UDSM Mgomo wa wanafunzi waanza nao

ndugu hebu badilisha kauli yako kwenye hii thread. hapo utawala hajatukanwa m2. wameimba wimbo wataifa 2. baada ya hapo wakaenda nkurumal 2. hajatukanwa m2. acha kuchochea upuuzi. udsm oyeee. kipara piga chini.
 
Hiyo ndio lugha pekee serikali inayoielewa...tuko pamoja sana katika hilo.....Aluta continua...!
 
nanukuu " MIGOMO INAYOENDELEA NCHINI INAONGOZWA NA KUCHOCHEWA NA VIONGOZI WA CHADEMA KUTIMIZA MALENGO YAO KITAIFA" Haya kayasema naibu katibu propaganda wa ccm Tambwe Hiza asubuh ya leo chanel 10

watu waogope kudai haki zao kwa kuhusishwa na CHADEMA?? Huyo Tambwe ndo anaishia
 
Oooh! my God... plz don let any one to close his/her eyez... si kwa UDSM peke yake... vyuo kaza wa kaza vinamatatizo chungu mzima ambayo kwa hiali serikali haiko tayari kuyatekeleza... itakuwa busara zaidi wakigoma ili matatizo hayo yatatuliwe mapema coz bila migomo hakuna utekelezaji....
 
nanukuu " MIGOMO INAYOENDELEA NCHINI INAONGOZWA NA KUCHOCHEWA NA VIONGOZI WA CHADEMA KUTIMIZA MALENGO YAO KITAIFA" Haya kayasema naibu katibu propaganda wa ccm Tambwe Hiza asubuh ya leo chanel 10

Yeyote yule anayedhani kwamba migomo ndani ya nchi yetu inasababishwa na CHADEMA hana uwezo wa kufikiri kwa kina ili kuelewa matatizo haya yanasababishwa na nini. Hakuna yeyote yule wa kulaumiwa kutokana na hali halisi ndani ya nchi yetu bali ni uongozi finyu ndani ya Serikali ambao unadhani kwamba matatizo mbali mbali ndani ya nchi yetu yataondoka yenyewe bila wao kutafuta njia muafaka ama za kuyapunguza kwa kiwango kikubwa ama kuyatatua kabisa.

Na kama huyo mropokaji akiambiwa alete ushahidi wa kuthibitisha kauli yake kwamba CHADEMA inachochea migomo nchini basi ataanza kuzungusha macho kama mshale wa saa.

Kama walidhani wataendelea kutesa kwa zamu baada ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi uliopita basi imekula kwao. Kwa kifupi Watanzania tumechoshwa na uozo mkubwa ndani ya Serikali na pia kuwaogopa mafisadi wanaoendelea kutafuna utajiri wa Tanzania kila kukicha huku Watanzania walio wengi wakiendelea kuishi maisha yenye dhiki kubwa.
 
Back
Top Bottom