Uchaguzi 2010: Masilahi Ya Taifa Kwanza!

Hii itasaidia sana ili wagombea wapitishwe kwenye tanuru la moto la constructive cricitism huku tukichambua strength na weak points zao, siku ya siku, tunachagua kile tunachokijua, na sio kujikuta kwenye majuto kama tulivyo sasa.

- Saafi sana mkuu tupo pamoja sana hapo!

Respect.

Field Marshall Es!
 
- Heshima mbele sana Mkulu Ogah, maneno yenye nyekundu ni mazito sana, vipi mkuu kuhusu vita against mafisadi, huyu kiongozi anafaa? Ipo record?

Respect.

Field Marshall Es!
Record ya JPM kuhusu vita ya ufisadi iko wazi, pia nadhani inaeleweka ametupiwa kwenye insignificant ministry ili kumpunguza kasi yake.

Uogawangu kuhusu huyu jamaa, ni too practical, anataka vitendo bila kuchelewa, asingeweza kuvumilia delayings tactic kwa kisingizio cha utawala wa sheria, hivyo ana risk ya kuwa dictator kama ambayo Mrema alivyo.
 
Kwa maoni yangu kwenye urais, tusipendekeze ngombea wa CCM maana its a fact yupo, ni JK, huo ndio utaratibu wao. Hivyo tunapomtafuta mgombea wa upinzani atakaekubalika na wote, lazima awe na sifa za kumzidi JK, vinginevyo tunajadili washiriki sio washindani.

- Mkulu Pasco, with due respect sioni ubaya kutaja any CCM leader anayeweza kuwa na sifa za kumzidi na hata kuweza kua effective rais, tunaweza kum-influence mtu huko akachukua fomu, kama kuna anayefaa huko atajwe na sifa zake!

Respect and Later!

Field Marshall Es!
 
.
Huyo huyo unayemuita Lucifer, ndiye atatawala milele, sasa wewe peponi utakwenda kupitia wapi?.

Dawa ya kumshinda Lucifer ni ndogo nayo ni kumkataa tu, si unajua tena hana mamlaka yoyote ila ni mjanja tu na msipo angalia anakutawala milele.

Mzee vipi hukuanglia Star Tv leo wenzio tumepewa leo silaha nyingine ya kumshinda Lucifer nayo kufunga milango tu kwa yeye anasubiri mpaka mlango uwe wazi lakini hana uwezo wa kuifungua Simple!
 
Record ya JPM kuhusu vita ya ufisadi iko wazi, pia nadhani inaeleweka ametupiwa kwenye insignificant ministry ili kumpunguza kasi yake.

- Mkulu Pasco, vipi ukiiweka wazi hapa hiyo record ya huyu waziri na vita dhidi ya ufisadi? Wengine hatuifahamu!

Respect.

Field Marshall Es!
 
Mh. John Magufuli angefaa zaidi, ila mwakani nadhani Mh. Jakaya Kikwete atagombea tena ili akamilishe kipindi cha miaka 10.
 
- Mkulu Pasco, with due respect sioni ubaya kutaja any CCM leader anayeweza kuwa na sifa za kumzidi na hata kuweza kua effective rais, tunaweza kum-influence mtu huko akachukua fomu, kama kuna anayefaa huko atajwe na sifa zake!

Respect and Later!

Field Marshall Es!

Mkuu FMES,
Usitake kututwangisha maji kwenye kinu, huu ni utaratibu, japo pia kiasi fulani nakuunga mkono, utaratibu sio sheria wala sio kanuni, unaweza kubadilishwa kama walivyokabadilisha kale ka utaratibu ka zamu toka bara na visiwani, 2005 ilikuwa zamu ya Salim, King Maker akageuza kibao. Nashukuru kale ka mpokezano ka dini kanaendelea.

Tatizo la huko, ni mpaka the King Maker aridhie, jee hata akipatikana mtu safi CCM asiye na mawaa, unadhani kwa dhati kweli kautaratibu kwanaweza kuvunjwa? kuna kazi kwelikweli!.
 
Record ya JPM kuhusu vita ya ufisadi iko wazi, pia nadhani inaeleweka ametupiwa kwenye insignificant ministry ili kumpunguza kasi yake.

.

Wache wampange kwenye hivyo viwizara vidogo kwani anastahiri hilo kuna mambo aliyafanya ambayo hakutumia akili hivyo duniani unatakiwa kuwa makini kwa kila jambo.

CCM walipofanya tathimini yao juu ya nani anaongelewa na wanachi kuwa awe mrithi wa mkapa huyu jamaa ndiye aliibuka kidedea, nadhani alipata asilimia 11. jamaa kuona hivyo wakajua kuwa jamaa ni tishio kwao basi wakaanza kumwandikia speech ndipo pale magufuli alipoanza kila mkutano wake ni kutukana wapinzani kumbe jamaa walikuwa wanajua kuwa kwenye li chama wangemtafutia dawa wasi wasi wao ulikuwa akienda upinzani naye akaingia mkenge.

basi hapon ndipo jamaa alivyopoteza nafasi yake ya kuja kuwa raisi ambayo kwangu ilkuwa nyeupe kwa utendaji wa huyu jamaa labda naye aongoke kama mleta mada hii na kulamba matapishi yake
 
Matatizo ya Mtanzania ni Elim na si Ufisadi, tukiangalia eti watu wanaojifanya wanapinga ufisadi tutakuwa tunapotoka. ukosefu wa elim ndo unafanya watu kuwaweka mafisadi madarakani,mfano vijijini hawajui maana na jinsi ufisadi ulivyo hapa kwetu Tanzania. Kwahiyo basi tukitaja kiongozi tuangalie vigezo vya kiongozi na si eti anaejifanya au anaepinga kweli ufisadi.
 
Pasco,

Haya ndiyo masilahi ya taifa unayoyapigania hapa kazi kweli kweli!
Shalom, facts are sturbon things, its a fact ndiye rais wako kwa sasa, uwe ulimchagua au hukumchagua, akishaapishwa ni rais wa wote, hii ni fact, haina mjadala,

Kwa upinzani legelege tulionao kwa sasa, tutake tusitake, 2010 ni JK tena, its sad but its a fact, ndio maana napendekeza tumtafutie mshindani wa kikweli kweli ili kumsafishia njia ya 2015 na sio msindikizaji. Wote alioshindana nao 2005 walikuwa wasindikizaji ndio maana jamaa akaibuka na ushindi wa kishindo.

Akisimama na jabali kweli kweli, ndio bado atashinda lakini sio kwa tsunami, hicho kitakuwa kiashiria 2015 mabadiliko yanawezekana, vinginevyo i watu wale wale kwa mbinu zile zile na tutaendelea kuwapa ridhaa yetu watutawale milele.
 
- Mkulu Pasco, vipi ukiiweka wazi hapa hiyo record ya huyu waziri na vita dhidi ya ufisadi? Wengine hatuifahamu!

Respect.

Field Marshall Es!

To be honest sina any specific, ila ukiondoa yale maroroso yake kwenye uuzaji nyumba za serikali, na kuichepusha lami ya Mwanza-Bukoba, iliyotakiwa kupitia Biharamulo, akaipitishia kwake Chato, Jamaa is a man of impecable integrity, kwanza ni genius, pili he means what he says. He is a no nonsense man, angekuwa ni yeye, hizi kesi za EPA zingefall under Sabotage Acts, hakuna dhamana, jamaa wangeozea jela, ila pia labda, wafungwa wote zaidi ya 2000 waliohukumiwa kifo, wasingeendelea kula dola la bure pale Isanga!.
 
Hii topic me naona tujadili wagombea wabunge kuliko wa urais wa 2010.
Mbona tuna discuss kitu ambacho kipo wazi?ni bora tudiiscuss wabunge wa jimbo flani kuliko urais ambao upo wazi kabisa kuwa ni JK.
 
Mhh kama sifa ndo hizo kazi sana Tanzania, yaaani angenyima watu dhamana wakati sheria inaruhusu Mazee...soma kesi ya Daudi Pete....rule of law kuifwata ni jambo moja kubwa sasa kwa viongozi wa sasa.
 
Hii topic me naona tujadili wagombea wabunge kuliko wa urais wa 2010.
Mbona tuna discuss kitu ambacho kipo wazi?ni bora tudiiscuss wabunge wa jimbo flani kuliko urais ambao upo wazi kabisa kuwa ni JK.
Pamoja na ukweli huu, hakuna ubaya, JK akijulishwa kuwa yes yeye ndiye kinara, but he is not the best, he was the best 2005, he is not 2010, asimamishiwe jabali ili usikie Watanzania wanasema nini. Hii itamfanya awe a bit serious 2010 baada ya kujijua sasa kumbe ameendelea kwa kuhatisha kwa sababu ule ushindi wa kishindo wa 2005, umemlevya na masifa, hivyo atawala kama mwana mfalme, ki laiser affair na kila wakati yuko vakasheni.
 
Mhh kama sifa ndo hizo kazi sana Tanzania, yaaani angenyima watu dhamana wakati sheria inaruhusu Mazee...soma kesi ya Daudi Pete....rule of law kuifwata ni jambo moja kubwa sasa kwa viongozi wa sasa.
.
Yes dhamana ni haki ya mshtakiwa, sheria mbaya zinazominya haki za msingi za binadamu tumezitunga wenyewe, ukishitakiwa kwa kosa la uhujumu wa uchumi, hakuna dhamana, so do mauaji, kwenye unyanganyi wa kutumia nguvu, sheria mpaka inawalazimisha majaji wawapige mvua 30!.

Sheria hizi tumezitunga wenyewe, ila pia serikali inaziepuka baadhi yake, mfano Mramba, Yona na Mgonja, wameshitakiwa kwa kesi ndogo sana, wako nje kwa dhamana na kesi watashinda tuu anyway, Liumba amebambikiwa kesi kubwa, japo pia atashinda, lakini yuko selo. Ingekuwa kamanda ni Magufuli, ingekuwa habari ingine, kwanza asingeruhusu hata zile VIP Cell pale Ukonga zijengwe, ndani ni full AC, Plasma na menu Kempiski.
 
Siasa za Tanzania ni ngum sanaa, na zinakera na kusikitisha.
Ni kweli, ila pia nazo zinatumia Newtons law of motion, kuwa mambo yatabaki hivi hivi yalivyo mpaka ije force nyingine ibadilishe mambo.

Kama sio mimi na wewe, yeye na yule, sisi na wele na wao waliopo wataendelea kuwepo miaka nenda miaka rudi, huku tukibaki tunalalamika, tufike mahali tuache kulalamika, tufanye kweli, hata kwa kuandika tuu, JK hatufai 2010 kwa sababu moja.. mbili... tatu... na badala yake tumpe fulani kwa sababu moja.. mbili... tatu... kuna mtu atasikia na kura haitapotea bure!
 
Back
Top Bottom