokuwa katika ubongo wake lilikuwa ni jinsi ya kukamilisha kazi aliokuwa amepewa na wakuu wa mtandao na yeye akiwa mmoja wapo, kazi hio ilikuwa ni kujua ni wapi nyaraka zilizokuwa zikihusu mali za bruno zilipokuwepo , kwani simu aliokuwa amepokea kutoka kwa kijana wake derick ilimfanya aone ni ugumu wa aina gani kufumbua fumbo hilo , lakini pia hakutaka kusbindwa kazi hio kwani aliamini wakuu wake wasingemuelewa na pia kwake ilikuwa kazi ya kwanza ambayo alikuwa akitaka kuikamilisha kwa ufanisi mkubwa sana ili aweze kupanda cheo zaidi .

Alijizungusha kwenye kiti chake hapo ofisini na kuangalia nje ya jiji kama mtu alkekuwa amevutiwa na jambo fulani kwenye barabara iliokuwa ipo bize kuruhusu magari kupita huku na huko .
" kama nyaraka anazo danny itakuwa ngumu sana kwa vijana wangu kuzipata , lazima ni mtumie mtu mwenye ujuzi wa hali ya juu kupambana na danny ili kufanikisha swala hili " Aliwaza .
" Lakini ni nani anaweza swala hilo ???" mawazo yalikwama kwenye swali hilo hakujua ni mtu gani sahihi ambaye alikuwa akipaswa kufanya kazi ambayo ilikuwa mbele yake .

Aliwaza kwa muda na kujikuta akitabasamu kwani kuna jina lilikuwa limejipenyeza kwenye akili yake .
"Carlos cardoso " jina hili liliibuka kwenye kichwa chake na kujikuta akitabasamu " he is perfect candidate for the work " aliongea huku akisimama .
" Lakini nampataje kwa maana yupo gerezani na sijui ni gereza lipi , kuna haja ya kuongea na sam anisaidoe katika hili " aliongea na hapo hapo hakutaka kupoteza muda kwani alichukua simu yake iliokuwa mezani na kisha alianza kutafuta jina la sam na baada ya kulipata alipiga na simu ilianza kuita upande wa pili .
" hellow ! Sam"
" vipi rafiki yangu ?"
" Safi lakini sio shwari "
" kwanini unasema hivyo , kazi imekuwa ngumu ?" .
" kazj imekuwa ngumu , kwani mtu tulokuwa tukimshuku kwa kuwa na nyaraka. alizoacha bruno anaonekana kutokuwa nazo "
" kwanini unasema kwamba inaonekana hakuwa nazo , kama ushahidi wote unamuangukia yeye?"
" Tumemkamata na kumpa mateso ataje ni wapi nyaraka hizo , ila hakuweza kusema mahali zilipo , na kwa mateso ya daraja la kwanza kwa mtu ambae hana mafunzo ya aina yoyote ni ngumu kuvumilia , hivyo tukaja na jibu kwamba kijana huyo hana nyaraka hizo "
" kama unayo ongea ni kweli unahisi ni nani ana nyaraka hizo ?"
" Dannieli mtalemwa , huyu ndio aliekuwa akishirikiana mambo mengi na bruno , na sio kushirikiana tu pia bruno alikuwa akimuamini sana " .
" kama ni kweli swala hilo litakuwa na ugumu , maana nadhani hapa unajua tunamzungumzia mtu wa namna gani " .
" Ndio maana nimekupigia simu hii , nahitaji msaada wako "
" msaada wangu upi kimbona ?"
" Nahitaji kuonana na mheshimiwa raisi ".
" unataka kuongea nini na muheshimiwa bruno , na swala hilo litakuwa gumu kidogo “.
" Naelewa. kuwa ni gumu lakini unajua umuhimu wa swala la nyaraka za bruno katika kupata mali zake ,na wewe ndio moja ya watu wanaotaka swala hili lifanikiwe , nina plani za kupata nyaraka hizo ila ni baada ya kuonana na raisi" kilipita kimya kifupi .
" Sawa nitakukutanisha nae "
" Nashukuru sam " waliagana na bwana kimbona alikata simu lakini ukawa ni mwanzo mwingine wa kupokea simu nyingine , aliangalia jina likikuwa ni derick .
" vipi derick "
" boss mambo sio shwari huku tumevamiwa vijana wamejeruhiwa na , damiani katoroka " .
" ni nani aliewavamia ?".
" boss sijabahatika kumuona sura lakini anahaiba ya mwanamke , na anaonekana ana mafunzo ya kijeshi " .
" wewe uko wap ?"
" nipo ndani ya ngome vyumba vya chini".
" sawa namtuma meja afike mahali hapo " aliongea na kisha simu ilikatwa , kimbona alitafuta jina la meja na kupiga na kumpa maelekezo ya kwenda ngomeni .
" Lazima watakuwa watu wa mwenda zake " alijiongelesha

********
Hali ya Patrick kumpenda na kutomkatia tamaa merina hatimae wiki moja mbele tokea aongee na merina juu ya mabadiliko yake hatimae alifanikiwa kumrudisha mrembo huyo katika himaya yake .
“ahmedi nakwambia mtoto nishamrudisha kwenye mikono yangu sasa hivi katulia “ aliongea Patrick siku hio alipokutana na ahmedi rafiki yake club .”
‘ hongera sana , ila sasa nikushauri usizembee , hakikisha unamvua nguo yule mtoto atatulia tuh “ aliongea ahmedi na kumfanya Patrick akune kichwa .
“ come on Patrick yaani na umafia wako uliokuwa nao kwanzia chuo , unashindwaje kwa mwanamke kama merina “
“unajua ahmedi sio kama nashindwa , kuna ugumu Fulani mbao unatokea na hio yote ni kutokana nampenda sana merina , na nishaweka ahadi wake “
“ hhahaha.. dah ! rafiki yangu yaani utadhani leo ndio kwanza unakutana na wanawake , hio ni misimamo tu , bro ukishamfikisha kitandani ukamlegeza kazi kwisha “
“ sasa ulifikiri namfikishaje kitandani , wakati hata kuja kwangu hataki “
“ nendeni vacation , na kwakuwa mmepatana juzi lazima atakubali kwenda na wewe vacation “.
“ hapo kweli umeongea , ngoja nijaribu “.
Patrick baada ya kuachana na rafiki yake hatimae alirudi nyumbani kwenye muda wa saa tatu hivi , alifika na kujitupa kitandani katika nyumba yake iliokuwa maeneo ya kigamboni na kisha alitoa simu yake na kumpigia merina na simu haikukawia kupokelewa na mlimbwende huyo .

Walianza kuongea kimahaba kwa muda mrefu na hapo ndio ikawa nafasi kwa Patrick kuomba waende vacation na mrembo huyo , pasipo kutarajia mrembo huyo alikubali jambo ambalo kwa Patrick lilikuwa ushindi mkubwa sana .

“ mambo view hotel “ lilikuwa ni wazo lililomjia Patrick kichwani , ni hoteli ambayo ilikuwa ikipatikana mkoani tanga ndani ya wilaya ya lushoto ikiwa kati ya kijiji cha mtae na sunga , ni moja ya hoteli iliokuwa ikimilikuwa na bwana Bruno lamberk .

Wiki moja mbele hatimae waliaga wote makazini kwao na kusafiri kuelekea mambo view , ilikuwa ni safari ndefu lakini ambayo haikuchosha hata kidogo kutokana na vijimambo walivyokuwa wakifanya wapenzi hao .

“ bebi huku ni kuzuri “ aliongea msichana merina huku akishangaa milima hio ya usambara .

“ ndio ni kuzuri sana kumetulia na kuna hewa safi ni mahali pazuri kwa ajili ya kupumzika .”
Walifika ndani ya hoteli hio na kupatiwa vyumba viwili japo Patrick alisema wanahitaji chumba kimoja lakini kwa merina alisema anataka vyumba viwili , patrick ilimkera lakini hakutaka sana kuonesha dhamira yake .

Siku hio kila mtu alichoka sana , kwani baada ya chakula waliingia kila mtu chumba chake na kulala.

Merina baada ya kujirusha kitandani na kujifunika shuka , alijikuta mawazo juu ya damiani yakimjia ,, alikuwa na hisia kali sana na mwanaume huyo na alikuwa akimtesa sana , japo alikuwa amemkatia tamaa ya kuonana nae , lakini bado taswira yake haikumtoka akilini kabisa .

Hatimae kulipambazuka mtu wa kwanza kuamka alikuwa ni merina , alijiswafi na kwenda kwenye chumba cha Patrick na kumgongea .
Walisalimiana kwa kukumbatiana na mabusu kibao huku Patrick mhogo ukiwa umesimama maana alikuwa amevaa kibukta tu baada ya kukutanisha miili ulimgusa merina ambae alipata msisimko wa ajabu lakini alijikaza na kujitoa kwenye mwili wa Patrick huku akimuambia akaoge ..

Walikunywa chai na kisha ilivyotimu muda wa saa nne walitoka nje na kushangaa eneo hilo jinsi lilivyokuwa likivutia kwani hoteli hio ilikuwa kwenye mwamba , walipiga picha na kuburudika mpaka muda wa saa kumi hapo ndipo waliporudi ndani kwenye chumba cha Patrick na kuagalia muvi , wakati wanaangalia muvi Patrick aliona hio ndio ilikuwa nafasi ya kutimiza azma yake , na ni kama kuna kitu alikuwa akikisubiria kifike kwenye muvi hio , na kweli baada ya muda muvi ile ilifikia sehemu pendwa wahusika wakifanya mapenzi .

Japo kwa merina aliona aibu lakini pia alianza kupata msisimko wa mwili , wakati huo alikuwa amemuegamia mpenzi wake na pumzi ya Patrick ilikuwa ikimpuliza kwenye kisogo .

Patrick aligundua hali aliokuwa nayo mrembo merina na hakutaka kabisa kuchelewesha mambo , wakati huo merina alikuwa amevalia gauni refu kidogo lililoishia magotini .

Patrick alipitisha mkono wake kwenye kiuno cha merina , na ni kama mtu aliekuwa akipima kama mtoto atautoa , lakini hakukutana na kipingamizi cha aina yoyote ile , aliendelea kuzungusha mkono wake taratibu kwenye kiuno cha mlimbwende huyo , huku merina alianza kukunja vidole vya miguu .

Mambo yalizidi kuwa mambo kwani Patrick alimgeuza merina kwani alikuwa mbele yake na kisha walianza kunyonyana ndimi , huku merina joto lilikuwa juu , kwa upande wa Patrick alikuwa fundi kweli na alijua ashike wapi aachie wapi , na hali hio ilimmaliza kabisa kabisa nguvu mlimbwende huyo.

Dakika chache mbele merina alikuwa hana gauni mwilini mwake tena , alikuwa amebakiwa na nguo ya ndani tu , na kwa Patrick vile vile , yeye alikuwa na boksa tu , Patrick aliendelea kumnyonya merina kwanzia shingoni kushuka huku merina akiwa anajikunja kunja kama nyoka aliejeruhiwa , alishuka taratibu , huku akipania kufanya utundu wake wote ili kumpagawisha mrembo huyo , alifika mpaka kwenye kufuri na hakutaka kuchelewa alilitoa taratibu na kumbakiza mlimbwende huyo bila nguo yoyote , alishuka na kuanza kumlamba mdada wa watu kitu kilichopelekea kilio kwa merina , alikuwa na hali mbaya sana kama mgonjwa wa malaria kali .

Baada ya Patrick kuona mtoto kakolea hapo ndipo alipo toa dushelele lake na kulipaka mate kisha alimchanua merina miguuu na kulengesha .

“stoop Patrick , ilikuw ni sauti ya umakini kweli kutoka kwa merina na hakuongea tu lakini pia alikuwa tayari ashaamka na kumsukuma Patrick , kwakuwa Patrick hakutegema alijikuta akidondokea upande mwingine .

Merina alinyanyuka na kukimbilia nguo zake , lakini Patrick hakutaka swala hilo litokee kwani aliona akimruhusu mrembo huyo kutoka hapo ndani bila kumng`ata asingepata nafasi kama hio tena .
“ unataka kufanya nini Patrick? “
“acha kunifnyia hivyo merina , nakupenda naomba unionee huruma leo tu mpenzi “
“ hapana haiwezekani Patrick , kumbuka kiapo chako na makubaliano yetu “

Kuna kasauti kalikuwa kakimwambia Patrick atumie nguvu , na hata mwenyewe hakujua kalikuwa kakitokea wapi , lakini kasauti hako kalikuwa na ushawishi kweli .(shetani kazini ).
“Patrick niachie “ merina alifurukuta kwani Patrick alikuwa amemkamata vilivyo , alimtupia kitandani na kisha kwakutumia nguvu alifanikiwa kumchania gauni merina , macho ya patrick yalikuwa yamebadilika na muda huo hakuwa hata na huruma shetani alikuwa akimmiliki haswa.

Merina alikuwa akilia lakini sauti haikumtoka na haikuweza kutoka hapo ndani , Patrick alifanikiwa kumvua nguo ya ndani merina na sasa alikuwa akilengesha dushe , lakini merina alikuwa amebana miguu , merina katika furukauta yake alikuwa akinyoosha mkono afikie chupa ya pombe iliokuwa hapo ndani na bahati nzuri ilikuwa karibu yake kwenye juu ya bedside .
“ paaa ,” ulikuwa ni mpasuko wa chupa iliompiga Patrick na kwakuwa merina alitumia nguvu , Patrick alidondoka na kuzimia , merina alikimbilia nguo zake kisha akazivaa huku akijifuta damu sehemu za siri kwani patrick alifanikiwa kupenya kidogo na kumchana na kisha alichukua funguo ya gari na kukimbilia chumbani kwake ambako alichukua kila kinachomhusu na kutoka mpaka mapokezi alikabidhi ufunguo na kutembea mpaka eneo la parking , bahati nzuri mapokezi alikuwa ni kijana mwingine sio yule aliewapokea kwa hio ilikuwani ngumu kujua kuwa mlimbwende huyo kaja na mpenzi wake , aliwasha gari huku akiwa hana hata uhakika wa njia yenyewe , muda huo ilikuwa ni saa kumi na nusu jioni na kijua kilikuwa kikikaribia kuzama .

Aliendesha gari huku akiwa anatoa machozi ,huku akijilaumu kwa kitendo alichofanya cha kumpiga Patrick na chupa kwani muda huo alikuwa akidhania tayari ameua na alijua muda si mrefu atashtakiwa na hatimae kwenda mahakamani .

Huku nyuma zilipita dakika kumi na tano Patrick ndipo alirejewa na ufahamu , alishangaa , akiwa chini ya sakafu , alijaribu kurudisha kumbukummbu zake hapo ndipo alipokumbuka tukio zima , na kuanza kujutia kwa kile alichokifanya, alivaa bukta haraka haraka na kisha alitoka kukimbilia kwenye chumba cha merina na kugonga lakini hakukuwa na majibu kabisa , aliita lakini hakukuwa na majibu , alirudi ndani na kuchukua simu na kuvaa tisheti kisha alitoka mpaka mapokezi na kuulizia huku akiwa amesahau kuwa amepiga namba ya merina na simu ilikuwa ikiiita .
“ vipi kaka , namuulizia merina , kachukua chumba namba 97 “ aliongea
“ asharudisha ufunguo na kuondoka “ aliongea na jibu hilo lilikuwa kama msumari kwa Patrick , alijilaumu sana kwa tamaa za mwili wake , alitoka mpaka kwenue parking na kukuta gari hakuna hapo alichoka Zaidi pili alikuwa akihofia usalama wa mlimbwende huyo kwani hakuwa mzoefu wa kuendesha gari kwenye barabara kama hio
ITENDELEA ITAENDELEA USIKOSE WAJAMENI
 
Hongera kwako mtunzi lakini vipi kuhusu mwendelezo lini mkuu na ni saa ngapi maana hii kitu isije kutuacha na alosito
 
MTUNZI : SINGANOJR
MAWASILIANO :0687151346

SEHEMU YA 11
Merina wakati akiwa kwenye mwendo huku akiwa anatokwa na machozi , huku hofu ikiwa imemtawala , mara baada ya kufika sunga mbele kidogo , ndipo simu yake ilianza kuita , , aliitoa kwa mkono mmoja kwenye mkoba na kisha kuangalia jina la mpigaji , moyo ulipiga kwa nguvu na kuona labda ni simu ya taarifa mbaya maana jina lilisomeka “love pat”, alijishauri kupokea ama asipokee , lakini roho ya kupokea ilikua na nguvu Zaidi , aliegesha gari pembeni , na kisha alipokea bila kuongea chochote .
“ vipi kaka , namuulizia merina , kachukua chumba namba 97 “ aliongea ilikuwa sauti ya Patrick , alijikuta moyo wake ukifurahi mno , kwani alidhania alikuwa ameua , aliendelea kusikilza mazunguzo na kuhakikisha kabisa kuwa patrick alikuwa mzima , kwani sauti ilikuwa yake , alijikuta akivuta pumzi nyingi na kuzitoa huku akimshukuru mungu na kisha alikata simu ile , na kuendesha gari kusonga mbele huku akijiapia kutokuja kumsamehe tena Patrick kwa kitendo cha kutaka kumbaka na pia kumuingiza katika kesi ya mauaji .

Simu ziliendelea kupigwa mfululizo na Patrick , lakini hakuwa tayari kabisa kupokea , muda huo kidogo umakini barabarani ulikuwa mkubwa huku akiongozwa na ramani(Navigation map ) iliokuwa ikisomeka kwenye gari , aliendesha gari kwa mwendo mkubwa kwani alitaka afike lushoto mjini mapema ili alale hapo , japo aliogopa kukutana na Patrick .

Bada ya kama lisaa kupita akiwa amefika eneo moja linaitwa makumbara kwa mbele kwenye kajimsitu ndipo aliposhuhudia mtu mbele yake akipunga mkono kumsimamisha , kwanza aliogopa sana na ukizingatia muda huo giza lilikuwa lishaanza kuingia , lakini kilichomshangza Zaidi ni baada ya mtu yule kudondoka chini , alijikuta akivaa ujasiri na kusimamisha gari pembeni na kisha akashuka na kumsogelea mtu yule kwa tahadhari kubwa .

“ damiani “ alijikuta haamini macho yake , japo mtu huyo alikuwa na majeraha usoni hakushindwa kutambua sura yake , alikuwa ni damiani , alijikuta akiinama na kumtingisha lakini hakukuwa na dalili ya kuamka kabisa , akiwa anamwamsha bahati alisikia sauti ya bodabida ikija upande wake alisimma na yeye katikati ya barabara na kisha aliipungia mkono , na ndani ya pikipiki hio kulikuwa na watu wawili mwnaume na mwanamke na mwanamke alionekana kuwa abiria .

“ naombeni msaada jamani “ aliongea na yule mbaba ,alisogea karibu na kumwangalia damiani .

“ amepatwa na nini ?” alielezea na bila kuchelewa walimbeba na kumpandisha kwenye gari na yule mama aliomba aongozane nae kwani alikuwa akielekea lushoto pia .

Merina alishukuru sana kwani alikuwa akiwaza sana safari hio ya kwenda lushoto peke yake , kwani alikuwa muoga sana .

Upande wa Patrick hakutaka kuendelea kubaki hotelini hapo , alinuia kuondoka muda huo huo kuelekea mjini lushoto , ili kumuwahi merina , aliamini kwamba merina asingeweza kufika dar , hivyo kwa vyovyote lazima angelala lushoto mjini .

Uzuri ni kwamba ndani ya hoteli ile kulikuwa na usafiri wa dharula , hivyo mara baada ya kueleza shida yake , alikubaliwa na kupewa gari aina ya noah na dereva na safari ikaaanza .

Walichukua masaa matatu kufika lushoto mjini na muda huo ilikuwa ni saa moja kamili kwenda saa mbili , walisimamisha gari katika hoteli ya highland na Patrick alishuka kisha akaagana na dereva , aliingia ndani ya hoteli hio huku akiangalia parking kama angeona gari yake , lakini hakuiona , alienda mpaka m apokezi na kisha alichukua chumba , na kukaa chini na kuanza kuwaza , moyo wake ulikuwa ukimuumma kweli , hakujua kama merina angemsamehe , ila shida yake ilikuwa ni kukutana nae na kumuomba msamaha tu .
“Robert vipi ndugu “ alionekana akiongea na simu
“ safi vipi “
“ kuna kazi nataka unisaidie ndugu yangu “
‘ kazi gani?? “.
“ gari yangu ina gps nataka uitrak ilipo nijue “
“ imeibiwa au?? “
“ hapana wewe fanya hivyo tu, nina haraka sana , nakutumia namba zake “huyo alikuwa ni patrick akiongea na Robert kitengo cha IT ikulu .

Basi baada ya kumtumia haikuchukua muda mrefu alittumiwa link kwa njia ya watsapp na aliifungua na hapo aliona ramani ya mji wa lushoto huku kialama cha rangi nyekundu kikionesha gari lake lilipo .

“ lushoto district hospital “ alijikuta moyo wake ukimpiga kite , kwani aliamini lazima merina atakuwa amepatwa na matatizo , hakutaka kukaa hapo ndani tena , alikuwa ni kama mwehu , alitoka mpaka nje ya barabara , aliangalia huku na huko lakini hakuona usafiri eneo hilo , alitembea kwa mguu mpaka kwenye jengo la benki ya CRDB mbele kidogo ya gereza na hapo ndipo alipopata bodaboda na kumuelekeza apelekwe hospital ya wilaya ,

Dakika tano tu walikuwa tayari nje ya geti hilo la hospital , mlinzi aliwazuia kuingia kwani haukuwa muda wa kuona wagonjwa , alijeleza pale kwa walinzi na mwishowe walimkubalia na kumruhusu , aliingia mpaka mapokezi na kuulizia jina la mgonjwa merina lakini mtu wa mapokezi alimwmbia kuwa hakukuwa na mtu wa jina hilo .hapo ndipo alipochoka
“ hakuna mgonjwa wowote aliepata ajali na kuletwa hapa mwanamke ?”
“ hakuna kaka yangu “
“ magari mnapark wapi ?”
“ kule nyuma “

Alitoka hadi upande uliokuwa na magari na kisha aliangalia na kuliona gari lake alilikagua kwa umakini , na walah hakuona aina yoyote ya mikwaruzo kama kuna ajali iliotokea Zaidi ya vumbi tuh , alijikuta akivuta pumzi ndefu na kurudi tena mapokezi .
“Hivi umesema mgonjwa wako unaemtafuta anitwa nani ?”
“ merina sosteness”.
“ okey nimelipata , kuna mgonjwa kaja nae hapa kasema ni mpenzi wake , mgonjwa huyo kalazwa wodi ya daraja la kwanza “. Hapo ndio patrick alipo toa macho
“ ndio ziko wapi ?”
“ panda na hiko kibaraza kunja kushoto utaona kibao kimeandikwa jiko , endelea mbele ndio utaona wodi , ingia namba nne “ aliongea dada huyo wa makamo mweupe na patriick alitoka hapo na kuelekea upande aliokuwa ameelekezwa .

Merina alkuwa akimuangalia damiani muda wote huku moyo wake ukiwa na furaha ajabu , japo damiani alikuwa kwenye usingizi lakini bado alikuwa na furaha isio na kifani , hakutaka kuondoka hapo hospitalini , alitaka damiani akiamka mtu wa kwanza kumuona awe yeye , hakuamini kabisa kwamba mtu aliekuwa akimuota mchana na usiku alikuwa mbele yake .

Wakati akifurahia uwepo wa damiani eneo hilo , ndio wakati aliposikia mlango ukigongwa , alinyanyuka na kuusogelea mlango na kuufungua , lakini sura alio iona ilikuwa sura ambayo alikuwa akiichukia .

“ merina please naomba unisamehe naaomba tuongee mpenzi wangu “ aliongea Patrick mara tu baada ya merina kufungua mlango , merina alijikuta akianza kukumbuka kile kitendo alichotaka kufanyiwa na patrick na hapo hapo alifunga mlango na funguo huku akimuacha Patrick nje aliekuwa akiita jina lake .

“ merina alienda mpaka kwenye mkoba wake na kisha alitoa ufunguo wa gari na kisha aliutupia chini ya mlango na kutokelezea nje.

“ Patrick naomba usinisumbue tena , na kamwe sitokusamehe naomba uondoke tuh “ aliongea merina na kisha alirudi mpaka kwenye kitanda na kuanza kutoa machozi .

Patrick aliongea ongea hapo nje ya mlango lakini hakusikilizwa , mpaka pale nesi alipokuja kumfukuza na kumwambia anapigia kelele wagonjwa ndipo alipookota ufunguo na kisha aliondoka mpaka kwenye maegesho ya magari na kufungua mlango na kuegamiza kiti na kulala.( mapenzi muda mwingine ni uchizi )

Ilikuwa asubuhi mapema tu muda wa saa moja ndio muda ambao Patrick alishituka , alijifikicha macho kisha alishuka kwenye gari , lakini kabla ya kushuka aliona begi la merina , alilichukua kisha akaelekea upande wa wodini .

Alifika wodi ya jana yake na kisha hakutaka hata kugonga , aliingia ndani ya wodi hio hio na hapo ndipo alipomkuta merina akiwa amelala huku akiwa ameshikilia mkono wa mgonjwa ambae kwa harakaharaka alitambua ni mwanaume , roho ilimuuma ajabu , kwani hakujua mwanume huyo alikuwa na uhusiano gani na merina kiasi cha kumfanya merina alale huku kashililia mkono wa mgonjwa , aliweka zile nguo na hakutaka kumuamsha kisha alitoka .

Alifika kwenye gari huku akianza kukumbuka maneno ya nesi ya

” , kuna mgonjwa kaja nae hapa kasema ni mpenzi wake “ jibu hili lilimfanya akae vizuri na kuanza kutafakari uhusiaono wa mgonjwa na merina , lakini kila akijaribu kuunganisha dot hakuweza kufanikiwa kung`amua .

“Haiwezekani labda aliamua tu kusema ivyo , hawezi kupata mpenzi ndani ya masaa machache tu , au alimgonga ?” .

Alitoa gari nje ya geti na kuendesha kuelekea hotelini , alifika na kujisafisha huku akitafuta kifungua kinywa , hata wazo la kumpelekea merina chai lilipotea kwani alikuwa na mawazo sana , alikunywa chai baada ya kumaliza alipumzika na kujiandaa kwenda tena kumbembeleza merina , lakini ni kwamba hakupata hata nafasi ya kujielezea kwani mwanamke huyo alionesha kumchukia sana .

Siku ya pili yake asubuhi aliamua kumpelekea merina chai , kule hospitalini , alifika vizuri na kupaki gari na kuelekea upande wa wodini .

Alijikuta akifungua mlango bila hata ya hodi , lakini tukio alilolikuta lilimuacha mdomo wazi kiasi kwamba adondoshe mzigo aliokuwa ameshikilia , kwani alimshuhudia merina akimpiga busu la paji la uso mgonjwa , wakati huo akiwa ameduwaa , hakujua hata ni muda gani merina alimpita ,kwani alijikuta macho yake yakikosa nguvu na kudondoka chini .

Merina alienda mpaka ofisi ya daktari kumtaarifu kuwa mgonjwa wake kafumbua macho , lakini mara baada ya kumkosa kwenye wodi hizo za daraja la kwanza , ilibidi atimue mbio mpaka upande wa chini ambako kulikuwa na madaktari , lakini ile anafika dirisha la kutolea dawa alikutana na nesi akija upande wake na hapo hapo alimwambia kuwa mgonjwa wake amefumbua macho na nesi alimwambia warudi akampigie daktari simu .

“katika hali ambao haikuwa ya kawaida baada kufika kwenye wodi , walimkuta Patrick kalala chini hajitambui tena karibu na mlango , hata nesi alishangaa na pia merina alishangaa , japo alikumbuka kwamba alimpita hapo mlangoni pasipo kumsemesha , lakini kitendo cha kumuona yupo chini kalala alishangaa na kumsogelea huku nesi akimwangalia na merina kufungua mlango , lakini hapo ndipo walipopigwa na mshangao mwingine , kwani damiani hakuwepo kitandani na dripu zilikuwa zimechomolewa .

Nesi alitoa taarifa na muda mfupi daktari alikuja na kumbeba Patrick na kulazwa kitandani chumba na kitanda alipokuwa damiani na kupewa huduma ya kwanza , huku nesi na merina wakizunguka kwenye vyoo wakimtafuta damiani lakini hawakumuona .

Merina alijikuta machozi yakianza kumlenga lenga na mwishowe aliachia kilio , taarifa ilitolewa haraka kwa ulinzi wa hospitali kama kuna mgonjwa alikuwa amepotea , na msako ukaanza , lakini hakupatikana , polisi nao hawakukawia walikuja na walianza kumuhoji merina na yeye alitoa maelezo kwamba wakati anatoka mgonjwa alikuwa amefumbua macho , na ndipo alipo enda kumuita daktari na baada ya kumkosa alieondoka na kuelekea upande wa chini huku akimuacha Patrick nje ya mlango , lakini baada ya kurudi walimkuta Patrick kapoteza fahamu na mgonjwa hakuwepo .
Patrick na yeye aliamka huku akiwa na wenge , alitulizwa na akili yake ilipo kaa sawa akahojiwa

“nilijisi kuguswa kwenye shingo na hapo hapo sikujua kilichoendelea “ aliongea na kuwafanya wale mapolisi waangaliane .
“ wewe ulisema ulimuokota akiwa na majeraha “ aliuliza polisi swali kwenda kwa merina
“ nesi hebu leta faili lake “ aliongea polisi na faili lililetwa kisha alipitia pitia kisha akaanza kutingisha kichwa
“hili tukio sio la kawaida kabisa , kwa maelezo yenu inaonekana kuna mtu kamteka , na mtu huyo lazima atakuwa na ujuzi wa hali ya juu , ila ngoja tutalifatilia kwa ukaribu Zaidi “ aliongea polisi na kuondoka na kumuacha merina aanze kulia huku akilitaja jina la damiani . jambo hilo kwa Patrick lilimuuma sana na alijua lazima merina na mgonjwa huyo walikuwa wnafahamiana na walikuwa wapenzi .

Patrick alimshawishi merina waondoke hapo hospitalini , lakini merina aligoma na kusema ana kaa hapo hapo kumsubiri damiani .
Patrick hasira zilimpanda na kuondoka zake , ila hilo halikumshitua merina kwanza alikuwa akimchukia .

Zilipita siku mbili bila ya damiani kuonekana na polisi hawakuwa na taarifa ya kuridhisha kabisa , merina alikuwa na mawazo mengi , siku hio alikuwa ndani ya kituo cha polisi kwa ajili ya kufatilia swala la damiani na uchunguzi ulifikia wapi .
“ karibu sana “
“ nimekuja kufatilia uchunguzi umefikia wapi afande “
“ kwa uchunguzi tulioufanya tumegundua mambo kadhaa lakini mpaka sasa bado hatujafanikiwa kumpata “

Damiani rabani amezaliwa mwaka 1994 katika wilaya ya lushoto kata ya mkuzi , umri wake ni miaka 25 ni mhitimu wa chuo kikuu TIA( TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY ) , mnamo tarehe tajwa , majambazi wasiofahamika walivamia nyumbani kwao na kumuua mama yake kwa kumpiga risasi mbili kifuani na kupoteza maisha hapo hapo huku sababu ya uvamizi huo ikiwa haijulikani , mnamo tarehe tajwa kijana huyo ariripotiwa kupotea bila mawasiliano mpaka siku ambayo ni juzi kuonekana hospitalini na kupotea tena “ aliongea afande kighenda na kumfanya merina alowe machozi hakuamini kama damiani alikuwa akipitia kipindi kigumu namna hio , hapo ndipo alipokuja kujua sababu ya damiani kutokuripoti kazini pale alipopewa tarifa ya kuchaguliwa , alimuonea huruma sana , moyo ulimuuma ajabu .

“ pole sana mpaka sasa tunaamini kupotea kwake tarehe tajwa , ulikuwa ni utekaji na watu hao hao ndio waliohusika katika utekaji wa tukio la juzi hivyo basi majambzi yaliomuua mama yake ndio yaliomteka na kwakuwa operesheni ya kuyakamata majambazi hayo inaendelea basi yatakapokamtwa ndipo na damiani atapatikana kwa hio kuwa na subira “

Merina hakuwa na jinsi na kuamua kukubaliana na majibu ya polisi na kuondoka kurudi zake hotelini akiwa na mawazo mengi huku furaha yake ya siku mbili zilizopita sasa ,ilikuwa ni machungu

Patrick japo alikuwa na hasira sana , lakini hakutaka kumuacha merina ndni ya wilaya hio , alijitahidi kumshawishi na baadae merina alikubaliana na Patrick, huku meerina akichukua namba za polisi kwa ajili ya mawasiliano .

Patrick hakutaka kuuliza lolote , wala kuongea lolote , kwanza alijilaumu kuja kwenye safari hio , kwani ilikuwa ni safari ya mikosi sana kwake , furaha yote aliokuwa amekuja nayo haikuwepo tena .

Walifka jijini dar mapema tu na alimfikisha merina hadi kwao na kisha aliondoka zake , huku akiwa na mawazo na maumivu ya moyo , kila alipofikiria merina alivyokuwa akilia kule hospitalimni alijikuta akijua kuwa mwanamke huyo hakuwa akimpenda hata kidogo , mapenzi yalikuwa kwa kidume damiani .
ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom