William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
- Thread starter
- #21
- Kwa kuanza ninasema hivi wa-Tanzania tulizoea sana kulia lia mapembeni kuhusu uwezo mkubwa kipesa waliokuwa nao baadhi ya viongozi wetu wa taifa, huku vipato vyao vikionyesha kutokuwa sawa na mali walizonazo.
- Under Mwalimu tumelia sana kichini chini kuhusu ulimbikizaji mali wa viongozi wetu, alipokuja Mwinyi ndio kabisaa ikawa kama hawa viongozi wameruhusiwa kujichotea tu, na ndipo alipoingia baba yao wa ufisadi Mkapa lo! tukajionea maajabu ya Musa na sasa awamu ya nne, kote huko tulikuwa tukilia chini chini tu, mpaka mwaka jana alipotokea kiongozi shujaa aliyeyaweka hadharani madhambi ya viongozi 10 kuhuisiana na uhujumu wao kwa taifa, na ndipo jina maarufu la mafisadi likazaliwa.
- Sasa ninasema hivi, katika jimbo la Karatu tunasema Dr. Slaa ambaye ni mbunge wa huko ni lazima arudi bungeni by any means necessary, wananchi wote wa taifa hili tupigane kuhakikisha kurudi bungeni kwa huyu shujaa wa taifa maana vita vya ufisadi vinaanza na huyu, wengine wote wamerukia treni tu, lakini huyu ni jabali tunayemuhitaji, ni kiongozi na hana uoga katika kumuangalia shetani na kumpa ukweli huku akitumia facts na evidence kama mwendo wa kisasa unavyotaka.
- Dr. Slaa kwa masilahi ya taifa ni namba moja na wananchi wote wa taifa hili tuna deni la kumlipa kwa kumrudisha bungeni tena! Sasa nitachukua maswali kabla sijaendelea na mjadala huu ambao ninaamini utachukua muda mrefu sana kuufikia mwisho.
Respect.
Field Marshall Es!