commited
JF-Expert Member
- Feb 27, 2012
- 1,626
- 870
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, amenusurika kipigo baada ya kutuhumiwa kuvuruga uchaguzi wa mkoa wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) akidaiwa kutaka kumpitisha mmoja wa wagombea, Dk. Harold Adamson.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tisa alasiri wakati Chatanda ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo, alipoamuru zoezi la uchaguzi huo lirudiwe baada ya kuwa ulishafanyika, kwa madai kwamba idadi ya wajumbe kutoka wilaya za Monduli na Arumeru haikuwa sahihi.
Hali hiyo ililazimu Jeshi la Polisi na maafisa Usalama wa Taifa kuingilia kati kuhakikisha amani inarejea ambapo polisi walioletwa kwenye gari aina ya Land Rover yenye namba za usajili PT 0746, waliamua kuwaamrisha waandishi kutoka nje ili wasione kilichokuwa kikiendelea ndani ya ukumbi huo.
Mara baada ya hali kutulia uchaguzi huo ulirudiwa huku ulinzi ukiwa umeimarishwa na milango ya kuelekea eneo hilo ikiwa imefungwa.
Hata hivyo vurugu hizo zinahusishwa na makundi hasimu ya urais 2015 ndani ya CCM kwani tokea chaguzi hizo zianze mkoani hapa kuanzia ngazi ya wilaya hali hiyo ilikuwa ikijidhihirisha wazi.