Udsm kesho kuchafuka zaidi

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
-Ni baada ya kubandika majina mengine ya watu 22 ambao kesho wanatakiwa kwenda kuchukua barua za kurudi nyumbani,ukiachia mbali wale 12 waliopewa barua lastly week na hali kesi zao mahakamani hazijafutwa na hakuna mategemeo ya kufutwa hivyo Jumla yao wote ni 34.
Mbao zote za matangazo usiku huu zimejaa tangazo la kukutana revolution square kesho saa saba mchana kwa ajili ya kutokubaliana na hilo.
 
Yes M' waloanzisha mgomo wanakula bata,wafukuzwe wengine.Japo siyo wote,
 
Oya,wengne tuko kwenye starehe zetu huku,hayo matangazo yamewekwa lini?
 
Pita sasa hivi hapa library kwenye mbao za matangazo, cafeteria na coET.Pembeni majina ya wanaitajiwa kwenda kuchukua barua na ilo tangazo.
 
Tutajua hiyo kesho mkuu' watu wapo emotional sana iyo kitu.
 
Kuweni na msimamo mmoja kuwanusuru wenzenu kukosa chuo

Migomo ya siku hizi ipo kimaslahi zaidi. Kuna makundi. Siasa za chuo zimeharibu msimamo ulikuwepo miaka ya nyuma. Watakaogoma ni kikundi kidogo sana!
Nawashauri msigome, tumieni busara na njia ya negotiations kuwanusuru wenzenu. Naamini DARUSO ina uwezo wa kushughulikia hili suala badala ya kuwaingiza wanafunzi wengine tena matatizoni!
 
daruso wameshindwa kazi toka juzi.
 
Bora mwandamane wote ili mkamatwe wengi washidwe kuwafukuza nguvu yenu ndiyo inaitajika
 
Kaka rejao! Nimependa ushauri wako ni wa kihekima zaidi hasa kama hiyo njia ingewezekana but I think haitafanikiwa kwa sababu UONGOZI WA CHUO WENYEWE NI WA KIDICTATOR.Sisi tulifikiri wangetumia busara pia kusolve hili tatizo lakini wanajua wanachuo bado wanamachungu ya kuwasuspend hao 12 bado wanawaongeza wengine tena WE UNAFIKIRI NINI KITOKEE? na tena ukumbuke kuwa bado kesi hazijaisha mahakamani,kwa hiyo wanazidi kutifua wanafunzi zaidi.
Kibaya zaidi malecture wenyewe design kama wako upande wa wanachuo.Mfano tu wakati 2po kwenye mgomo,baadhi ya watu walikuwa wanaendelea na lecture kwakuibia sasa utakuta lecturer anasema "Nyie mbona mnakuja darasani hali wenzenu wapo mahabusu?" hamwoni mnavunja umoja wenu?, hapo ndo unapoona hata baadhi ya malecturer wanasupport movts kudai haki zetu. Kaka rejao na wenginewo hiyo ndo hali halisi.
 
Habari nilizozipata toka moja ya wadau wa coET kitivo cha Science ni kwamba kuna baadhi ya wenzao wapo kwenye list ya suspended.So kesho nao watakuwa kwenye mgomo wao.
 
Kwa kifupi mgomo wa sa hzi utafana sana kwa sababu hadi wahandisi<coet> nao watatuunga mkono.over
 
Migomo ya siku hizi ipo kimaslahi zaidi. Kuna makundi. Siasa za chuo zimeharibu msimamo ulikuwepo miaka ya nyuma. Watakaogoma ni kikundi kidogo sana!
Nawashauri msigome, tumieni busara na njia ya negotiations kuwanusuru wenzenu. Naamini DARUSO ina uwezo wa kushughulikia hili suala badala ya kuwaingiza wanafunzi wengine tena matatizoni!

Hata uongozi wa chuo nao ni wa kimasilahi, unaonekana kutoa maamuzi kwa kutumia sababu za kiitikadi za chama na hata kuona kuwa hao wanaogoma labda ni wenye itikadi ya chama fulani. Hatuwezi kujenga nchi yetu kwa kuingiza siasa ktk kila taasisi ya umma. Maana hata kama chama kingine kikiingia madarakani bado tunahitaji watalaam na wasomi hawa bila kuangalia itikadi za kichama wala dini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom