Udini ukabila na taifa maskini

  • Uamsho na Fujo za Waislam nchi nzima ya Tanzania, Mauaji ya Police nani yupo juu ya Sheria

    Familia yeyote ile ambayo Baba hakai nyumbani ni Lazma kila Mtoto awe na Tabia yake maana hakuna wa kumwambia lipi zuri ama lipi jema

    Taifa kama Tanzania limepoteza Mvuto na Sifa ya Amani kama linavyojulikana Duniani....

    Tunaona Mengi mabaya zaidi ya haya ambayo tayari yalishatokea Endapo Viongozi wa Nch...i hawata amka na kuongea lolote Mapema
    Kama mmeona jana, Rais anarudi nyumbani anakuta fujo mbele ya geti la Ikulu je, nani alijua Dhamira ya Huyu Raia aliyepenya akiwa na nguo za kiislam mfukoni alipo karibia geti la Ikulu ndo akavaa? je, kama ndani ya huo mfuko kulikuwa na grunet la kujitoa mhanga Tukampoteza Rais wetu ingekuwaje?

    Tunajua wazi kuwa Serikali Haina Dini sasa kwanini wanashindwa kukemea huu uovu? Kuna Agenda gani ya Siri hapa?
    ''We need to Oversight''
    See More

    Like ·

    • 371108_100004025974983_445502264_q.jpg

      Write a comment...

  • Recent Posts by Others on OversightSee All:thinking:

Mimi siyo muislam na pia kwa vyovyote vile siungi mkono vurugu zinazoendelea nchini lakini pia Nina-sympathize nao kwa sababu wametengenezwa na mifumo dhaifu iliyopo, kwa mfano:

1. Waislam walitumiwa kisiasa na ccm katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa ilani ya uchaguzi ya ccm kuwa na kipengele kinahosema kwamba kama ccm itachukua dola, basi wataanzisha mchakato wa kupatikana kwa KADHI MKUU na hivyo kujizolea kura lukuki za waislam lakini baadae ccm ikawageuka. sasa ni kwa nini walichotwa na kuchezewa akili zao kama watoto wadogo?

2. ccm iliwatumia BAKWATA ili kutoa tamko la kutoichagua cdm igunga eti wameidhalilisha dini ya kiislam kwa kumvua HIJAB mama kimario aliyekuwa mkuu wa wilaya ya igunga na baadae ikabainika kwa mba kumbe yule mama alikuwa amevaa MTANDIO tu. kwa mujibu wa dini ya kiislam mwanamke akiolewa na mwanaume ambaye siyo muislam basi na yeye anakuwa siyo tena muislam.

3. kuanzia enzi za nyerere hadi sasa, serikali imejipa jukumu la kumweka shehe mkuu inayemtaka ili kulinda maslahi yake badala ya kuwaachia waislam wamchague shehe mkuu wao na hivyo muishia kumwona shehe issa ponda kuwa shehe mkuu wao nje ya mfumo rasmi.

4. serikali imekuwa ikiwatumia baadhi ya waislam kama vile marehemu shehe yahya kisiasa zaidi badala ya kuwaacha watumike kiroho zaidi ili kijenga na kuimarisha dini zao. mfano ni kama vile kumtumia marehemu shehe yahya kumtabiria kifo cha ghafla mtu yeyote atakayechukua fomu ili kunyang'anyana kitumbua na jk; kumtabiria kifo dk slaa wakati wa kapeni za uchaguzi mkuu uliopita; na kumtabiria kifo dk mwakyembe alipokuwa naibu waziri wa miundombinu; nk; nk.

kwa hali ninayoiona sasa ni kama vile waislam wanatuma ujumbe mzito sana wakisema kwamba TUMENYONYWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEDANGANYWA KIASI CHA KUTOSHA NA TUMETUMIWA KIASI CHA KUTOSHA NA SASA TUNATAKA UHURU WETU ILI TUMCHAGUE SHEHE WETU MKUU TUNAYEMTAKA (na sitashangaa shehe ponda akichaguliwa kwa kura zote na hatimaye awe kama ndugu musri alivyoacha siasa kali mara baada ya kuhaguliwa kuwa rais wa misri!) Kumshitaki shehe ponda siyo suluhu na in fact, virungu na mabomu ya macozi siyo muarobaini wa kila tatizo. wa kale walisema kwamba "when the only tool you have is a HAMMER, then you tend to convert every problem into na NAIL" mwisho wa kunukuu.
 
Sababu kubwa ni dini ya shetani ipo kazini.Tatizo sio Mkojo wa dogo.
 
Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya Taasisi ya kidini ya UAMSHO Zanzibar kwa muda mrefu. Jumuiya hii imesajiliwa kama taasisi ya kidini, lakini sasa inaonekana majukumu yake yamebadiliki na inafanya majukumu yanayopaswa kufanywa na chama cha upinzani katika Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Jamhuri ya watu wa Zanzibar baada ya kuaanzishwa kwa "serikali ya Umoja wa kitaifa" kati ya CUF na CCM wananchi walikosa ule uhuru wa kukosoa serikali yao, maana serikali yote inafikiria jambo moja. Zanzibar tangu kuanzishwa siasa za vyama vingi imekuwa katika hekaheka hiyo kwa takriban miaka 20, lakini ghafla wakakosa hiyo nafasi ya kufanya siasa za demokrasia.Dirisha lile la CUF lilokuwa linatumika kuwasilisha mawazo yao limefungwa ghafla na mungu kawapa mlango mpana unaoitwa UAMSHO. Hili ombwe la kukosekana kwa upinzani Zanzibar limezalisha UAMSHO na kuipa nguvu na limekuwa tumaini jipya kwa wazanzibari. Nasema hivi kwa sababu leo hii CUF haiwezi kusema jambo lolote linaloendelea kinyume na maoni ya serikali ya umoja wa Kitaifa. Kwa hiyo, tuilaumu serikali ya Umoja wa kitaifa maana ndiyo wamezalisha kikundi cha UAMSHO na imechukua nafasi ambayo inapaswa kuchukuliwa na Upinzani zanzibar. Zanzibar inapaswa kurudi kwenye utamaduni wake wa upinzani ili taasisi za kidini zifanye kazi zao badala ya kujaza OMBWE la kutokuwepo upinzani.:embarrassed:
Yote haya ni Mradi wa zamani na wa milele wa CUF Zanzibar irudi kama zamani kuwa nchi huru na ikiwezekana yenye Uarabu na Uislamu zaidi ya Uafrika na Umix wa dini. Hili lisingewezekana kama hawapo pamoja na CCM Zanzibar ila ilikuwa hajapatikanwa kiongozi nyuma hadi hapo alipokuja Amani Abeid Karume (mlezi wa kweli wa Uamsho) ambae ana nia na atafanikisha Uhuru wa Zanzibar, ndie aliwaita kina Maalim Seif na kwamba tafauti zao waweke pembeni wawahi kuipata Zanzibar kwanza, (japo karume aliunganisha serikali ili asipatikane wa kumkosoa kwa wizi wa kinyama na vitendo vyake vya kulipwa mabilioni na waleta dawa za kulevya ili waingize dawa visiwani zanzibar mfano nyuma ya airport mwenye yadi za magari yupo bwana Carlos yeye hupeleka pesa kwa magunia kwa Amani anapenda cash tu, pia yupo mhindi yule mfalme wa paje Noushad) amani amesaidiwa sana na kina Mansour Yusuf Himid ndugu yake na tapeli mkubwa, na pia Jaji Mkuu mstaafu Hamid Mahmoud sasa anakula bata Dar ndie alieandika katiba ya kusema ZANZIBAR NI NCHI FULL STOP mwaka 2009. aliongezewa mkataba asistaafu ili amalize hiyo katiba( cha ajabu Tanzania ilikaa kimya wakati sehemu yake inajifanyia katiba inayosema ni nchi tu bila hata kutaja kuwa ni sehemu ya Tanzania.) mkinikera nitazidisha mipasho
 
Sababu kubwa ni dini ya shetani ipo kazini.Tatizo sio Mkojo wa dogo.

hiyo dini unayoiita ya kishetani ni dini ambayo imeagizwa na mungu kuwakubali watume wakubwa walioshapita na watume wadogo wengine kabla ya mtume MUHAMMAD. do you really understand maana ya dini ya kishetani?
 
mkuu kidogo umenena *japo sehem nyingine sikubaliani nawe sana*,

watu wengine wanawalaumu waislam wanashindwa kuangalia chanzo cha tatizo.

Yote haya ni kutokana na kupuuzwa kwa madai ya muda mrefu ya waislam.

Sasa wanapambana na hasira za waislam na wanadhani wanaweza kuzizima kwa mabomu ya machozi kumbe wanajidanganya.
 
jakamoyo na mwanachit, hebu ni juzeni kuhusu madai sahihi ya waislamu ,na hii habari ya bakwata na serikali,pia mnijuze kuhusu nini kinatakiwa na kitafanyaje kazichukulia kama tanzania ni nchi isiyo na dini)
asanteni sana
 
Jana 19/10/2012 tumeshudia unofficial half day kwa siku ya ijumaa, kitu ambao haijawahi kutokea tangia tanganyika iwe.

Ni vizuri hili libeneke la hawa waislaam na polisi/jwtz liendele kwa muda angalau tuwe tunapata mapumziko ya mwisho wa wiki mapema kidogo.

Mnaonaje hili bandugu?
 
hapa ishu ni ile ishu ya yule mchokozi kukojolea msaafu. HAKUNA CHA UDINI WALA HAKUNA CHA JAZBA!!

Ishu ya mkojo ni tarehe 12 octoba, makanisa ya Zanzibar, Ruvuma, Kigoma na Madai ya Mfumo Kristo wa Kufikirika unayaweka wapi? Kutoa jibu rahisi kwa swali gumu ni sawa na kukikimbia kivuli chako!!

Iseme kweli nayo itakuweka huru

Kuna ajenga za siri, napata wasi wasi hata hao wanaleta hizi vurugu wana MoU na mkuu juu ya haya! Kwangu mimi ni ngumu kuelewa hawa jamaa wa uamsho waipe serikali masaa 26 kuwa Sheikh Farid aonekane, halafu in less than 12 hrs awe ameonekana!! Na naingiwa na shaka zaidi kuona haya yanatendeka baada ya Jk kurejea nchini.
 
Sababu kubwa ni dini ya shetani ipo kazini.Tatizo sio Mkojo wa dogo.

simchukii, Simpendi wala simtetei mtu, hapo kwenye red ni tatizo. Tuwe kama great Thinkers, vijembe havitajenga, tutazidi kugombana bure
 
sasa inabidi msiwachague tena sisiem maana kulalama sio suluhu, embu tendeni...angekuwapo slaa sasa mambo yenge kuwa shwari...tunajuta kuchagua nyinyiem
 
Watanzania wengi bado tukiwa hatuelewi ni sababu zipi hasa zilizopelekea kutokea kwa machafuko ambayo hayakupishana muda na siku .wengi bado tuko gizani ni madai gani hasa ya msingi yanayotakiwa yafanyiwe kazi kwa pande zote mbili .tunashauku ya kujua kutoka zanzibar hadi bara .nawakilisha.

Mkuu

Kuujuwa ukweli unahitaji hekima busara na maono

Inahitaji upendo na imani ya kweli kutoka moyoni sio imani ya makanisani au misikitini.

Inahitaji usiwe mnafiki wala mkurupukaji, bali uongozwe na hekima na zaidi utanzania

Tatizo ni kubwa na source zipo wazi. UCHOCHEZI- chuki zimepandikizwa na kukomaa sasa ni wakati wa mavuno

CCM & Kikwete - Uchochezi

Cuf & Uamusho - Uchochezi

Ponda na redio Imani - Uchochezi.

Udhaifu wa Rais - Hana maamuzi, hana vision wala hofu ya mungu (Ufisadi, mfumko wa bei, ukandamizaji wa demokrasia nk)

Mambo ya msingi na faida kwa watanzania kama elimu bora, afya bora, miundombinu bora, katika kuliletea heshima taifa

letu la Tanzania kama watanzania bila kujali itikadi zetu tumeviweka pembeni kabisa.

Mambo ya kipuuzi na yasiyo na tija kwa ustawi wa taifa la watanzania, ndiyo kigezo cha fujo na vurugu zote Tanganyika

mpaka visiwani.

CCM na kikwete - Siasa za maji taka Udini, Ukanda, ukabila nk lengo kuwagawa watanzania ili wabakie ikulu.....

CUF & Uamsho - Hawa wanatumia kila njia salama ama najisi kuhakikisha wanaipata zanziba kama taifa nje ya muungano

Ponda na Redio imani - Kila siku ni udini Nyerere, Udini - Necta, Udin - mgawanyo wa madaraka, Udini - huduma za kijamii MoU.

Unapokuwa na kiongozi anaefurahia kukuwa kwa pengo kati ya walionacho na wasionacho(masikini), asie chukuwa hatua

dhidi ya mafisadi, mfumko wa bei, huduma duni za afya, elimu na miundombinu inajenga chuki na hasira miongoni mwa

watanzania masikini. Chuki na hasira hizi huelekezwa popote palipo na sababu ilimraji jipu hupasuka popote pale.

Haya makundi manne yamejenga tofauti za kimtazamo ndani ya vichwa vya watanzania na kuwafanya kuchukiana bila sababu. Kwa sasa imekuwa kutafutwa sababu ya aina yoyote ile na watu kutoa hasira zao kutokana na UCHOCHEZI na mahubili yahayo makundi manne.

Hata hapa katika kuchangia, kila mtu atakuja na mtazamo wake na hakika mitazamo mingi itaegamia udini na kuacha

ukweli, na kwasababu watanzania hatutaki kuukubali ukweli basi lazima tuingie machafukoni, tukimwaga damu kama ilivyo

kwa wasomali nk labda mungu anaweza kuturudia.

Mungu ibariki TANZANIA.
 
Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya Taasisi ya kidini ya UAMSHO Zanzibar kwa muda mrefu. Jumuiya hii imesajiliwa kama taasisi ya kidini, lakini sasa inaonekana majukumu yake yamebadiliki na inafanya majukumu yanayopaswa kufanywa na chama cha upinzani katika Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Jamhuri ya watu wa Zanzibar baada ya kuaanzishwa kwa "serikali ya Umoja wa kitaifa" kati ya CUF na CCM wananchi walikosa ule uhuru wa kukosoa serikali yao, maana serikali yote inafikiria jambo moja. Zanzibar tangu kuanzishwa siasa za vyama vingi imekuwa katika hekaheka hiyo kwa takriban miaka 20, lakini ghafla wakakosa hiyo nafasi ya kufanya siasa za demokrasia.Dirisha lile la CUF lilokuwa linatumika kuwasilisha mawazo yao limefungwa ghafla na mungu kawapa mlango mpana unaoitwa UAMSHO. Hili ombwe la kukosekana kwa upinzani Zanzibar limezalisha UAMSHO na kuipa nguvu na limekuwa tumaini jipya kwa wazanzibari. Nasema hivi kwa sababu leo hii CUF haiwezi kusema jambo lolote linaloendelea kinyume na maoni ya serikali ya umoja wa Kitaifa. Kwa hiyo, tuilaumu serikali ya Umoja wa kitaifa maana ndiyo wamezalisha kikundi cha UAMSHO na imechukua nafasi ambayo inapaswa kuchukuliwa na Upinzani zanzibar. Zanzibar inapaswa kurudi kwenye utamaduni wake wa upinzani ili taasisi za kidini zifanye kazi zao badala ya kujaza OMBWE la kutokuwepo upinzani.:embarrassed:

mimi sioni tofauti kati yao na chadema
wote wanadai haki zao wanazoziamini kwa nguvu na jazba tofauti ni mbili tu

  1. chadema imesajiliwa na tendwa , uamsho wamesajiliwa kama asasi ya kiraia
  2. chedema wapo tanganyika na wanatetea maslahi ya kanisa na uamsho wapo zenji na wanetetea maslah ya waislam
ngoma drooo
 
Ishu ya mkojo ni tarehe 12 octoba, makanisa ya Zanzibar, Ruvuma, Kigoma na Madai ya Mfumo Kristo wa Kufikirika unayaweka wapi? Kutoa jibu rahisi kwa swali gumu ni sawa na kukikimbia kivuli chako!!

Iseme kweli nayo itakuweka huru

Kuna ajenga za siri, napata wasi wasi hata hao wanaleta hizi vurugu wana MoU na mkuu juu ya haya! Kwangu mimi ni ngumu kuelewa hawa jamaa wa uamsho waipe serikali masaa 26 kuwa Sheikh Farid aonekane, halafu in less than 12 hrs awe ameonekana!! Na naingiwa na shaka zaidi kuona haya yanatendeka baada ya Jk kurejea nchini.

Acha kutumia siasa kwenye haya machafuko kwani YOU WILL MAKE THINGS WORST!!!
 
Wabongo mnajulikana mna asili ya uvivu ndo maana umeleta thread kama hii. Siku moja tu ilitosha kupumzika.
 
Back
Top Bottom