Ufisadi TAA: Mhindi wa Flamingo apewa Tenda aliyonyimwa Mtanzania

Acha kwanza tuseme. Saidia kuonyesha tatizo liko wapi na si kulilia eti tunaleta UKABILA au UBAGUZI na mwisho tutowe SOLUTIONS ni kipi kwa maoni yetu kifanyike. Ukitunyamazisha, kumbuka ya KENYA.

Ahsante sana Sikonge.
 
Kuwa agressive kwenye biashara hakukatazwi.Lakini cha kujiuliza ni ..ni siri gani ya mtu mmoja kupata tenda za kuendesha biashara zifuatazo katika Kiwanja chetu cha Ndege cha Julius Nyerere International Airport;
1.Flamingo Restaurant
2.Tanzanite Lounge
3.Duty Free shops karibu zote
4.Migahawa departure Lounges
5.Bureau de Change

HIVI UNAFIKIRI HILO TU....WAMEKAMATA HADI JESHINI....NENDA PALE LUGALO ANAESUPPLY VILE VIFAA MNAVYOCHUKUA KWA BEI POA HUYUHUYU...SASA SIJUI WAMEKOSEKANA WATANZANIA WAKUFANYA HIZI BIASHARA
 
Mnacholaumu ni mhindi kupewa au tenda kugawiwa isivyo halali?

Msije ikawa na nyie ni wabaguzi wa rangi!


1))Tunalaumu mtu mmoja kupewa kila sehemu pale AIRPORT....

2))Tunalaumu kitendo cha wazawa kutopewa nafasi ya kumiliki biashara....ukiwa unaingia pale airport.......supermarket ya mtu mmoja,,ukiingia ndani lounge ya huyohuyo...nenda maduka ya duty free shop mmiliki huyo huyo...unataarifa alipewa na tender ile ya kulipia maegesho ya magari akapewa masharti ajenge .....labda kwa kukushtua alijenga wakati wenzako unaowatetea wakijipanga watu wakaenda juu yao...ndipo alipoambiwa asimamishe na mabosi wa TAA wakaitwa na kuambiwa wamalizie na kukodisha...unajua kilichofanyi,ka....akapewa mtu aendeshe hito sehemu ya maegesho.....huyo huyo tunaemzungumzia akamuingiza mtu ndani akashinda kwa niaba yake....TAA baada ya muda wakaja na mada mapato hayaonekani....unajua percent aliokuwa anapata. na TAA wanaondoka na ngapi.......mwachie mungu...

Hakuna udini.ukabila nduguzanguni....tupo hapa kuelimishana na kama babako ama mamako ameshika kisu kwenye hizo wizara husika lengo letu ni nyie/.sisi kuwashtua jamani haya mambo yanaendaje.......inasikitisha sanasaana ile supermarket ya nje alikuwa ameajiri watu kutoka india tupu......je hakukuwa na watanzania wenye hadhi ya kuuza supermarket???aliposikia minongono akaajiri vijana kama 4 wawili wako ndani kama walinzi na weengine wawili wanakaanje kufungua na kufunga milango wateja waingie....imagine anleta group la watu toka india anawaambia awape passport zao...na siku likilipuka ama kukosea wanaondolewa na AIR INDIA kama wakimbizii....kweli ni haki...swala kubwa kwa nini sisi watanzania tusijiamini kufanya vitu wanavyofanya wenzetu...ukitaka kuongelea swala la utaifa mi sibishani...maana owner ana passport ya INDIA,UGANDA,TANZANIA, na CANADA..Wapi tanzania tumeruhusiwa kuwa na passport zaidi ya mbili...anyway mlio karibu na hao vingunge wajulisheni watanzania nayo wana haki ya kumiliki ...katika nchi yao...tusipige makelele ya ukabila /udini tuongelee jambo muhimu lilopo hapa....
BARRICK wamekuja na kuchota madini yetu kwa raha zao na huku watu wa pembeni wankufa na maji ya sumu....sasa utasema kwasabababu ni ya kutoka canada watu waendelee kufa kisa JF wataona kuna URANGI oooooooooooooohh ni give m a break...lets open our eyes...ndio maana bunge la sasa sio lile lakina msekwa .......watu wanaamka.....nasi tuamke jamani....UTAJIRI uko hapahapa tanzania auitaji kukimbilia nje kuburn ur passport for a better life...na jinsi ya kutoka ni huku ,,,mtu ana elimu yak na uwezo apewe nafasi...
 
Inasikitisha sana wadau uwanja unaitwa wa kimataifa lakini hakuna maboresho yoyote, kwa mfano upande wa arival international and domestic passengers wanategemea matundu mawili ya choo,mvua zikinyesha ni aibu tupu makopo kila kona ya kukingia maji yanayovuja,cha kushangaza uongozi ni mahodari kupamba maeneo yote ya ndani, kuta zote zimejaa matangazo ya biashara .jamani watanzani lini uzaledo wa kujali chetu utatuingia?
 
Hivi kweli unaamini kinachogombwa hapa ni Tesha na Msangi kutoa tendo kiupendeleo bila kujali aliyepewa ni kabila gani? ... Kosa si la Mhindi. Kosa ni yeye kuwa Mhindi. Kuna tofauti.
Wewe ndio unaona tatizo ni kuwa Mhindi, una project trepidatious fears zako na ultra-sensitivity kwa Wahindi wa Flamingo. Kosa ni upendeleo unao sound in corruption, na mnufaikaji happens to be Mhindi. Unajaribu ku exude moral high ground kwa kujiweka kama mtetezi wa wanaobaguliwa, lakini mrengo wako ni Wahindi.

Kuna siku Wazawa Asilia walibaguliwa hotelini Arusha mpaka wahusika wakaomba msamaha kwa Waziri na kusema watabadilisha policy zao wewe ukaja hapa kutetea wabaguzi na wazungu. Such Judas-like, shameless failure of moral authority.

Pdiddy ameiweka hoja yake wazi katika kichwa cha mada alipotofautisha mtanzania na mhindi. Bado hauoni ubaguzi hapo?
Inawezekana Mhindi wa Flamingo sio Mtanzania, wewe na mimi hatujui anachojua Pdidy.

Kama hauwezi kuona kuwa Tesha analaumiwa si kwa kufanya upendeleo tu bali kwa kumpendelea mhindi basi hamna namna ninaweza kukuonyesha vingine. Kilichobaki nikubali kutofautiana.
Kuna subtext ambayo unai miss. Mtu akisema "Msangi kampendelea Mhindi" ujumbe ni kwamba kuna ufisadi umetokea maana Wahindi wanajulikana kwa utajiri na kwa uharaka wa kotoa rushwa. Hicho kitu unakikataa kwa sababu uko hell-bent kutetea Wahindi wa Flamingo.
Unanishutumu kwa intellectual dishonesty ninapowaingiza wapemba kwenye mada lakini wewe ukiwaingiza wagogo, wamasai ......ruksa!
Wagogo na Wamasai ni mifano ya perennial social-economic underclass Tanzania. Wengi wao ni walinzi, omba omba, wachunga mbuzi. Si hali nzuri maana inaweza kujenga mataba ya fukara wa kudumu. Ni tatizo la linalobidi kuangaliwa.

Posting ya Pdiddy hiyo hapo juu. Nionyeshe wapi kasema huyo Mhindi hana qualification?...Wapi aliposema huyo Pdiddy kuwa wakina Tesha kuwa huyo Mhindi ana qualification kuliko waswahili ?
Pdidy kasema hata Wazawa Asili tunaweza hizo tenda, sio Mhindi wa Flamingo peke yake. Pdidy alijadili qualification, mwanzoni ulisema hakuna aliyezungumzia, nikaku call out for hayo matundu kwenye facts zako. Aliyeoneka kinyemela kwamba ana qualification ni huyo - for descriptive purposes - Mhindi wa Flamingo.

Unajuaje kuwa hakukuwa na wahindi wengine kwenye kuomba hiyo tenda na wao wakaonekana hawana sifa za aliye shinda?
Inawezekana wapo, lakini unaposema "Sifa za aliyeshinda" kwa Tanzania inaweza kuwa ni mwenye bakshishi kubwa zaidi. Tanzania ndivyo ilivyo lakini wewe ni idealist unayeishi kwenye kiota cha Utopia, unajifanya hujui hali halisi. Unajuaje Mhindi wa Flamingo hakuhonga?

... Basi kwa nini walitangaza tenda ya wazi? Si wangesema tu kuwa hii tenda ni kw ajili ya wazawa, wengine wasijisumbue kuomba!
Issue sio uzawa, issue ni upendeleo kwa mfanyabiashara wa Flamingo, who happens to be Mhindi. Tenda ilitangazwa, wazawa asili wakaomba, mchakato ukasimishwa, tenda ikaibuka kwa Mhindi wa Flamingo. Ni sumu ya ufisadi na upendeleo unaoweza kuwa powder keg.

Unakuwa disingenious! Kwa hiyo aliyepewa tenda angekuwa mzigua kichwa cha habari kingesema amepewa mzigua wakanyimwa watanzania! Swali langu la kwanza lilikuwa 'je Mhindi hawezi kuwa mtanzania?'
Unajuaje Mhindi wa Flamingo ni Mtanzania?

Unaogopa nini kuitwa mbaguzi? Maneno yako si yanakushitaki?
Kama kulaani rushwa, zikiwemo zilizokithiri za Wahindi ni ubaguzi basi nihesabiwe kati ya wabaguzi.

...basi mnanitwisha mzigo wa kuwatetea wahindi! Sioni aibu kumtetea Mhindi...
Kama kuwatetea wahindi ni kutwishwa mzigo, basi usiseme huoni aibu kuwatetea. Unajifunga-funga. Huwezi kujenga hoja kwa kiswahili kisichoeleweka eleweka halafu ukadai ni maswala madogo ya "semantics." Hueleweki. Endelea kutetea Wahindi na uovu wao.

... Mantra yangu ni kuwa apimwe na ahukumiwe mtu kw kile alichofanya na si rangi yake.
Ya rangi ni wewe umeyaleta.
Mbona kwenye michezo huko ulaya na marekani wamejazana watu weusi?....
Sio tatizo weusi kujazana iwapo kuna level playing field ya kuingia huko. Kama hakuna, kuna tatizo. Sasa hivi kuna mwamko, kwenye michezo kwa mfano, kuongeza idadi ya makocha na wamiliki weusi kwenye American football. Kumekuwa na wazungu watupu, na imeonekana kuna tatizo. Kama Wahindi wamehodhi biashara kwa baadhi ya sababu za kibadhilifu, ni tatizo. Tulikomeshe.

Nimesema tatizo hapa linaelekea ni uhindi wa huyo...
"Inaelekea" kwako wewe! Sasa usitake kulazimisha kila mtu kwamba tatizo ni uhindi wao. Huwezi kuumiza kichwa na kuleta dissertational arguments ndefu based on "Inaelekea." Unaleta ma assumption yako, na ma trepidation ya kutetea Wahindi wa Flamingo based on "Inaelekea." Flimsy!

... Ndivyo tulivyofundishwa Middle School.
Oh, okay. sikupata hilo funzo, sikusoma middle school. Kumbe na wewe umefika Middle School, nilisikia ikisemwa Fundi Mchundo hakwenda hata shule, hakupenda kukanyaga umande. Sijui lipi ni la kweli sasa. Na ukasema "ashakhum si matusi," ashakhum ni nini?

... Hivi nyie mnaona kweli Mhindi hastahili kutetewa hata kama ameonewa? Halafu mnawalaumu wasipoonyesa mnachokiita uzalendo!
Uzalendo sio kitu unafanya in response to how fellow countrymen treat you. Kama unapenda nchi yako utaipigania hata iweje. Wamarekani Weusi walikanyagwa kupita kundi lolote duniani lakini Marekani ni kwao na wamepigania haki zao huku wakipigania nchi yao vitani, hawana pengine, ndio uzalendo. Wa Flamingo wengi ni wapita njia tu.


Leo hii magazeti ya uingereza ..Yanasema muingereza aachiwa na sio mtu mweusi aachiwa. ..
...Wanaposema mtu mweusi mwenye dreadlock wanafanya hiyo kuelezea ethnicity ya mtu na si utaifa! Hao wakiambiwa polisi alidhani wao sio wamarekani kwa sababu ni watu weusi, naam , watakuwa na haki ya kudai ni ubaguzi.
Hujaelewa. Issue ya Uingereza ina international dimension, ndio maana wanasema "Mwingereza aachiwa...Korea yawaachia Wamarekani." Ingekuwa domestic issue wasingesema Mwingereza aachiwa, maana tunajua tuna dili na Waingereza. Hapa kwetu tunasema Mhindi wa Flamingo in a descriptive context. Hatujasema loloter kuhusu Utaifa wake. Hiyo ndio ilikuwa context ya mfano wa "the fugitive rapist is a black male, wearing drealocks." Description kama hizo zipo na hazichukuliwa kibaguzi.

Wrong context again. Huwezi kuzungumzia upuuzi wa vita vya Iraq kujenga hoja yako. Mfano mzuri ni wakati wa mauaji Rwanda...
Umedai kwamba Wahindi ni wachache sana hivyo hawataweza/watashindwa kwenye kupigana. Nikakwambia, toka lini ushindi wa vita unaendana na idadi ya wapiganaji? Nikakupa mfano wa vita ya US-Iraq wakati Sadaam ana jeshi la nne kwa ukubwa duniani, (Gulf War), ni Wamarekani wangapi walienda kule kuteka Baghdad in a matter of hours/days? Hicho ndicho kilikuwa kituko, kutaka kuwaonyesha Wahindi ni so powerless, innocent and non-threatening. Ukichukua higher moral plane uwe balanced, sio biased.

Machafuko hayo unayoyazungumzia yakitokea itakuwa ni weusi kuwavamia wahindi na kuwachinja na si vinginevyo. Sasa mimi nitahusika vipi? Huyo Dewji atanifuatia Buguruni kwa malapa kunifanya nini?
Atakufuata? Kumbe hakuna Dewji Buguruni kwa Malapa? Kwa nini? Hawafiki huko, nhaa? Wana vi enclave vyao upanga, au? Watu wakianza "kumalizana" Tanzania usiwe na hakika kwamba hutaguswa. Halafu inawezekana wewe Fundi ukawa haupo, Mzee Mchundo jee? Umehamisha familia nzima? Huna jamaa unaowajali? Eti "mtamalizana." Kumbuka watu wako kidogo.

Kwa hiyo wewe msema kweli mwenye kujua facts...
Kwa hiyo mtu akisema Fundi Mchundo umekosea fact fulani unamwita "wewe mwenye kujua facts..."? Usi stoop down to Field-Marshian retorts bana. You aught to be bigger than that kama unataka ku espouse a higher moral ground kwa kutetea unaodhani wanaobaguliwa.

unataka kusema alipandishwa cheo mzungu huko New haven?
Hakuna aliyepandishwa cheo, nimerudia mara mia nne sasa. Ulitoa kahabari kalikopinda. Watu wana uchungu na ufisadi wa huyu Tesha na Msangi na Mhindi wa Flamingo, usidhani utakuja kuwatetea na facts zenye gaps ukadhani utapeteshwa peteshwa hapa. You will be called out.

Mwelekeo wenu unaelekea kuwa tatizo si kuhodhi maduka bali ni Mhindi kuhodhi maduka.
Muelekeo? Unabahatisha? Unaotea-otea tu na kubahatisha tu. "Muelekeo unaelekea..." huwasilishi vitu vikaeleweka, ndio maana labda hatuelewani. "Muelekeo unaelekea..."?

Self-entitled facts ndiyo nini tena?
Your own facts, which you are not entitled to.

Ubishi wa Kuhani ulikuwa tofauti na wa kwako...yeye angalau alikuwa...
Bado sioni uhusika wa huyo hapa mjadalani.

Dilunga unaanza kuni-boa.
Well, wapo watakao ku keep interested and excited, mimi sitaweza kukuhakikishia hilo.

Yadharau tu ninayotundika.

 
BARRICK wamekuja na kuchota madini yetu kwa raha zao na huku watu wa pembeni wankufa na maji ya sumu....sasa utasema kwasabababu ni ya kutoka canada watu waendelee kufa kisa JF wataona kuna URANGI oooooooooooooohh ni give m a break...lets open our eyes...ndio maana bunge la sasa sio lile lakina msekwa .......watu wanaamka.....nasi tuamke jamani....UTAJIRI uko hapahapa tanzania auitaji kukimbilia nje kuburn ur passport for a better life...na jinsi ya kutoka ni huku ,,,mtu ana elimu yak na uwezo apewe nafasi...

Kuna wakati, mercury ilikuwa dili maana wachimbaji wadogo walikuwa wanaitaka kwa udi na uvumba. Sasa unajua madhara ya mercury kwenye mwili? Leo mnataka kudai uchafuzi wa mazingira umeanza na Barrick!

Nchi zote zenye mapenzi na wananchi wake zinaweka vigezo na namna kemikali fulani zitakavyotumika nchini mwake bila kujali nani anahusika. Mzalendo na mgeni wote wanabanwa. Sasa kama sisi wenyewe hatutaki kuzikazia hizo sheria, utamlaumu mwekezaji? Na ukimlaumu mwekezaji, utamlaumu Barrick aliye husika au wacanada wote? Ukizungumzia hayo maafa utaishitaki Barrick au taifa la Canada? Ukiwahukumu waCanada wote kwa vitendo vya Barrick, nitakuita mbaguzi. Kama vile polisi wa Los Angeles akiamua kushika watu weusi wote kwa sababu Crips wamekuwa tatizo, nae ataonekana mbaguzi.

Utajiri wa nchi hii ni wetu sote bila kujali rangi, kabila, jinsia au dini. Ukianza kusema wanaostahili kuufaidi ni watu wa rangi fulani na si wale wengine ndipo unaingiza sumu ya ubaguzi.

Amandla.......
 
Kuna siku Wazawa Asilia walibaguliwa hotelini Arusha mpaka wahusika wakaomba msamaha kwa Waziri na kusema watabadilisha policy zao wewe ukaja hapa kutetea wabaguzi na wazungu. Such Judas-like, shameless failure of moral authority.

Nitaijibu hii peke yake. Nyingine zote kwangu mimi ni porojo. Kama unashuka hata kumuingiza FMeS katika majadiliano kati yangu na yako, basi sina haja ya kuendelea kujadiliana nawe. Hakuna jipya utalosema na mimi hakuna jipya nitakalosema.

Humu ndani neno ubaguzi mnalifanyia mzaha. Mtu anakataliwa kuingia kwenye hoteli kwa sababu amevaa kata mbuga basi nae atadai anabaguliwa kwa sababu ya rangi yake. Na mashabiki mtadandia bila kuhoji.

Nilichokisema mimi, na unisikilize kwa makini, ni kuwa kilichotokea Arusha si ubaguzi wa rangi bali ubaguzi wa kitabaka. Nikasema kuwa kama jamaa angeingia anaendesha Benz, amevaa Armani na watoto wake wananukia nukia ughaibuni angeruhusiwa kuingia bila tatizo. Kama jamaa angekuwa ni mwanasiasa maarufu, mfanya biashara maarufu mwenye rangi nyeusi angeingia bila tatizo.

Mbaguzi wa rangi hajali nafasi yako. Hata kama wewe ni mbunge, mfanya biashara maarufu utapitia mlango wa watwana. Ndivyo inavyokuwa. Cha msingi ni rangi yako na si nafasi yako. Mbaguzi wa rangi asingeweza kuwaweka watu weusi katika nafasi ya uongozi hata kama huyo mweusi ni mjomba Tom. Wabaguzi wenzake wasingekubali kuhudumiwa katika nafasi hiyo na mtu wa rangi nyeusi. Mtu mweusi atabeba masanduku lakini kamwe hatakuwa meneja.

Kinachotokea nyumbani ni ubaguzi wa kitabaka. Wenye nazo, bila kujali rangi yao, hawataki kuchanganyika na wasio nacho. Ndivyo ilivyo.

Sasa hao wenye nazo wenye rangi kama yetu wanapokorofishana na maswahiba zao wenye rangi tofauti nao basi hawakawii kuchezea kadi ya rangi ya ngozi. Kama atakosa kwenye biashara atadai ameonewa kwa sababu ni mtu mweusi. Kama atashikwa anakula basi atadai ni huyo mwenye rangi ya brown au nyeupe ndiye aliyemrubuni. Na nyie, kwa sababu mmevaa miwani ya kibaguzi hamkawii kubeba mundu kwenda kumtetea mweusi mwenzenu!

Mimi ninachosema kila wakati ni kuwa umefika wakati kila mmoja abebeshwe mzigo wa matendo yake bila kujali rangi yake. Kama yuko nasi katika mapambano yetu ya kujitoa katika umasikini, huyo ni mwenzetu bila kujali rangi yake. Kama anashiriki kuturudisha nyuma basi huyo asutwe bila kujali rangi yake.

Kwangu mimi ni tusi kuniambia kuwa sijaendelea ati kwa sababu ya Mhindi, miaka 46 baada ya kushika utamu. Kwa kufanya hivyo ni kuthibitisha kuwa mtu mweusi bila kubebwa hawezi kuwa sawa na hao wengine. Au kwa maneno mengine, mtu mweusi ni pungufu kwa hao wengine kwa hiyo anahitaji juhudi za ziada kubebwa.

Badala ya kurudia wimbo wa kuwa wahindi wote hawana uzalendo inabidi tujiulize lini tumemkubali Mhindi kuwa mwenzetu?

Nilikuwepo

Amandla.....
 
Tatizo ni kwamba wageni wengi wakifika pale wanadhani ndege imepotea ikaenda kutua Mumbai!

Ukienda San Francisco, kuna sehemu inaitwa China Town, utadhani uko Beijing lakini wamarekani hawaoni tatizo. Ukienda Silicon valley wamejazana wahindi na wachina, wamarekani hawaoni hilo ni tatizo. Mji wa Vancouver karibuni utaitwa Hongcouver kutokana na idadi ya wachina waliohamia. Badala ya kuwaona tishio, wacanada wamewakubali na leo wanawatumia kupenya soko la uchina! Wahindi kuwepo kwa wingi kwenye uwanja wa ndega bado sijaona tatizo.

Amandla........
 
Unless iwe sijaelewa mjadala huu una mantiki gani, nadhani kinachozungumziwa hapa ni suala la mtu mmoja tu kumiliki almost kila biashara pale JNIA.Kwa wenye kujua kinachoendelea pale nadhani wanajua kuwa huyu anayeendesha biashara pale ni nani - siyo watu kadhaa wenye asili ya kiasia,bali ni mtu mmoja .Sidhani kama ishu ni kujazana wahindi.

Inaeleweka kuwa maeneo kadhaa duniani kuna vijisehemu viko dominated na watu wa rangi au mataifa mbali mbali hadi kupelekea kubatizwa maeneo kama China Town, Little Italy, n.k .Ukienda Brussels utakuta maeneo kama Matongee ambayo yako dominated na Wakongo, hii inaeleweka. Tanzania pia yako maeneo yako dominated na wahindi na siyo ishu... maeneo ya katikati ya miji mingi ya Tanzania ni makazi ya wahindi na siyo tatizo. Very soon tutajikuta pia tuna china towns zetu kutokana na idadi kubwa ya wachina wanaoenda wakiongezeka kwa kasi na hili siyo tatizo.Wahindi tumekuwa nao miaka nenda rudi.

Tatizo la kuwa na mtu mmoja tu kuendesha kila kitu mahali pamoja nadhani tunaweza kukisia.Huo ndio wasiwasi wangu tu. Kama kuna wenye kuwapiga vita wahindi kwa uhindi wao , basi watakuwa na sababu zao.
 
mtoa hoja kwanini hataji wahusika kwa majina yao bila kuhusisha makabila? halafu anataja Wahindi, Wachaga, na Wapare, kwa kuhusika na ufisadi. kwanini hamtaji kwa kabila lake huyo aliyenyimwa tenda?

mchangiaji ana hoja ya msingi , lakini ameiharibu kwa kutumbukiza hisia zake za kikabila na ubaguzi wa rangi.

sasa naomba kumuuliza je katika kundi la walionyimwa tenda hakuna Wahindi, Wachaga, au Wapare?

arrrrrrrrrrrrghhhhhhhh!!!
 
Tatizo la kuwa na mtu mmoja tu kuendesha kila kitu mahali pamoja nadhani tunaweza kukisia.Huo ndio wasiwasi wangu tu. Kama kuna wenye kuwapiga vita wahindi kwa uhindi wao , basi watakuwa na sababu zao.
__________________


HATA MIMI NIMO HUMO..UNLESS SIJAELEWA KISWAHILI KILICHOANDIKWA......
TANZANIA KAZI IPO...UKIWA NJE UNAAMBIWA UKIFIKA TANZANIA UKIULIZA SWALI WANAKUULIZA SWALI KABLA YA KUJIBU...AAKAJA MMAREKANI AKAULIZA NASIKIA TANZANIA UKIULIZWA SWALI MNAULIZA SWALI AKAJIBIWA WHO TOLD YOU.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom