Ufisadi TAA: Mhindi wa Flamingo apewa Tenda aliyonyimwa Mtanzania

Kuwa agressive kwenye biashara hakukatazwi.Lakini cha kujiuliza ni ..ni siri gani ya mtu mmoja kupata tenda za kuendesha biashara zifuatazo katika Kiwanja chetu cha Ndege cha Julius Nyerere International Airport;
1.Flamingo Restaurant
2.Tanzanite Lounge
3.Duty Free shops karibu zote
4.Migahawa departure Lounges
5.Bureau de Change

1.Makao Makuu ya Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege Tanzania yalihamishiwa kutoka terminal 2 kwenda terminal 1 ili tu kumpa nafasi huyu mfanyabiashara kupanua Tanzanite Lounge ambayo huhudumia abiria wa business class ambao nao siyo wengi ki vile.

2.Maeneo ya kuondokea abiria yalipunguzwa ukubwa ili tu huyu mfanyabiashara apewe biashara.
3. Zaidi ya nusu ya staff kwenye hizo biashara ni waasia hata kuuza chai jamani watz HATUWEZI?

Sidhani kuwa nia ya hii thread ni ubaguzi dhidi ya wahindi ila ni kujiuliza kweli hakuna wengine wanaoweza hata kama siyo watanzania? Diversity/anuai ni muhimu.
 
Hii kweli inahitaji kufanyiwa kazi,

Kwa ufupi huo uwanja unatia Kinyaa kwa kila kitu, nafikiri watu wanaendekeza pesa kuliko kazi, creativeness = 0.

Hepu fikiria, sehem ya Passport Check kwa wanaowasili, Mnapanga mstari na Vyoo viko pembeni yenu kushoto na unasikia harufu....

Shame on them,

Hapa nakubaliana sana na wewe. Bora wawape Wahindi tenda ya ukarabati na usafi wa vyoo airport, maana watafanya kazi ya uhakika vyoo vyote vitakuwa vinang'ara. Zunguka sehemu za starehe na maofisi yanayomilikiwa na Wahindi/Wazungu na utaona jinsi vyoo vilivyo visafi.
 
Bora wawape Wahindi tenda ya ukarabati na usafi wa vyoo airport, maana watafanya kazi ya uhakika vyoo vyote vitakuwa vinang'ara. Zunguka sehemu za starehe na maofisi yanayomilikiwa na Wahindi/Wazungu na utaona jinsi vyoo vilivyo visafi.

Mbona kwenye hiyo listi niliyoitoa hapo juu vyoo havimo? Is it by design that hawajapewa tender ya usafi wa vyoo?
 
Mbona kwenye hiyo listi niliyoitoA Hapo juu vyoo havimo? Is it by design that hawajapewa tender ua usafi wa vyoo?

Kwani hizo sehemu zinazomilikiwa na Wahindi/Wazungu wanaofanya kazi ya usafi/ukarabati ni nani? Si haohao walioajiriwa na kulipwa mishahara na menejimenti za Wazawa, au? Ndiyo maana nimeshauri bora wangewapa hiyo tenda.
 
Wewe hutamalizwa? Au umehama nchi?

Kikwete nae anaongea hivyo hivyo; alipofungua mkondo wa Fiber Optics, anasema mkongo huu unatoka Tanzania, unaenda Rwanda, Uganda etc. hivyo shughuli zao zitapita hapa kwetu, na sisi tutapata kidogo, msipofanya hivyo "hampati." Kina nani hawapati? Nyinyi, wewe Fundi Mchundo na Kikwete sio Watanzania?

Kama kuna wafanyabiashara wa makabila na rangi zote nchini, lakini opportunity fulani wanapata watu wa rangi na asili moja tu, hapo kuna tatizo. Hilo tu linaweza kuzua machukizo yanayoweza kupelekea machafuko. Wawe wamepata hizo biashara kihalali au kiharamu mwisho wa siku ukijaza Wahindi tu sehemu si busara, si fair. Akitokea right wing nativist mmoja akawa-sensitive watu watamsikiliza, kama Ujerumani ya Hitler na Wayahudi .

Ni sisi ndio tutakaomalizana, wewe Fundi Mchundo labda hautakuwepo, tutakaomalizwa tuko concerned.

Nimesema mtamalizana nyie ambao mtakaotoana macho kwa vile tu mtu wa rangi fulani au kabila fulani amepata na wewe haukupata. Kwa vile mimi kwenye hiyo tafrani sitakuwepo basi natumaini nitapona.

Hivi kuna ushahidi wowote kuwa hao watu wanapendelewa kutokana na rangi zao na si ujuzi wao? Sasa kama hao mnaowaita wahindi wenye uraia wa Tanzania wanatimiza kila sharti wanyimwe tu kwa sababu si weusi? Basi tutangaze wazi kuwa hatutafuata uwezo (nadhani mnaita meritocracy) bali tutawawekea quota. Kama katika nafasi hiyo hakuna mwenye sifa bali mhindi basi heri hiyo nafasi ibaki tupu au apewe mweusi asie na sifa ( kama walivyofanya New Haven, Conn. kwenye kupandishwa vyeo zima moto.). Kama katika tenda, mhindi mtanzania ametimiza kila kitu na ameonyesha dhahiri ana uwezo wa kutekeleza, anyimwe apewe mtu mweusi. Na akituingiza mkenge basi tutaridhika maana ni mtu mweusi mwenzetu aliyetudhulumu. Halafu tukimaliza wahindi basi tuwawekee quota wahaya, wachaga, wapare na wengine.

Hao mnaowalaamu wamewaachia utawala na serikali karibu yote watu weusi. Hao wanaotoa hizo tenda, wanaogawa maduka ni watu weusi wenzenu. Lakini leo mnamlaumu huyo mnayemuita mhindi badala ya kuwauliza wenzenu kwa nini wanawapendelea wahindi? Wakiwatolea mifano ya mara ngapi wamelizwa na weusi wenzao sitoshangaa. Nina rudia, tuliwanyang'anya kila kitu, tukagawana na tukaviua. Leo tumewakabidhi mizoga, wanaifufua basi tunaanza kuwaonea gele? Tunataka tuwanyang'anye ili tuharibu tena? Bila kujiangalia na kujikosoa hatutatoka hapa tulipo. Tutabaki kulia kuwa tumeonewa. Huo wimbo ushaanza kukosa ladha. Siku hizi jini likujualo linakula mpaka mifupa!

Kama mko concerned kuhusu kumalizana, basi anzeni kuwekana sawa wenyewe badala ya kutaka kila kitu mpewe.

Amandla.......
 
Hapa nakubaliana sana na wewe. Bora wawape Wahindi tenda ya ukarabati na usafi wa vyoo airport, maana watafanya kazi ya uhakika vyoo vyote vitakuwa vinang'ara. Zunguka sehemu za starehe na maofisi yanayomilikiwa na Wahindi/Wazungu na utaona jinsi vyoo vilivyo visafi.

Mi sikubaliani nawe kabisa. Suala si wahindi; kuna ofisi za wahindi kisutu huko ni chafu hakuna mfano.

Ishu hapa ni malengo, kama ofisi ni ya mweusi na anamkalati wa kuifanya ionekane nadhifu itakuwa bora tu. awe mhindi, mzungu au mweusi yeyote anaweza kuwa mchafu au msafi. ziko ofisi za weusi safi tu, au wataka sema zote zaweusi chafu????!!!!!!!!! labda yako!
 
Nimesema mtamalizana nyie ambao mtakaotoana macho kwa vile tu mtu wa rangi fulani au kabila fulani amepata na wewe haukupata. Kwa vile mimi kwenye hiyo tafrani sitakuwepo basi natumaini nitapona.

Hivi kuna ushahidi wowote kuwa hao watu wanapendelewa kutokana na rangi zao na si ujuzi wao? Sasa kama hao mnaowaita wahindi wenye uraia wa Tanzania wanatimiza kila sharti wanyimwe tu kwa sababu si weusi? Basi tutangaze wazi kuwa hatutafuata uwezo (nadhani mnaita meritocracy) bali tutawawekea quota. Kama katika nafasi hiyo hakuna mwenye sifa bali mhindi basi heri hiyo nafasi ibaki tupu au apewe mweusi asie na sifa ( kama walivyofanya New Haven, Conn. kwenye kupandishwa vyeo zima moto.). Kama katika tenda, mhindi mtanzania ametimiza kila kitu na ameonyesha dhahiri ana uwezo wa kutekeleza, anyimwe apewe mtu mweusi. Na akituingiza mkenge basi tutaridhika maana ni mtu mweusi mwenzetu aliyetudhulumu. Halafu tukimaliza wahindi basi tuwawekee quota wahaya, wachaga, wapare na wengine.

Hao mnaowalaamu wamewaachia utawala na serikali karibu yote watu weusi. Hao wanaotoa hizo tenda, wanaogawa maduka ni watu weusi wenzenu. Lakini leo mnamlaumu huyo mnayemuita mhindi badala ya kuwauliza wenzenu kwa nini wanawapendelea wahindi? Wakiwatolea mifano ya mara ngapi wamelizwa na weusi wenzao sitoshangaa. Nina rudia, tuliwanyang'anya kila kitu, tukagawana na tukaviua. Leo tumewakabidhi mizoga, wanaifufua basi tunaanza kuwaonea gele? Tunataka tuwanyang'anye ili tuharibu tena? Bila kujiangalia na kujikosoa hatutatoka hapa tulipo. Tutabaki kulia kuwa tumeonewa. Huo wimbo ushaanza kukosa ladha. Siku hizi jini likujualo linakula mpaka mifupa!

Kama mko concerned kuhusu kumalizana, basi anzeni kuwekana sawa wenyewe badala ya kutaka kila kitu mpewe.

Amandla.......

Vizuri sana mkuu
Hii tabia ya kulia lia kwa kila kitu kwa kigezo cha ufisadi nafikiri tuikkomeshe, na tuangalie namna bora sahihi ktk ushindani ,hichi kigezo cha ufisadi nafikiri mbele ya safari kitatudumaza.

Ukienda nchi za mashariki mwa europe wawekezaji kwenye ma supermarket ,viwanda nk ni watu wa magharibi lakini jamaa hawaliilii upendeleo wanapigana na kuparangana kupiganisha fikra huru .
 
Kuwa agressive kwenye biashara hakukatazwi.Lakini cha kujiuliza ni ..ni siri gani ya mtu mmoja kupata tenda za kuendesha biashara zifuatazo katika Kiwanja chetu cha Ndege cha Julius Nyerere International Airport;
1.Flamingo Restaurant
2.Tanzanite Lounge
3.Duty Free shops karibu zote
4.Migahawa departure Lounges
5.Bureau de Change

1.Makao Makuu ya Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndge Tanzania yalihamishiwa

2.Maeneo ya kuondokea abiria yalipunguzwa ukubwa ili tu huyu mfanyabiashara apewe biashara.
3. Zaidi ya nusu ya staff kwenye hizo biashara ni waasia hata kuuza chai jamani watz HATUWEZI?

Huyu mtu ni nani anaemiliki biashara zote hizo? Tatizo ni kuwa ni mhindi au mtu mmoja kumiliki biashara hizo? Hivi angekuwa mweusi mwenzetu ndiye anaemiliki biashara hizo zote tungekubali kwa vile tuu ni mwenzetu? Na kama biashara hizo zinamilikiwa na watu tofauti lakini wana rangi moja tatizo liko wapi kama wamefuata utaratibu? Tunasahau hao tunaowaita wahindi nao wanamakabila kama sisi. Kama kila mmoja wao kivyake vyake aliingia na kushinda tenda kwa nini tunamlaumu? Au mna ushahidi kuwa alihonga au hakufuata utaratibu. Kama mnao, uwekeni wazi achukuliwe hatua kama mhalifu yeyote mwingine lakini si kwa sababu ati ni mhindi!

Badala ya kuuliza kwa nini anaajiri wahindi, tujiulize kwa nini wadogo zetu hawaajiriki? Si wahindi tu hata kwenye mashirika ya nje hawawataki wadogo zetu. Hatujitumi, tunataka kufanya ushap kila tunapokuweko, hatujui kuchangamkia wateja, tunadhani kuongea kama 50 cent ndiyo maendeleo, tunajua stahili zetu kuliko wajibu wetu n.k. Tuambiane ukweli badala ya kulalama tuu.

Amandla........
 
Mi sikubaliani nawe kabisa. Suala si wahindi; kuna ofisi za wahindi kisutu huko ni chafu hakuna mfano.

Ishu hapa ni malengo, kama ofisi ni ya mweusi na anamkalati wa kuifanya ionekane nadhifu itakuwa bora tu. awe mhindi, mzungu au mweusi yeyote anaweza kuwa mchafu au msafi. ziko ofisi za weusi safi tu, au wataka sema zote zaweusi chafu????!!!!!!!!! labda yako!

Hata India kuna uchafu uliokithiri zaidi hata ya ule tunao ujua Tanzania. Kwa vyovyote vile, nadhani hapo juu umejijibu mwenyewe: Ukweli ni kwamba usafi wa sehemu kama vyoo siyo malengo/kipaumbele ya menejimenti nyingi za biashara/shule/idara na sehemu nyinginezo zinazotumiwa na umma.
 
Wewe hutamalizwa? Au umehama nchi?

Kikwete nae anaongea hivyo hivyo; alipofungua mkondo wa Fiber Optics, anasema mkongo huu unatoka Tanzania, unaenda Rwanda, Uganda, Burundi, hivyo shughuli zao zitapita hapa kwetu, na sisi kibiashara tutapata kidogo, msipofanya hivyo "hampati." Kina nani hawapati? Nyinyi, wewe Fundi Mchundo na Kikwete sio Watanzania?

Kama kuna wafanyabiashara wa makabila na rangi zote nchini, lakini opportunity fulani wanapata watu wa rangi na asili moja tu, hapo kuna tatizo. Hilo tu linaweza kuzua machukizo yanayoweza kupelekea machafuko. Wawe wamepata hizo biashara kihalali au kiharamu mwisho wa siku ukijaza Wahindi tu sehemu si busara, si fair. Akitokea right wing nativist mmoja akawa-sensitize watu watamsikiliza, kama Ujerumani ya Hitler na Wayahudi .

Ni sisi ndio tutakaomalizana, wewe Fundi Mchundo labda hautakuwepo, tutakaomalizwa tuko concerned.

... ... ???
 
Huyu mtu ni nani anaemiliki biashara zote hizo? Tatizo ni kuwa ni mhindi au mtu mmoja kumiliki biashara hizo? Hivi angekuwa mweusi mwenzetu ndiye anaemiliki biashara hizo zote tungekubali kwa vile tuu ni mwenzetu? Na kama biashara hizo zinamilikiwa na watu tofauti lakini wana rangi moja tatizo liko wapi kama wamefuata utaratibu? Tunasahau hao tunaowaita wahindi nao wanamakabila kama sisi. Kama kila mmoja wao kivyake vyake aliingia na kushinda tenda kwa nini tunamlaumu? Au mna ushahidi kuwa alihonga au hakufuata utaratibu. Kama mnao, uwekeni wazi achukuliwe hatua kama mhalifu yeyote mwingine lakini si kwa sababu ati ni mhindi!

Badala ya kuuliza kwa nini anaajiri wahindi, tujiulize kwa nini wadogo zetu hawaajiriki? Si wahindi tu hata kwenye mashirika ya nje hawawataki wadogo zetu. Hatujitumi, tunataka kufanya ushap kila tunapokuweko, hatujui kuchangamkia wateja, tunadhani kuongea kama 50 cent ndiyo maendeleo, tunajua stahili zetu kuliko wajibu wetu n.k. Tuambiane ukweli badala ya kulalama tuu.

Amandla........

Fundi Mchumdo..mimi nimeongeza tu maoni yangu kuhusu mtu mmoja kumiliki kila kitu..sijali kama ni muhindi, mchina au mswahili.Mimi nimeshangaa tu kuwa ni siri gani mtu mmoja/proprietor mmoja kufanikiwa kupata biashara zote hizi mahali pamoja?
NB Hizi biashara zote anazimiliki huyu mtu mmoja na siyo hata wawili.
 
Lakini leo mnamlaumu huyo mnayemuita mhindi badala ya kuwauliza wenzenu kwa nini wanawapendelea wahindi?

Nionyeshe wapi kalaumiwa Mhindi kwenye lead post ya Pdidy. Tumemlaumu huyo mzee Tesha, mtoa tenda.

Ukiona ni Wahindi tu ndio wana qualify, you must do something about it. Hata tukichukulia mfano wa nchi zenye historia ya discrimination, kuna USA Civil Rights ya 1982, hususan section 5, ambayo kimsingini inafundisha kwamba kuna wakati inabidi utilie mashaka matokea ya mtihani au tender invitation ambayo ni Wachagga na Wapare tu wana pasi. Je ni kwa sababu ni Wapare tu ndio wana mitaji ya bureau de change za airport? Kwa nini? Inatupasa kuaangalia pia jinsi ya kuwawezesha Wamakua wa Mtwara kujenga miundo mbinu ya biashara. Au ungependa Wagogo waendelee kuwa omba omba mjini, Wamasai walinzi wa wachagga, Wahehe wafanyakazi wa ndani wa wapare, Wamakonde wachongee vinyago wazungu wa Mwenge, Wakurya watumwe kufa vitani Uganda? Ndio ma French Revolution yanavyoanza hivyo.

Nilibahatika kumsoma mtafiti mmoja ambaye alisema ukiona ni Wachina tu wamejaa kwenye kumiliki dry cleaners, au Wahindi tu
wanajaza mafuta kwenye gas station, au Wa Mexico tu wanasafisha maofisi, ujue hizo ndio nyanja ambazo tabaka tawala liliwaruhusu waingie, msingi wake ni discrimination. Must do something about it.

Halafu siku ya mzeta mzeta wa kukatana majambia kimatabaka au kikabila usidhani utapona kwa sababu eti wewe hukuwa mkabila. Usituambie "mtamalizana" unless wewe hutakuwepo nyumbani.

Halafu New Heaven, CT, hakuna mweusi aliyependelewa na kupandishwa cheo. Promotion zote zilifutwa, na baadae mahakama kuu ikasema haikuwa sawa, wazungu wale walitakiwa wapate promotion zao. Kwa hilo Fundi Mchundo usitake kunipeka hapa, ( I'm cracking up to death over on this end, kwa sababu, nothing is sweeter than kumkamata Fundi Mchundo with his hands in the cookie jar trying to pull a fast FMESian narration!)
 
Mnacholaumu ni mhindi kupewa au tenda kugawiwa isivyo halali?

Msije ikawa na nyie ni wabaguzi wa rangi!
 
Ila kweli je Mungu sii ametoa vipaji mbali2 kwa kila watu?

Wachaga- elimu na biashara, Wahindi- biashara, Mara- jeshi, Wahaya- sheria.. n.k n.h!!

Sasa utamlazimisha Mdengereko awe kama Mengi kweli je ataweza?? Sii kumwonea tu???

Ni mawazo tu!!
 
Nionyeshe wapi kalaumiwa Mhindi kwenye lead post ya Pdidy. Tumemlaumu huyo mzee Tesha, mtoa tenda.

Kichwa cha habari kinam/wasuta.

Ukiona ni Wahindi tu ndio wana qualify, you must do something about it. Hata tukichukulia mfano wa nchi zenye historia ya discrimination, kuna USA Civil Rights ya 1982, hususan section 5, ambayo kimsingini inafundisha kwamba kuna wakati inabidi utilie mashaka matokea ya mtihani au tender invitation ambayo ni Wachagga na Wapare tu wana pasi. Je ni kwa sababu ni Wapare tu ndio wana mitaji ya bureau de change za airport? Kwa nini? Inatupasa kuaangalia pia jinsi ya kuwawezesha Wamakua wa Mtwara kujenga miundo mbinu ya biashara. Au ungependa Wagogo waendelee kuwa omba omba mjini, Wamasai walinzi wa wachagga, Wahehe wafanyakazi wa ndani wa wapare, Wamakonde wachongee vinyago wazungu wa Mwenge, Wakurya watumwe kufa vitani Uganda? Ndio ma French Revolution yanavyoanza hivyo.

Si kutilia mashaka ati kwamba hawa wanakwiba mitihani. Ni kuangalia ni namna gani hao wachaga na wapare wanakuwa na advantage katika hiyo mitihani. Kama maswali yote yanahusu mazao ya kahawa, ndizi na pombe ya pingu basi tutasema hamna namna mzaramo wa mwaneromango anaweza kufaulu. Badala ya kupiga marufuku maswali ya kahawa, ndizi na pingu tunaongeza yanayohusu ngoma na kumfundisha mzaramo huyo kuhusu kahawa, ndizi na pombe ya pingu.

Sasa unataka kusema ili kumzuia mgogo kuwa omba omba basi tumnyang'anye mpemba taksi na kumkabidhi mgogo?

Kwani French Revolution ilikuwa kupinga utawala wa rangi au wa tabaka? Hao wakina Robespierre walikuwa rangi tofauti na Marie Antoinette? Mbona unataka kuchanga mambo! Mnyanyasaji ni mnyanyasaji tu bila kujali rangi. Anaenyanyaswa akichukia hatajali rangi ya kiatu kilicho shingoni mwake. Wote kwake watakuwa halali. Ninachopinga mimi ni hii dhana kuwa tatizo ni rangi na siyo vitendo vya mhusika bila kujali rangi. Tatizo si mhindi kuhodhi maduka bali mtu yeyote kuhodhi maduka.

Nilibahatika kumsoma mtafiti mmoja ambaye alisema ukiona ni Wachina tu wamejaa kwenye kumiliki dry cleaners, au Wahindi tu wanajaza mafuta kwenye gas station, au Wa Mexico tu wanasafisha maofisi, ujue hizo ndio nyanja ambazo tabaka tawala liliwaruhusu waingie, msingi wake ni discrimination. Must do something about it.

Wrong context. Hao wanafanya hivyo kwa sababu wananyimwa nafasi kwengine. Au unataka kuema wahindi kujazana kwenye biashara ni kutokana na sisi weusi kuwabagua katika maeneo mengine (Mara ya mwisho nilipoangalia, utawala umeshikwa na weusi na si wahindi.)? Kama ni hivyo basi tujilaumu sisi kwa kutowapa nafasi serikalini, jeshini n.k. na kuwalazimisha wabanane kwenye biashara.

Halafu siku ya mzeta mzeta wa kukatana majambia kimatabaka au kikabila usidhani utapona kwa sababu eti wewe hukuwa mkabila. Usituambie "mtamalizana" unless wewe hutakuwepo nyumbani.

Hapa atakae shika jambia ni nani? Mhindi au mtu mweusi? Kama ni hivyo, mtanichinjaje mimi mweusi mwenzenu? Au mtachinja wote ambao hawatawasaidia kuwachinja wahindi?

Halafu New Heaven, CT, hakuna mweusi aliyependelewa na kupandishwa cheo. Promotion zote zilifutwa, na baadae mahakama kuu ikasema haikuwa sawa, wazungu wale walitakiwa wapate promotion zao. Kwa hilo Fundi Mchundo usitake kunipeka hapa, ( I'm cracking up to death over on this end, kwa sababu, nothing is sweeter than kumkamata Fundi Mchundo with his hands in the cookie jar trying to pull a fast FMESian narration!)

Matokeo ya mtihani yalifutwa kwa sababu hakuna mweusi aliyefaulu. Wangefuata matokeo wangepandishwa cheo weupe watupu na hii ingeenda kinyume na miongozo yao ya kuhakikisha diversity katika sehemu ya kazi. Kutokana na hili, wazungu wakadai ni reverse discrimination kuwa ingawa wamefaulu mitihani na kutimiza vigezo vyote bado walinyimwa vyeo kwa sababu tu wana rangi isiyotakiwa. Wangekuwa weusi , wangepandishwa vyeo. Na huko ndiko mnakotaka kutupeleka. Mhindi anyimwe nafasi kwa sababu tu ni mhindi hata kama hakuna mweusi aliye'qualify' au hata kuonyesha anaitaka nafasi.

Hiyo cookie jar iko wapi? You should know me better by now! Kuhani wala asingefanya hilo kosa.

Amandla........
 
Ubaguzi ni sumu na laana mbaya sana. Let's say mmiliki wa biashara hizo angekuwa Mchaga. Ungesikia baadhi ya watu wanahoji inakuwa kuwaje huyu mchaga mmoja kumiliki biashara zote hizo. Human race ina safari ndefu kweli ya kuelekea huko kwenye usawa na haki bila ya kujali rangi, dini, jinsia, nasaba, asili ya utaifa, n.k.
 
Kichwa cha habari kinam/wasuta.
Bado hujaonyesha ni wapi kalaumiwa Mhindi, zaidi ya Tesha, mtoa tenda.
Sasa unataka kusema ili kumzuia mgogo kuwa omba omba basi tumnyang'anye mpemba taksi na kumkabidhi mgogo?
Intellectual dishonesty! Kwa maneno mengine, umejifanya hujui jibu la hilo swali: ambalo ni, tujaribu kuangalia, kwa mfano, ni kwa nini Wagogo hawana vitega uchumi wamegeuka omba omba. Ni mashule yamepungua kwao, au viongozi wao wabovu, au ni msisitizo mdogo wa elimu, au ni jadi tu? Haya yanaweza kuponywa bila kumnyang'anya Mpemba taxi. Kitu ambacho sikusema, na unajua siwezi kusema. Niiteje intellectual dishonesty yako kwa kiswahili, uongo wa kiakili?

Kwani French Revolution ilikuwa kupinga utawala wa rangi au wa tabaka? ... Mbona unataka kuchanga mambo!

Tabaka.

Mifano yangu yote haikuongelea rangi. Nilisema tabaka la makabila fulani kuwa watwana wa tabaka la makabila mengine: walinzi wamasai, omba omba wagogo, housegirl wahehe. Hayo yote ni aina za tofauti za hali za maisha zinazojenga matabaka, kama ambavyo Wahindi walikuwa tabaka la kati wakati wa ukoloni. Wana rangi ya kihindi, lakini wamefanyika tabaka. Rangi, makabila, dini, hujenga matabaka. Wafaransa hawakuwa na makabila, wana dini tofauti, wala rangi tofauti. Matabaka yao yalitokana na ubujuazii. Sisi matabaka yetu yatatokana na dini, kabila, rangi. Lakini bado, kama Ufaransa, bado ni matabaka. Haya, niambie nimechanganya wapi?

Ninachopinga mimi ni hii dhana kuwa tatizo ni rangi na siyo vitendo vya mhusika bila kujali rangi.

Hapa napo unakosea au unakosesha kusudi. Hakuna aliyesema tatizo ni rangi. Tatizo ni kundi moja kumilikishwa nyanja za uchumi, imetokea tu kwamba kundi lenyewe ni la Wahindi. Again, nionyeshe paliposemwa tatizo ni Mhindi kwenye lead post ya Pdidy.

Tatizo si mhindi kuhodhi maduka bali mtu yeyote kuhodhi maduka.
Sasa kama tatizo ni mtu yeyote kuhodhi maduka, kwa nini unatetea Mhindi kuhodhi maduka?

Hapa atakae shika jambia ni nani? Mhindi au mtu mweusi? Kama ni hivyo, mtanichinjaje mimi mweusi mwenzenu? Au mtachinja wote ambao hawatawasaidia kuwachinja wahindi?
Kwa hiyo Wahindi na Wazawa Asilia wakianza kuchinjana wewe utapona kwa vile wewe ulikuwa unatetea wahindi. Yani Dewji na bunduki vitani kwenye mshike mshike atasimama atakuuliza "wewe nyeusi Fundi Chundo iko pande gani?" Utamwambia "nilikuwa nakuteteeni kabla ya vita" halafu atakuacha? You kidding me.
Matokeo ya mtihani yalifutwa kwa sababu hakuna mweusi aliyefaulu...
Ndio, mwanzoni ulitoa maelezo potofu, na context ikawa potofu. Hakuna mweusi aliyepandishwa cheo.

Hiyo cookie jar iko wapi? You should know me better by now! Kuhani wala asingefanya hilo kosa.
Cookie jar ni metaphor tu. I should know you better what, kwamba huwezi kukosea katika kuelezea mkasa wa Zimamoto wa New Heaven? FMESian narration ni maelezo yenye factual shortcomings, kama ulivyoelezea kisa cha CT mwanzoni, nilitegemea ungeelewa. Huyo ambaye asingeweza kufanya kosa la kukukosoa labda hajui kwamba yeyote aweza kukosea. Na pia, the vintage Fundi Mchundo asingetaka kupigiwa pigiwa makofi tu kwa kila anachosema.

Wrong context. Hao wanafanya hivyo kwa sababu wananyimwa nafasi kwengine. Au unataka kuema wahindi kujazana kwenye biashara ni kutokana na sisi weusi kuwabagua katika maeneo mengine (Mara ya mwisho nilipoangalia, utawala umeshikwa na weusi na si wahindi.)? Kama ni hivyo basi tujilaumu sisi kwa kutowapa nafasi serikalini, jeshini n.k. na kuwalazimisha wabanane kwenye biashara.
Kweli. Mfano wa wahindi kujazana kwenye ku pump gas una angle ya discrimination ya Kimarekani-Marekani na ni wrong context kwa Tanzania ambapo nguvu ya kisiasa tunayo weusi. Nilikosea. Ila usitetee wanaohodhi maduka kwa vile tu ni wahindi. Na usituambie "mtamalizana... mtachinjana," kuwa na chembe ya uzalendo.
 
FMESian narration ni maelezo yenye factual shortcomings, .

- Dilunga, Mr. Hard Talk nani ameiba ID yako mkuu? This is not you no facts na research, mapovu kila kona ya pua na mdomo mpaka kila kona ya JF, kwani lazima ulale humu masaa 24/7?,

- Sometimes unaweza kupumzika hata siku moja tu ndugu yangu kuja hapa uka-refresh na ku-reset ili uanze upya tena maana ukishaona unaongea na Fundi Mchundo halafu bado unaweweseka na FMEs ni wakati wa timeout bro!

- For years sasa unalilia ya uongo wangu lakin i never ukaweza hata mara moja kuthibitisha kwa facts, evidence wala dataz, sasa unaona hata wananchi hawa-pay mind tena maana imekua kero na kelele za mlango, siku utakayo nikamata na uongo hapa JF, au nje ya hapa nitakulipa mkuu wangu, au angalau nishike na house girl wa mtu, Bwa! ha! ha! au ninamuomba kwenda naye Cinema badala ya kwenda na mke wangu, waite polisi mara moja au kimbilia huku JF uripoti factual narration zangu,

Hard Talk my foot, take a break mkuu huwezi kushinda humu 24/7 ukawa mzima it shows sasa wazi kwamba you are loosing it! Jamaa ndio kwanza ametoka kwenye mapumziko nyumbani si unaona alivyo-reset na ku-refresh sijui kwa nini hakusaidii mawazo!

Eti unataka na mimi nianzishe mis-Factual narration zako na mahousegirls wa watu patatosha kweli hapa?

Respect.

FMEs!
 
Back
Top Bottom