OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,289
- 104,127
Katika uchaguzi uliopita 2010, Nassari wa CHADEMA alipata kura 27,000 wakati Sumari wa CCM ambaye alishinda na kuwa Mbunge wa jimbo alipata kura 32,000. "Mwaka 2010 niligombea ikiwa muda mfupi tu baada ya mimi kuhitimu masomo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuleta changamoto kubwa katika uchaguzi huo na rekodi zangu zinajieleza kwa kura nilizopata," anaisema kamanda Nassari. "Kwa sasa nimejipanga sana nikiwa na mtaji wa kura zaidi ya 27,000 na vyama vingine hasa CCM, hawana tena nafasi ya kupenya katika jimbo hili, nina imani kama tutaungana viongozi, wanachama na mashabiki wa CHADEMA tutashinda kwa urahisi," anazidi kufunguka kamanda Nassari...............Magamba kwisha habari yao Wanajamvi, kwa matokeo hayo mnaweza kusema nini, hasa ukizingatia nguvu ya umma kwa kipindi hiki ikiwa hot kupita kipindi chote, Naomba kuwasilisha