Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Uchaguzi wa Wabunge katika Majimbo ya Mpanda Mjini, Mpanda Vijijini, Majimbo kadhaa Pemba na Unguja umeahirishwa ati karatasi za kupigia kura hazikutosha! Maandalizi yote, gharama zote, muda wote huo uliopotezwa kuandaa uchaguzi huu matokeo ndo haya!
Tume ya Uchaguzi (NEC) hadi wiki ilopita ilitoa taarifa kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 98 na vifaa vilikuwa vimefikishwa kunakopaswa. Ajabu leo wanaahirisha uchaguzi kwenye baadhi ya Majimbo, NEC watuambie karatasi za kura zimepotelea au kupelekwa wapi? Nani atalipa gharama za kurudia uchaguzi majimbo hayo? Ni hao hao NEC walidai kuwa kuna nyongeza ya asilimia 10 za karatasi za kupigia kura, leo imekuwaje, zimeenda wapi?
HAwa kina Makame, Kiravu et al wajiuzulu mara moja kwa kuliingizia Taifa hasara.