Chimbuko na Upotofu wa kanisa la Waadventista Wasabato

KIXI

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
1,624
1,885
Kumekuwa na mijadala mingi na mawazo mengi yenye kukinzana katika Tanzania kuhusiana na mafundisho ya Kanisa la Waadventista Wasabato. Hivyo niliamua kuchunguza misingi ya imani ya Kanisa hili ili kupata picha kamili ya mafundisho yao. Ilikuwa dhahiri kuwa imani ya Waadventista Wasabato ni dini ya uongo yenye mafundisho ya kupotosha mafundisho hayo yanatokana na roho za udanganyifu, ambazo mtume Paulo alisema zitajitokeza katika siku za mwisho. “Basi roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watujitenga na Imani, wakisikiliza roho zindanganyazo, na mafundisho ya mashetani.” (1Tim. 4:1). Mafundisho ya Adventista Wasabato yanawakilisha ‘injili nyingine’, injili ya uongo ambayo Paulo anatuonya vikali kabisa katika Wagalatia 1:3-9 na 2 Wakorintho 11:1-4.

Kwangu mimi, ilikuwa muhimu kujifunza kitu kimoja tu kuhusu mafundisho yao ili kugundua kuwa mafundisho hayo yalikuwa uongo mtupu. Mmoja wapo wa waasisi muhimu wa kanisa la Waadventista Wasabato mnamo miaka ya 1800 alikuwa Ellen G. White. Alifundisha tarehe ya 22 Oktoba 1844 kuwa Yesu Kristo alitoka katika ‘patakatifu’ mbinguni naye akaingia “patakatifu pa patakatifu”. Hili wazo sio tu liko kinyume na Maandiko lakini pia halina mantiki. Ni nani anaweza kuamini katika upuuzi huu ambao haujaandikwa mahala popote katika Maandiko? Jibu la hili swali ni kwamba, hili ni kazi ya roho idanganyayo ifanyayo kazi kwa nguvu kwa wanaume na wanawake walio vipofu wa ukweli na uelewa wa Injili ya Yesu Kristo.

Neno la Mungu linatufundisha kwamba baada ya kufufuka kwake, Yesu Kristo aliingia Patakatifu pa Patakatifu (mbinguni) kwa damu yake (Waebrania 9:7,8-12; 10:19). Patakatifu pa Patakatifu ni ishara ya uwepo na utukufu wa Mungu pale anapoketi na kutawala; zaidi ya haya, Maandiko yanatufundisha kwamba watu wa Mungu waliokombolewa, wao wenyewe wana ujasiri wa Kuingia Patakatifu Pa Patakatifu kwa sababu ya damu na kafara ya Yesu Kristo (Waebrania 4:16; 6:19,20; 10:19-23). Kitabu cha Waebrania kinatudhihirisha kuwa ile Hema jangwani inawakilisha vitu vya kiroho vilivyopo mbinguni, na kwamba sasa Wakristo wanao uwezo wa kuingia uwepo kwenye Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu (Waefeso 2:18).

Kwa nini mtu anaweza kuachana na akili na kuamini kitu ambacho kinapinga dhahiri mafundisho ya Biblia? Jibu ni kama ifuatavyo: kulikuwa na watu katika miaka ya 1800 ambao walikuwa wanaamini kuwa Yesu atarudi duniani tarehe 22 Oktoba 1844. Hii ilitokana na tafsiri yao ya Danieli 8:14 na zile siku 2300 zilizotajwa humo. Mmoja ya waanzilishi wa kwanza wa mafundisho haya ni mwanaume aitwaye William Miller na wafuasi wake waliitwa “Millerites” (Wafuasi wa Miller) au ‘Waadventista’. Tayari hapa tunaona udanganyifu uliokuwa ukifanya kazi katika mioyo ya hawa watu kwa kufikiria kwanza wangeweza kuikokotoa siku ya kurudi kwake Bwana, wakati Bwana mwenye ameisha tuonya kabisa kuhusu mambo haya ( Mathayo 24:23-27,44; 25:13). Ni kweli kwamba Bwana hakurudi siku hiyo na kulikuwa na kukatishwa tama sana miongoni mwa ‘Waadventista’ – kwa ujumla waliitwa ‘Adventists’ kwa sababu walitazimia ‘Kuja’ (yaani, ‘Advent’) kwake Yesu kutatokea wakati ule. Badala ya kutubu wengine walizidi kujidanganya ili kuhararisha tafsiri zao za Danieli sura ya 8.

Hiram Edson alikuwa miongoni wa wale waliovunjwa moyo, lakini alisema siku iliofuata, alipokuwa akikatisha katika shamba fulani alipumzika ili kusali na ilikuwa kama mbingu zilifunguka mbele yake. Ansema kwamba “Iliwekwa dhahiri kwake” kwamba sio kuwa ilimbidi Yesu kurudi duniani Oktoba 22, 1884, lakini siku hiyo Kristo alitoka patakatifu mbinguni na kuingia patakatifu pa patakatifu ili kufanya kazi iliyo takatifu zaidi (F.D Nichol, The Midnight Cry p.458).

Edson bila kuchelewa alishirikisha tafsiri hii wafuasi wengine ambao wote waliiona kama habari njema! Hawa watu walikuwa wamepagawa sana na tafsiri yao kuhusu Daniel 8:14 kaisi cha kwamba ilikuwa rahisi kudanganywa na shetani kupitia ndoto mbalimbali na maono waliyokuwa wakipata. Walijaribu kutumia kitabu cha Waebrania sura za 8 na 9 ili kuhalalisha mawazo yao ya kuwa Yesu alihama kutoka patakatifu na kuingia patakatifu pa patakatifu tarehe hiyo ya 22 Oktoba 1884!

Edson alianza kujifunza Biblia pamoja na waamini wengineo wawili, O.R.L Crosier na Franklin B. Han, ambao walichapisha matokeo yao kwenye makala yao iitwayo “Day-Dawn”. Hivyo maono ya Edson ndiyo yakawa msingi wa “Mafundisho ya Patakatifu” (ambayo nitayaongelea hivi punde), na watu walioamini mafundisho haya ndiyo walikuwa kundi ambalo liliinuka kutoka kwenye makundi mengine ya Waadventista na kuwa kanisa la Waadventista Wasabato. Ufunuo huu wa uongo ulikuwa wenye kuhamasisha sana kwa Waadventista. Ellen White aliandika baadaye, “Maandiko ambayo kuliko chochote kile ndiyo yalikuwa msingi na nguzo kuu ya Imani ya Waadventista, yalitoa tamko kuwa ‘Itachukuwa siku 2,300 ndipo mahali patakatifu patawekwa wakfu tena.’ ’’ (Danieli 8:14).

Ellen White na Waadventista waliamini kuwa zile siku 2,300 zilizotajwa na Daniel ziliisha Oktoba 22, 1884, na kuanzia hapo Kristo alianza awamu mpya ya huduma yake! Na Ellen White aliita hii “msingi na nguzo kuu ya Imani ya Waadventista”! Na hii bado ni msingi wa Imani za dini ya Waadventista Wasabato hadi leo. (Sitajishughulisha na mambo ya majina ambayo makundi mbalimabli ya Waadventista wasabato waliyatumia kutofautiana na wengine mwanzoni mwa historia yao. Muhimu kwetu kwa ajili ya somo hili ni mwanzo wa msingi wa imani ya Waadventista Wasabato.)

Ellen White aliandika kitabu cha maono yake. Baadhi ya maono yake inawakilisha makufuru kwa kupotosha na kuchanganya kabisa maono na mifano ya Biblia (Early Writings p 54,55). Hiki kitabu kilikuwa ni kazi ya udanganyifu. Anadai kwamba alipata maono ya mbinguni na aliongea na malaika na Kristo. Haya maono na ufunuo ilibidi kuhalalisha mafundisho yao ya uongo kuhusu Yesu kuinga katika patakatifu pa patakatifu Oktoba 1844. Hii ilibidi itokee Oktoba 22, 1844! Anadai alipata maono mengi kama haya, ambayo kiukweli sio ongezeko la maandiko tu ila pia ni kuharibu thamani ya maandiko. Waadventista wanadai kuwa mafunuo haya ya Ellen White ni ‘yenye mamlaka’ kwa Waadventista Wasabato. Tunajua kuwa kitabu cha Ufunuo kinaongelea kuhusu watu watakaokiongezea! (Ufunuo 22:18).

Waadventista wanaweza wakasema kuwa Ellen White haongezei kwenye kitabu cha Ufunuo, lakini kwa sababu ya mambo mengi mapya na yenye kupotosha kwenye ‘maono yake’, na kwa sababu wafuasi wake wana amini kazi zake ni zenye ‘mamlaka’, hiki ndicho anachofanya. Kuhusu kazi zake Ellen White anasema, “Shuhuda hizi ni za Roho wa Mungu au shetani” (Testimonies for the Church, Vol. 4, p.230). Ni dhahiri kuwa shuhuda zake sio za Roho wa Mungu.

Kama nilivyosema, kama hii ndio mwanzo na chanzo cha mafundisho ya Waadventista, inatosha kwa mimi kutambua kuwa mafundisho haya yanatokana na uongo mtupu. Hata hivyo, sio ajabu kwamba kadiri tunavyoendelea kuyaangalia mafundisho yao tunaendela kukutana na udanganyifu na makosa mengine. Wakiendelea kushikilia tafsiri yao ya Danieli 8:14, Waadventista wanafundisha kuwa Yesu aliingia mahali patakatifu pa patakatifu Oktoba 22 1844 ili ‘kupasafisha mahali patakatifu’. Hivyo wanaamini Yesu amekuwa akipasafisha mahali patakatifu pa patakatifu kuanzia 1844 hadi leo! Hii iko wapi katika Bibla? Haipo. Inatokana ‘maono’ ya Edison Hiram na Ellen White tu! Basi!

Walitaka kutoa umuhimu wa tarehe walioichagua kama tafsiri ya Danieli 8:14. Lakini huu mstari unaongelea kuhusu kusafishwa kwa mahali ‘patakatifu’, na siku 2,300. Kwanza, kama tulivyoona, mwanzoni walidhani ‘kusafishwa kwa mahali patakatifu’ ni kurudi kwake Yesu duniani, lakini hii haikutokea, hivyo Waadventista walitunga tafsiri mpya kuhusu ‘kusafishwa kwa mahali patakatifu’ ambayo mstari wa 14 unaongelea. Hivyo walitunga kitu ambacho hakijafundishwa kwenye Maandiko, ambayo wanaiita “Hukumu ya Uchunguzi”. Kuhusu Yesu kuingia patakatifu pa patakatifu, Ellen White anaandika,

“Baada ya kupaa, mkombozi wetu akaanza kazi ya ukuhani mkuu… Huduma ya kuhani (katika Agano la Kale) katika mwaka mzima ndani ya sehemu ya kwanza ya patakatifu… inawakilisha kazi ya huduma ambayo Yesu aliianza baada ya kufufuka. Ilikuwa ni kazi ya kuhani wa kila siku kupeleka mbele za Mungu damu ya sadaka ya dhambi… Kwa hivyo Yesu akamsihi Mungu Baba kwa damu yake kwa ajili ya wakosefu na kuleta maombi ya toba ya waumini mbele yake. Hiyo ilikuwa kazi ya huduma katika sehemu ya kwanza ya patakatifu mbinguni”.

“Kwa karne kumi na nane, kazi hii ya ukuhani imendelea katika sehemu ya kwanza ya patakatifu. Damu ya Kristo inaombea kwa niaba ya waamini wajutao, ilileta msamaha na kukubaliwa na Baba ingawa bado dhambi zao zimebaki katika vitabu vya kumbukumbu. Kama ilivyokuwa kwa kila ibada, kulikuwa na kazi ya upatanisho katika kila mwisho wa mwaka. Kwa hiyo kabla ya kazi ya Yesu kwa ajili ya ukombozi wa wanadamu kukamilika kuna kazi ya upatanisho kwa ajili ya kuondoa dhambi patakatifu. Hii ni huduma iliyoanza siku 2,300 zilipoisha, yaani 1844. Katika muda huo kama ilivyotabiriwa na Nabii Danieli, Kuhani wetu mkuu aliingia patakatifu (pa takatifu) kufanya sehemu ya mwisho ya kazi yake ya pekee ili kutakasa madhabahu”

“Kama zamani za kale dhambi za watu kuipitia imani yao juu ya sadaka za dhambi zilizohamishiwa patakatifu pa duniani, hivyo katika Agano Jipya dhambi za waungamaji kupitia imani yao katika Kristo zinahamishiwa patakatifu pa mbinguni. Utakaso wa kidunia ulikamilishwa kwa ondoleo la dhambi zilizoichafua, hivyo utakaso halisi wa mbinguni unakamilishwa kwa ondoleo, kufutwa au kufichwa kwa dhambi zilizoandikwa pale. Lakini kabla ya hili kutimia, lazima kuwa na tathmini ya vitabu kujua nani, kupitia kutubu dhambi na imani kwa Kristo anastahili kupata faida ya upatanisho. Utakaso wa patakatifu unahusisha kuchunguza kazi ya hukumu. Na hii ni lazima ifanyike kabla ya Kristo kuja na kuwakomboa watu wake.” (Great Controversy p.421, 422).

Hii ni dhana ya udanganyifu ambayo Waadventista wanatembea. Kung’ang’ania kwao tafsiri ya Danieli 8:14, kunapotosha si maandiko tu bali pia hueleza mambo ambayo Biblia haijafundisha na pia hupingana na kazi ya ukombozi ya Kristo. Ellen White na Waadventista wanafundisha kuwa baada ya kupaa kwa Yesu Kristo, alikaa miaka 1800 katika kile kinachohusiana na sehemu ya kwanza ya hema huko mbinguni, akiingilia kati kwa niaba ya waaminio kuwatetea kupitia damu yake mbele ya Baba yake! Baada ya hii miaka 1800 anamaliza huduma yake na kuanza kazi ya ‘hukumu ya uchunguzi’ katika patakatifu pa patakatifu ili kusafisha mahali patakatifu! Wazo hili ni la kwao wenyewe. Ni jambo la kushangaza jinsi watu wanavyoweza kujidanganya!

Haikuishia hapo. Ellen White anasema kwamba ingawa maombezi ya Kristo yalitoa msamaha wa waaminii waliotubu, lakini dhambi zao zinabaki zimeandikwa katika kitabu cha kumbukumbu kilichopo patakatifu pa patakatifu! Hivyo anasema kabla kazi ya ondoleo la dhambi kuisha lazima kumbukumbu hizi ziondolewe! Waadventista wanafundisha kwamba mnamo 1844 Kristo akaingia patakatifu pa patakatifu ambako kumbukumbu zipo. Kumbukumbu hizi zimeandikwa dhambi na kila matendo ya mwamini, na kwamba Kristo ataanza kuchunguza vitabu hivi na kujua nani anafaa ondoleo la dhambi. Ellen White anaandika kwamba dhambi za waungamaji zimewekwa kwa Yesu na kupitia imani zimehamishiwa patakatifu pa patakatifu! Je dhambi hizi zinapelekwaje?

Maana hizi dhambi zimeandikwa katika vitabu vya kumbukumbu huko patakatifu pa patakatifu, na kwa kuwa huko zinachafua au unajisi patakatifu! Je patakatifu panapataje utakaso? Panasafishwa na Yesu kwa kuchunguza maisha ya waamini na kuamua ni nani anastahili kwa sababu ya kutubu kwake kwa kweli na kukua katika neema! Kufutwa kwa dhambi katika vitabu viliyopo patakatifu pa patakatifu kunaitwa “kutakasa patakatifu”. Hii imeanzishwa na Waadventista na wanasema baada ya kazi hii kuisha ndipo Yesu atakapokuja kuchukua walio wake. Mambo hayo yanawakilisha aina ya wazimu! Ni mbali sana sana na ukweli wa Biblia.

Nukuu zifuatazo zinaonyesha wazi kuwa Waadventista wanafikiri kuwa kazi ya upatanisho bado inaendelea, “Damu ya Yesu, wakati ikimuweka huru muungamaji kutoka katika hukumu za kisheria haikuwa ikifuta dhambi … dhambi itasimama patakatifu mpaka upatanisho wa mwisho,” (Patriarch’s and Prophets, p.357)…. “sasa wakati kuhani wetu mkuu anafanya upatanisho kw ajili yetu; yatubidi kuwa wakamilifu katika Kristo,” (The Great Controversy, p.623)… “badala ya kuja duniani katika mwisho wa siku 2300 ndani ya mwaka 1844, ikiisha Kristo aliingia patakatifu pa mbinguni, ikimalizika kazi ya upatanisho ndio maandilizi ya ujio wake.” (The Great Controversy, p.422). Watu wanawezaje kumfuata mwanamke anayesema kwamba baada ya ufufuo Yesu akafanya maombezi kwa ajili yetu, lakini damu yake haikutosha kufuta dhambi, na baada ya kama miaka 1800 ilikuwa lazima kazi ya hukumu yenye uchunguzi ianze ili dhambi ziweze kuondolewa? Hii ni kazi ya udanganyifu kwa wamfuatao!

Hakuna moja kati ya haya linalofundishwa katika Biblia, lakini yote ni katika kupinga au kukinzana na kazi ya Yesu Kristo pale Kalvari. Katika Kalvari mwana wa Mungu alilia kwa sauti kuu, “Yametimia!” Mara baada ya hapo, pazia la hekalu lililotenganisha pataatifu na patakatifu pa patakatifu lilipasuka. Hii ilimaanisha kwamba kupitia damu yake Yesu alifungua njia ya patakatifu pa patakatifu mbinguni, yaani kwenda kwenye uwepo wa Mungu! Waebrania 9:8 inasema, “Njia ya kupaingia patakatifu pa patakatifu mbinguni ( kwa maana ya Kigiriki) ilikuwa haijadhihilishwa bado, hapo hema ya kwanza ilipokuwa ingaliikisimama”.

Kwa hiyo pale ambapo pazia la hekalu liligawanyika mara mbili ilimaanisha kwamba Mungu alihitimisha na kusitisha kazi ya hema, na kwa sababu ya damu ya Yesu tunapata uwezo wa kuingia katika ufalme wa mbinguni, kama mwandishi anavyoelezea katika kitabu cha Waebrania 13:10-22. Kwa sababu ya kifo cha Yesu na ufufuko wake tuna uwezo mkubwa wa kuingia katika patakatifu pa patakatifu kwa damu ya Yesu, kama Waebrania 10:19 inavyoeleza kwa ufasaha. Lakini Wasabato wanataka kusema kuwa Kristo hakuingia patakatifu pa patakatifu hadi hapo mwaka 1844! Hili siyo fundisho la pembeni lao! Ni fundisho la msingi!

Siku ya upatanisho katika Agano la Kale ilitoa msamaha wa dhambi za Israeli kwa kutoa sadaka ya fahali na mbuzi. Kufanya upatanisho kwa watu mara mmoja kwa mwaka, damu ya wanyama hawa ilipelekwa patakatifu pa patakatifu na kuhani mkuu na ilinyunyuziwa kwenye kiti cha rehema (Walawi 16). Waebrania sura ya 9 na 10 inatueleza kwamba ni kuhani mkuu peke yake ndiye aliyeenda patakatifu pa patakatifu mara moja kwa mwaka na damu ya fahali na mbuzi, kwa hiyo Kristo kama kuhani wetu mkuu aliingia patakatifu pa patakatifu kupitia damu yake mwenyewe baada ya ufufuko wake na “na kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele” (Waebrania 9:12). Lengo moja kuu la kitabu cha Waebrania ni kutuonyesha kwamba Yesu Kristo ni kuhani wetu mkuu, ambaye baada ya kuteswa na kufa Kalvari, aliingia patakatifu pa patakatifu mbinguni kwa damu yake kwa msamaha wa dhambi na kwa wokovu wa watu. Ellen White anakinzana na mafundisho ya kitabu cha Waebrania kwa kudai kuwa Yesu hakuingia patakatifu pa patakatifu hadi mwaka 1844!

Zaidi ya hayo mafundisho ya Ellen White yanakinzana na maneno ya Mungu kwa kunena kuwa kazi ya ukombozi haijaisha bado kwa sababu kuna uhitaji wa “takaso la patakatifu”. Neno la Mungu linasema kwamba kwa sadaka moja ya Yesu tumepata uzima wa milele na ya kwamba hao katika Kristo wamekwisha kombolewa kwa damu ya mwana kondoo – 1Petro 1:18. Mwandishi kwa Waebrania anasema, “lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu… maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao watakaotakaswa.” (Waebrania 10:12-14).

Haya na maandiko mengine yanasema waziwazi kwamba ilikuwa sadaka moja ya Kristo iliyofanywa katika tukio moja la kifo chake msalabani ambalo liliimarisha ukombozi wetu na utakaso wa ndani wa roho zetu! Kristo hakusubiri miaka 1800 baada ya kufufuka kwake kabla ya kuingia patakatifu pa patakatifu! Je! Kuhani mkuu katika Agano la Kale alitumia miaka 1800 katika mahali pa hema kabla ya kuingia patakatifu pa patakatifu pamoja na damu ya fahali na mbuzi? Hayo ni jambo la wazimu tu.

Biblia haizungumzii zaidi juu ya kazi au huduma ambayo Kristo inabidi aibebe ili kuimaliza kazi ya ukombozi, utakaso na msamaha! Mafundisho ya Wasabato yanashambulia moyo wa Injili ya Yesu Kristo. Dini ya Wasabato ni adui ya Injili. Aina yoyote ya huduma aliyonayo Kristo kwa sasa inategemea na kumalizika kwa kazi yake ya ukombozi ambayo aliikamilisha kupitia kifo chake na kufufuka! Hata hivyo Ellen White na Waadventista wanataka tuamini ya kwamba kazi ya utakaso wa patakatifu kupitia ‘hukumu ya uchunguzi’ imekuwa ikiendelea toka 1884 na bado inaendelea.

Ellen White anaweka maneno yake mwenyewe kuwa “ni ujio huu (yaani, kuingia patakatifu pa patakatifu) na sio ule wa mara ya pili duniani ambao umetamkwa katika utabiri na utathibitika mwisho wa siku 2300 mnamo 1844. Ikihudhuriwa na malaika wa mbinguni, kuhani wetu mkuu anaingia patatifu pa patakatifu katika uwepo wa Mungu kuingia katika matendo yake ya kazi za wokovu kwa niaba ya mwanadamu – kufanya kazi ya ‘hukumu ya uchunguzi’ na kufanya upatanisho kwa wale ambao wameonyesha kustahili faida zake… wale tu waliokwenda mbele za Mungu kwa toba na ungamo, ambao dhambi zao kupitia damu ya sadaka ya dhambi, zilihamishiwa au zilipelekwa patakatifu na zilikuwa sehemu ya kazi ya siku ya upatanisho. Kwa hiyo katika siku ya upatanisho na hukumu ya uchunguzi, mada zitakazohusishwa ni zile za wale waliofanywa watu wa Mungu.” (The Great Controversy, p.480).

Mafundisho haya pia huhoji uungu wa Yesu Kristo. Je, Kristo ni mwanadamu mpaka atumie miaka mingi kupitia vitabu ili kuona ni nini watu wamefanya? Je, Kristo si Mungu? Je, Kristo si mwana wa Mungu? Je majina ya hao watakatifu hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu kuumbwa kwa ulimwengu? (Ufunuo17:8). Je, hatukuchaguliwa katika Kristo kabla kuwekwa misingi ya ulimwengu kama inavyosema Efeso 1:4? Yesu alijua kwamba Petro atamkana mara tatu! Yesu Kristo aliwaambia makanisa kwenye kitabu cha ufunuo kwamba “Ninajua kazi yenu…” . Ukweli ni kwamba Mwana wa Mungu anatujua (kwa undani zaidi) zaidi ya tunavyofikiri na hahitaji kuchukua miaka 200 au zaidi kutuchunguza maisha yetu! Mafundisho yao ni jambo la uzushi.

Waadventista Wasabato wana jumla ya misingi 28 ya Imani (unaweza kusoma kwenye tovuti yao), na mafundisho hayo hapo juu ni moja ya misingi hiyo 28 ya kuamini kwao! Ellen White ameandika, “Suala la hekalu la Mungu takatifu na hukumu ya uchunguzi yapaswa yajulikane na watu wa Mungu. Wote wanahitaji kuwa na ufahamu juu ya nafasi na kazi ya makuhani wakuu. Vinginevyo itakuwa ni vigumu kuitendea kazi imani ambayo ni ya msingi sana kwa wakati huu au kuichukua nafasi ile ambayo Mungu amekwisha itayarisha kwa ajili yao kuijaza. Wote waliopokea nuru kutokana na masomo haya wanapaswa wabebe ushuhuda wa kweli kuu ambayo Mungu ametenda kwao.” (Great Controversy p.480). Kwa mujibu wa maneno yake mwandishi huyu anasema kwamba sio tu unapaswa kuelewa mafundisho haya ili kutimiza hatima yako katika mpango wa Mungu, lakini pia unapaswa kuwashirikisha na wengine!

Kwa habari ya hukumu maandiko yanasema wazi kwamba sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu (Rum.14:10; 2 WaKor. 5:10), na pia wale wote ambao majina yao hayapo kwenye kitabu cha uzima watateswa kwenye hukumu ya milele. Biblia pia ina maonyo makali sana kwa wale waamini walioigeukia dunia baadaya kumuamini Kristo. Lakini maandiko hayakubaliani kabisa hata kwa mstari mmoja wazo la Waadventista juu ya “Hukumu ya Uchunguzi”. Pia haikubaliani na dhana kwamba Kristo alisubiri miaka 1800 baada ya ufufuo kabla ya kuingia patakatifu pa patakatifu! Tuelezeje machanganyiko na udanganyifu huo? Kuamini mambo hayo ni jambo la kuacha akili ambayo Mungu alitupa, na kuwaruhusu pepo kukuongoza na kukufanya kipofu juu ya mambo yale yaliyo wazi kabisa!

Kutokana na msingi huu wa uongo hii imepelekea makosa na uongo mwingi kuendelea, kwa mfano Ellen White alisema kwamba mwisho wa nyakati dhambi zote zitawekwa juu ya shetani, ameandika:

“Ilionekana kwamba kama vile Kristo alifanyika dhabihu ya sadaka ya dhambi, kuhani mkuu alimuwakilisha Kristo kama kiunganishi na kondoo wa dhabihu kama shetani, mwanzilishi wa dhambi, ambaye juu yake dhambi zote za waliotubu zitawekwa juu yake.” (The Great Controversy p.422). “Dhambi zao zina hamishiwa kwa mwanzilishi wa hizo dhambi.” (Testimonies for the Church Vol. 5, p.475).

Hii ni dhana potofu na inapingana kabisa na maandiko ambayo yanamuelezea mwana wa Mungu kama mwana kondoo wa Mungu aondoaye dhambi za ulimwengu. Isaya anasema, “Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.” (Isaya 53:6). Na mwandishi kwa Waebrania anasema, “lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake.” (Waebrania 9:26). Kristo Yesu aliihukumu dhambi katika mwili (Rumi 8:3). Tena inasema, “Yeye asiyejua dhambi alifanyika kuwa dhambi kwa ajili yetu ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye (2 Wakorintho 5:21). Na Petro anatuambia, “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti…” (1 Petro 2:24). Sura ya 9 na 10 Waebrania inaeleza wazi kwamba Kristo anawakilisha ile dhabihu ambayo ilitolewa kwenye Agano la Kale kufanya upatanisho kwa ajili ya watu na sio shetani. “Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi…” (Waebr.9:28). Wazo kwamba dhambi zetu zitabebeshwa na shetani ni uongo na la kuchanganya, na linaonyesha upungufu wa uelewa wa kile Mungu alichofanya kwetu kupitia Kristo pale Calvary.

Ellen White alichukia dhana ya hukumu ya milele, hakutaka kukubaliana kwamba Mungu atatuma watu kwenye hukumu ya milele. Aliukataa huu ukweli kabisa, katika hili anakubaliana na mafundisho ya Mashahidi wa Yehova. Alifundisha kwamba wasioamini na wenye dhambi wataangamizwa kabisa na kumbukumbu lao litapotea kabisa. Aliandika,

“Haikubaliani kabisa na kila hisia za upendo na huruma au hata za utashi wetu wa haki, dhana kwamba waliokufa katika hali ya dhambi au uovu wapo wanateseka milele kwenye moto jehanamu.” (The Great Controversy,p.535). “Lakini niliona kwamba Mungu hatawaacha wateseke jehanam wala hata wapeleka mbinguni. Bali atawaangamiza na kuwafanya kama vile hawakuwahi kuwapo hapo awali.” (Early Writings p.221).

Bado dhana hii inaendelea kufundishwa kwa upana na bado imejengeka kwenye mabaraza ya kiimani. Ni wapi kwenye kurasa za neno la Mungu mafundisho kama hayo yanapatikana? Anandika haya kana kwamba hajawahi kusoma Biblia! Anajiinua juu ya neno la Mungu na huruma ya Mungu! Maandiko yanaeleza wazi kabisa juu ya hukumu ya milele. Katika sura ya 25 Matayo, Yesu alisema wasio haki wataiendea ile hukumu ya milele lakini wenye haki watapata uzima wa milele (Mathayo 25:46). Katika tafsiri ya Kigiriki ya Agano Jipya, neno ‘milele’ ni sawa na ndilo linalozungumziwa sehemu hizo mbili, yaani ‘adhabu’ na ‘maisha’; kwa maneno mengine, kama adhabu sio ya milele vivyo hivyo na maisha ya milele kwa waamini sio ya milele! Kwenye mstari 41 wa sura hii Yesu anawaambia wasio wa haki au wenye dhambi waondoke kwenda moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya shetani na malaika zake. Kuna maandiko mengi yanauthibitisha ukwelii huu na kuuweka dhahiri – Daniel 12:2; Mathayo 18:8, Marko 9:43,44; 2 Wathess. 1:9; Ufunuo 14:11; 19:3; 20:10; 21:8. Kwa akili ya kibinadamu jambo la hukumu ya milele linaonekana ni jambo kubwa na lisilokuwa la kawaida lakini siku ya hukumu, Hukumu ya Mungu itaonekana ni jambo la haki kabisa na wala hakuta kuwa na mtu wa kumlaumu au kumshitaki Mungu kwa kukosa huruma na rehema. Binadamu katika kujivuna kwao wanatukuza kujiona kwao wenye huruma na rehema kinyume na Mungu.

Waadventista Wasabato na Mashahidi wa Yehova bado wanaamini kwamba malaika mkuu Michael ndiye YESU KRISTO, hata hivyo, Waadventista bado wanaamini Kristo ni mwana wa Mungu na yu na utukufu wa Mungu.

Tukielekezea macho yetu kwenye kiini cha somo letu juu ya “siku ya saba ya Wadventista”, yaani fundisho lao juu ya siku ya sabato. Somo hili zaidi ya vitu vingine linaonyesha Uadventista sio Ukristo, sio kwa asili wala kwa tafsiri ya maandiko. Mwaka 1847 Ellen White alidai kwamba alipata maono juu ya mji mtakatifu huko mbinguni na alipelekwa sehemu takatifu. Alidai kwamba Kristo alifungua pazia na akaingia patakatifu pa patakatifu na akaona kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano. Anasema kwamba aliona amri kumi zimeandikwa kwenye mbao mbili na zilikuwa ziking’aa sana, na moja ilikuwa iking’aa zaidi, na ndio inayozungumzia Sabato, yaani, amri ya nne. (Early Writings of Ellen G. White, p.32,33).

Hebu tukae na tufikiri mambo hayo. Mengi yaliyoamuriwa na Mungu kipindi cha Agano la Kale yalikuwa ni udhihirisho wa Kristo ambaye angekuja baadaye. Ni Yesu Kristo ambaye sasa ni mkate wa uzima aliyekuja ulimwenguni kutoka mbinguni (Yoh.6:32, 33); chaguo la Mungu kwa habari ya kuhani mkuu sio Haruni wala uzao wa kabila la LAWI bali chaguo la Mungu ni YESU KRISTO! Je Ellen White hakuelewa kwamba tunaye Kristo badala ya Manna siku za leo? Je, hakutambua kwamba Kristo amechukua nafasi au Mungu amebadili ukuhani wa kilawi (Waebrania7;11-22)? Unaona vipi Ellen White alivyotukuza mambo ya Agano la Kale na hakujali Mwana wa Mungu Yesu Kristo?

Mungu ameweka Agano Jipya ambapo YESU ndiye nuru; YESU ndiye mkate wa Mbinguni na chaguo la Mungu la milele kama kuhani wetu mkuu! YESU amejawa na utukufu unaong’aa kwa njia ya pekee sana kiasi kwamba sio Mussa (torati) wala Elia (nabii) anaweza kulinganishwa naye kwa njia yoyote! (Mathayo17:4-8; 2 Wakor. 3:10). Ellen White alisema katika patakatifu pa patakatifu amri ya nne iling’aa kuliko zote – kana kwamba Yesu si kitu! Hapa ndipo tunaona udanganyifu wa kiasi kikubwa wa Ellen na Waadventista. Inaonyesha hawaelewi sio tu juu ya Agano Jipya la kweli bali pia juu ya Injili ya kweli, na hawaelewi kazi ya YESU msalabani na yale aliyoyafanya kwa niaba yetu!

Neno la Mungu linatufundisha kwamba Torati ililetwa na Musa lakini neema na kweli imekuja kupitia Kristo Yesu, “Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.” (Warumi 10:4), na kwamba hatuko tena chini ya sheria (Rum.6:14). Je, hii inamaanisha kwamba tudumu katika dhambi? La hasha! Mungu ametuosha kwa damu ya mwanakondoo na ametupa Roho na kuweka sheria yake ndani ya mioyo yetu (Waebrania 8). Sasa tunaishi kwa imani na kwa ‘sheria ya Roho na Uzima ulio katika Kristo Yesu’ sawasawa na Warumi 8:4. Na katika dhana ile ya kwamba Kristo alikuja kuitimiza torati – hii ni juu ya yale ambayo sheria ama Torati haikuweza kutufanya wenye haki. Mungu amefanya hayo kupitia kifo na ufufuo wa Mwanae kwa kuyaweka maisha Yake kwetu ili tuweze kuzaa matunda ya haki kupitia Kristo (Wafilipi 1:11)! Paulo anatumia sura nzima ya tatu ya Wakorintho wa Pili kuzungumzia jinsi Torati inavyoleta hukumu ya kifo, na jinsi utukufu wa Kristo na maisha yake yanavyoizidi torati na sheria ya Musa. Sura ya kwanza ya Waebrania inamdhihirisha Kristo kama ndio nuru ya Mungu na anaonyesha sura ya Mungu halisi! Lakini maono ya Ellen White yanamtazama Kristo kama mtu aliyemsindikiza hekaluni tu, na anatilia mkazo zaidi kwenye mambo ya Agano la Kale la zamani kama “kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka”! Na kwake katika hili ni amri kumi ndizo zilizong’aa sana na amri ya nne ndio iliyong’aa zaidi kuliko zingine zote. Mafundisho ya Wasabato yanatokana na maono hayo ya uongo.

Katika 2 Wakorintho sura ya 3, Paulo anasema Mungu amewafanya mawakili wa Agano Jipya, na sio wa andiko (kwa maneno mengine, sio katika vibao vya mawe, kama anavyosema katika mstari wa tatu) bali kwa Roho wa Mungu aliye hai. Paulo anatufundisha kwamba, “andiko huua, bali Roho huhuisha.” Kwa maneno mengine, wale wanaohubiri na kutilia mkazo katika kutunza amri zilizoandikwa kwenye vibao mawe sio mawakili wa Agano Jipya, sio mawakili wa YESU. Sio hivyo tu bali ni mawakili wa kifo kwa wasikilizaji wao, sio uhai. Kwa maneno mengine, ni huduma ya Roho Mtakatifu tu inayotupa uzima, uzima uliobeba tunda la haki. Wale wanaosisitiza sheria zilizoandikwa kwenye vibao za mawe, wanasisitiza mauti, kwa sababu sheria iliyoandikwa kwenye vibao vya mawe hazina nguvu kutufanya tuwe hai wala kutufanya tuwe wenye haki!

Paulo anaendelea kusema kwamba “huduma ya kifo” iliyoandikwa kwenye jiwe ilikuwa na aina ya utukufu katika ule muda ambao Musa alipewa. Lakini Paulo anaelezea kwamba ‘utukufu wa Roho Mtakatifu” – ambao Paulo sasa anauita “huduma ya haki” – ni mkubwa zaidi kuliko “utukufu wa andiko”, ambao Paulo sasa anauita “huduma ya hukumu”. Anatufundisha kwamba utukufu wa Roho (kwenye Agano Jipya) ni mkubwa kuliko wa utukufu wa amri ulioandikwa kwenye vibao vya mawe, ni kama vile utukufu wa amri ulioandikwa kwenye mawe hauna utukufu sasa (mstari wa 10). Kiuhalisia anatuambia kwamba utukufu wa huduma ya Roho na wa haki ni mkubwa sana kiasi kwamba Mungu ameacha utukufu wa huduma ya maandishi ya kwenye vibao iliyoandikwa kwenye jiwe (mstari wa 11). Waadiventista hawaelewi neno la Mungu katika sura hii, na katika mafundisho yao wanafufua au wanarudisha ‘huduma ya andiko iliyoandikwa kwenye vibao vya mawe’ ambayo inawafanya watu waendelee kubaki katika kifo cha kiroho na hukumu. Wanaitukuza huduma hii kinyume na Agano Jipya la Mungu ambalo linaweka sheria zake ndani ya mioyo yetu kwa Roho wake. Waadventista wanafuata haki, ila katika kutilia mkazo katika sheria ya Musa, wanasababisha kifo na hukumu. Na ni haki ambayo Waadventista wanasema wanaishi kwayo, ambayo kabisa wanakosa na kushindwa kuipata kwa mafundisho yao kuhusu sheria. (Warumi 10:2,3).

Naelezea zaidi kuhusu hili katika makala yangu nyingine (Je, Tukusanyike Siku Gani Kati ya Jumamosi na Jumapili?), ila acha nioneshe hapa kwamba wale wanaohubiri kutunza/kufuata sheria ya Musa wapo kinyume na huduma ya Roho, wala hawajui huduma ya Roho katika maisha yao inayozaa matunda ya haki. Kwa kupitia huduma ya Roho tu ndio tunapata ubatizo katika Roho anayetupa uzima, uzima wa Yesu ndani yetu ambao kwa huo tunaishi maisha ya kitakatifu na kuzaa matunda ya haki. Kwa kutilia mkazo katika kufuata amri kumi, Waadventista wanazuia neema ya Kristo (Wagal. 1:6) na kujaribu utakatifu uliokamilika “katika mwili” badala ya katika imani na katika Roho ya Kristo (Gal 3:2,3). Waadventista hawaelewi nguvu ya Injili kama ilivyotangazwa katika Warumi 8:1-4. Kwa mantiki hii wale wanaofuata mafundisho ya Waadventista wamewekwa nje katika kujua nguvu ya ukombozi wa Kristo katika kuwafanya wenye haki na watakatifu, na katika mantiki hii, Uadventista sio Ukristo; zaidi ya hili, kiuhalisia, unapinga Injili kama Paulo alivyoweka wazi katika barua yake yote kwa Wagalatia.

Katika maono yake, tunaona kwamba Ellen White na Waadventista kwa kupitia upotefu huu wamebadilisha sehemu sahihi ambayo Mungu amempa Kristo Yesu, na badala yake, Sheria, na hasa sheria ya Sabato! Wanataka wawapeleke watu kwenye Agano la Kale na waishi huko! Ni udanganyifu gani huu, hii ni kuinua sheria juu ya Yesu Kristo!

Ellen White alisema kwamba amri ya nne iling’aa juu ya zote na kuzungukwa na duara linalong’aa na ilitengwa kutunza heshima ya jina la Mungu! Anaendelea kusema kwamba kama amri ya nne inaweza kuvunjwa basi amri nyngine zote zinaweza kuvunjwa! (Early Writings of Ellen G. White, p.32,35). Labda hii inaweza kukusaidia kuelewa kwa nini Waadventista wengi wanasema kwamba kama tusipotunza sabato ni sawa na kusema tunaweza kufanya dhambi za kuvunja amri nyingine tisa! Hawaelewi kabisa Agano Jipya wanaposema “kama tunaweza kuvunja sabato ni sawa na kusema tunaweza kuzini!” (Haishangazi Waadventista hawawezi kusikia au kuelewa tunayosema wakati akili zao zimepofushwa na roho hii ya udanganyifu). Akili za Waadventista yamepotoshwa na mafundisho haya, na matokeo kwamba kushika sheria ni sehemu muhimu ya dini yao na ni aina hii ya dini ambayo Paulo alihubiri dhidi yake katika barua yake kwa Wagalatia. Tunaona kuwa mafundisho ya Wasabato juu ya siku ya saba hayatokani na maandiko bali yanatokana moja kwa moja na maono ya Ellen White ambayo yaliipa sheria nafasi ya kwanza badala ya Yesu Kristo. Nao Waadventista walitafsiri maandiko kufuatana na maono yake, na kwa kufanya hivyo wanapotosha maandiko yote!

Waadventista wana orodha ya imani 28 za msingi (unaweza kusoma mwenyewe kwenye tovuti yao ya rasmi). Namba 20 inahusu sabato, na inasema, “amri ya nne ya sheria ya Mungu isiyobadilika inahitaji kushikwa kwa siku hii ya saba ya sabato…. Ni ishara ya ukombozi wetu katika Kristo, ishara ya utakaso wetu, ishara ya utii wetu.” (“The fourth commandment of God’s unchangeable law requires the observance of this seventh-day Sabbath… It is a symbol of our redemption in Christ, a sign of our sanctification, a token of our allegiance.”) Kwa hiyo wanasema kwamba kushika sabato ni ishara ya ukombozi wako na utakaso! Watu hawa wamezua dini mpya lakini hakika sio Ukristo! Sisi tunakombolewa kwa damu ya Yesu Kristo; sisi tunatakaswa dhambi zetu kwa damu yake na kwa Roho wa Mungu. Hili limeshatimizwa kwa ajili yetu na Yesu Kristo, na utakaso wetu umeonyeshwa kwa kupitia maisha yaliyobadilishwa kwa imani katika Kristo na si kwa utunzaji wa sheria ya sabato!

Namba 19 ya sheria ya msingi ya imani ya Waadventista (inayoitwa “Sheria ya Mungu”) inasema, “Kanuni kuu za sheria ya Mungu ni ilivyo katika amri kumi, na imeonyeshwa kwa mfano katika maisha ya Kristo. Maagizo haya ni msingi wa Agano la Mungu na watu wake na kiwango katika hukumu ya Mungu.” (“The great principles of God’s law are embodied in the Ten Commandments and exemplified in the life of Christ… These precepts are the basis of God’s covenant with His people and the standard in God’s judgment.”)

Ni wazi kuwa kwa sentensi hizi Waadventista wamekataa ukweli wa Injili na hawana uelewa wa Agano Jipya. Msingi wa Agano Jipya la Mungu na watu wake ni damu ya mwanae Yesu Kristo – sio amri kumi! (Luka 22:20, Waebrania 9;14-20;12:24; 13:20). Ukamilifu wa Mungu umewekwa katika Yesu Kristo – na sio katika amri 10! (Wakolosai 2:9). Mungu sio maandiko yaliyoandikwa kwenye vibao vya mawe; Yeye ni uzima wenyewe, na kutimiza haki ya sheria tunahitaji maisha yake ndani yetu na kuishi kwa imani ndani yake. Yesu Kristo alisema yeye ni njia ya ukweli na uzima! Kristo anayeishi ndani yetu ni njia ya kutimiza haki – na sio kutunza sheria (warumi 8:2-4). Msingi wa Agano la Mungu na sisi ni kifo na ufufuo wa mwanawe! Kama mafarisayo, ndivyo wasabato hao wanashika kwa makini sheria. Wanaabudu maadhimisho ya mambo ya sheria na kukataa njia ya Mungu katika uzima na haki kwa njia ya imani katika mwana wake Yesu Kristo. Kupitia bidii yao katika sheria wanakosa kabisa haki ya sheria; wanashindwa kutimiza haki kwa mujibu wa sheria hata kama inasemwa katika Warumi 10:2-4. Je, hawajasoma, “hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria.” (Warumi 3:20)? Kiwango katika hukumu ya Mungu siyo amri kumi kama Wasabato wanadai katika udanganyifu wao, bali ni Yesu Kristo mwenyewe,

“Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na Injili yangu, kwa Kristo Yesu.” (Warumi 2:16).

“Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda… Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama Yeye alivyo mtakatifu… Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.” (1 Yoh. 2:6; 3:2,3; 4:17.)

Ingawa mengi zaidi yanaweza kuongelewa kuhusu sheria na imani, nimeandika kikamilifu kuhusu hili katika makala nyingine inayoitwa “Tukusanyike siku gani kati ya jumamosi na jumapili?” Kwa hiyo tafadhali soma makala hiyo ambapo nimeenda katika maandiko mengi ambayo yanahusiana na tofauti kati ya kuishi kwa imani na kuwa chini ya sheria.

Maria alikuwa mama wa Yesu duniani, lakini wale wakatoliki wanaoomba kwake hufanya ibada ya sanamu. Mungu alitoa sheria kupitia Musa, lakini katika Agano Jipya Mungu ametupa Yesu Kristo ili tupate kutimiza haki kwa njia ya “imani ndani yake” – si kwa “kushika sheria ya Musa”. Kwa mafundisho yao Waadventista hufanya ibada ya sanamu na kuinua sheria juu ya Yesu Kristo. Kwa kuitukuza sheria, hasa ya amri ya nne, wamepotoshwa kuhusu maana ya Agano Jipya na wametolewa nje ya wokovu kutoka kwa Mwana wa Mungu.

Ibada hii ya sanamu inajionyesha yenyewe katika udanganyifu zaidi na Ellen White katika habari za siku ya sabato. Yeye hufundisha kwamba utunzaji wa sabato utakuwa upimaji mkubwa wa uaminifu miongoni mwa Waristo – itawatofautisha kati ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia! Alisema wale waumini wanaokutana jumapili huonesha ‘uhaini’ wao kwa Mungu kwa kuiinamia “sheria ya nchi”, na katika nyakati za mwisho wao ndio watakaokuwa na chapa ya Mnyama! ‘Waumini’ wanaotunza sabato wanaonyesha uaminifu kwa mamlaka ya Mungu na wao atawapa “muhuri ya Mungu” uliotajwa katika kitabu cha Ufunuo. Wengine wote (pamoja na wale wanaokiri Kristo) watapokea chapa ya Mnyama! Waadventista mara nyingi huwaita Wakristo wasiotunza sabato na sheria ya Musa “kanisa potofu” , “makanisa yaliyoanguka” au “babeli”. Na wanafanya hivyo pia kwa Wakristo wasiokubaliana nao kwenye vikao kama vile vikundi vya facebook. Hiki ndo ambacho Ellen White aliandika,

“Niliona kwamba sabato ni, na itakuwa, ukuta utakaotenganisha Waisraeli wa kweli wa Mungu (yaani, wale wanaoshika siku ya sabato) na wasioamini (yaani, wote wasioshika siku ya sabato).” Early writings p.32,33.

“Alama au muhuri ya Mungu ni sabato yake, na muhuri au alama ya Mnyama na kupinga sabato.” (The Great Controversy page 691, 1888 edition.)

“Niliona kwamba Mungu ana wana waaminifu miongoni mwa makanisa yalioanguka na kabla mapatilizo hayajaachiwa, wahubiri na watu wataitwa kutoka katika makanisa haya na kwa furaha watapokea ile kweli… Wote walio waaminifu wataondoka katika makanisa yaliyoanguka, na kusimama na masalia.” (Early Writings p.261.)

Hivyo fundisho hili linafikia kiwango cha uongo kamili. Linasema kuwa, si tu kwamba tunatakiwa kutunza sheria ya Musa kwa ujumla wake, lakini iwapo hatutatunza hii sabato ya nje tutakuwa ni sehemu ya haya makanisa yaliyoanguka (au Babeli) na tutakuwa ni sehemu ya wale wanaopokea chapa ya mnyama! Je, hapo unaweza kuona kanisa la Wasabato linavyotuingiza kwenye mtego wa kanisa la vifungo na hofu?

Kanisa la Wasabato lina mfumo wa kuamini ambao sio tu kwamba unawaweka nje ya Injili ya kikiristo, bali hata katika upinzani dhidi ya injili! Katika maana hii kanisa la Sabato ni kama kanisa la Mormons na kanisa la Mashahidi wa Jehova. Joseph Smith, aliyeanzisha kanisa la Mormons alidai kuwa aliona maono na kusema kuwa malaika alimsaidia kutafsiri kwa Kiingereza kitabu cha sahani za dhahabu. Vivyo hivo usabato hutegemea kwa wingi maono na mafundisho ya Ellen White kwa ajili ya kuelewa na tafsiri ya maandiko. Kanisa la Sabato hujitahidi sana kukataa dhana hii, wakisema kuwa Biblia iko juu zaidi katika mafundisho na matendo. Na kwa wazi kabisa husema,

“Hatuamini kuwa maandiko ya Ellen White yanaweza kutumika kama msingi wa mafundisho… Hatuamini kuwa Biblia inaweza tu kueleweka kupitia maandiko ya Ellen White” (“We do not believe that the writings of Ellen White may be used as the basis of doctrine… We do not believe that Scripture can be understood only through the writings of Ellen White.”)

Hii sio kweli; hebu angalia matumizi ya neno “tu” katika sentensi iliyotangulia! Wanachomaanisha ni kuwa tafsiri yao ni inafanana na ya Ellen White na hivyo hawamtegemei yeye (lakini ni tafsiri inayofanana na ya kwake kwa sababu waliathiriwa na yeye!). Hii ni hoja inaendelea katika mzunguko! Tunakaribia ukweli halisi tunapoangalia kauli nyingine wanazotoa kuhusu maandiko ya Ellen White:

“Hatuamini kuwa ubora au kiwango cha uvuvio (inspiration) katika maandiko ya Ellen White ni tofauti na maadiko ya biblia… Tunaamini kuwa Ellen White alivuviwa na Roho Mtakatifu na kuwa maandiko yake, yatokanayo na uvuvio huo, yanahusu na yana mamlaka, na hasa kwa Waadventista Wasabato” (“We do not believe that the quality or degree of inspiration in the writings of Ellen White is different from that of scripture… We believe that Ellen White was inspired by the Holy Spirit and that her writings, the product of that inspiration, are applicable and authoritative, especially to Seventh-day Adventists.” The Adventist Review, December 23, 1982, The Inspiration and Authority of the Ellen G. White Writings, Ten Affirmations and Ten Denials on Ellen White’s Authority).

Hivyo hapa wanaeleza kwa uwazi kabisa kuwa ubora au kiwango cha uvuvio cha Ellen White ni sawa na cha Biblia (hata kama siku hizi wanajaribu kuzikana), na kuwa maandiko yake yanaendana na yana mamlaka. Wasabato wanaamini kuwa maono na mafundisho ya Ellen White nilioorodhesha hapo juu yamevuviwa na Mungu! Hii inaonesha jinsi kanisa zima la Wasababto lilivyodanganyika. Hakuna kanisa la kikristo linaloweza kueleza hivi juu ya mwandishi wao yeyote yule, hata kama wanamwamini au kufuata mafudisho yake kiasi kwa gani.

Tuliwahi kuwa na semina Morogoro na nilikuwa na majadiliano na muumini wa kanisa la sabato. Baada ya kumwonyesha maandiko toka Wagalatia na Wakolosai hatimaye alikubali kuwa ni makosa kuwaeleza watu kuwa wanatakiwa kukusanyika siku ya sabato. Shauku yangu ni kuwa watu wasizuiwe kupata wokovu kamili ambao upo katika Yesu Kristo na ndio sababu nimeandika makala haya. Ni kwa ajili ya watu wale ambao hawana uhakika na wanahitaji wa maelezo ya kimaandiko na ufafanuzi, na kwa hao ambao ijapokuwa ni wasabato, hawajaarithiriwa na kupofushwa na mafundisho ya namna hiyo. Mungu huangalia mioyo yetu na ninafikri inawezekana kwamba mtu akisikia kwa mara ya kwanza kupitia kanisa la sabato habari za Yesu kufa kwa ajili ya dhambi zao na kuamini, Mungu aweza kutenda katika maisha yao. Iwapo moyo wa mtu huyu ni wazi na kweli mbele za Mungu, basi kusoma kwake neno la Biblia kutamwongoza kutoka katika uongo huu wa kanisa la Sabato. Na hivyo, makala hii imeandikwa katika matumaini hayo, kwa sehemu, ili kuwafikia watu kama hao. Lakini kwa wale ambao tayari wameshaathriwa kwa kina sana na mafundisho haya Wasabato na ambao wana bidii sana katika Sheria, upofu na uongo ambao hutenda kazi mioyoni mwao hufanya vigumu kwao kukiri ukweli na kuelewa kile ambacho kiko wazi kabisa katika maandiko ya Biblia. Kama mafarisayo watapinga na kupambana na ukweli wa Injili.

Baadhi ya watu hubishana na Wasabato kana kwamba wasabato ni Wakristo ambao hushika mafundisho yaliyo tofauti na Wakristo wengine. Watu wanaofanya hivyo wanakuwa hawawatendei haki Wasabato! Kushindana na Wasabato kana kwamba ni Wakristo wenzao ni kuwadanganya! Iwapo unataka kuwa rafiki wa kweli na iwapo unataka kuwapenda upendo ule wa Injili, inakubidi kuwaasa kuwa wanafundisha “injili nyingine” (Gal 1:8) na kwamba wanajiweka chini ya laana (Wagal. 3:10), kwamba dini yao ni bure (Gal 4:11), kwa Yesu hana faida yoyote kwao na kuwa wameanguka kutoka kwenye neema (Gal 5:4)! Hii sio kuwahukumu; hii sio kuwakashifu wala sio kuwa katili kwao. Bali huu ni uhalisia ambao pendo letu kwa Bwana Yesu na ukweli wake vinatakiwa kutuongoza katika kutangaza.
 
Na pumziko la kweli na halisi ni Yesu, siyo siku fulani. Mathayo 11:28
 
Mimi ni msabato.Sijasoma andiko lote kwa kuwa nimeona ulijaribu kupotosha baadhi ya mambo.
Hata hivyo bado nami huwa nina maswali mengi kila nikisoma kitabu cha warumi.

Lakini pia,kwa nini tunaapa wakati wa ubatizo na wakati wa ndoa na imeandikwa usiape?

Kwa nini mgawanyo wa kiutawala unafuata mpangilio wa free masons.Division 13,sabato ya 13,n.k?
 
Yesu mwenyewe aliitunza sabato
Na hata mbinguni kutakuwa na pumziko la sabato milele na milele zote .

WAEBRANIA 4:9-12.

[9]Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.

[10]Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake.

[11]Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.

[12]Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
 
Mimi ni msabato.Sijasoma andiko lote kwa kuwa nimeona ulijaribu kupotosha baadhi ya mambo.
Hata hivyo bado nami huwa nina maswali mengi kila nikisoma kitabu cha warumi.

Lakini pia,kwa nini tunaapa wakati wa ubatizo na wakati wa ndoa na imeandikwa usiape?

Kwa nini mgawanyo wa kiutawala unafuata mpangilio wa free masons.Division 13,sabato ya 13,n.k?
KUTOKA 20:7.

[7]Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.

Unapaswa utaje jina la Mungu wako ikiwa una sababu maalum na uko katika usahihi (ukweli) kwa 100%, kinyume na hapo utakuwa umetenda dhambi mana Mungu ni kweli na kamwe huwa hachangamani na uwongo.

Kumbuka Baba wa uwongo ni shetani tangu bustanini Eden.
 
wakristo wengi wanaojidai kuwa ni wakristo .....hawajawa wa KRISTO mpaka leo naye BWANA wa wote wenye mwili yu karibu kurudi mara ya pili🏇🏇🏇
 
Woah.ahsante sana Mtumishi wa Bwana Yesu.Nilikuwa na maswali mengi kichwani hivi karibuni juu ya usabato na kwa hakika nimepata majibu mengi sana.Na sio hivo bali nimepata na chakula muhimu kwa ajilo ya makuzi ya kiroho.Kwa hakika neema tuliyoyano wale tuliomwamini na kumuishi Bwana Yesu kristo ni yapekee sana.Ahsante Roho mtakatifu kwa vile ulivoyafunua haya kupitia Mtumishi huyu.

Neno ni muhimu sana kwa waamini.
 
Kuna mambo ambayo tunafanana dini zote......

Usiue, usizini, usiibe, usiseme uongo na zaidi ya yote mpende jirani yako kama nafsi yako.

Binafsi nikishaweza kushinda haya ya kawaida ambayo tunafanana nitaangaika na patakatifu pa watakatifu na hayo mengine ya ukatoliki na usabato na ulokole na ushahidi wa yehova na uislamu.
 
Mimi ni msabato.Sijasoma andiko lote kwa kuwa nimeona ulijaribu kupotosha baadhi ya mambo.
Hata hivyo bado nami huwa nina maswali mengi kila nikisoma kitabu cha warumi.

Lakini pia,kwa nini tunaapa wakati wa ubatizo na wakati wa ndoa na imeandikwa usiape?

Kwa nini mgawanyo wa kiutawala unafuata mpangilio wa free masons.Division 13,sabato ya 1t
Tupe madini
 
Back
Top Bottom