Udini hapa nautafsiri kuwa ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani ya uongozi ukilinganisha na ngazi nyingine. Katika pita pita yangu na kuchunguza nimegundua kuwa asilimia 65.78 ya uongozi wa Kamati Kuu ya CCM ni watu wa dini moja. Kama udini ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani, tunaweza kusema kusema kuwa Kamati Kuu ya CCM ina udini? Je kuna sababu yoyote ya msingi ya kwanini watu 25 kati ya 38 wawe ni wa dini moja? Je imeshindindikana kwa CCM kutafuta njia ya kuweza kugawa nafasi hizi kwa kuangalia uwiano wa dini?
Nikiwa mtu mwenye maslahi ya pekee kwenye CCM naona jambo hili si zuri na litazua manung'uniko yasiyo ya lazima. Kama kikundi, taasisi, au jumuiya fulani ina watu wenye sifa moja inayolingana, sifa ambayo inawatofautisha na watu wengine hasa ya vitu kama kabila, rangi, au dini basi mahali hapo ni pa kuangaliwa kwa karibu.
Katika siasa, tukitumia "Wangwe's Doctrine" kuwa endapo asilimia 50 ya watu wenye sifa hizo wakakutwa mahali pamoja ni ukabila/ukanda basi ni wazi mahali ambapo pana asilimia 65 ya watu wenye kulingana sifazao kutofautishwa na wengine basi napo patakuwa na tatizo, in this case udini (yaani idadi ya watu wa dini moja mahali pamoja ambayo haina maelezo ya kuridhisha).
Katika haya maelezo yako nimekuelewa kwamba 66% ya wajumbe wa Kamati kuu ya CCM ni waislamu, na huoni kwamba hili ni jambo zuri kwani linaweza kuzua manung'uniko yasiyo ya lazima. Lakini ukweli ni kwamba hao wajumbe 66% ndani ya kamati kuu ya CCM hawajachaguliwa na waislamu misikitini na kuambiwa waende huko kwenye kamati kuu ya CCM, na pia hawajachaguliwa na kiongozi mkuu wa nchi ambaye ni muislamu, bali walipigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM ambao una watu wa dini zote. Na wazee wetu wa zamani wanaingia kwa kutumia kofia zao walizokuwa nazo huko nyuma kwa maana kwamba hata Nyerere angekuwa hai angeingia kwa kofia hiyo hiyo, jamani suala la udini linatoka wapi hapa?.