Wabunge waangushwa kwenye uchaguzi wa CCM Mkoa Singida

Kanyunyu

JF-Expert Member
May 2, 2012
335
495
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wabwagwa kwenye uchaguzi wa CCM Mkoa wa Singida, wabunge hao ni Mbunge wa Jimbo la Singida mjini Musa Sima na Mbunge wa Jimbo la Singida kaskazini bwana Ramadhan Ighondo waliokuwa wakigombea ujumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa (NEC) kutoka Mkoa Singida.

Wabunge hao wameangushwa na mwanasiasa machachari Yohana Msita aliyekuwa akitetea nafasi yake kwa miaka mitano ijayo.

Duru za siasa kutoka Singida zinaeleza kwamba wabunge hao pamoja na kutumia Fedha za nyingi kusaka nafasi hiyo wameishia kulambishwa mchanga na mwanasiasa wa kawaida asiyekuwa na ukwasi wa Fedha . Inaelezwa sababu ya kuanguka wabunge hao inatokana na kutokukubalika kwao katika majimbo yao na katika siasa za Mkoa wa Singida

. Uchaguzi huu umetoa taswira halisi kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa wabunge hao ambapo wapiga kura waliowakataa kwenye uchaguzi huu ndiyo hao hao watawachagua wagombea Ubunge kwenye kura za maoni 2025 .

Maoni ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Singida wanawaona wabunge hao kupoteza mvuto wa kisiasa mbele ya wananchi na ndiyo maana wameshindwa kwenye uchaguzi na mgombea wa kawaida tu asiye na misuli ya kiuchumi hivyo uchaguzi huu unatoa taswira halisi kuelekea uchaguzi Mkuu 2025.

Nawasalisha.
 
HUKO MKOA WA RUKWA MBUNGE WA SUMBAWANGA MJINI Bw.Aishe Hilal nae AMEBWAGWA NA Bw SULTAN SALEH SEIF (MAMBA) kwa WINGI wa KURA ktk Nafasi ya UJUMBE wa NEC MKOA wa RUKWA ktk Uchaguzi Uliofanyika Leo Mjini Sumbawanga.

Hongera sana Sultan kwa USHINDI wa KISHINDO

Tunamwandaa Mwingine kwa ajili ya UBUNGE 2025

Bw.Aishey Hilal Katucheleweshea sana MAENDELEO Mjini Sumbawanga na Mkoa wa RUKWA.
 
Back
Top Bottom