Udini ukabila na taifa maskini

hawa watu ni wapuuzi sana kuna gaidi lingine nimekaa nalo hapa jiran saizi linasema tutachoma nyumba zote za askali uko zanzibar uku akiita wakiristo makafiri. Yan nimetamani kumtemea mate...ha ha sasa walitaka kwenda ikulu kufanya nn? Ama kweli kikwete anacheza sana na hawa watu watamvua nguo ngoja azubae
 
watu weusi wa jabau sana,

wanauana kwa ajili ya mungu allah na mungu jehovah!

kiukweli utumwa wa kifikra ni hatari sana hasa unapochanganywa na imani (life after death philosofi).hakika wafrika weusi hakuna atayekwepa kwani mila na desturi zetu zote zimekwisha potezwa zamani.
 
HUNIJUI
Sababu ni Kama Ifuatavyo:

1. Quran Kukojolewa - hekima ingetumika kutatua tatizo sio kuchoma makanisa Shekhe mkuu Dar es salaam (Alhad Salum)
2. Shekhe Ponda Kukamatwa. _ Angetumia ushekhe wake vema yasingempata ni matokeo ya uchochezi kwa sauti yake (Imani radio)
3. Shekhe Faridi ajulikani alipo huko Zanzibar.- Nani alaumiwe kila mtu hajui na serikali inajitahidi kumtafuta, mwenye habari asaidie kuipeleka polisi
4. Waislam Kuonewa na Kuteswa kwa sababu ya Mbagala - Walipaswa kutumia hekima, kuchoma nyumba za ibada ni dhambi na kiuchumi ni uharibifu wa mali na kuingilia uhuru wa watu kuabudu (katiba)
5. Akina mama Wa Kiislam Kudhalilishwa wakati wa Kichapo Mbagala. - walishindwa kutambua nafasi yao katika jamii na kujihusisha na uvunjanji wa katiba siku nyingine wasikubali kutumika (haki ya kuabudu - katiba)
6. Msikiti Umepigwa Bomu la Machozi mbagala. Wanaofanya vurugu huko nje ya nyumba za ibada wasipewe hifadhi kwenye misikiti wala makanisa hayo sio maficho ya wavunja sheria
7. Askari wameingia na Viatu Msikitini - ukifanya fujo na kuvunja sheria serikali na askari watakufuata popote hata ukiingia kwa papa benedict au kwa khamenei.
8. Rais amewapa pole Wakristo - siku zote pole hupewa mfiwa na sio mharifu, akawape pole waliochoma makanisa ili nayeye awe sehemu ya wavunja sheria haiwezekani
9. Maaskofu kuwapongeza Polisi Kuwakamata Waislam na kuwaweka ndani -siku zote polisi inapodhibiti uhalifu inahitaji kutiwa moyo kwa kupongezwa na ikiharibu lazima ikosolewe na kulaaniwa.

Wanavuna wanachopanda
 
Hii Katiba yetu pamoja na mapungufu yake mengi lakini bado ninaiheshimu sana mpaka pale tutakapotengeza mpya. Yanayotokea leo ni ukosefu wa umakini wa watawala wetu. Kama wangezingatia Article 19 ya katiba isemayo:

1. Every person has the right to thefreedom of thought or conscience, belief or faith, and choice in matters of religion,including the freedom to change his religion of faith.
2. Without prejudice to the relevant laws of theUnited Republic the profession of religion, worship and propagation of religionshall be free and a private affair of an individual; and the affairs andmanagement of religious bodies shall not be part of the activities of the stateauthority.

Leo hii tusingefika hapa tulipo.


 
SUALA LA VITABU VITAKATIFU

Nafikiri ni makosa kufikiri kwamba kila mtu anaamini kuwa kuna vitabu vitakatifu. Kuna watu wengi wasioamini mambo ya dini. Hao wako huru na hawafungi na dini yoyote. Anayeamini habari ya vitabu vitakatifu ni wale wenye dini.
Mtu asiye na dini anajua kwamba vitabu vyote vimetungwa na watu waliozaliwa na vipaji maalum. Tukiwalazimisha waamini juu ya vitabu vyetu kwamba vimetoka kwa Mungu tunakosea sana; tunapaswa kuwaelimisha kwa upole mpaka wagundue tofauti iliyopo kati ya kitabu kilichotungwa na Mungu na kile kilichotungwa na wanadamu.
Mtu yeyote anayeamini juu ya Dini, anapaswa kuchukuliana na wale wasioamini mambo ya dini, wakiwemo watu ambao akili zao hazijatulia, walevi, n.k, watu ambao kwa kujua au kutokujua wanaweza kuviharibu vitabu vikiwepo vya dini.
Katika mambo ya dini, tumwache Mungu mwenye dini, ajitetee mwenyewe. Makosa madogo madogo kama kuchomeana vitabu n.k, tuyapeleke katika vyombo vya sheria mhusika awajibishwe kulipa kitabu kingine.
Kuchomeana nyumba za ibada na kuuana ni hasara ya taifa nzima. JE, wewe mwenye kuharibu nyumba ya mwenzako utaponea wapi, endapo kuna kulipizana kisasi? Tafakari.
MTU MWEMA HUUTOA UHAI WAKE MWENYEWE KUOKOA UHAI WA MTU MWINGINE; NA MTU MBAYA YUKO RADHI KUMUUA MTU MWINGINE ILI YEYE AISHI. KUUA MTU KWA KUTETEA DINI YAKO NI UBAYA MKUBWA.
 
Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya Taasisi ya kidini ya UAMSHO Zanzibar kwa muda mrefu. Jumuiya hii imesajiliwa kama taasisi ya kidini, lakini sasa inaonekana majukumu yake yamebadiliki na inafanya majukumu yanayopaswa kufanywa na chama cha upinzani katika Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Jamhuri ya watu wa Zanzibar baada ya kuaanzishwa kwa "serikali ya Umoja wa kitaifa" kati ya CUF na CCM wananchi walikosa ule uhuru wa kukosoa serikali yao, maana serikali yote inafikiria jambo moja. Zanzibar tangu kuanzishwa siasa za vyama vingi imekuwa katika hekaheka hiyo kwa takriban miaka 20, lakini ghafla wakakosa hiyo nafasi ya kufanya siasa za demokrasia.Dirisha lile la CUF lilokuwa linatumika kuwasilisha mawazo yao limefungwa ghafla na mungu kawapa mlango mpana unaoitwa UAMSHO. Hili ombwe la kukosekana kwa upinzani Zanzibar limezalisha UAMSHO na kuipa nguvu na limekuwa tumaini jipya kwa wazanzibari. Nasema hivi kwa sababu leo hii CUF haiwezi kusema jambo lolote linaloendelea kinyume na maoni ya serikali ya umoja wa Kitaifa. Kwa hiyo, tuilaumu serikali ya Umoja wa kitaifa maana ndiyo wamezalisha kikundi cha UAMSHO na imechukua nafasi ambayo inapaswa kuchukuliwa na Upinzani zanzibar. Zanzibar inapaswa kurudi kwenye utamaduni wake wa upinzani ili taasisi za kidini zifanye kazi zao badala ya kujaza OMBWE la kutokuwepo upinzani.:embarrassed:
 
Nadhani kuna hoja hapa,ngoja waje wachambuzi wa mambo tupate mwanga zaidi.
 
Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya Taasisi ya kidini ya UAMSHO Zanzibar kwa muda mrefu. Jumuiya hii imesajiliwa kama taasisi ya kidini, lakini sasa inaonekana majukumu yake yamebadiliki na inafanya majukumu yanayopaswa kufanywa na chama cha upinzani katika Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Jamhuri ya watu wa Zanzibar baada ya kuaanzishwa kwa "serikali ya Umoja wa kitaifa" kati ya CUF na CCM wananchi walikosa ule uhuru wa kukosoa serikali yao, maana serikali yote inafikiria jambo moja. Zanzibar tangu kuanzishwa siasa za vyama vingi imekuwa katika hekaheka hiyo kwa takriban miaka 20, lakini ghafla wakakosa hiyo nafasi ya kufanya siasa za demokrasia.Dirisha lile la CUF lilokuwa linatumika kuwasilisha mawazo yao limefungwa ghafla na mungu kawapa mlango mpana unaoitwa UAMSHO. Hili ombwe la kukosekana kwa upinzani Zanzibar limezalisha UAMSHO na kuipa nguvu na limekuwa tumaini jipya kwa wazanzibari. Nasema hivi kwa sababu leo hii CUF haiwezi kusema jambo lolote linaloendelea kinyume na maoni ya serikali ya umoja wa Kitaifa. Kwa hiyo, tuilaumu serikali ya Umoja wa kitaifa maana ndiyo wamezalisha kikundi cha UAMSHO na imechukua nafasi ambayo inapaswa kuchukuliwa na Upinzani zanzibar. Zanzibar inapaswa kurudi kwenye utamaduni wake wa upinzani ili taasisi za kidini zifanye kazi zao badala ya kujaza OMBWE la kutokuwepo upinzani.:embarrassed:

Kwa mbali kuna hoja lakini bado. Uhusiano wa mambo uliyoyasema ni dhana!
 
jaman tumeona jinsi taasisi hii ilvyofanya machafuko katka Nchi yetu haina haja ya mimi kuyasema sote twajua naona serikali wanailea kwa upande wangu wakuu naona hii taasisi ifutwe kabisa npe maoni
 
Sijawai kuona serikali ya mazuzu kama hii ya SMZ nashangaa kuona watu wachahe wakiatarisha aman ya Nchi na kuwafumbia macho....wakitoa vitisho SMZ vcvyo na utendaji ni aibu kwa Serikali ya Nchi SMz imekosa heshma sababu imeshndwa kufanya maamuzi. Uhamsho walianza taratbu kwa kutukana viongozi na wasisi wetu wa Nchi wakafika mbali zaidi kufanya uharbfu wa mali za wananchi na serikali bado SMZ haikuchukua hatua, Uhamsho wakazidi kufanya uharbfu katka Nchi mpaka kufkia kujifanya Sheikh farid katekwa kumbe ni mchezo SMz imekuwa kama jiwe kwan wanashindwa kumata wote na kupeleka Jela?? Au wanawalea kwa kuwa ni ndugu zao?? Jana polisi fulani walikuwa wakiongea na Mzee wa hapa mtaani kwetu wakisema huyu kamishna wa hapa Mussa Ally hafai wafanye Aondolewe sababu anakataza polisi kuwashkisha Adabu Uhamsho wakat wao washauwa mwenzao na hata Risasi hataki warushe hata wakizidiwa na si hayo kamishna huyu amekuwa akifumbia mambo meng ya Uhamsho.....Wananchi wa Zanzibar wanasema hakuna serikali na jeshi la polisi limeshndwa kulinda Raia na Usalama wake, kama limeshindwa basi watoke hawa Viongozi JK na Shein sababu wameshindwa kuongoza Nchi......Nchi gan watu wanajiamulia kufanya Uharibifu jaman.......tena wanawajua na kuwaacha huu si UPOLE NI UJINGA WA SHEIN NA KIKWETE UKICHEZA NA MBWA UTAINGIA NAE MSIKITINI NDO MATOKEO YA KUWALEA UHAMSHO.....MAANA UHAMSHO NDO CUF NA CUF UHAMSHO TOFAUT YA MAJINA SMZ NA SMT FANYENI KAMA CHINA
 
Watanzania wengi bado tukiwa hatuelewi ni sababu zipi hasa zilizopelekea kutokea kwa machafuko ambayo hayakupishana muda na siku .wengi bado tuko gizani ni madai gani hasa ya msingi yanayotakiwa yafanyiwe kazi kwa pande zote mbili .tunashauku ya kujua kutoka zanzibar hadi bara .nawakilisha.
 
hapa ishu ni ile ishu ya yule mchokozi kukojolea msaafu. HAKUNA CHA UDINI WALA HAKUNA CHA JAZBA!!
 
Back
Top Bottom