Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Udini hapa nautafsiri kuwa ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani ya uongozi ukilinganisha na ngazi nyingine. Katika pita pita yangu na kuchunguza nimegundua kuwa asilimia 65.78 ya uongozi wa Kamati Kuu ya CCM ni watu wa dini moja. Kama udini ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani, tunaweza kusema kusema kuwa Kamati Kuu ya CCM ina udini? Je kuna sababu yoyote ya msingi ya kwanini watu 25 kati ya 38 wawe ni wa dini moja? Je imeshindindikana kwa CCM kutafuta njia ya kuweza kugawa nafasi hizi kwa kuangalia uwiano wa dini?

Nikiwa mtu mwenye maslahi ya pekee kwenye CCM naona jambo hili si zuri na litazua manung'uniko yasiyo ya lazima. Kama kikundi, taasisi, au jumuiya fulani ina watu wenye sifa moja inayolingana, sifa ambayo inawatofautisha na watu wengine hasa ya vitu kama kabila, rangi, au dini basi mahali hapo ni pa kuangaliwa kwa karibu.

Katika siasa, tukitumia "Wangwe's Doctrine" kuwa endapo asilimia 50 ya watu wenye sifa hizo wakakutwa mahali pamoja ni ukabila/ukanda basi ni wazi mahali ambapo pana asilimia 65 ya watu wenye kulingana sifazao kutofautishwa na wengine basi napo patakuwa na tatizo, in this case udini (yaani idadi ya watu wa dini moja mahali pamoja ambayo haina maelezo ya kuridhisha).

Katika haya maelezo yako nimekuelewa kwamba 66% ya wajumbe wa Kamati kuu ya CCM ni waislamu, na huoni kwamba hili ni jambo zuri kwani linaweza kuzua manung'uniko yasiyo ya lazima. Lakini ukweli ni kwamba hao wajumbe 66% ndani ya kamati kuu ya CCM hawajachaguliwa na waislamu misikitini na kuambiwa waende huko kwenye kamati kuu ya CCM, na pia hawajachaguliwa na kiongozi mkuu wa nchi ambaye ni muislamu, bali walipigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM ambao una watu wa dini zote. Na wazee wetu wa zamani wanaingia kwa kutumia kofia zao walizokuwa nazo huko nyuma kwa maana kwamba hata Nyerere angekuwa hai angeingia kwa kofia hiyo hiyo, jamani suala la udini linatoka wapi hapa?.
 
Hii ni nafasi nyingine kwa Mwenyekiti wa ccm kuweka usawa kwenye chama kinachoongoza nchi yetu. Suala la kuwa na viongozi wengi wa kamati kuu ya ccm ambao ni kutoka dini moja linaleta picha ambayo haionyeshi usawa wa dini mbili kubwa Tanzania za Ukristo na Uislam.

Huu ni ushauri tu, ni muhimu sana kwa Kikwete kushawishi wanaccm kuwa na katiba ambayo itaweka usawa wa kidini kwenye chama tawala.

Majina haya yanaonyesha kile kinachoendelea CCM:

1. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti - Muslim
2. Ndugu Pius Msekwa - Makamu Mwenyekiti (Bara) -
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar) - Muslim
4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu - Muslim
5. Capt. (mst) George Huruma Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)- Muslim
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe - Muslim
8. Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe - Muslim
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe - Muslim
11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe - Muslim
13. Dr. Salmin Amour - Mjumbe - Muslim
14. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe
15. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Mjumbe
16. Ndugu Amos Gabriel Makala - Mjumbe
17. Ndugu Bernard Kamilius Membe - Mjumbe
18. Ndugu Kidawa Hamid Saleh - Mjumbe - Muslim
19. Ndugu Samwel John Sitta - Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe - Muslim
21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe - Muslim
23. Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe - Muslim
24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe
25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe
26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe - Muslim
27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe - Muslim
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe - Muslim
29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe - Muslim
30. Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe - Muslim
31. Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe - Muslim
32. Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe -
33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe - Muslim
34. Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe - Muslim
35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe - Muslim
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
37. Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe - Muslim
38. Ndugu Yussuf Moh’d Yussuf - Mjumbe - Muslim

Wajumbe hawa wako ambao wanaingia kwa kutumia kofia walizokuwa nazo sasa ama huko nyuma na wako wajumbe ambao wanapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM. Na wajumbe hao wa mkutano mkuu wa CCM kuna wakristo, waislamu, wahindi na wapagani. Hapa udini unaingiaje?
Ulitaka Jakaya afanye nini katika hili?, si yeye anayechagua wajumbe hawa na wala hawachaguliwi misikitini.
Sasa ulitaka Kikwete afanye nini katika hili suala
 
Mimi naona tukiwa kila kitu tunaangalia kwa njia za udini,basi tunaweza tukaanza kuchinjana hapo baadaye.Na kibaya zaidi Mtoa mada ameangalia ktk chama hajaangalia idadi ya mawaziri, ajangalia hali ikoje ktk wizara na sehemu mbalimbali za kazi.

Mada aliyoitoa Mgaya ni mzuri lakini kwa muda mrefu amekuwa anapotosha watu kwa kusema wakristo wako wanane tu, wakati wako 13.Lakini kana kwamba hiyo haitoshi Mgaya alitakiwa aiangalie nini katiba ya Chama cha Mapinduzi inasema.Ni kazi mzuri umeifanya kwa kuja na concrete evidence lakini ukasahau kuwa kuna waatu ambao wantoka Zanzibar wanaingi kwa nyazifa zao katika Kamati kuu.Sasa pamoja na kutoa evidence mzuri lakini bado nadhani ulitakiwa uiangalie katiba ya CCM inasema nini kuhusu wanachama wa Zanzibar na iddi yao. Wasiwasi wangu mkubwa ni kuwa kama tukiwatoa waislamu wa Zanzibar amabao kule Wakristo wako wachache basi huku bara kama watabakia wako wachache.

Hivyo basi Mgaya ,topic yako bado ina lack vitu ambavyo ni muhimu ili kuweza kufanya justification.Mgaya mtu akitofautiana na wewe kwa hoja hailazimishi awe mwana CCM,mwana CUF au CHADEMA mimi nadhani twaweza tofautiana kwa misimamo tofauti kulingana na justification na the way we view societies.

Nawasilisha.
 
Ndugu yangu Mwanakijiji naona hoja yako haina msingi na umejaa ubabaishaji. sidhani kama wale wajumbe walichaguliwa kwa dini zao lakini wacha nikuchambulie kidogo. Kati ya wajumbe 38 wa Kamati Kuu wajumbe 17 wanatoka Zanzibar. Ni mategemeo yetu kuwa kwa asilimia 99% ya wajumbe hao toka Zanzibar watakuwa waislam kwa vile Zanzibar ina waislam 99%. Sasa ukitoa hao 17 tunabakia na 21 ambao wanatoka bara. Sasa wacha tutizame kati ya hao wanaotoka Bara Idadi ya Waislam ni wangapi? ni 6 tu kwa hiyo waliobakia 15 ni wakristo sasa kama utaondoa wajumbe hao wa zanzibar halafu uchukue uwiano wa kidini kwa wajumbe wa bara basi utakuta ni asilimia 71% ni Wakristo Duh unaona palipokaa hapo Mzee Mwanakijiji. Labda cha kufanya uombe wapunguze wajumbe wa Zanzibar maana ndio wote waislam watupu na hapo utazaa tatizo jengine la masuala ya Muungano watalalamika tunamezwa sasa unaona mambo yalivyo magumu hapo. Kimsingi hoja yangu ni kwamba suala la kamati Kuu kuwa na wajumbe wengi waislam linasababishwa na Wajumbe wa zanzibar na si vyenginevyo naomba uwe makini katika kuweka hoja usikurupuke
 
Ukiwa Na Mtazamo Wa Kutumia Ukabila Au Udini Kama Ndo Kigezo Chako Cha Kujadili Au Kupia Wenzako, Basi Ujue Wewe Ndo Mkabila Ua Mdini Namba Moja
 
1) Asilimia Ngapi Ya Wanachama Wa Ccm Ni Wakristu?

2) Asilimia Ngapi Ni Waislamu?

3) Kikwete Ndio Anachagua Wajumbe Wa Ccm?
 
Msilete mambo yenu ya kuuwa issue!
Mlijificha kwenye mijadala ya kimataifa na sasa bado tuko na nyie huku kwani nilishawaambia before!Wewe kama hutaki tukate issue nyeti basi na wewe una maslahi ya kifisadi!
EPA ILIANZIA ccm kwenye utitiri wa waislam...Sasa IDDI SIMBA NI MKRISTO?AMA MCHAGGA?
ccm MSILETE UCHAWI HAPA JF HAUFANYI KAZI!

Sikutaka kukujibu lakini naona pengine itakuwa vyema nikikufahamisha mimi natokea wapi. Sina kawaida ya kujibu rants. Na bahati mbaya mengi unayoandika ni ranting. Bila shaka kuna watu wanafurahia na kukuona kuwa ni shujaa lakini mimi si mmoja wao.

So I will try to be as polite as I can: Get out of my face!

nitajibu hoja zako pale tu ambapo nitaziona (mimi Fundi Mchundo na si mwengineyo) kuwa zina mantik. Otherwise usijisumbue kunitafuta.
 
Mimi nilisits kuchangia hii mada kwa sababu mbili; kwanza ni kichefuchefu ninachokipata kwa yeyote anayeanza kuangalia katika kundi la watanzania kwa mtazamo wa kidini, ukabila au ujimbo na la pili niliona hili ni tatizo la CCM wenyewe kwani ndio waliona haki ya kuona chmama chao kina viongozi wa aina gani. Lakini baada ya kuona kuwa wengi wanachangia nimeona na mimi nitoe mchango wangu - Ndugu Mgaya katika hizo takwimu zako umeangalia vigezo gani na kutaka kukusaidia nataka ujue kuwa pengine wingi huo unaousema umesababisha na wajmbe kutoka Znz amako wakaazi wake wengi ni waislamu na ni vigumu sana kupata wajumbe wengi wa KK ya CCM kutoka Znz wakawa wakristo - la kuangalia ni wajumbe kutoka Bara jee idadi yao wengi ni waislam? pengine hapo unaweza kupata kuungwa mkono kutoka kwa wale wanazingatia udini na ukabila lakini si kwangu mimi. Jengine nikuulize hii analysis yako imekuja kipindi hichi cha Muungwana tu ? mbona hukuileta wakati wa Mkapa ambapo kulikuwa na wakiristo wengi?

Naomba utusaidie na katika Baraza la Mawaziri utwambie kuna wakiristo wangapi na waislamu wangapi? na usiishie hapo tu endele manaibu waziri, Makatibu wakuu hadi madiwani utatusaidia sana.

Ama kuhusu CCM kama unataka idadi iwe sawa au izidi kwa upande wa wakiristo basi kampeni inaendele na usijali katika kipindi cha miaka kumi hadi ishirini kule Znz kutatoka wajumbe wengi tu wakiristokwani kama wanavyodai wenyewe Wazanzibari kuwa kama Marekani alivyoivamia Iraq kwa ajili ya mafuta basi nia ya kuibana Znz kubwa ni kuporomosha uislam na maadili ya watu wa huko na hili lina back-up ya Taasisi nyingi za ndani na nje ya nchi.

Nasubri hizo takwimu za serikalini kwani nafikiri ndio zinatugusa moja kwa moja kuliko hizo za Chama Cha Mafisadi
 
Sikutaka kukujibu lakini naona pengine itakuwa vyema nikikufahamisha mimi natokea wapi. Sina kawaida ya kujibu rants. Na bahati mbaya mengi unayoandika ni ranting. Bila shaka kuna watu wanafurahia na kukuona kuwa ni shujaa lakini mimi si mmoja wao.

So I will try to be as polite as I can: Get out of my face!

nitajibu hoja zako pale tu ambapo nitaziona (mimi Fundi Mchundo na si mwengineyo) kuwa zina mantik. Otherwise usijisumbue kunitafuta.

Mchundo....MASHUJAA WETU WAKO BONGO!

However...Kama kuna wanaoona kuwa mimi ni shujaa...Then I WONT TAKE IT FOR GRANTED!

Therefore...Nataka nikwambie something...Wewe hujui umaarufu na ushujaa wa jf! Ungekuwa makini...Usingeyaita maneno yangu simply RANTINGS! At the same time comparing rantings to me bein a hero in some people's mind! Umechanganya hapo kukubali ushujaa na kudai ni rantings!

Sasa kwa taarifa yako...jf haikuapata umarufu kwa sababu tu ya mijadala ya udini na ukabila! Hapa macho yote ya watanzania yapo hapa...Na wewe kuwa makini na kauli zako! Wanapoyasoma haya...Hawataki siasa...Wanajuwa tuna data za EPA,MEREMETA NK...!

Wewe ukiwaletea siasa za miyeyusho na kusafishana ni sawa na kuvua nguo zote na kubakia uchi huku kila mtu akikukimbia na wewe bado kudhani uko na nguo!

Mafisadi nyeti zote zilizoko hapa ni kama wako uchi! Na wanapokuja kujishafisha ni sawa na mchangiaji mmoja aliposema kuwa hata wakitumia jiki haifai ama hata kujaribu kujichanganya na wenye nguo huku wakiamini kabisa kuwa hawako uchi!

MBUNI KUJIFICHA KICHWA NA WAKATI MWILI WOTE NJE NJE!
 
Tatizo ni Zenji Factor. Nadhani Zenji wanachangia 50% ya members wanaoingia kwenye CC. Hapo sijaweka wale ambao wanaingia huko kwa heshima ama kwa nyadhifa zao (viongozi wakuu wa Chama wa pande zote mbili, marais wastaafu na wazee wa chama kama akina Kawawa).

Ukishaweka hiyo Zenji factor automatically lazima utaishia kwenye conclusion ya Mwanakijiji.

Labda swali la kujiuliza ni kwanini Zenji inapewa nafasi sawa na Bara?

Congratulation, YOU ARE THINKING BIG!!!
 
Ndugu yangu Mwanakijiji naona hoja yako haina msingi na umejaa ubabaishaji. sidhani kama wale wajumbe walichaguliwa kwa dini zao lakini wacha nikuchambulie kidogo. Kati ya wajumbe 38 wa Kamati Kuu wajumbe 17 wanatoka Zanzibar. Ni mategemeo yetu kuwa kwa asilimia 99% ya wajumbe hao toka Zanzibar watakuwa waislam kwa vile Zanzibar ina waislam 99%. Sasa ukitoa hao 17 tunabakia na 21 ambao wanatoka bara. Sasa wacha tutizame kati ya hao wanaotoka Bara Idadi ya Waislam ni wangapi? ni 6 tu kwa hiyo waliobakia 15 ni wakristo sasa kama utaondoa wajumbe hao wa zanzibar halafu uchukue uwiano wa kidini kwa wajumbe wa bara basi utakuta ni asilimia 71% ni Wakristo Duh unaona palipokaa hapo Mzee Mwanakijiji. Labda cha kufanya uombe wapunguze wajumbe wa Zanzibar maana ndio wote waislam watupu na hapo utazaa tatizo jengine la masuala ya Muungano watalalamika tunamezwa sasa unaona mambo yalivyo magumu hapo. Kimsingi hoja yangu ni kwamba suala la kamati Kuu kuwa na wajumbe wengi waislam linasababishwa na Wajumbe wa zanzibar na si vyenginevyo naomba uwe makini katika kuweka hoja usikurupuke

Great Analysis, musipomshitukia Mzee Mwanakijiji atatupeleka pabaya!!! Namshauri kuwa makini sana wakati anabonyeza key board yake pale anapoandika kitu chochote kinachohusiana na imani.

Namkumbusha kwamba Tanzania hatutaweza gawanyika kwa ukabilia... lakini we are equally very vulnerable with UDINIs...
 
Swali la Mwanakijiji kuhusu CCM kujaa udini lina mantiki. Udini na Ukabila ni mambo mawili ambayo yanaendana, na bado yapo katika vichwa vya wananchi na kama yako katika vichwa vya watu, ni dhahiri hata kwenye vichwa vya viongozi yatakuwepo. Kama viongozi wanajua kwamba mawazo ya udini bado yapo miongoni mwa wananchi, kutakuwa na tatizo gani kwa uteuzi kufanywa kwa misingi ya kuweka uwiano wa kidini katika idadi ya wajumbe ili kuondoa hisia na utata unaoweza kujitokeza iwapo uteuzi utafanyika bila kujali hisia za watu?

Nadhani kiongozi makini ambaye anajua kwamba udini bado upo vichwani mwa watu anaowaongoza, atapaswa kujua kwamba hilo ni tatizo kubwa la ubaguzi, atachukua hatua za kuendelea kuwaelimisha wananchi hatari za kuwepo udini. Halikadhalika, atachukua tahadhari kwa kuhakikisha kwamba kuna uwiano wa idadi katika teuzi mbalimbali, ili kujiepusha na manung'uniko yasiyo ya lazima.
 
Nadhani mzee, huko kijijini njaa imezidi, ulikuwa wapi hukuuliza swali hili kwa zaidi ya miaka 10 Mkapa akiwa M/kiti Rais Sumai Mjumbe na W/mkuu magúla katibu.
kama utafanya uchunguzi utaona kwamba siku zote swala la UDINI linaibuka tuu pale, jamaa wa dini fulani wakionekana kwamba wamekua zaidi ya vile - watu wenye mawazo kama yako - wanavyotaka iwe!
Kuna kamati kadhaa ambazo zina watu wadini mmoja tu na kuna post kadhaa ambazo (km Makatibu wakuu na wakurugenzi ktk wizara) - hali kwa tafsiri ya msimamo wako zisinge kuwa na waliomo kwa sasa. hali kama hii ikijitokeza jibu la watu kama wewe huwa hii inatokana na 'merites"
Kula la kheri kaka
Kiganja
 
Kamati Kuu ya CCM imejaa Udini?

--------------------------------------------------------------------------------

Una uhakika gani kwamba wote hao wanateuliwa kwa merits?
 
Pia utatusaidia sana sisi tusiojua, ukitutajia ni merits gani zinazotumika kuteua wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM?
 
Back
Top Bottom