Ufisadi TAA: Mhindi wa Flamingo apewa Tenda aliyonyimwa Mtanzania

walipoulizia akaambiwa amepewa yule yule muhindi wa flamingo...ambae ndie huyo amepewa lounge.amepewa supermarket..amepewa dutyfree shop.......amebakiza kupewa uwanja wa kutulia ndege......
BWA MSANGI NA BWANA TESHA....HAPO HIYO COMBINATION YA MCHAGA NA MPARE...INATUREJESHA KWENYE UTUMWA KABISA...WANA DHARAU SANA ...HATA IKITOKEA UKIPINGANA NA HUYO MUHINDI AKIKUFIKISHA KWAO UMEKWISHA BILA HATA YA KUJIELEZA....
UFISADI UTAISHA LINI JAMANI??????????????

Hivi ndivyo alivyosema mleta mada. Kichwa cha habari unakikataa. Na hii nayo utakataa?

Bado hujaonyesha ni wapi kalaumiwa Mhindi, zaidi ya Tesha, mtoa tenda.

Tesha analaumiwa kwa kumpa mhindi. Kosa lake linaonekana ni kumpa Mhindi na sio kufanya upendeleo! Maana yake ni kuwa hatutaki Mhindi apewe. Au ndiyo unataka kuchambua unywele? Unataka tuanze kushindana kwenye semantics!

Intellectual dishonesty! Kwa maneno mengine, umejifanya hujui jibu la hilo swali: ambalo ni, tujaribu kuangalia, kwa mfano, ni kwa nini Wagogo hawana vitega uchumi wamegeuka omba omba. Ni mashule yamepungua kwao, au viongozi wao wabovu, au ni msisitizo mdogo wa elimu, au ni jadi tu? Haya yanaweza kuponywa bila kumnyang'anya Mpemba taxi. Kitu ambacho sikusema, na unajua siwezi kusema. Niiteje intellectual dishonesty yako kwa kiswahili, uongo wa kiakili?
Tunarudi pale pale. Lawama (?) zote za waswahili kukosa maduka pale airport zinaelekezwa kwa wahindi. Hakuna mtu anayezungumzia qualifications zao au uwezo wao. Tatizo letu ni mhindi kuwepo pale. Hivyo hivyo kwa hao wagogo. Tukitumia mfano huo huo wa airport, matatizo ya wagogo kuomba omba ni mpemba kuendesha taksi. Asingekuwa mpemba amehodhi taksi, wagogo wasingeomba omba na wangeendesha taksi. Vile vile, ili weusi wapate maduka airport ni lazima wahindi wanyang'anywe na wazuiwe kupata. Nilisema toka awali kama mtoa hoja angesema huyo aliyepewa maduka yote hayo alicheza faulu bila kuingiza uhindi ningemuunga mkono. Hata ukatae vipi, mada imeletwa kibaguzi na hata waliounga mkono wameunga kibaguzi. Mbaya zaidi hamjatofautisha kati ya mhindi raia na mhindi mgeni! Kutokana na kichwa cha habari, hamna mhindi mtanzania. Sasa nani ni muongo wa kiakili?

Mifano yangu yote haikuongelea rangi. Nilisema tabaka la makabila fulani kuwa watwana wa tabaka la makabila mengine: walinzi wamasai, omba omba wagogo, housegirl wahehe. Hayo yote ni aina za tofauti za hali za maisha zinazojenga matabaka, kama ambavyo Wahindi walikuwa tabaka la kati wakati wa ukoloni. Wana rangi ya kihindi, lakini wamefanyika tabaka. Rangi, makabila, dini, hujenga matabaka. Wafaransa hawakuwa na makabila, wana dini tofauti, wala rangi tofauti. Matabaka yao yalitokana na ubujuazii. Sisi matabaka yetu yatatokana na dini, kabila, rangi. Lakini bado, kama Ufaransa, bado ni matabaka. Haya, niambie nimechanganya wapi?
Kwa kifupi, unataka kutuambia kuwa ndani ya hayo makabila, rangi na dini hamna matabaka? Wahindi wote ni matajiri na wagogo wote ni ombaomba? Sisi matatizo yetu yanatokana na haya matabaka na si rangi. Hayo maskandali yote ni watu wa rangi tofauti na kabila tofauti ndiyo walioshirikiana kukwapua. Hao matajiri wetu wakina Mengi, Mkono n.k. washirika wao wakubwa ni wahindi matajiri wenzao na si wakina Fundi Mchundo. Mnapoingiza rangi ndipo mnapokosea. Na ndivyo waovu weusi wenzetu wanavyotuchezea kwa kujifanya ati wako nasi wakati sivyo. Umechanganya kwa kuleta mfano wa mapambano ya kitabaka katika mada inayohusu mapambano ya rangi. Hapo airport, lawama si bepari mmoja kuhodhi kila kitu. Ingekuwa hivyo, mfano wako ungekuwa na mantik. Kwa bahati mbaya lawama ni kwa nini mtu wa rangi fulani amepewa kila kitu? Angepewa mweusi pasingekuwa na lawama.

Hapa napo unakosea au unakosesha kusudi. Hakuna aliyesema tatizo ni rangi. Tatizo ni kundi moja kumilikishwa nyanja za uchumi, imetokea tu kwamba kundi lenyewe ni la Wahindi. Again, nionyeshe paliposemwa tatizo ni Mhindi kwenye lead post ya Pdidy.
Nasita kusema lakini, ashakhum si matusi, naona unaleta ubishi usio na maana. Kichwa kimemtaja mhindi. Kwenye text yenyewe ametajwa mhindi lakini bado unataka nikuonyeshe wapi ametajwa Mhindi! Kama wewe unaona tatizo si uhindi basi usitake kubadilisha aliyosema mwenzako.

Sasa kama tatizo ni mtu yeyote kuhodhi maduka, kwa nini unatetea Mhindi kuhodhi maduka?
Mnapunguza nguvu za hoja yenu kwa kuingiza ubaguzi. Kama tatizo ni mtu kunyang'anywa haki yake, tuko pamoja. Hata kama aliyemnyang'anya ni mdogo wake wa kuzaliwa baba na mama. Kama tatizo ni huyo unayemuita mhindi kufanya biashara kwenye uwanja huo wa ndege, basi huko siko. Naona wengine wameishawaingiza wapare na wachaga katika rada yao! Mtakuja kumalizana mkiendekeza upuuzi huu!
Huyu mtu ni nani anaemiliki biashara zote hizo? Tatizo ni kuwa ni mhindi au mtu mmoja kumiliki biashara hizo? Hivi angekuwa mweusi mwenzetu ndiye anaemiliki biashara hizo zote tungekubali kwa vile tuu ni mwenzetu? Na kama biashara hizo zinamilikiwa na watu tofauti lakini wana rangi moja tatizo liko wapi kama wamefuata utaratibu? Tunasahau hao tunaowaita wahindi nao wanamakabila kama sisi. Kama kila mmoja wao kivyake vyake aliingia na kushinda tenda kwa nini tunamlaumu? Au mna ushahidi kuwa alihonga au hakufuata utaratibu. Kama mnao, uwekeni wazi achukuliwe hatua kama mhalifu yeyote mwingine lakini si kwa sababu ati ni mhindi!
Unapotosha niliyosema. Wapi nimetetea Mhindi au mtu yeyote kuhodhi maduka? Nimesema toka awali kama huyo aliyehodhi, bila kujali rangi au kabila lake, alifanya hivyo kinyume cha utaratibu, achukuliwe hatua. Ninachokataa ni yeye kuhukumiwa kwa sababu tu ni Mhindi.Ndiyo maana nimesema kama tatizo lenu kubwa ni Mhindi kufanya biashara pale ( na si suala la kuhodhi) basi huko simo. Labda niiweke wazi zaidi. Kama kuna mtu anahodhi maduka nje ya utaratibu uliowekwa basi achukuliwe hatua bila kujali rangi yake. Lakini kama mtu huyo amepata hizo sehemu kihalali aachiwe aendelee na biashara yake bila kujali rangi yake.

Kwa hiyo Wahindi na Wazawa Asilia wakianza kuchinjana wewe utapona kwa vile wewe ulikuwa unatetea wahindi. Yani Dewji na bunduki vitani kwenye mshike mshike atasimama atakuuliza "wewe nyeusi Fundi Chundo iko pande gani?" Utamwambia "nilikuwa nakuteteeni kabla ya vita" halafu atakuacha? You kidding me.
Dilunga, mbona unakamata chelewa? Kutokana na scenario yako ni weusi ( ambao unadai wanakandamizwa na wahindi) watakaowashambulia wahindi na si vice versa. Haitakuwa kuchinjana, bali weusi kuchinja wahindi. Sasa huyo Dewji atatoka na bunduki yake kwenda kuwatafuta weusi alipize kisasi? Wahindi wote hawafiki milioni moja, huo ubavu utatoka wapi?

Kama katika nafasi hiyo hakuna mwenye sifa bali mhindi basi heri hiyo nafasi ibaki tupu au apewe mweusi asie na sifa ( kama walivyofanya New Haven, Conn. kwenye kupandishwa vyeo zima moto.).
Ndio, mwanzoni ulitoa maelezo potofu, na context ikawa potofu. Hakuna mweusi aliyepandishwa cheo.

Wapi niliposema mweusi amepandishwa cheo? Mtihani ulikuwa wa kupandishwa cheo na nimesema nafasi ibaki tupu au apewe mweusi asiye na sifa. New Haven waliamua kuacha nafasi tupu bila kupandisha mtu cheo. Sasa wapi nilipokosea?

Cookie jar ni metaphor tu. I should know you better what, kwamba huwezi kukosea katika kuelezea mkasa wa Zimamoto wa New Heaven? FMESian narration ni maelezo yenye factual shortcomings, kama ulivyoelezea kisa cha CT mwanzoni, nilitegemea ungeelewa. Huyo ambaye asingeweza kufanya kosa la kukukosoa labda hajui kwamba yeyote aweza kukosea. Na pia, the vintage Fundi Mchundo asingetaka kupigiwa pigiwa makofi tu kwa kila anachosema.
Metaphor maana yake nini? Sijaomba kupigiwa makofi lakini vile vile sikubali kuwekewa maneno mdomoni. Hiyo 'factiual shortcoming' iko wapi? Kuwa mtihani haukuwa wa kupandishwa vyeo? Au kuwa nafasi za vyeo hivyo hazikujazwa? Zikabaki wazi. Ndiyo maana nimesema, angekuwa Kuhani angesoma vizuri nilichoandika na si kuona 'apewe mweusi' na sio 'ibaki tupu'.

Tutamkumbuka sana Kuhani.

Kweli. Mfano wa wahindi kujazana kwenye ku pump gas una angle ya discrimination ya Kimarekani-Marekani na ni wrong context kwa Tanzania ambapo nguvu ya kisiasa tunayo weusi. Nilikosea. Ila usitetee wanaohodhi maduka kwa vile tu ni wahindi. Na usituambie "mtamalizana... mtachinjana," kuwa na chembe ya uzalendo.
Sasa unataka niseme 'tutachinjana' wakati sina mpango wa kumchinja mtu? Na tangu lini uzalendo unapimwa na utayari wa mtu kumchinja mwenzake? Kama huo ndio uzalendo wenu, basi mkae nao. Sina haja nao. Hata chembe.

Amandla.......

Hivi ndivyo alivyosema mleta mada. Kichwa cha habari unakikataa. Na hii nayo utakataa?

Tesha analaumiwa kwa kumpa mhindi. Kosa lake linaonekana ni kumpa Mhindi na sio kufanya upendeleo! Maana yake ni kuwa hatutaki Mhindi apewe. Au ndiyo unataka kuchambua unywele? Unataka tuanze kushindana kwenye semantics!

Tunarudi pale pale. Lawama (?) zote za waswahili kukosa maduka pale airport zinaelekezwa kwa wahindi. Hakuna mtu anayezungumzia qualifications zao au uwezo wao. Tatizo letu ni mhindi kuwepo pale. Hivyo hivyo kwa hao wagogo. Tukitumia mfano huo huo wa airport, matatizo ya wagogo kuomba omba ni mpemba kuendesha taksi. Asingekuwa mpemba amehodhi taksi, wagogo wasingeomba omba na wangeendesha taksi. Vile vile, ili weusi wapate maduka airport ni lazima wahindi wanyang'anywe na wazuiwe kupata. Nilisema toka awali kama mtoa hoja angesema huyo aliyepewa maduka yote hayo alicheza faulu bila kuingiza uhindi ningemuunga mkono. Hata ukatae vipi, mada imeletwa kibaguzi na hata waliounga mkono wameunga kibaguzi. Mbaya zaidi hamjatofautisha kati ya mhindi raia na mhindi mgeni! Kutokana na kichwa cha habari, hamna mhindi mtanzania. Sasa nani ni muongo wa kiakili?

Kwa kifupi, unataka kutuambia kuwa ndani ya hayo makabila, rangi na dini hamna matabaka? Wahindi wote ni matajiri na wagogo wote ni ombaomba? Sisi matatizo yetu yanatokana na haya matabaka na si rangi. Hayo maskandali yote ni watu wa rangi tofauti na kabila tofauti ndiyo walioshirikiana kukwapua. Hao matajiri wetu wakina Mengi, Mkono n.k. washirika wao wakubwa ni wahindi matajiri wenzao na si wakina Fundi Mchundo. Mnapoingiza rangi ndipo mnapokosea. Na ndivyo waovu weusi wenzetu wanavyotuchezea kwa kujifanya ati wako nasi wakati sivyo. Umechanganya kwa kuleta mfano wa mapambano ya kitabaka katika mada inayohusu mapambano ya rangi. Hapo airport, lawama si bepari mmoja kuhodhi kila kitu. Ingekuwa hivyo, mfano wako ungekuwa na mantik. Kwa bahati mbaya lawama ni kwa nini mtu wa rangi fulani amepewa kila kitu? Angepewa mweusi pasingekuwa na lawama.

Nasita kusema lakini, ashakhum si matusi, naona unaleta ubishi usio na maana. Kichwa kimemtaja mhindi. Kwenye text yenyewe ametajwa mhindi lakini bado unataka nikuonyeshe wapi ametajwa Mhindi! Kama wewe unaona tatizo si uhindi basi usitake kubadilisha aliyosema mwenzako.

Unapotosha niliyosema. Wapi nimetetea Mhindi au mtu yeyote kuhodhi maduka? Nimesema toka awali kama huyo aliyehodhi, bila kujali rangi au kabila lake, alifanya hivyo kinyume cha utaratibu, achukuliwe hatua. Ninachokataa ni yeye kuhukumiwa kwa sababu tu ni Mhindi.Ndiyo maana nimesema kama tatizo lenu kubwa ni Mhindi kufanya biashara pale ( na si suala la kuhodhi) basi huko simo. Labda niiweke wazi zaidi. Kama kuna mtu anahodhi maduka nje ya utaratibu uliowekwa basi achukuliwe hatua bila kujali rangi yake. Lakini kama mtu huyo amepata hizo sehemu kihalali aachiwe aendelee na biashara yake bila kujali rangi yake.

Dilunga, mbona unakamata chelewa? Kutokana na scenario yako ni weusi ( ambao unadai wanakandamizwa na wahindi) watakaowashambulia wahindi na si vice versa. Haitakuwa kuchinjana, bali weusi kuchinja wahindi. Sasa huyo Dewji atatoka na bunduki yake kwenda kuwatafuta weusi alipize kisasi? Wahindi wote hawafiki milioni moja, huo ubavu utatoka wapi?

Wapi niliposema mweusi amepandishwa cheo? Mtihani ulikuwa wa kupandishwa cheo na nimesema nafasi ibaki tupu au apewe mweusi asiye na sifa. New Haven waliamua kuacha nafasi tupu bila kupandisha mtu cheo. Sasa wapi nilipokosea?

Metaphor maana yake nini? Sijaomba kupigiwa makofi lakini vile vile sikubali kuwekewa maneno mdomoni. Hiyo 'factiual shortcoming' iko wapi? Kuwa mtihani haukuwa wa kupandishwa vyeo? Au kuwa nafasi za vyeo hivyo hazikujazwa? Zikabaki wazi. Ndiyo maana nimesema, angekuwa Kuhani angesoma vizuri nilichoandika na si kuona 'apewe mweusi' na sio 'ibaki tupu'.

Tutamkumbuka sana Kuhani.

Sasa unataka niseme 'tutachinjana' wakati sina mpango wa kumchinja mtu? Na tangu lini uzalendo unapimwa na utayari wa mtu kumchinja mwenzake? Kama huo ndio uzalendo wenu, basi mkae nao. Sina haja nao. Hata chembe.

Amandla.......

Sielewi Fundi na huyo jamaa mnabishana nini wakati kichwa cha habari cha mada kinasema "Mhindi wa Flamingo apewa Tenda aliyonyimwa Mtanzania" . Hii ni lugha ya kibaguzi hata mtu aiteteeje. Yaani vitu vingine viko so clear cut lakini watu kwa kupenda ligi wanavifanya viwe kama ni vigumu na vinavyochanganya.
 
Mkuu Fundi Mchundo kwa takwimu za kukisia Tanzania ina watu karibu milioni arobaini (40,000,000). Kwa takwimu hizo hizo wanaoitwa Wahindi ni karibu watu laki mbili (200,000) tu sawa na asilimia 0.5%. Kwa hesabu za haraka haraka ni kwamba katika kila watu mia mbili (200) yuko mhindi moja tu. Kwa hesabu nyingine katika bunge letu na kwa uwiano ule ule tungekuwa na mbunge mhindi moja tu - lakini tunao zaidi.

Sasa kwa uwiano huo huo unategemea tuwe na wahindi wangapi serikalini kama lengo ni kutoa fursa sawa kwa watanzania wote. Halafu hapa si swala la ubaguzi, ukweli ni kuwa Wahindi hawapo serikalini kwa mapenzi yao wenyewe na kutoa mfano kwa kuangalia hali hiyo ni kutumia njia potofu. Kwa Mhindi moja kupewa tenda zote hizo ni sawa na kuwanyima fursa watanzania wengine lukuki - anayefanya hivyo ndio ama mbaguzi au mla rushwa.
 
Hapa utakuwa unakosea sababu sera ya uchumi ambayo Tanzania inafuata kwa sasa inaendana na misingi ya Uchumi wa Soko Huria i.e., "Free Market Economy". Mambo ya uwiano kati ya matabaka tofauti ya watu katika jamii na nafasi yao kiuchumi, kisiasa, kijamii, nk hayaamuliwi na Serikali au dola bali ushindani wa mtu binafsi/kundi/kampuni nk katika jamii (ambayo kwa ujumla, na kwa vigezo mablimbali, unaweza kuichukulia kama soko moja kubwa huria.) Kama mshindani ana sifa duni ya kifedha, utoaji huduma, nk basi asilalamike akipata ushindani mgumu kutoka kwa matabaka ya Wafanyabiashara katika jamii ambao kwa bahati nzuri au mbaya wametokea kuwa na rangi na tamaduni tofauti na walio wengi kwenye jamii ile. Afterall, mediocrity, in all its forms, and in all sectors of life, is a huge setback in our society.
 
Last edited:
Kwa Mhindi moja kupewa tenda zote hizo ni sawa na kuwanyima fursa watanzania wengine lukuki - anayefanya hivyo ndio ama mbaguzi au mla rushwa.

Kwanza kabisa, haya mazoea ya kutumia hizi ethnic labels i.e. "Wahindi" au "Muhindi" ni lugha ambayo inaweza ikatafsirika kuwa ya kibaguzi. Huyo uliyemuita "Mhindi" pengine naye yeye ni Mtanzania kama wewe na mimi.

Pili, je kama huyo jamaa aliyepewa hizo tenda alizipata kihalali kwa kufuata taratibu zote, ina maana apunguziwe hizo tenda ili aende akapewe Mtanzania mwingine (as if kama yeye siyo Mtanzania) hata kama hana uwezo au hakufuata taratibu zilizopo?

Huu ubaguzi huu...ni sumu mbaya kweli.
 
Mkuu Fundi Mchundo kwa takwimu za kukisia Tanzania ina watu karibu milioni arobaini (40,000,000). Kwa takwimu hizo hizo wanaoitwa Wahindi ni karibu watu laki mbili (200,000) tu sawa na asilimia 0.5%. Kwa hesabu za haraka haraka ni kwamba katika kila watu mia mbili (200) yuko mhindi moja tu. Kwa hesabu nyingine katika bunge letu na kwa uwiano ule ule tungekuwa na mbunge mhindi moja tu - lakini tunao zaidi.

Sasa kwa uwiano huo huo unategemea tuwe na wahindi wangapi serikalini kama lengo ni kutoa fursa sawa kwa watanzania wote. Halafu hapa si swala la ubaguzi, ukweli ni kuwa Wahindi hawapo serikalini kwa mapenzi yao wenyewe na kutoa mfano kwa kuangalia hali hiyo ni kutumia njia potofu. Kwa Mhindi moja kupewa tenda zote hizo ni sawa na kuwanyima fursa watanzania wengine lukuki - anayefanya hivyo ndio ama mbaguzi au mla rushwa.

Mfano wako ni potofu. Tuwachukulie hao wahindi kama kabila moja tu Tanzania. Na tukiwa sahihi zaidi hata hao wahindi tuwagawe, kuna wapunjabi, wapakistani, masingasinga,wanaotoka Kerala, wanaotoka Goa, wanaotoka Iran, waliokuja nchini miaka ya 1800s n.k. n.k. Wote hao sisi tunawaita wahindi bila kujali.

Hatugawani vyeo, ubunge au nafasi serikalini kutokana na kabila. Kama ni hivyo, basi wasukuma wangedai watoe wabunge wengi. Na wahadzabe ndiyo walie kabisa maana hawana haki ya kuwa serikalini kutokana na idadi yao!

Wahindi hawako serikalini si kwa kujitakia tu. Tulipopata uhuru tulikuwa na zoezi la Africanisation ambapo weusi walipewa upendeleo. Mifumo ya utendaji wetu katika maeneo mengine yaliwafanya wahindi wasipende kwenda huko. Huko JKT wahindi walikuwa wakinyanyasika. Kwenye mashule yetu, majeshi yetu, n.k. vyakula vyetu haviendani na imani ya baadhi yao. Pamoja na hayo mimi sijali kama wahindi wako au hawako serikalini. Ni uamuzi wao kuona wapi wanaweza kuchangia na kufaidika zaidi. Na wana haki ya kuhukumiwa sawa na watanzania wengine. Kama mmoja wao amehonga na kuhodhi maduka airport, basi yeye achukuliwe hatua na sio tutumie nafasi hiyo kunyooshea vidole jamii nzima ya wahindi.

Kwangu mimi tatizo si Mhindi kupewa tenda zote pale airport. Inawezekana kweli amezishinda kihalali au/na ametumia mbinu zinazokubalika za kibiashara kuwanunua washindani wake. Tangu lini imekuwa kosa kwa mfanya biashara kutaka ku-dominate market? Kwani wakina Microsoft, Google, Apple n.k. wanafanya nini? Kwa nini iwe vibaya mtu kutaka kutawala biashara pale airport? Kama hatutaki iwe hivyo basi ni wajibu wetu kuweka sheria na taratibu zitakazozuia hiyo badala ya kulalama tu. Lakini pamoja na hayo, kama ametoa rushwa au amependelewa kwa namna yeyote anastahili kuchukuliwa hatua kama ambavyo ingekuwa kwa mtu mweusi. Tudai level playing ground na si upendeleo kwa sababu tu ya rangi yetu. Hapo mbeleni tutaumbuka.

Unaposema kupewa mhindi tenda zote hapo ni ishara ya ubaguzi una maana gani? Ni yeye au aliyempa ndiye anastahili kuitwa mbaguzi? Na kwa vile aliyempa ni mweusi mwenzetu, tutamuitaje mbaguzi akimpa tenda mhindi? Kama amekula rushwa basi si lazima awe mbaguzi. Rushwa haina rangi.

Amandla........
 
Fundi niliandika hivi - Kwa Mhindi moja kupewa tenda zote hizo ni sawa na kuwanyima fursa watanzania wengine lukuki - anayefanya hivyo ndio ama mbaguzi au mla rushwa. Hapo umeelewa nini ? Hata weusi hubagua na kubaguana.

Wahindi hawa ninaowaongelea wengi wao wana uraia wa zaidi ya nchi moja. Hata wale wanaozaliwa Tanzania baadaye hutafuta uraia nje ya nchi - subirini tu siku machafuko yakipiga hodi Bongo, wahindi wote haoooo !
 
Vipi hakuna Watanzania weusi/waafrika wenye uraia zaidi ya nchi moja? Au yakitokea machafuko hawa watabakia?
 
Vipi hakuna Watanzania weusi/waafrika wenye uraia zaidi ya nchi moja? Au yakitokea machafuko hawa watabakia?

Mimi mwenyewe nawajua kibao! Bila shaka hata humu kuna wanaJF kibao wenye pasi mbili au zaidi. Tangu lini kuwa na pasi zaidi ya moja imekuwa kipimo cha uzalendo? Mbona humu kuna watu wanajiita watanzania lakini ni raia wa nchi nyingine? Mbona wakati wa vita na Idi Amin hao weusi (pamoja na wahindi) wengi tu hawakujipeleka kupigania nchi yao? Hasa hao wanaoitwa wasomi! Kila mtu anapenda uhai. Yakitokea machafuko watakimbia wengi bila kujali rangi yao.

Amandla........
 
Last edited:
Hivi ndivyo alivyosema mleta mada. Kichwa cha habari unakikataa. Na hii nayo utakataa?

Mzawa Asilia alijibu tender invitation, mchakatao ukasimamishwa ghafla, hatujakaa sawa akapewa Mhindi wa Flamingo. Watoa tenda ni Tesha na Msangi ambao ndio wameitwa mafisadi. Ukilalamika, Pdidy anasema, kesi yako itaishia kwa hao hao Msangi na Tesha, umekwisha. Wapi kalaumiwa Mhindi kwenye lead post ya Pdidy?

Tesha analaumiwa kwa kumpa mhindi. Kosa lake linaonekana ni kumpa Mhindi...
Linaonekana na nani? Wewe ndio unaona kosa ni la Mhindi. Una project trepidation zako na oversensitivity zako kwa Wahindi kwa wengine. Unatafsiri kivyako kwamba kosa ni la Mhiondi. Onyesha paliposemwa kosa ni la Mhindi!

Unataka tuanze kushindana kwenye semantics!
Kwa hiyo wewe unataka useme weeeee, lakini mwingine akisema unalia "mashindano ya semantics"! Onyesha paliposemwa kwamba Mhindi ndio tatizo.

Hakuna mtu anayezungumzia qualifications zao au uwezo wao. Tatizo letu ni mhindi kuwepo pale.
La qualification limejadiliwa, unataka kupotosha sasa. Pdidy amesema kina Msangi na Tesha walidai mhindi ana qualification za kutengeza biashara ya kimataifa kuliko waswahili. Na Pdidy akapinga hilo, akisema hata sisi Wazawa Asili tunaweza. Usidai hapa kwamba "hakuna anaezungumzia qualifications," please.
Tukitumia mfano huo huo wa airport, matatizo ya wagogo kuomba omba ni mpemba kuendesha taksi. Asingekuwa mpemba amehodhi taksi, wagogo wasingeomba omba na wangeendesha taksi. Vile vile, ili weusi wapate maduka airport ni lazima wahindi wanyang'anywe na wazuiwe kupata.
Hii imetunga. Hakuna iliposemwa kwamba tatizo la omba omba ni wapemba. Ndio hapo nilipokwambia una commit intellectual dishonesty. Acha.

Nilisema toka awali kama mtoa hoja angesema huyo aliyepewa maduka yote hayo alicheza faulu bila kuingiza uhindi ningemuunga mkono.
Mtoa hoja katoa identity ya beneficiary wa hii faulu, who happens to be Mhindi wa Flamingo. Sasa angesemaje, Mnyasa? Hata kwenye nchi zinazopigana ubaguzi wanasema kwenye taarifa za habari, the robbery suspect is a black male, of short stature, wearing dreadlocks. Sasa weusi, wafupi, na wafuga rasta walalamike ubaguzi maana polisi wametaja rangi na maumbile? Mnufaikaji wa ufisadi wa airport ni Mhindi, sio Mzigua, Mhindi!
Hata ukatae vipi, mada imeletwa kibaguzi na hata waliounga mkono wameunga kibaguzi.
Sasa unataka kunitwisha mzigo wa waliounga mkono hoja kibaguzi? Duuu... Lead post imelaani ufisadi wa Tesha na Msangi. Wahindi umeanza kuwatetea wewe!

Mbaya zaidi hamjatofautisha kati ya mhindi raia na mhindi mgeni! Kutokana na kichwa cha habari, hamna mhindi mtanzania. Sasa nani ni muongo wa kiakili?
Hiyo umetengeza wewe, hakuna paliposemwa Mhindi wa Flamingo sio Mtanzania!

Kwa kifupi, unataka kutuambia kuwa ndani ya hayo makabila, rangi na dini hamna matabaka? Wahindi wote ni matajiri na wagogo wote ni ombaomba? Sisi matatizo yetu yanatokana na haya matabaka na si rangi. Hayo maskandali yote ni watu wa rangi tofauti na kabila tofauti ndiyo walioshirikiana kukwapua. Hao matajiri wetu wakina Mengi, Mkono n.k. washirika wao wakubwa ni wahindi matajiri wenzao na si wakina Fundi Mchundo. Mnapoingiza rangi ndipo mnapokosea. Na ndivyo waovu weusi wenzetu wanavyotuchezea kwa kujifanya ati wako nasi wakati sivyo. Umechanganya kwa kuleta mfano wa mapambano ya kitabaka katika mada inayohusu mapambano ya rangi.
Unapokuwa na wagogo na wamachinga na wahehe ndio wafanyakazi wa wapare na wachaga na wahindi, umeshatengeza matabaka. Kuna ukabila ambao umejenga matabaka. Sijui usichoelewa ni nini. Usifurahi kuona Wahindi tu ndio wamehodhi maduka. Hayo matabaka sio mazuri kwa mustakabali wetu.

Nasita kusema lakini, ashakhum si matusi
Okay, ashakhum si matusi, ashakhum ni nini?

naona unaleta ubishi usio na maana.
right, wewe ubishe siku nzima, mwingine akisema kitu, "ubishi usio na maana...semantics"

Kichwa kimemtaja mhindi. Kwenye text yenyewe ametajwa mhindi lakini bado unataka nikuonyeshe wapi ametajwa Mhindi!
Unaona unavyojua kutunga vitu. Wapi nimesema nionyeshe alipotajwa Mhindi. Nimesema, nionyeshe paliposemwa tatizo ni Mhindi, kama sio Tesha na Msangi.

Kama wewe unaona tatizo si uhindi basi usitake kubadilisha aliyosema mwenzako.
Aliyosema mwenzangu yepi? Onyesha paliposemwa tatizo ni Mhindi!

Unapotosha niliyosema. Wapi nimetetea Mhindi au mtu yeyote kuhodhi maduka?
Umesema hupendi yeyote ahodhi maduka. Sisi tunapinga na kulaani Mhindi kuhodhi maduka. Wewe unawaka kutupinga. Sasa, hasa hasa unachosimamia wewe ni nini?

Ndiyo maana nimesema kama tatizo lenu kubwa ni Mhindi kufanya biashara pale ( na si suala la kuhodhi) basi huko simo.
Unarudia kosa lile lile. Utatoaje mishutuma based on "kama tatizo lenu ni..." Kama? Huna hakika? Tatizo ni mtu kuhodhi maduka, which happens to be Mhindi. Kusikia Mhindi una bend over backwards kumtetea wakati wengine tunalaani wanavyohodhishwa maduka. Hebu acha kusujudia tabaka hodhi.

Labda niiweke wazi zaidi. Kama kuna mtu anahodhi maduka nje ya utaratibu uliowekwa basi achukuliwe hatua bila kujali rangi yake. Lakini kama mtu huyo amepata hizo sehemu kihalali aachiwe aendelee na biashara yake bila kujali rangi yake.
Duuh, leo bluu, nyekundu, nyeusi... nimeshawahi kuona unampiga mtu dongo kwa kosa la kutumia marangi mengi kujenga hoja. Naona umetumia tactic hiyo hiyo, japo bado hueleweki.

Hakuna anaejali race ya mtu. Tunajali kuhodhishana biashara, in this case kwa Wahindi.

Dilunga, mbona unakamata chelewa?
Kukamata chelewa maana yake nini? Lugha gani hiyo unaongea hapo? Hata hueleweki yani.

Kutokana na scenario yako ni weusi ( ambao unadai wanakandamizwa na wahindi) watakaowashambulia wahindi na si vice versa. Haitakuwa kuchinjana, bali weusi kuchinja wahindi. Sasa huyo Dewji atatoka na bunduki yake kwenda kuwatafuta weusi alipize kisasi? Wahindi wote hawafiki milioni moja, huo ubavu utatoka wapi?
Ukiwa outnumbered na maadui basi hawawezi kukupiga? duu, hiki sasa kituko! Wamarekani wangapi walienda kumtuliza Sadam na jeshi lake la nne kwa ukubwa duniani? Zikitokea zogo za kimatabaka kati ya Wazawa Asili na Wahindi basi itakuwa ni mshike mshike usiotabirika, na hata wewe unaweza kukumbwa, unless hutakuwepo nchini. Usituambie "mtachinjana...mtamalizana."

Wapi niliposema mweusi amepandishwa cheo? ...Metaphor maana yake nini? ...sikubali kuwekewa maneno mdomoni. Hiyo 'factiual shortcoming' iko wapi?
Metaphor ni figure of speech; hands in the cookie jar nilimaanisha umekamatwa makosani, ulitoa hadithi za zimamoto iliyokuwa factually wanting. Ulidai: "Kama katika nafasi hiyo hakuna mwenye sifa bali mhindi basi heri hiyo nafasi ibaki tupu au apewe mweusi asie na sifa ( kama walivyofanya New Haven, Conn. kwenye kupandishwa vyeo zima moto.)." Again, hakuna mweusi asiye na sifa aliyepewa nafasi New Haven, ulitoa hadithi yenye self-entitled facts.

... Ndiyo maana nimesema, angekuwa Kuhani ...Tutamkumbuka sana Kuhani.
Sielewi relevance ya huyo unae m-miss kwenye huu mjadala.

Sasa unataka niseme 'tutachinjana' wakati sina mpango wa kumchinja mtu? Na tangu lini uzalendo unapimwa na utayari wa mtu kumchinja mwenzake? Kama huo ndio uzalendo wenu, basi mkae nao. Sina haja nao. Hata chembe.
Uzalendo ni kujali ya nchi yako bila kujitoa katika matatizo yake kwe kutumia lugha kama za "mtachinjana...mtamaliza." Khaa! Sasa wewe kama hutachinjwa, hii pilipili basi ya shamba. Isikuwashe, hutakuwepo nyumbani.

"Tunawa bore wengine."
 
Dilunga unaanza kuni-boa. Hivi kweli unaamini kinachogombwa hapa ni Tesha na Msangi kutoa tendo kiupendeleo bila kujali aliyepewa ni kabila gani? Pdiddy ameiweka hoja yake wazi katika kichwa cha mada alipotofautisha mtanzania na mhindi. Bado hauoni ubaguzi hapo? Kama hauwezi kuona kuwa Tesha analaumiwa si kwa kufanya upendeleo tu bali kwa kumpendelea mhindi basi hamna namna ninaweza kukuonyesha vingine. Kilichobaki nikubali kutofautiana.

Kwa hiyo wewe unataka useme weeeee, lakini mwingine akisema unalia "mashindano ya semantics"! Onyesha paliposemwa kwamba Mhindi ndio tatizo.

Unadai nimesema kosa ni la Mhindi. Wapi nimesema hivyo? Kusema inaelekea kosa ni kupewa kazi au tenda Mhindi ni tofauti na kusema mkosaji ni Mhindi. Kosa si la Mhindi. Kosa ni yeye kuwa Mhindi. Kuna tofauti.

Unanishutumu kwa intellectual dishonesty ninapowaingiza wapemba kwenye mada lakini wewe ukiwaingiza wagogo, wamasai ......ruksa!

Ndugu wapendwa ,...mmmh haka kakidudu cha ufisadi naona akaishi kabisa...sasa dawa yake naona si maneno tuamue kufanya na vitendo...hivi karibuni afisa mmoja wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa tanzania BW TESHA....,alifanya vituko vya ajabu...kwa wale wanaoujua uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere..ukiwa unaingia kuna open space iko upande wa kulia...hiyo sehemu ilitangazwa wanaongeza uwanja kwa ajili ya parking...gafla wakaambiana chinichini kuna sehemu imebaki tunwezatengeneza hotel...ikatangazwa wazi....mtanzania mmoja akaenda kuomba wakiwepo baadhi ya watu...gafla ile tenda ikawa dili.....,yule ofisa akatangaza wamesitisha hawana mpango wa kujenga tena ile sehemu....
Baada ya muda kama mmefika karibuni kuna ujenzi ulikuwa unakamalika ..kabla ya mmoja wa waliomba tenda akaambiwa wamesitisha mpaka alipoingia hivi karibuni na kukuta ujenzi unamalizika ...walipoulizia akaambiwa amepewa yule yule muhindi wa flamingo...ambae ndie huyo amepewa lounge.amepewa supermarket..amepewa dutyfree shop.......amebakiza kupewa uwanja wa kutulia ndege......
Ndugu watanzania inafika wakati lazima tuwathamini watanzania wenzettu...kwamba wanauwezo wa kufanya chochote...alipokuwa akiulizia aliambiwa amepewa kwa sababu wanaitaji mtu anaeweza kuitengeneza ikaonekana ati sehemu ya kimataifa...tobaaa ilala,,,,mi nafikir kuna umuhimu mkubwa wa kuwachunguza sana hawa mabwana ambao wako TAA miaka na miaka...BWA MSANGI NA BWANA TESHA....HAPO HIYO COMBINATION YA MCHAGA NA MPARE...INATUREJESHA KWENYE UTUMWA KABISA...WANA DHARAU SANA ...HATA IKITOKEA UKIPINGANA NA HUYO MUHINDI AKIKUFIKISHA KWAO UMEKWISHA BILA HATA YA KUJIELEZA....
UFISADI UTAISHA LINI JAMANI???????????????

La qualification limejadiliwa, unataka kupotosha sasa. Pdidy amesema kina Msangi na Tesha walidai mhindi ana qualification za kutengeza biashara ya kimataifa kuliko waswahili. Na Pdidy akapinga hilo, akisema hata sisi Wazawa Asili tunaweza. Usidai hapa kwamba "hakuna anaezungumzia qualifications," please.

Posting ya Pdiddy hiyo hapo juu. Nionyeshe wapi kasema huyo Mhindi hana qualification? Kama ana qualification za kuifanya hiyo kazi, tatizo liko wapi kama si uhindi wake? Na baada ya hapo kama haitoshi, amewavisha hao wakina Tesha na Msangi dhambi ya uchaga na upare.! Mimi yote haya naona ni dalili za ubaguzi. Kama wewe hauoni basi iwe hivyo. Wapi aliposema huyo Pdiddy kuwa wakina Tesha kuwa huyo Mhindi ana qualification kuliko waswahili ? Unajuaje kuwa hakukuwa na wahindi wengine kwenye kuomba hiyo tenda na wao wakaonekana hawana sifa za aliye shinda? Kama huyo aliyeshinda amewapiku wote basi unataka kusema kuwa asipewe kwa sababu kuna huyo unaemuita mzawa anaedai nae angeweza kufanya hiyo kazi? Basi kwa nini walitangaza tenda ya wazi? Si wangesema tu kuwa hii tenda ni kw ajili ya wazawa, wengine wasijisumbue kuomba!

Mtoa hoja katoa identity ya beneficiary wa hii faulu, who happens to be Mhindi wa Flamingo. Sasa angesemaje, Mnyasa? Hata kwenye nchi zinazopigana ubaguzi wanasema kwenye taarifa za habari, the robbery suspect is a black male, of short stature, wearing dreadlocks. Sasa weusi, wafupi, na wafuga rasta walalamike ubaguzi maana polisi wametaja rangi na maumbile? Mnufaikaji wa ufisadi wa airport ni Mhindi, sio Mzigua, Mhindi!

Unakuwa disingenious! Kwa hiyo aliyepewa tenda angekuwa mzigua kichwa cha habari kingesema amepewa mzigua wakanyimwa watanzania! Swali langu la kwanza lilikuwa 'je Mhindi hawezi kuwa mtanzania?' Sasa kama hata uraia tunawakatalia bado utasema sio wabaguzi. Kwenye nchi hizo unazozingumzia hawatoi description ili kuondoa utaifa wa mtu. Wanaposema mtu mweusi mwenye dreadlock wanafanya hiyo kuelezea ethnicity ya mtu na si utaifa! Hao wakiambiwa polisi alidhani wao sio wamarekani kwa sababu ni watu weusi, naam , watakuwa na haki ya kudai ni ubaguzi.

Sasa unataka kunitwisha mzigo wa waliounga mkono hoja kibaguzi? Duuu... Lead post imelaani ufisadi wa Tesha na Msangi. Wahindi umeanza kuwatetea wewe!

Unaogopa nini kuitwa mbaguzi? Maneno yako si yanakushitaki? Mimi ninakataa ni mtu kuhukumiwa kwa sababu ya rangi yake basi mnanitwisha mzigo wa kuwatetea wahindi! Sioni aibu kumtetea Mhindi au mtu wa rangi nyingine yeyote pale anapoonewa kwa sababu ya rangi yake. Vile vile sisiti kumlaumu mtu wa rangi yeyote (pamoja na hao unaowaita wahindi) wanapokosea. Mantra yangu ni kuwa apimwe na ahukumiwe mtu kw kile alichofanya na si rangi yake.

Hiyo umetengeza wewe, hakuna paliposemwa Mhindi wa Flamingo sio Mtanzania!

Kichwa cha habari kinakusuta.

Unapokuwa na wagogo na wamachinga na wahehe ndio wafanyakazi wa wapare na wachaga na wahindi, umeshatengeza matabaka. Kuna ukabila ambao umejenga matabaka. Sijui usichoelewa ni nini. Usifurahi kuona Wahindi tu ndio wamehodhi maduka. Hayo matabaka sio mazuri kwa mustakabali wetu.

Kila jumuia kuna sehemu ambako imeegemea. Wahindi na wachaga kwenye biashara. Wanyasa kwenye uvuvi. Wakurya kwenye upolisi n.k. Sasa tukianza kudai kuwa kuna quota za aina ya kazi ambazo kila kabila itaruhusiwa hatutafika mbali. Kwenye maduka kuna wahindi, wapemba, wachaga, wakinga n.k. Mbona tunawaona wahindi peke yao? Kama wanahodhi kwa kutumia mbinu chafu kuzuia wengine kufungua maduka hapo watastahili kulaaniwa. Lakini kama wameshindana na kumiliki soko basi ni stahili yao. Mbona wasomali wamehodhi biashara ya magari makubwa? lakini mbona humo humo utawakuta watu weusi na wahindi? Tatizo liko wapi kama siyo mawazo potofu ya kibaguzi?

Mbona kwenye michezo huko ulaya na marekani wamejazana watu weusi? Mbona kwenye biashara ya motel huko marekani wamejazana wahindi? Mbona kwenye take Away huko uingereza wamejazana wahindi na wachina? Mbona kwenye vyuo vikuu wamejazana watu wa kutoka Asia? Mbona kwenye Financial sekta wamejazana wayahudi? Vyote hivyo utaita ni tabaka?

Unaona unavyojua kutunga vitu. Wapi nimesema nionyeshe alipotajwa Mhindi. Nimesema, nionyeshe paliposemwa tatizo ni Mhindi, kama sio Tesha na Msangi.

Nimesema tatizo hapa linaelekea ni uhindi wa huyo jamaa wa Flamingo. Kuweko kwa wakina Tesha na msangi katika kundi hilo hakubadilishi ukweli huo.

Umesema hupendi yeyote ahodhi maduka. Sisi tunapinga na kulaani Mhindi kuhodhi maduka. Wewe unawaka kutupinga. Sasa, hasa hasa unachosimamia wewe ni nini?

Nasimamia pale pale nilipo kila siku. Sijasema sipendi mtu yeyote kuhodhi maduka. Nilichosema ni kuwa kama kuna mtu amehodhi maduka nje ya utaratibu basi achukuliwe hatua. Lakini kama taratibu zinaruhusu basi hata kama ni mhindi aliyehodhi aachiwe aendelee na biashara yake. Mwelekeo wenu unaelekea kuwa tatizo si kuhodhi maduka bali ni Mhindi kuhodhi maduka. Angekuwa mweusi ( pengine asiwe mchaga au mpare) msingekuwa na tatizo. Hapo ndipo tunapotofautiana.

Kukamata chelewa maana yake nini? Lugha gani hiyo unaongea hapo? Hata hueleweki yani.

Mtu anapozama hata chelewa atakamata akitegemea itamuokoa. Ndivyo tulivyofundishwa Middle School.

Unarudia kosa lile lile. Utatoaje mishutuma based on "kama tatizo lenu ni..." Kama? Huna hakika? Tatizo ni mtu kuhodhi maduka, which happens to be Mhindi. Kusikia Mhindi una bend over backwards kumtetea wakati wengine tunalaani wanavyohodhishwa maduka. Hebu acha kusujudia tabaka hodhi.

Haya sasa. Sasa imekuwa wahindi wanahodhishwa maduka na si Mhindi wa Flamingo amehodhishwa maduka. Haya ndiyo mawazo ya kibaguzi ninayoyapinga. Yanaelekea kwenye racial profiling. Haiwezekani Mhindi akapewa maduka yale kwa sababu amequalify. Ni lazima alipendelewa au alihonga. Mimi hilo sitakubali hata siku moja. Mkiwaonea kwa sababu ya rangi yao nitawatetea. Na ikibidi kubend over backwards nitafanya hivyo. Hivi nyie mnaona kweli Mhindi hastahili kutetewa hata kama ameonewa? Halafu mnawalaumu wasipoonyesa mnachokiita uzalendo!

Ukiwa outnumbered na maadui basi hawawezi kukupiga? duu, hiki sasa kituko! Wamarekani wangapi walienda kumtuliza Sadam na jeshi lake la nne kwa ukubwa duniani? Zikitokea zogo za kimatabaka kati ya Wazawa Asili na Wahindi basi itakuwa ni mshike mshike usiotabirika, na hata wewe unaweza kukumbwa, unless hutakuwepo nchini. Usituambie "mtachinjana...mtamalizana."

Wrong context again. Huwezi kuzungumzia upuuzi wa vita vya Iraq kujenga hoja yako. Mfano mzuri ni wakati wa mauaji Rwanda, ni watutsi wangapi walitoka kwenda kuwachinja wahutu? Au ni wayahudi wangapi walitoka kwenda kuwauwa wajerumani au wa-pole wakati wa vita vya dunia vya pili? Machafuko hayo unayoyazungumzia yakitokea itakuwa ni weusi kuwavamia wahindi na kuwachinja na si vinginevyo. Sasa mimi nitahusika vipi? Huyo Dewji atanifuatia Buguruni kwa malapa kunifanya nini?

Metaphor ni figure of speech; hands in the cookie jar nilimaanisha umekamatwa makosani, ulitoa hadithi za zimamoto iliyokuwa factually wanting. Ulidai: "Kama katika nafasi hiyo hakuna mwenye sifa bali mhindi basi heri hiyo nafasi ibaki tupu au apewe mweusi asie na sifa ( kama walivyofanya New Haven, Conn. kwenye kupandishwa vyeo zima moto.)." Again, hakuna mweusi asiye na sifa aliyepewa nafasi New Haven, ulitoa hadithi yenye self-entitled facts.

Kwa hiyo wewe msema kweli mwenye kujua facts unataka kusema alipandishwa cheo mzungu huko New haven? Kama hakuna aliyepandishwa cheo hii ina tofauti gani na nafasi kuachwa tupu? Self-entitled facts ndiyo nini tena?

Sielewi relevance ya huyo unae m-miss kwenye huu mjadala.

Ubishi wa Kuhani ulikuwa tofauti na wa kwako. Wewe unataka kulazimisha lakini yeye angalau alikuwa anajaribu kubaki kwenye hoja. Ndiyo maana nina m-miss.

Uzalendo ni kujali ya nchi yako bila kujitoa katika matatizo yake kwe kutumia lugha kama za "mtachinjana...mtamaliza." Khaa! Sasa wewe kama hutachinjwa, hii pilipili basi ya shamba. Isikuwashe, hutakuwepo nyumbani.

"Tunawa bore wengine."

Uzalendo si kilemba. Kama wewe unaona maneno yangu ni dalili ya mimi kutokuwa mzalendo basi so be it.

Ni kweli, tunawaboa wengine.

Amandla.......
 
Haya majadiliano kati ya Dilunga na Fundi..hayaelekei vizuri!

Rushwa na upendeleo ni mbegu mbaya! awe Mhindi, Mchaga, Mdengereko!
 
Dilunga

Leo hii magazeti ya uingereza yanazungumzia kuhusu raia wao kuachiwa jela Laos akiwa mja mzito. Yanasema muingereza aachiwa na sio mtu mweusi aachiwa. Majuzi Bill Clinton amerudi na waandishi wa habari wa kimarekani, Laura Ling na Euna Lee, waliohukumiwa kifungo Korea ya kaskazini. Taarifa hazisemi wachina/wakorea( Ling na Lee) waokolewa na mmarekani ( Clinton) bali zinawazungumzia wote kama wamarekani. Hayo ya ethnicities zinakuja nyuma ya utaifa wao. Hivyo ndivyo inavyotakiwa.

Amandla........
 
Last edited:
Haya majadiliano kati ya Dilunga na Fundi..hayaelekei vizuri!

Rushwa na upendeleo ni mbegu mbaya! awe Mhindi, Mchaga, Mdengereko!

Rushwa na upendeleo ni m'baya, period. Kwa hii kuingiza rangi na kabila ndiyo tunawapa watu loop hole ya kujitetea kuwa wao wametumiwa tuu na hao wahindi.

Kama Tesha na Msangi walivuta pesa basi isemwe wazi na wachukuliwe hatua bila kujali wao ni wachaga au wapare. Kama hawakufanya hivyo waachiwe waendelee na kazi zao.

Kama huyo wa Flamingo alihonga au hakufuata utaratibu nae achukuliwe hatua bila kujali kama yeye ni Mhindi au sio! Kama hakufanya hivyo, aachiwe aendelee na biashara zake.

Tusifike mahali tukaanza kusema ati kwa sababu mchaga/mpare ndiyo waliotoa tenda na ni Mhindi aliyepata tenda hiyo basi kuna mchezo m'baya bila uthibitisho. Hicho ndicho ninachokipinga. Na nitaendelea kupinga kwa nguvu zangu zote.

Amandla.......
 
Ndugu wapendwa ,...mmmh haka kakidudu cha ufisadi naona akaishi kabisa...sasa dawa yake naona si maneno tuamue kufanya na vitendo...hivi karibuni afisa mmoja wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa tanzania BW TESHA....,alifanya vituko vya ajabu...kwa wale wanaoujua uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere..ukiwa unaingia kuna open space iko upande wa kulia...hiyo sehemu ilitangazwa wanaongeza uwanja kwa ajili ya parking...gafla wakaambiana chinichini kuna sehemu imebaki tunwezatengeneza hotel...ikatangazwa wazi....mtanzania mmoja akaenda kuomba wakiwepo baadhi ya watu...gafla ile tenda ikawa dili.....,yule ofisa akatangaza wamesitisha hawana mpango wa kujenga tena ile sehemu....
Baada ya muda kama mmefika karibuni kuna ujenzi ulikuwa unakamalika ..kabla ya mmoja wa waliomba tenda akaambiwa wamesitisha mpaka alipoingia hivi karibuni na kukuta ujenzi unamalizika ...walipoulizia akaambiwa amepewa yule yule muhindi wa flamingo...ambae ndie huyo amepewa lounge.amepewa supermarket..amepewa dutyfree shop.......amebakiza kupewa uwanja wa kutulia ndege......
Ndugu watanzania inafika wakati lazima tuwathamini watanzania wenzettu...kwamba wanauwezo wa kufanya chochote...alipokuwa akiulizia aliambiwa amepewa kwa sababu wanaitaji mtu anaeweza kuitengeneza ikaonekana ati sehemu ya kimataifa...tobaaa ilala,,,,mi nafikir kuna umuhimu mkubwa wa kuwachunguza sana hawa mabwana ambao wako TAA miaka na miaka...BWA MSANGI NA BWANA TESHA....HAPO HIYO COMBINATION YA MCHAGA NA MPARE...INATUREJESHA KWENYE UTUMWA KABISA...WANA DHARAU SANA ...HATA IKITOKEA UKIPINGANA NA HUYO MUHINDI AKIKUFIKISHA KWAO UMEKWISHA BILA HATA YA KUJIELEZA....
UFISADI UTAISHA LINI JAMANI???????????????

Mkuu hii mada nzuri sana hata mimi pale pameshanikera sana! Lakini ningelikuomba usitumie sana ukabila, maana fisadi hana kabila! hana!
 
Fundi Mchundo,

Naona kila pakisemwa MHINDI, unakuwa kama Waislaam wakorofi (hata hapa wataanza sasa hivi) wakisikia tu neno ISLAAM. Wewe hili neno Mhindi kila likitokea unakuwa MKALI si kawaida.
Ujumbe umelaani Tesha na Msangi. Imeandikwa pale kuwa Maduka yote wamepewa MHINDI mmoja (tafadhali, siyo wala wahindi 2) na WAPARE. Hilo la Wapare hata hujaliona. Hayo maneno kama "Tesha alifanya kituko cha mwaka " wala hujayaona.

FM, kwa hali inavyokwenda, kuna siku Tanzania tutapata Hitler wetu na amini usiamini, Wahindi watachomwa wakiwa hai. Na lazima ujuwe kitu kimoja, wote wanaoandika humu ndani ya JF, hawatahusika na upuuzi huo. Sasa wewe kama unakaa hapa kutuhubiri sisi eti tutachinjana, ni kwamba unapoteza muda na pia unasema ukweli. Kuna siku watu watachinjana. Wengine tunasema hilo ili watu kama Tesha na Msangi na pia huyo Mhindi wa Flamingo (siyo WAHINDI) na wahindi wengine wa namna hiyo waanze kubadili tabia zao.

Hii tumeiona hata Kenya juzijuzi tu hapa. Nilipokuwa JKT, Kaptain Mrimba alikuwa akituambia siku zote kuwa "Ukitaka kuwa na amani, basi JIANDAE NA VITA".
Wengine wakijiandaa na vita, FM unakuja na maneno TUTAKUJA CHINJANA. Kwa hiyo tuliache liendelee hadi siku moja BOOOM!!!!!
Kumbuka tena na tena "UKITAKA AMANI, JIANDAE NA VITA".

Please, FIKIRI MARA 2 neno JIANDAE NA VITA.
 
Huyu mtu ni nani anaemiliki biashara zote hizo? Tatizo ni kuwa ni mhindi au mtu mmoja kumiliki biashara hizo? Hivi angekuwa mweusi mwenzetu ndiye anaemiliki biashara hizo zote tungekubali kwa vile tuu ni mwenzetu? Na kama biashara hizo zinamilikiwa na watu tofauti lakini wana rangi moja tatizo liko wapi kama wamefuata utaratibu? Tunasahau hao tunaowaita wahindi nao wanamakabila kama sisi. Kama kila mmoja wao kivyake vyake aliingia na kushinda tenda kwa nini tunamlaumu? Au mna ushahidi kuwa alihonga au hakufuata utaratibu. Kama mnao, uwekeni wazi achukuliwe hatua kama mhalifu yeyote mwingine lakini si kwa sababu ati ni mhindi!

Badala ya kuuliza kwa nini anaajiri wahindi, tujiulize kwa nini wadogo zetu hawaajiriki? Si wahindi tu hata kwenye mashirika ya nje hawawataki wadogo zetu. Hatujitumi, tunataka kufanya ushap kila tunapokuweko, hatujui kuchangamkia wateja, tunadhani kuongea kama 50 cent ndiyo maendeleo, tunajua stahili zetu kuliko wajibu wetu n.k. Tuambiane ukweli badala ya kulalama tuu.

Amandla........
Tatizo ni kwamba wageni wengi wakifika pale wanadhani ndege imepotea ikaenda kutua Mumbai!
 
Kuwa agressive kwenye biashara hakukatazwi.Lakini cha kujiuliza ni ..ni siri gani ya mtu mmoja kupata tenda za kuendesha biashara zifuatazo katika Kiwanja chetu cha Ndege cha Julius Nyerere International Airport;
1.Flamingo Restaurant
2.Tanzanite Lounge
3.Duty Free shops karibu zote
4.Migahawa departure Lounges
5.Bureau de Change

1.Makao Makuu ya Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege Tanzania yalihamishiwa kutoka terminal 2 kwenda terminal 1 ili tu kumpa nafasi huyu mfanyabiashara kupanua Tanzanite Lounge ambayo huhudumia abiria wa business class ambao nao siyo wengi ki vile.

2.Maeneo ya kuondokea abiria yalipunguzwa ukubwa ili tu huyu mfanyabiashara apewe biashara.
3. Zaidi ya nusu ya staff kwenye hizo biashara ni waasia hata kuuza chai jamani watz HATUWEZI?

Sidhani kuwa nia ya hii thread ni ubaguzi dhidi ya wahindi ila ni kujiuliza kweli hakuna wengine wanaoweza hata kama siyo watanzania? Diversity/anuai ni muhimu.

WOS aliandika hapo juu na kujitahidi saana kujiweka mbali na maneno kuwa WAHINDI WALAUMIWE kwa matatizo hayo. Akasema wazi kabisa, tatizo ni pale MTU MMOJA AMEMILIKI kila kitu. Wewe tayari ukaja na jibu hapa chini:

Huyu mtu ni nani anaemiliki biashara zote hizo? Tatizo ni kuwa ni mhindi au mtu mmoja kumiliki biashara hizo? Hivi angekuwa mweusi mwenzetu ndiye anaemiliki biashara hizo zote tungekubali kwa vile tuu ni mwenzetu? Na kama biashara hizo zinamilikiwa na watu tofauti lakini wana rangi moja tatizo liko wapi kama wamefuata utaratibu? Tunasahau hao tunaowaita wahindi nao wanamakabila kama sisi. Kama kila mmoja wao kivyake vyake aliingia na kushinda tenda kwa nini tunamlaumu? Au mna ushahidi kuwa alihonga au hakufuata utaratibu. Kama mnao, uwekeni wazi achukuliwe hatua kama mhalifu yeyote mwingine lakini si kwa sababu ati ni mhindi!

Badala ya kuuliza kwa nini anaajiri wahindi, tujiulize kwa nini wadogo zetu hawaajiriki? Si wahindi tu hata kwenye mashirika ya nje hawawataki wadogo zetu. Hatujitumi, tunataka kufanya ushap kila tunapokuweko, hatujui kuchangamkia wateja, tunadhani kuongea kama 50 cent ndiyo maendeleo, tunajua stahili zetu kuliko wajibu wetu n.k. Tuambiane ukweli badala ya kulalama tuu.

Amandla........

Fundi Mchumdo..mimi nimeongeza tu maoni yangu kuhusu mtu mmoja kumiliki kila kitu..sijali kama ni muhindi, mchina au mswahili.Mimi nimeshangaa tu kuwa ni siri gani mtu mmoja/proprietor mmoja kufanikiwa kupata biashara zote hizi mahali pamoja?
NB Hizi biashara zote anazimiliki huyu mtu mmoja na siyo hata wawili.

FM,
Tatizo lako, hata tukishaanza kuongelea "hivi kwa nini Wahindi wanatupiga magoli?", wewe tayari utakuja na maneno "sisi wabaguzi". Hutoi hata muda au kusoma maneno mengine. Wengine huwa wanasema hata maneno ya TUFANYE NINI. Mfano maneno ya Dilunga juu ya makabila fulani kufanya kazi ya ovyoovyo na mengine kazi nzurinzuri. Wagogo wanajulikana kwa kuombaomba. Ila ona mfano mdogo tu wa WAGOGO wa MVUMI MISSION. Hapo Mvumi Mission ndiyo wanatoka akina Balisidya (Marehemu Ndyanao, Patrick), Malecela, Lusinde, Kabudi (sheria UDSM) na wengine wengi. Wengi wao kwa sasa wana maisha mazuri saana. Hii imetokana na nini? Genetics????? Jibu lake lipo. Sasa hata umasikini wa Watanzania, uvivu, wizi, na kila tabia mbaya ULIZOTUITA WATOTO WA WANAUME WENZIO ni kuwa ZIMELELEWA au kupandikizwa kwetu. Hizo zingeliweza kabisa kufutwa na hata kutengeneza taifa lenye watu wachapakazi na waaminifu kama WAJAPAN.
Sasa ili U-SOLVE, lazima kwanza uonyeshe tatizo. Ukianza kulionyesha tatizo na hapo FM huyooooo na maneno yake ya kibaguzi. Ila yeye hapohapo anasema "Si wahindi tu hata kwenye mashirika ya nje hawawataki wadogo zetu. Hatujitumi, tunataka kufanya ushap kila tunapokuweko, hatujui kuchangamkia wateja, tunadhani kuongea kama 50 cent ndiyo maendeleo, tunajua stahili zetu kuliko wajibu wetu n.k." Yaani unataka kusema mie hapa SIJITUMI, nafanya ushap kila ninapokuwepo na ninaongea kama 50cent? KAMAN!!!
Mbona hapa JF kuna Watanzania wengi tu wanafanya kazi nje na kwenye mashirika na makampuni makubwa? Wanaaminika na hata kutegemewa. Sasa huoni hayo maneno yako (tukitumia hii tabia yako) ni kuwa UMETUTUKANA WATANZANIA wote?????

Acha kwanza tuseme. Saidia kuonyesha tatizo liko wapi na si kulilia eti tunaleta UKABILA au UBAGUZI na mwisho tutowe SOLUTIONS ni kipi kwa maoni yetu kifanyike. Ukitunyamazisha, kumbuka ya KENYA.
 
Back
Top Bottom