Mara: Uongozi Mgodi wa Cata Mining wasema utawalipa Wafanyakazi wake waliogoma kwa kutolipwa mishahara

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Siku chache baada ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu, CATA MINING ulioko Kijiji Katalyo Wilayani Butiama Mkoani Mara kufanya mgomo wakishinikiza kuliwa mshahara wao wa miezi miwili, uongozi wa Mgodi umetoa ufafanuzi.

Mbali na Mishahara wafanyakazi hao wanadai michango yao katika mfuko wa hifadhi ya Jamii NSSF kutowasilishwa na mwajiri wao, licha ya michango hiyo kukatwa kwenye mishahara yao zaidi ya miaka saba sasa.

Wafanyakazi hao zaidi ya 200, wanadai mishahara yao ya miezi miwili, Novemba na Desemba 2023, ambapo toka jana wameanza mgomo wa kutofanya kazi wakishinikiza kulipwa kwa madai hayo.

Ufafanuzi…
Afisa Rasilimali Watu (HR) wa Mgodi wa Cata Mining, Richard Bendera amesema:

“Ni kweli walikuwa wanadai mishahara ya miezi miwili, na waligoma lakini tayari tumemalizana, tumekaa chini tukazungumza na tumekubaliana kuwa tutawalipwa Januari 11, 2024.”

“Mgomo woa haukuwa na athari wala madhara yoyote kwa pande zote, kilichotokea ni changamoto za kawaida kwenye biashara.

“Tulisimama uzalishaji kwa kuwa kulikuwa na vitu vya kurekebisha katika masuala ya kiufundi, pia huu ni msimu wa mvua, zimenyesha sana kipindi hiki, hivyo ikachangia kuka muda mrefu bila kufanya uzalishaji.”

Pia soma - Wafanyakazi mgodi wa CATA Mining Mara, waanza mgomo kushinikiza kulipwa mishahara, michango NSSF

- Mara: Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu CATA MINING warejesha mgomo, walala ofisini wakisubiri mshahara
 
hatari sana
 
Back
Top Bottom