Elections 2010 Uchaguzi wa Wabunge kurudiwa Mpanda, Unguja, Pemba; NEC Ivunjwe/ Wajiuzulu!

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Uchaguzi wa Wabunge katika Majimbo ya Mpanda Mjini, Mpanda Vijijini, Majimbo kadhaa Pemba na Unguja umeahirishwa ati karatasi za kupigia kura hazikutosha! Maandalizi yote, gharama zote, muda wote huo uliopotezwa kuandaa uchaguzi huu matokeo ndo haya!

Tume ya Uchaguzi (NEC) hadi wiki ilopita ilitoa taarifa kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 98 na vifaa vilikuwa vimefikishwa kunakopaswa. Ajabu leo wanaahirisha uchaguzi kwenye baadhi ya Majimbo, NEC watuambie karatasi za kura zimepotelea au kupelekwa wapi? Nani atalipa gharama za kurudia uchaguzi majimbo hayo? Ni hao hao NEC walidai kuwa kuna nyongeza ya asilimia 10 za karatasi za kupigia kura, leo imekuwaje, zimeenda wapi?

HAwa kina Makame, Kiravu et al wajiuzulu mara moja kwa kuliingizia Taifa hasara.
 
Jamani hii tume kweli imeshindwa kazi. Hawakujua idadi ya wapiga kura wao? wapiga kura wameongezeka ghafla??????????
 
Ukisikia ulimbukeni ni huu wa NEC, kwani huu uchaguzi ni Sunami ndo wasijiandae?? hata Sunami siku hizi watu wanajua wanahama makazi...Hawana cha kujibu mbele ya wananchi ..waachie ngazi vinginevyo wataondolea kwa aibu kwani muda wao unahesabika.
 
Hiyo ni janja ya NYANI TAKA CHAKACHUA jamani hamjaliona hiloo. Imepengwa hiyo wasituzuge . Ukweli inauma saana natamani kuvuruga hiyo NEC au shingo. Wamepanga hao sio bure.Baada ya kuona mwelekeo, watakuja kuongezea kwa FISADI wao kura ashinde. Hii haikubaliki.
 
Delay tactics is very effective in political combats because you have enough time to analyse the situation.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom