Uchunguzi; Tatizo la walioajiriwa ni utegemezi; usimpe pesa mtu ambaye hajaitolea jasho

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
UCHUNGUZI; TATIZO LA WALIOAJIRIWA NI UTEGEMEZI. USIMPE PESA MTU AMBAYE HAJAITOLEA JASHO

Anaandika, Robert Heriel.

Tatizo sio kuajiriwa, tatizo ni wategemezi, tatizo ni extended Family.
Tofauti ya mtu aliyejiajiri na aliyeajiriwa IPO kwenye utegemezi.
Waliojiajiriwa hawategemewi Sana ukilinganisha na walioajiriwa.

Siku utakayoajiriwa familia na Ukoo mzima itajua. Wewe ndio utakuwa IMF Kama sio WB wa kutoa misaada katika familia na Ukoo wako.
Mbaya zaidi utakaokuwa unawasaidia sio kwamba ni watoto wadogo au Wazee Bali watu wazima wenye nguvu zao Kabisa.
Mbaya zaidi sio kwamba watataka uwakopeshe pesa alafu watarudisha, noo! Wataomba pesa kama vile watoto, utasikia; Dada au Kaka nimepata shida hapa naomba niazime laki moja unusu, Mungu atakubariki.
Usipompa shida ukimpa napo ni shida.
Na hata watakaokukopa hawatokurudishia.

Simu za karibu na mwisho WA mwezi zitakuwa nyingi mno.
Mtoto wa shangazi anataka Pesa ya sare ya shule.
Mdogo wako anataka Pesa ya Kodi anadaiwa,
Baba Mdogo anataka Pesa ya kulimia shambani. N.k.

Hii ni tofauti na aliyejiajiri, yeye hawezi kupata simu hizo labda biashara yake iwe na matokeo makubwa ya dhahiri.
Alafu hata ikiwa na matokeo ya dhahiri bado atasema amechukua mkopo mkubwa na yupo kwenye marejesho.
Utetezi mkubwa wa watu waliojiajiri ni kuwa "biashara ngumu" " vyuma vimekaza" "maisha magumu" "Vita vya Ukraine" miongoni mwa sababu zingine

Lakini aliyeajiriwa hawezi toa sababu hata moja kujitetea,
Kibongo bongo IPO hivi; KAZI YAKWAKO, MSHAHARA NI WETU.
Yaani wewe sulubika utakavyosulubika Sisi hatujui, lakini ifikapo kwenye Mshahara tutakuomba na kukupangia maisha.

Ukinunua kigari ndugu watapiga kelele na minong'ono ya chini Kwa chini,
Ooh! Ananunua Gari wakati ndugu zake ni masikini, hasaidii ndugu zake.
Ukipeleka mtoto shule za pesa, tasikia, oooh! Anatumia pesa vibaya, si ampeleke shule za kawaida tuu, mbona yeye kasomea shule hizohizo na kafaulu, mbona Sisi watoto wetu wanasomea shule za kawaida.
Alafu ni mchoyo huyo! Ukimuomba pesa anajifanya Hana, kazi kuvaa nguo za gharama"
Ajabu ni kuwa nguo zenyewe zinazoitwa za gharama sasa😀😀. Kumbe wewe unavaa ili uendane na mazingira ya kazini kwako au kazi yako.

Kuajiriwa ni KAZI Sana sio Kwa sababu ya Mshahara Mdogo hapana, Bali Kwa sababu wategemezi ni wengi Mno.

Ukiajiriwa utategemewa Kwa uhakika na watu wafuatao;
1. Wazazi wako
Hawa ni wanahaki ingawaje sio 100% percent ya kukutegemea, hawa wanapaswa wakutegemea angalau 10% tuu. Zingine wapambane na hali zao

2. Ndugu zako WA kuzaliwa
Hawa wanahaki ya kukutegemea lakini sio zaidi ya 5%
Yaani Kama anashida ya milioni moja, basi anatakiwa aombe kwako Tsh 50,000/=
Hizo nyingine wapambane na hali Yao.

3. Ndugu wa karibu
Hawa wanahaki ya mbali lakini utegemezi kwako unatakiwa uwe 1% kwako. Yaani kwenye milioni moja basi wakutegemee Tsh 10,000/=

4. Ndugu wa Mbali
Hawa wanahaki ya mbali zaidi Ila wanatakiwa wakutegemee Kwa 0.1% yaani shida Yao ya milioni moja, basi wape Tsh 5000/= 😀😀

5. Michango makanisani.
Walioajiriwa wanategemewa pia huko madhabahuni. Kanisani baada ya zaka ya 10% ambayo ni lazima, wanapaswa wakutegemee Kwa kiwango cha chini.
Sio wajipangie tuu.
Kwamba kila Muumini 50,000/= big noo.
Labda utoe Kwa mapenzi tuu na sio vinginevyo.

Waliojiajiri wao ni ngumu Sana kutegemewa na makundi hayo nje ya Wazazi au familia yake yaani mke na watoto.

Sio ajabu hapa mjini ni rahisi Sana bodaboda kununua kiwanja na kujenga kabla ya muajiriwa.
Ni rahisi Kwa watu wasio na kazi mahususi za kueleweka kununua viwanja, kujenga nyumba na kununua magari kabla ya waajiriwa kutokana na kuwa wao utegemezi huwa upo chini Sana.

Muajiriwa ili afanye maendeleo itampasa awe na roho ya Shaba, roho ngumu Kwa Kupunguza wategemezi wote Kwa kipindi Fulani ili afanye mambo yake.
Abaki tuu na Wazazi, mkewe na Watoto wake.
Tena hata hao wazazi wajue kuwa Mtoto wao anaroho ngumu anahana tabia ya kusaidia. Hii itapunguza virungu visivyo na ulazima.
Hata hivyo ukiwa na roho ngumu inatarajiwa utapata malalamiko, kashfa kama umekaliwa na Mkeo au mumeo anatumia pesa zako, ikiwezekana unaweza kulogwa Kabisa.

Kwa mtu mwenye Mshahara wa TSH 500,000/= anamke na watoto labda wawili, na mkewe anamshahara au kipato cha Tsh 300,000/= anaweza kufanya maendeleo makubwa tuu Kama atakuwa anamahesabu na nidhamu ya pesa.
Pia Kama familia itakuwa na mambo haya inaweza kufanikiwa Kwa kipato kidogo;
i. Umoja, ushirikiano na mshikamano
ii. Dira na Sera
iii. Malengo, mipango na mikakati
iv. Bajeti
v. Kiasi na mipaka

Lakini familia nyingi haziendelei sio Kwa sababu hazipati pesa Bali ni Kwa sababu zikipata pesa kila mwenza anazitumia vile atakavyo.
Ni Kama vile nchi yetu, kila kiongozi akiingia anaingia na agenda zake na kuacha za mwenzake.

Familia inajengwa nà Mke na mume, familia haijengwe na mtu mmoja, hata awe na kipato kikubwa kiasi gani. Kama hakuna umoja na ushirikiano hapo hakuna maendeleo yaani kila mtu anajali ubinafsi wake.

Walioajiriwa wengi wanajenga familia za watu wengine kuliko familia zao.
Yaani anasaidia zaidi wazazi au ndugu kuliko anavyoisaidia familia yake.
Mke anasaidia wakwao, mume anasaidia wakwao. Yaani ni mashindano ya kusaidia watu wa nje kuliko familia yenu. Mnajenga vya nje mnasahau kujenga yenu.

Hapa ndipo Gap baina ya walioajiriwa na waliojiajiri linapotekea.
Unakuta mtu anagenge lake anaingiza Mia mbili Mia mbili lakini hizo hizo ndogondogo ndizo zinanunua kiwanja, anajenga nyumba na kupangisha watu.
Kama utachunguza nyumba nyingi hapa mjini au huko kijijini niza watu waliojiajiri.

Sisemi watu wasisaidie ndugu Hasha, Bali nasema Saidia ndugu wenye uhitaji na sio kuendekeza utegemezi usio na ulazima.

Kijana akishafikisha miaka 20 afanye kazi aingize kipato, hata Kama ni kibarua cha elfu mbimbili.
Binti akishafikisha umri wa miaka 18 amemaliza shule afanye kazi ya kuingiza kipato au aolewe.

Mambo ya kukaa Kwa Ndugu burebure yanawagharimu Sana Waajiriwa Kwa sababu hawana sehemu za kuwapeleka HAO ndugu zao.
Waliojiajiri wao wanawachukua hao ndugu kwenda kusaidia Maeneo Yao ya kazi labda kuuza Duka, kulima au kufuga kuku, au kuuza genge au mkaa.
Hivyo aliyejiajiri anapata Cheap Labour kwa Mshahara wa sehemu ya kuishi na chakula.

Yakobo alivyoenda Kwa Labani alikuwa Mchungaji wa Mbuzi na ng"'ombe. Hakukaa burebure.
Na baadaye akahangaika mpaka akawa na mifugo yake.
Musa alivyoenda Midiani alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwewe Yethro.

Waajiriwa usikubali kutoa pesa kiholela, pesa lazima itolewe jasho hiyo ndio kanuni ya pesa. Ili ubarikiwe na Mungu au falme za kiroho ni lazima mtu unayempa jasho lako lazima naye atoe jasho lake kikamilifu au alishawahi kutoa jasho lake kwako. Hiyo ndio kanuni.

Sio mtoto wa mjomba sijui Ba. Mdogo au shangazi ndio iwe kigezo cha kumpa pesa za burebure.
Big noo. Kigezo cha kutoa pesa ni kuvuja jasho yaani kufanya kazi.

Ukitaka kuwa Masikini, basi endekeza tabia ya kutoa pesa burebure/utegemezi.

Vijana, hata unapompa demu pesa yako hakikisha ameitolea jasho kikamilifu, usipofanya hivyo ninakuhakikishia utaanza kuona Pesa inakukataa.

Pesa inapenda watu wanaoiheshimu ambao wengi huitwa Wabahili au wachumi. Chunguza makabila au mataifa yanayoiheshimu Pesa ndio matajiri Duniani kote.

Ukiona mtu ameajiriwa na anapesa basi jua anatumia kanuni niliyoieleza hapo.
Anaepuka utegemezi.

Mtu ale Kwa jasho, hakikisha Hilo Kwa maana ni uhakika kuwa Maisha yatahakikisha ili upate pesa lazima uhenyeke sasa iweje wewe mtu apate kwako pesa kirahisi, hauoni kuwa unatatizo kubwa la kufikiri?

Heshimu watu lakini isikufanye uwe mjinga.

Jumapili NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa FASIHI
Kwa sasa Dar es salaam.
 
UCHUNGUZI; TATIZO LA WALIOAJIRIWA NI UTEGEMEZI. USIMPE PESA MTU AMBAYE HAJAITOLEA JASHO

Anaandika, Robert Heriel.
Huwezi mpangia Mtu pesa yake Mkuu
Waajiriwa wengi wapo depressed kwa sababu mshahara Mdogo huku wakiwa na watoto kibao.
 
Sio lazma uhenyeke ndo upate pesa. Mbona yule jamaa wa singida anapata pesa zetu za tozo huku amekaa tu kwenye vieite anapgwa na kiyoyoz
 
Sio lazma uhenyeke ndo upate pesa. Mbona yule jamaa wa singida anapata pesa zetu za tozo huku amekaa tu kwenye vieite anapgwa na kiyoyoz

Unafikiri alifika hapo kirahisi?
Unafikiri waliosema No pain no gain walikuwa wajinga 😀😀

Tatizo watu wengi mnawafahamu wakishapata mafanikio.
Kipindi wakiwa wanasota hamuwajui.
 
Utegemezi unafanya watu wengine kudumaa fikra hajui namna ya kufanya aweze kuingiza chochote, lakini atakutajia wachezaji wa Yanga na Simba hata akiamka usingizini ghafla.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Unafikiri alifika hapo kirahisi?
Unafikiri waliosema No pain no gain walikuwa wajinga 😀😀

Tatizo watu wengi mnawafahamu wakishapata mafanikio.
Kipindi wakiwa wanasota hamuwajui.
Ok achana na huyu mnyiramba, vp kuhusu rizimoko na mwenzie february marope ambao wanapiga pesa kupitia channel walizotengenezewa na baba zao? Hawa wametoa jasho gan kupata hzo pesa?
 
Kaka umegusa mule mule na pia tegemea komenti kuwa chache maana umegusa kidonda cha wengi

Kuna muda unaweza jikuta unafurahia kuwa yatima na kwenu kubaki mwenyewe tu maana huna wa kukupigia kelele kihivyo hasa pale ukisimuliwa yanayowakuta wafanyakazi wenzio .

ROBERT HERIEL kongole kwa haya
 
Habari mbaya kuhus maisha hizi. Kuna sehem wasio kuwa na kazi za kufanya pia wanategemewa. Binafs sioni haja ya kuyazungumzia maisha y wat wengine
 
Sijasoma yote maana mda hautoshi... lakini nadhani tatizo halisi la kuajiriwa hasa izi ajira za 80% ya watu:-
Ni kuwa na mshahara duni lakini usioongezeka kulingana na matakwa yako au mabadiliko ya mahitaji, ... huwezi ukakua kwene ajira mpaka uongeze cv ama kupanda vyeo labda
Ila mtu aliejiajiri ana room ya kukua... kama yuko smart kama mwaka huu alikuwa na kibanda kimoja cha chips na kikaenda vizuri mwakani anaweza kuongeza viwili akaajiri vijana wakamuongezea pato... haya huwez kufanya ndani ya ajira
 
Back
Top Bottom