Uchaguzi UVCCM vurugu tupu Arusha; Chatanda apigwa, ajificha chini ya meza

commited

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,626
870
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, amenusurika kipigo baada ya kutuhumiwa kuvuruga uchaguzi wa mkoa wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) akidaiwa kutaka kumpitisha mmoja wa wagombea, Dk. Harold Adamson.

Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tisa alasiri wakati Chatanda ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo, alipoamuru zoezi la uchaguzi huo lirudiwe baada ya kuwa ulishafanyika, kwa madai kwamba idadi ya wajumbe kutoka wilaya za Monduli na Arumeru haikuwa sahihi.

Hali hiyo ililazimu Jeshi la Polisi na maafisa Usalama wa Taifa kuingilia kati kuhakikisha amani inarejea ambapo polisi walioletwa kwenye gari aina ya Land Rover yenye namba za usajili PT 0746, waliamua kuwaamrisha waandishi kutoka nje ili wasione kilichokuwa kikiendelea ndani ya ukumbi huo.

Mara baada ya hali kutulia uchaguzi huo ulirudiwa huku ulinzi ukiwa umeimarishwa na milango ya kuelekea eneo hilo ikiwa imefungwa.

Hata hivyo vurugu hizo zinahusishwa na makundi hasimu ya urais 2015 ndani ya CCM kwani tokea chaguzi hizo zianze mkoani hapa kuanzia ngazi ya wilaya hali hiyo ilikuwa ikijidhihirisha wazi.
 
kumbe ndo maana jana niliwaona mitaa ya CCM mkoa na maeneo mengi ya mjini Arusha jana walikuwa walikuwa wanaonekana na minguo yao ya kijani. Watajiju.
 
Hizo ni ishara kwamba chama bado imara, na watu wana uchu wa kushika madaraka katika chama.

hapo kuna uimara gani wa chama wakati watu wanagawanyika na kutaka kurithishana madaraka? We utakuwa umelewa magamba,nakushauri uyavue na uvae magwanda.
 
Siku hizi chaguzi za magamba unatakiwa uwe unapasha vuma na kuna wa mbio.. anyway Tendwa ni kipi chama chenye vurugu?
 
watamalizana mwaka huu, alafu dhaifu anasema magamba itadumu daima kweli kuna watu wana2mia vichwa kufuga nywele!
 
Hapo tendwa atasema ni changamoto za kisiasa.

Huyu mama alishawahi kusema uhisiano wake na rais unaenda beyond kazi za chama na serikali,yeye,mkuu wa mkoa waliletwa kwa kazi maalumu lkn cha kushangaza mkoa wa Arusha umekuwa ngome ya kubwa ya CDM,kavuruga chaguz ili mtu anayetakiwa na Ritz 1 ashinde pamoja na kumwaga hela zote hizo bado mipango yao imekwama....
 
wale wazee WAKISHILI bado wapo? nafikiri watamsaidia Tendwa kutoa tamko la hli
 
Yale yale yaliotekea Mara ya kupeana kichapo cha mbwa mwizi tena anayeiba kuku.
 
Chitanda ni katibu mkuu wa CDM Arusha, chama ambacho ni cha vurugu, alienda kufanya nini ktk uchaguzi wa CCM?
Mh Nape bado haujarudi toka shopping na kuishitaki CDM kwa kuleta vurugu ktk chaguzi zenu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom