Uchaguzi 2010: Masilahi Ya Taifa Kwanza!

Apr 27, 2006
26,588
10,375
- Wakuu uchaguzi mkuu wa taifa uko kwenye kona, Mzee Mandela aliwahi kusema kwamba kwenye ishu muhimu za taifa kama hizi kuwa kimyaa au kuwa neutral ni dalili za kuwa coward.

- Kwa wale tulio na influence ya namna moja au nyingine kwa taifa, ni vyema tukaweka wazi msimamo wetu kwa public kuhusu wagombea ambao tunaamini kwamba wanafaa katika kutusaidia taifa, nimekuwepo JF kwa muda mrefu sana sasa nikiwa na lengo moja tu, nalo ni siku moja kuliona taifa langu likiongozwa kwa kuheshimu sheria.

- Kwa hiyo leo nitaanza rasmi kuwataja wagombea ninaona wanafa kwa masilahi ya taifa letu, na sababu.

Respect.

FMEs!
 
Prof. Ibrahimu Lipumba for 2010 presidency...wapinazni wote wamuunge mkono tafadhali..right person in a right time.
 
- wakuu uchaguzi mkuu wa taifa uko kwenye kona, mzee mandela aliwahi kusema kwamba kwenye ishu muhimu za taifa kama hizi kuwa kimyaa au kuwa neutral ni dalili za kuwa coward.

- kwa wale influence ya namna moja au nyingine ni vyema tukaweka wazi msimamo wetu kwa public kuhusu wagombea ambao tunaamini kwamba wanafaa katika kutusaidia taifa, nimekuwepo jf kwa muda mrefu sana sasa nikiwa na lengo moja tu, nalo ni siku moja kuliona taifa langu likiongozwa kwa kuheshimu sheria.

- kwa hiyo leo nitaanza rasmi kuwataja wagombea ninaona wanafa kwa masilahi ya taifa letu, na sababu.

respect.

fmes!

nasuburi hao wagombea wako.
 
Hii itasaidia sana ili wagombea wapitishwe kwenye tanuru la moto la constructive cricitism huku tukichambua strength na weak points zao, siku ya siku, tunachagua kile tunachokijua, na sio kujikuta kwenye majuto kama tulivyo sasa.
 
Nitafurahi sana Prof. Lipumba na Maalim Seif wasipokuwepo kwenye list ya wagombea, macho na masikio yetu yamewachoka!
 
- Wakuu uchaguzi mkuu wa taifa uko kwenye kona, Mzee Mandela aliwahi kusema kwamba kwenye ishu muhimu za taifa kama hizi kuwa kimyaa au kuwa neutral ni dalili za kuwa coward.

- Kwa wale influence ya namna moja au nyingine ni vyema tukaweka wazi msimamo wetu kwa public kuhusu wagombea ambao tunaamini kwamba wanafaa katika kutusaidia taifa, nimekuwepo JF kwa muda mrefu sana sasa nikiwa na lengo moja tu, nalo ni siku moja kuliona taifa langu likiongozwa kwa kuheshimu sheria.

- Kwa hiyo leo nitaanza rasmi kuwataja wagombea ninaona wanafa kwa masilahi ya taifa letu, na sababu.

Respect.

FMEs!

Biblia inasema "kunakuwa na furaha sana mbinguni mwenye zambi mmoja akitubu " na kwa kweli leo hapa JF ni furaha kubwa sana mkerekwetwa unapofunguka macho na kuanza kuongelea masilahi ya taifa kuliko li chama lako.

Karibu sana naona neema inakuja!
 
Yaani Lipmba ataendelea kugombea tu? si atawaachia wengine sasa? Obama alisema kama unafanya vitu vilevile kwa namna ile ile usitegemee kupata matokeo tofauti.
 
kuanza kuongelea masilahi ya taifa kuliko li chama lako.

Karibu sana naona neema inakuja!
.

This is not fair comments kukiita chama cha mtu li chama, hebu wafikirie wale wengine wote wenye vyao vyao kikiwepo cha kwako ulichomo kikitwa lichama.

Tunapozungumzia maslahi ya taifa, ni over above party politics, sie wengine na mimi nikiwemo, tunaona bado hatuna hata chama kimoja cha kujiunga nacho lakini maslahi ya taifa tumo.
 
Nitafurahi sana Prof. Lipumba na Maalim Seif wasipokuwepo kwenye list ya wagombea, macho na masikio yetu yamewachoka!
Duh mbona wengi bado hatuchawachoka kila siku wanazidi kuwa makini zaidi it is time give them a chance...
 
.

This is not fair comments kukiita chama cha mtu li chama, hebu wafikirie wale wengine wote wenye vyao vyao kikiwepo cha kwako ulichomo kikitwa lichama.

Tunapozungumzia maslahi ya taifa, ni over above party politics, sie wengine na mimi nikiwemo, tunaona bado hatuna hata chama kimoja cha kujiunga nacho lakini maslahi ya taifa tumo.

Mkuu no offense lakini nadhani uswahilini tunatumia sana hiyo term ya lichama... ila sijui kama kuna maana nyingine

Tukija kwenye mada, njia rahisi ni kuweka jedwali litakaloonyesha kila jimbo na potential candidates then tunakata kila wanapopungua... nadhani wiki hii pekee kuna vijana kama watano ndani ya chama tawala wameweka wazi nia zao na kuanza kushtua wakubwa majimboni

au mnaonaje?
 
Yes its good tukianza vyovyote, pia tuandae rules of the game to avoid character assasinations na to maintain their right to privacy wakati tukiwachambua ili tuwavue nguo na kuwatia aibu.
 
Biblia inasema "kunakuwa na furaha sana mbinguni mwenye zambi mmoja akitubu " na kwa kweli leo hapa JF ni furaha kubwa sana mkerekwetwa unapofunguka macho na kuanza kuongelea masilahi ya taifa kuliko li chama lako.

Karibu sana naona neema inakuja!

- Mkuu jaribu kuheshimu taifa, kama huna cha kuchangia kuhusu masilahi ya taifa basi waachie wanaoweza,

- Na ninaomba nikukumbushe wewe na wengine wote kwamba mimi ni mwanachama mkereketwa wa CCM, sijawahi kutokwua na msimamo wala kuwa neutral katika maisha yangu huku Duniani, ninaamini kwamba chama cha CCM hakina tatizo lolote, isipokuwa tuna viongozi wachache wabovu ambao demokrasia inahitaji tuwarekebishe ili waweze kurudi tena kwenye mstari.

- Now back to the ishu ni kwamba kwa mawazo na maoni yangu ufisadi, ndio hasa tatizo kubwa linaloliangamiza taifa letu, ninaamini kwamba tukiweza kuuthibiti ufisadi, yaani kuwashughulikia viongozi wezi wa mali za taifa, yaani za wananchi basi taifa letu litafanikiwa sana katika mbio zetu za kusonga mbele. Na the only way foward ni kukazania utawala unaoheshimu sheria kwanza kabla ya anything.

- Nafasi ya Rais kwa sasa ninaiacha wazi mpaka nitakapojua wanaoiwania kutoka vyama vyote ndio tutasema wazi msimamo wetu, ingawa for now tunaweza ku-speculate na kushauri pia nani anayefaa, lakini tutasema msimamo wetu kwa wagombea walioko kwenye nafasi tayari na wale walioonyesha nia ya kutaka kugombea.

- Na kila member hapa JF, anakaribishwa sana kutoa maoni yake kuhusu nani anatufaa kiuongozi katika taifa letu.

Respect.

FMEs!
 
Yes its good tukianza vyovyote, pia tuandae rules of the game to avoid character assasinations na to maintain their right to privacy wakati tukiwachambua ili tuwavue nguo na kuwatia aibu.

chukua tano kamili pasco, maana mada nzuri ya FMES inaweka ikaharibika bila ground rules!!
 
.

This is not fair comments kukiita chama cha mtu li chama, hebu wafikirie wale wengine wote wenye vyao vyao kikiwepo cha kwako ulichomo kikitwa lichama.

Tunapozungumzia maslahi ya taifa, ni over above party politics, sie wengine na mimi nikiwemo, tunaona bado hatuna hata chama kimoja cha kujiunga nacho lakini maslahi ya taifa tumo.

Sasa Pasco nifanyeje nianze kumpamba Lucifer eti kwa sababu tu anawafuasi?
 
nafikiri ni wakati umefika upinzani ukapewa nafasi kuona kama wataweza kutupeleka mbele taifa hili angalau hatua tatu mbele na mbili nyuma!! tumekuwa na chama tawala cha sasa kwa muda na hamna makubwa zaidi yaliyofanyika!democrasia ni kuwa na vyama vingi na kama chama tawala chachemsha basi wangine wapewe nafasi, na kama nao wakichemsha nafasi apewe mwingine!
swali ni kwamba ni mgomea gani wa chama pinzani ambaye ana visifa kidogo vya kuwa rais?
 
- Mkuu jaribu kuheshimu taifa, kama huna cha kuchangia kuhusu masilahi ya taifa basi waachie wanaoweza,

- Na ninaomba nikukumbushe wewe na wengine wote kwamba mimi ni mwanachama mkereketwa wa CCM, sijawahi kutokwua na msimamo wala kuwa neutral katika maisha yangu huku Duniani, ninaamini kwamba chama cha CCM hakina tatizo lolote, isipokuwa tuna viongozi wachache wabovu ambao demokrasia inahitaji tuwarekebishe ili waweze kurudi tena kwenye mstari.

- Now back to the ishu ni kwamba kwa mawazo na maoni yangu ufisadi, ndio hasa tatizo kubwa linaloliangamiza taifa letu, ninaamini kwamba tukiweza kuuthibiti ufisadi, yaani kuwashughulikia viongozi wezi wa mali za taifa, yaani za wananchi basi taifa letu litafanikiwa sana katika mbio zetu za kusonga mbele. Na the only way foward ni kukazania utawala unaoheshimu sheria kwanza kabla ya anything.

- Nafasi ya Rais kwa sasa ninaiacha wazi mpaka nitakapojua wanaoiwania kutoka vyama vyote ndio tutasema wazi msimamo wetu, ingawa for now tunaweza ku-speculate na kushauri pia nani anayefaa, lakini tutasema msimamo wetu kwa wagombea walioko kwenye nafasi tayari na wale walioonyesha nia ya kutaka kugombea.

- Na kila member hapa JF, anakaribishwa sana kutoa maoni yake kuhusu nani anatufaa kiuongozi katika taifa letu.

Respect.

FMEs!

Mkuu FMEs! heshima mbele kaka.

Hii kitu nyekundu mkuu.....mimi nadhani hii kitu tungeiacha iwe open na tuwaachie wana JF wapendekeze ni nani na kwa sababu zipi..huwezi jua labda kuna watu watakaosukumwa na maoni ya watanzania na baadaye kuchuka form za kugombea.

Mada safi sana hii, hongera kiongozi.

Vipi Tingatinga atajaribu tena 2010 au basi tena?..

MJ
 
FMES,
Mimi nachukua msimamo tofauti kidogo na wako. Kwa kuwa umesema maslahi ya taifa nadhani itakuwa muhimu tuorodheshe kwanza matatizo tunayokabiliwa nayo kama taifa halafu ndio tuangalie katika matatizo haya ni vioingozi gani, waliopo au wanaodhaniwa, wanaweza kutusaidia kujikwamua nayo. Nimepoteza imani katika personalities.
Mimi kwa kuanza tu nataja ufisadi na rushwa kama tatizo la kwanza. La pili ni ukosefu wa uzalendo na la tatu ni tamaa ya kujitajirisha haraka kwa migongo ya walala hoi.
Tuendelee.
 
Back
Top Bottom