Udini ukabila na taifa maskini

  • Uamsho na Fujo za Waislam nchi nzima ya Tanzania, Mauaji ya Police nani yupo juu ya Sheria

    Familia yeyote ile ambayo Baba hakai nyumbani ni Lazma kila Mtoto awe na Tabia yake maana hakuna wa kumwambia lipi zuri ama lipi jema

    Taifa kama Tanzania limepoteza Mvuto na Sifa ya Amani kama linavyojulikana Duniani....

    Tunaona Mengi mabaya zaidi ya haya ambayo tayari yalishatokea Endapo Viongozi wa Nch...i hawata amka na kuongea lolote Mapema
    Kama mmeona jana, Rais anarudi nyumbani anakuta fujo mbele ya geti la Ikulu je, nani alijua Dhamira ya Huyu Raia aliyepenya akiwa na nguo za kiislam mfukoni alipo karibia geti la Ikulu ndo akavaa? je, kama ndani ya huo mfuko kulikuwa na grunet la kujitoa mhanga Tukampoteza Rais wetu ingekuwaje?

    Tunajua wazi kuwa Serikali Haina Dini sasa kwanini wanashindwa kukemea huu uovu? Kuna Agenda gani ya Siri hapa?
    ''We need to Oversight''
    See More



    Like ·
    • 371108_100004025974983_445502264_q.jpg



      Write a comment...






  • Recent Posts by Others on OversightSee All:thinking:

mimi sioni tofauti kati yao na chadema
wote wanadai haki zao wanazoziamini kwa nguvu na jazba tofauti ni mbili tu

  1. chadema imesajiliwa na tendwa , uamsho wamesajiliwa kama asasi ya kiraia
  2. chedema wapo tanganyika na wanatetea maslahi ya kanisa na uamsho wapo zenji na wanetetea maslah ya waislam
ngoma drooo
 
mimi sioni tofauti kati yao na chadema
wote wanadai haki zao wanazoziamini kwa nguvu na jazba tofauti ni mbili tu

  1. chadema imesajiliwa na tendwa , uamsho wamesajiliwa kama asasi ya kiraia
  2. chedema wapo tanganyika na wanatetea maslahi ya kanisa na uamsho wapo zenji na wanetetea maslah ya waislam
ngoma drooo
Nayaheshimu mawazo yako kwa kuwa huo ni uhuru tuliopewa na mwenyezi mungu ila zikubaliani dhana yako.
 
Ijumaa ifanywe siku ya mapumziko, mimi sioni tatizo. WASERBIA WA BOSNIA wamepata faida gani?
 
Nakubaliana na Point ya 1o na 11 uko sawa mleta Uzi. Pia wapo wanaoendesha Media zenye kutoa "Hate Speech" juu Dini zingine, Viongozi wa nchi walio hai na Wafu. Gazeti fulani lilisifu wale waliotinga Geti la Ikulu bila polisi kuwatambua wakasema hizo mbinu ni za Intelejinsia yao si ajabu kwa mbinu hizo wakatinga Mezani kwa Rais. Hawa ni watu hatari wasije kuvaa Mabomu wakalipua wasioafikiana Nao
 
viongozi wetu ndio wanaoasisi haya mambo
Hii kitu itatukosti.
Ukiacha ya udini, kuna Wanyakyusa pale dar wameanzisha chama chao na wameenda mbali zaidi wamechapisha polo shirts zimeandikwa "Mimi ni Mnyakyusa".

Huku tunakoelekea sasa ni kubaya.
 
CHRISTIAN MISSION FELLOWSHIP
P.O. Box 55024 Dar Es Salaam Tanzania, E-mail:info@cmftz.org, website: www.cmftz.org
Tel: 0715200551, 0755200550 : Tarehe 28/10/2012
MAOMBI YA KUHAMASISHA AMANI NCHINI
Neno la Mungu limetuagiza katika 1Timotheo 2:1-2; kuwa, kabla ya mambo yote nataka DUA, SALA, MAOMBEZI NA SHUKURANI vifanyike kwa watu wote; kwaajili ya Wafalme na wenye mamlaka, tuishi kwa utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Tukiwa Kanisa la Mungu, tumechukua hatua hii ya kuanza kuliombea Taifa kwa kuugua mno ili Amani tuliyopewa na Mungu na kuenziwa na waasisi wa Taifa hili iweze kudumishwa. Ndugu zangu Watanzania sote tufahamu kuwa, msimamo tuliyojiwekea katika Katiba yetu ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, ni kupiga marufuku kila namna ya ubaguzi ukiwemo wa kijinsia, rangi na kidini. Katiba Ya 1977 Ibara 13(5). Kwa upande wa madhehebu ya Dini Tanzania tuna dini kubwa tatu na nyingine ndogondogo; Dini kubwa ni Ukristo, Uislamu na Dini za Kijadi. Wakristo na waislamu tumekuwa tukishirikiana pamoja katika misiba, sherehe mbalimbali, kuoleana, kuishi katika Nyumba moja na kufanya shughuli za Kijamii kwa pamoja bila kubaguana kabla na baada ya miaka hamsini (50) ya uhuru Nchi yetu. Ndugu zangu wakristo na watanzania wezangu kwa ujumla napenda kuwafahamisha kuwa, hakuna nchi yeyote katika bara la Afrika yenye idadi kubwa ya wakristo na waislam wanao ishi kwa amani na upendo kama Tanzania.Ila kwa sasa watu wasioitakia amani Nchi yetu wanataka kupenyeza chuki za kidini ili isiwe nchi ya amani bali vurugu. Hivi karibuni, tumeshuhudia kuwepo kwa vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa kidini kwa baadhi ya vikundi toka makundi ya dini kubwa kudai haki zao ambazo kimsingi wanaona wanastahili kuwa nazo sawa na Dini nyingine. Hali hii imefanya vikundi hivi vitumie vyombo vya habari; Mathalani: Redio, Magazeti na Machapisho mbalimbali kueleza hisia zao kwa Jamii, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa mgawanyiko katika Jamii iliyokuwa imeshikamana. Aidha, mgawanyiko huu unazidi kukua na kusababisha hali ya Chuki kwa mamlaka ya Nchi, na hatimaye Dini moja na nyingine. Baada yakufanya utafiti wa kina kwanini kuwe na Chuki baina ya makundi ya Dini na Serikali tumeona kuwa, makundi haya ya Dini yanaiona serikali inawanyima haki zao na inapendelea Dini moja na hivyo kutumia mfumo wake katika utawala. Hata hivyo, Madai ya kundi hili yanawapelekea kuwafanyia Vurugu waumini wa kundi wanalosadiki kuwa linapendelewa na Serikali, jambo ambalo linawafanya (wanaofanyiwa vurugu) wasitumie uhuru wao wakufanya ibada ambao kimsingi wamepewa Mungu na kuandikwa katika Katiba ya Nchi Yetu. Tukiwa Kanisa la Mungu, hali hii inatupelekea kuona kuwa bado serikali yetu haijawajibika ipasavyo katika kuelekeza sera na shughuli zake kwa lengo la kuhakikisha kuwa sheria za Nchi zinalindwa na kutekelezwa. Kimsingi, haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma vinapaswa kutoathiriwa kabisa na matumizi mabaya ya uhuru wa haki za watu binafsi. Hivyo, Kanisa baada ya Kumlilia Mungu kwa machozi na maombi mengi, tumeamua kuchukua mwelekeo wa uwajibikaji usio wa maneno tu; kwani suala la kutoa matamko ya kulaani limefanywa na Dini na Serikali kwa mkazo mkubwa. Kwa upande wa Serikali, watawala wa Nchi yetu wamekuwa wakilaani na kukemea, ubaguzi wa Dini, rushwa na ufisadi katika Taifa hili bila mafanikio na hata leo tunawaona vijana wanatwangana hadharani kutokana na kushamili kwa rushwa ,hii yote ni kwa sababu hii ni vita ya kiroho na inapaswa kukemewa na viongozi wa dini na watawala wanapaswa kuchukua hatua. Kwa jinsi hii, Kanisa limelitazama jambo hili kiroho zaidi kwa kutambua kuwa chuki na rushwa ni roho kamili inayotoka kwa Shetani; hivyo watu wa kiroho tunalo jukumu la kuziopinga hila za Shetani kwa DUA, SALA NA MAOMBI ili kuleta amani ya kudumu katika Taifa letu, ambalo linasifika kuwa ndiyo kitovu cha amani Afrika na Duniani. Ndugu zangu wakristo na viongozi wa dini; ikumbukwe na izingatiwe kuwa nyumba za ibada ni sehemu ya kumwabudu Mungu, hivyo zitumike kuhubiri dini tuliyo amuriwa na Mungu na sio siasa, na pasiwe mahali pa kuandaa na kuchochea vurugu na chuki miongoni mwetu. Viongozi wa dini wanaaminiwa sana na waumini wao na lolote watakalo waambia waumini, huaminiwa kuwa limetoka kwa Mungu. Aidha tukumbuke kuwa, tunafanya kila kitu vizuri zikiwemo ibada zetu kwasababu ya amani tuliyonayo. Amani isipokuwepo hakuna kitu kinaweza kufanyika katika Nchi; iwe kwa waumini na wasio wauimini, iwe kwa maskini au matajiri. Amani ikishaondoka, matajiri au wenye pesa watakimbia na kuwa wakimbizi wa Nchi zingine, huku masikini wakikosa mahali pa kwenda na kuishia kuuawa na kupoteza maisha. Kawahiyo ni vema kuitunza amani yetu na kuilinda; kamwe tusiichezee amani tuliyonayo katika nchi yetu; hii ni tunu tuliyopewa na Mungu na kuachiwa na waasisi wa Nchi yetu ili tuienzi, hivyo kila mmoja wetu ni mdau wa amani. Mkulima anahitaji amani ili aweze kupata mazao shambani mwake; daktari anahitataji amani ili afanye kazi zake vema Hospitalini, kadhalika mfanya biashara na mwanasiasa wote wanahitahi amani. Nichukue fursa hii kumpongeza Kamanda Suleiman Kova kwa juhudi zake za kuifanya Dar-es-salaam iendelee kuwa bandari ya Amani; Kamanda Kova ameonyesha ushupavu na umadhubuti mkubwa katika kauli zake, kwani mchango wake umeleta heshima iliyotukuka katika vyombo vya dola nchini na kwa watanzania wote. Kanisa la Mungu ambao tumeitwa kwa Jina la BWANA, leo hii tunaomba na kuutafuta Uso wa BWANA tukiwakilisha zaidi ya makabila 120 ya Tanzania kwa Kutumia Lugha Zetu za Makabila kama alama ya Umoja na mshikamano wetu, tukimsihi Mungu aiponye Nchi yetu. Tunaitakia Nchi yetu amani na Utulivu, katika Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Amini.
NDIMI NDUGU YENU KATIKA KRISTO YESU
……………………………………………….
ASKOFU MKUU DKT. MGUL
 
Back
Top Bottom