January 2024
TATHMINI YA ZIGO ZITO ALILOTWISHWA MUENEZI PAUL MAKONDA KURUDISHA IMANI KWA RAIA
Ziara ndefu ya Paul Makonda ambaye ni katibu uenezi, itikadi na mafunzo wa CCM imeibua na kuweka wazi jinsi chama hiki kongwe dola kimeshindwa kuweka mifumo ya utawala bora. '
View: https://m.youtube.com/watch?v=PIP2WWD5wls
Kundi la burudani la CCM TOT Plus wakipasha moto jukwaa ktk ziara ya muenezi Paul Makonda
Ziara hiyo ya muenezi wa CCM imeanzia mkoa wa Dar ikaenda Pwani na kuingia Tanga, kisha Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Singida, Tabora, Shinyanga kuelekea kanda ya Ziwa .
Baadhi ya watanzania ambao bado walikuwa wanadhani matatizo yao yanawakumba wao wachache, wamegundua kumbe wapo kwa mamia wenye matatizo kama yao.
Wananchi wamejionea wenyewe kuwa wametukana na wenzao waliobeba bahasha za kaki zenye nyaraka zao ambazo zinabeba haki zao za kila aina walizotegemea mifumo ya serikali ya CCM ingetatua lakini haijawezekana na hivyo wote kuelekeza matumaini yao kwa mtu mmoja Paul Makonda atafanya miujiza.
Picha: Katibu muenezi Paul Makonda akijaribu kutatua matatizo kwa kuongea na simu.
Miujiza ambayo kwa uhakika haiwezi kutokea kwa kuwa mfumo rasmi wa utawala bora, utendaji kazi, kuwajali watu na rasilimali za kuwezesha serikali ifanye kazi haipo.
Na udhaifu huo wa CCM umeonekana hadi kwa wanaosemekana ni viongozi wa kuchaguliwa yaani wabunge wa 2020.
Picha: Hon. Emmanuel Adamson Adamson, Mwakasaka, Mbunge (CCM) wa Jimbo, Tabora Mjini
Wananchi wa Tabora mjini wamemuambia wazi Makonda kuwa mbunge wao Hon. Emmanuel Adamson Mwakasaka, Mbunge wa Jimbo, Tabora Mjini haishi tena Tabora wala hawamuoni jimboni, ametoweka na kuwaacha kama mayatima.
Mbunge mwingine wa CCM ya 2020 wa jimbo la Same magharibi Kilimanjaro Hon. Dr. David Mathayo David naye amekataliwa wazi na watu wengi waliojitokeza waliovaa mashati ya kijani na mayowe kutanda katika mkutano Same magharibi kuwa hawamtaki.
Dr. David Mathayo David mbunge (CCM) Same Magharibi
Wananchi wengi wa kawaida sasa kweli ni wanyonge kwa kuwa wana hati za umiliki ardhi lakini haki hiyo imeporwa. Wengine wana hukumu za Mabaraza ya Ardhi au Mahakama lakini wanazungushwa kupata haki ya kurudishiwa ardhi zilizoporwa.
Wengi wamejaribu kufika ofisi wa wakuu wa wilaya ambao waliteuliwa kwa kigezo cha waligombea kuomba ubunge na kushindwa kura za wajumbe wa CCM, hivyo kupewa uDED na uDC kama kukiimarisha chama kongwe dola ngazi ya wilaya na majimbo.
Lakini hao maDC na maDED na ma RAS makada wa CCM wameonesha kushindwa kutumikia vyeo hivyo vyenye mamlaka ya maamuzi ngazi hizo za wilaya na halmashauri.
Imebidi muenezi Paul Makonda jeshi la mtu mmoja kuanza kuwapigia simu mawaziri waliopo Dodoma na Dar es Salaam ili kujaribu kuwapoza wananchi wenye kero kibao zilizoshindikana ngazi za maeneo yao.
Ni jambo la kushangaza kuwa wananchi wanaweza kumuamini waziri mgeni aliye mbali na maeneo yake ataweza kupata ufumbuzi wa kero zinazowasumbua badala ya kuwepo mifumo bora ya utawala bora kuanzia chini kwenda juu.
Je swali kuu ziara ya katibu muenezi itikadi na mafunzo yeye pekee yake kama Paul Makonda bila mifumo thabiti ya utawala katika ngazi serikali za mitaa na serikali ndiyo inaweza kuipa CCM kupata ushindi wa kishindo 2024 na 2025?
Swali jingine imani hii kwa CCM iliyobaki kiduchu huko kote anapopita Paul Makonda mwezi January 2024 inaweza kuendelea kubaki katika mioyo ya raia.
Au baada ya wananchi wenyewe kubaini na kuona wazi kwa mamia yao wameshindwa kusaidiwa, mbali walijitahidi kunyoosha vidole kama wanafunzi ktk darasa la wazi au kuonesha bahasha za hati zao, mabango ya kero wamebaini jinsi uozo wa kimfumo wa serikali ya CCM ulivyo mkubwa kumzidi Paul Makonda na hivyo mzigo umemshinda msukuma.
Na hivyo kuna uwezekano sasa kuamua kuingia katika maandamano ya amani kudai haki zao mbalimbali?