Uchaguzi 2010: Masilahi Ya Taifa Kwanza!

- Kwa kuanza ninasema hivi wa-Tanzania tulizoea sana kulia lia mapembeni kuhusu uwezo mkubwa kipesa waliokuwa nao baadhi ya viongozi wetu wa taifa, huku vipato vyao vikionyesha kutokuwa sawa na mali walizonazo.

- Under Mwalimu tumelia sana kichini chini kuhusu ulimbikizaji mali wa viongozi wetu, alipokuja Mwinyi ndio kabisaa ikawa kama hawa viongozi wameruhusiwa kujichotea tu, na ndipo alipoingia baba yao wa ufisadi Mkapa lo! tukajionea maajabu ya Musa na sasa awamu ya nne, kote huko tulikuwa tukilia chini chini tu, mpaka mwaka jana alipotokea kiongozi shujaa aliyeyaweka hadharani madhambi ya viongozi 10 kuhuisiana na uhujumu wao kwa taifa, na ndipo jina maarufu la mafisadi likazaliwa.

- Sasa ninasema hivi, katika jimbo la Karatu tunasema Dr. Slaa ambaye ni mbunge wa huko ni lazima arudi bungeni by any means necessary, wananchi wote wa taifa hili tupigane kuhakikisha kurudi bungeni kwa huyu shujaa wa taifa maana vita vya ufisadi vinaanza na huyu, wengine wote wamerukia treni tu, lakini huyu ni jabali tunayemuhitaji, ni kiongozi na hana uoga katika kumuangalia shetani na kumpa ukweli huku akitumia facts na evidence kama mwendo wa kisasa unavyotaka.

- Dr. Slaa kwa masilahi ya taifa ni namba moja na wananchi wote wa taifa hili tuna deni la kumlipa kwa kumrudisha bungeni tena! Sasa nitachukua maswali kabla sijaendelea na mjadala huu ambao ninaamini utachukua muda mrefu sana kuufikia mwisho.

Respect.

Field Marshall Es!
 
FMES,
Mimi nachukua msimamo tofauti kidogo na wako. Kwa kuwa umesema maslahi ya taifa nadhani itakuwa muhimu tuorodheshe kwanza matatizo tunayokabiliwa nayo kama taifa halafu ndio tuangalie katika matatizo haya ni vioingozi gani, waliopo au wanaodhaniwa, wanaweza kutusaidia kujikwamua nayo. Nimepoteza imani katika personalities.
Mimi kwa kuanza tu nataja ufisadi na rushwa kama tatizo la kwanza. La pili ni ukosefu wa uzalendo na la tatu ni tamaa ya kujitajirisha haraka kwa migongo ya walala hoi.
Tuendelee.

Mkuu hauoni kwamba matatizo tumeshayasema hadi basi!!? kwanini tusiweke majina ya potentials halafu tuangalie kama wanafit kwenye jedwali la shida zetu??

Ni maoni tu kaka
 
Mkuu hauoni kwamba matatizo tumeshayasema hadi basi!!? kwanini tusiweke majina ya potentials halafu tuangalie kama wanafit kwenye jedwali la shida zetu??

Ni maoni tu kaka

MTM heshima mbele mkuu,

Nakubaliana na wewe, matatizo tumeshayazungumza sana humu ndani, kama watu wanataka kujikumbusha waangalie thread nyingi zilizopita then warudi hapa tukate hii issue.

MJ
 
Field marshal,
Tatizo la Tanzania ni umaskini...hivi unafikiri umaskini umesababishwa na ufisadi tu? basi siyo kitu kingine? that will be wrong hypothesis to start with? kwanini wakati wa Mwalimu hakukuwa na ufisadi lakini mbona umaskini ulikuwa mbaya zaidi? mpaka kununua nyembe tunapanga foleni? tatizo ni uchumi na Prof. Lipumba ni right person for a job.
 
Mimi naanza na nafasi ya U-Rais

Napendekeza Mh. John Pombe Magufuli

kama kuna baadhi ya watu wanaoifanya CCM iwe na heshima ni pamoja na kazi anayoifanya huyu Mheshimiwa....watu wapende wasipende huo ndio ukweli wenyewe.

Sababu
Ni mchapakazi na rekodi yake inajulikana kokote kule alikofanyia kazi

Ana nia ya kweli kumpigania mtanzania, in some issues anahitaji guidance though

Ni Msomi aliyebobea (PhD Scholar) pale UDSM

Wapinga Ufisadi
Dr Slaa
Mwakyembe
Kilango
Seleli
Manyanya
et al.........

Wafanyakazi Serikalini
Blandina Nyoni

Hawa walioko kwenye Blue sub titles......wapewe madaraka pia kwenye ngazi ya uwaziri

.......tuendelee,............
 
FMES,
Mimi nachukua msimamo tofauti kidogo na wako. Kwa kuwa umesema maslahi ya taifa nadhani

1. Nimepoteza imani katika personalities.

2. Mimi kwa kuanza tu nataja ufisadi na rushwa kama tatizo la kwanza.

3. La pili ni ukosefu wa uzalendo na la tatu ni tamaa ya kujitajirisha haraka kwa migongo ya walala hoi.
Tuendelee.

- Mkuu Jasusi, hapa tupo ukurasa mmoja kwa 100%.

Respect.

Field Marshall Es!
 
- Mkuu jaribu kuheshimu taifa, kama huna cha kuchangia kuhusu masilahi ya taifa basi waachie wanaoweza,

- Na ninaomba nikukumbushe wewe na wengine wote kwamba mimi ni mwanachama mkereketwa wa CCM, sijawahi kutokwua na msimamo wala kuwa neutral katika maisha yangu huku Duniani, ninaamini kwamba chama cha CCM hakina tatizo lolote, isipokuwa tuna viongozi wachache wabovu ambao demokrasia inahitaji tuwarekebishe ili waweze kurudi tena kwenye mstari.

- Now back to the ishu ni kwamba kwa mawazo na maoni yangu ufisadi, ndio hasa tatizo kubwa linaloliangamiza taifa letu, ninaamini kwamba tukiweza kuuthibiti ufisadi, yaani kuwashughulikia viongozi wezi wa mali za taifa, yaani za wananchi basi taifa letu litafanikiwa sana katika mbio zetu za kusonga mbele. Na the only way foward ni kukazania utawala unaoheshimu sheria kwanza kabla ya anything.

- Nafasi ya Rais kwa sasa ninaiacha wazi mpaka nitakapojua wanaoiwania kutoka vyama vyote ndio tutasema wazi msimamo wetu, ingawa for now tunaweza ku-speculate na kushauri pia nani anayefaa, lakini tutasema msimamo wetu kwa wagombea walioko kwenye nafasi tayari na wale walioonyesha nia ya kutaka kugombea.

- Na kila member hapa JF, anakaribishwa sana kutoa maoni yake kuhusu nani anatufaa kiuongozi katika taifa letu.

Respect.

FMEs!

Sasa mimi nimekosea wapi mazee? Mimi nimesema kuwa ni furaha kwetu leo wewe unaongelea masilahi ya taifa na siyo li chama lako!

Kama unabisha tunaweza kuzipekuwa comments zako humu nyingi tu ambazo uliweka lichama lako mbele kuliko utaifa. natumaini kwa faida ya hii thread amabyo kwa kweli ni nzuri hautataka tufike huko kwani tutapindisha hii mada.

Si unajua tena mpaka beast atakapo panda juu ya hekalu na kusema mimi ndiye masiha, fahamu pale pale zitawajia watu na kutambua kuwa jamaa amewaingiza mkenge. Hivyo hivyo mafisadi wanapoendelea kusema wazi wazi kuwa wao ndiyo wenye chama wengi watafunguka akili na kukimbilia masalhi ya taifa

Halafu ebu nioneshe kimoja nilichosema kinachoonesha kuwa sieshimu taifa?
 
Kama tuna nia ya kweli ya kuboresha hii mada basi tujaze majimbo yafuatayo
Kyela
Kinondoni
Monduli
Ilala
Temeke
Morogoro mjini
Muleba
Dodoma mjini
Hai
Arusha mjini
Ngorongoro
Tarime
Nyamagana
Mtera
Kondoa kaskazini
Babati
Rufiji
Mkuranga
Moshi njini

Nimeanza
 
Field marshal,
Tatizo la Tanzania ni umaskini...hivi unafikiri umaskini umesababishwa na ufisadi tu? basi siyo kitu kingine? that will be wrong hypothesis to start with? kwanini wakati wa Mwalimu hakukuwa na ufisadi lakini mbona umaskini ulikuwa mbaya zaidi? mpaka kununua nyembe tunapanga foleni? tatizo ni uchumi na Prof. Lipumba ni right person for a job.

- Mkuu ninaamini kwamba haya ni maoni yako tu na sio lazima kwamba ni ya kwangu pia, lakini unaweza kuanzisha thread ambayo utauweka umasikini kama sababu, mimi kwa maoni yangu tatizo letu ni ufisadi, ninaamini hata under Mwalimu ufisadi ulikuwepo lakini kwa level ndogo sana ndio maana wananchi wengi at large hatuku-feel it, lakini sasa sio siri tena kwamba taifa tunapewa mkopo na wafadhili the next thing we know viongozi wa juu wanaporomosha majumba huko baharini, wananchi tunazidi kuwa masikini,

- Tukiziba njia za wizi, basi tutaweza kuuushinda umasikini haya ni maoni yangu na wewe una haki ya kuwa na ya kwako, isipokuwa tu tatizo hapa litakuwa hii thread yangu haitakidhi matakwa yako ya umasikini as the leading ishu!

es
 
Sasa mimi nimekosea wapi mazee? Mimi nimesema kuwa ni furaha kwetu leo wewe unaongelea masilahi ya taifa na siyo li chama lako!

Kama unabisha tunaweza kuzipekuwa comments zako humu nyingi tu ambazo uliweka lichama lako mbele kuliko utaifa. natumaini kwa faida ya hii thread amabyo kwa kweli ni nzuri hautataka tufike huko kwani tutapindisha hii mada.

Si unajua tena mpaka beast atakapo panda juu ya hekalu na kusema mimi ndiye masiha, fahamu pale pale zitawajia watu na kutambua kuwa jamaa amewaingiza mkenge. Hivyo hivyo mafisadi wanapoendelea kusema wazi wazi kuwa wao ndiyo wenye chama wengi watafunguka akili na kukimbilia masalhi ya taifa

Halafu ebu nioneshe kimoja nilichosema kinachoonesha kuwa sieshimu taifa?

- Mkuu naomba kurudia tena CCM ni chama changu, record yangu hapa JF na nje ya hapa iko wazi, taifa kwanza chama baadaye,

- mengine siwezi kukusaidia maana najua una matatizo mengi sana, pole sana! ila mchawi wako sio mimi ni wewe mwenyewe na tabia zako, sasa mkuu naomba kurudi kwenye kujadili taifa!

Respect.

FMEs!
 
FMES,
Mimi kwa kuanza tu nataja ufisadi na rushwa kama tatizo la kwanza. La pili ni ukosefu wa uzalendo na la tatu ni tamaa ya kujitajirisha haraka kwa migongo ya walala hoi.
Tuendelee.

Jasusi tatizo la rushwa kwa kweli linakera sana ila kuna nchi zina rushwa kuzidi sisi na zinakimbia kimaendeleo ( Ukitaka muongozo wa kitaalam hapo hebu mfuatilie Prof mmoja wa oxford nadhani anitwa Khan). Lakini hakuna nchi ambayo imeendelea bila kuweka mazingira ya kibiashara kuwa mazuri na nchi yetu kwa ilivyo sasa si nchi ya kibiashara kabisa na hatutaendelea.

Halafu ukitaka kujua kuwa tuna viongozi laana kabisa wakati watu wa bara la ulaya miaka ya 50's walipotaka kuwatoa watu kwenye umaskini walichofanya ni kuwatoa watu kwenye kilimo na kuwapeleka kwenye biashara sis leo tunaanza kufanya kinyume chake na "Kilimo kwanza"
 
Duh mbona wengi bado hatuchawachoka kila siku wanazidi kuwa makini zaidi it is time give them a chance...

Nakuunga mkono, haijalishi mtu amejaribu mara ngapi, kinachomatter anakuja na sera gani. Abraham Lincoln alijaribu urais wa Marekani kwa mara 7, akafanikiwa mara ya 8.
 
Prof. Ibrahimu Lipumba for 2010 presidency...wapinazni wote wamuunge mkono tafadhali..right person in a right time.

- Nafikiri wapinzani watakuwa wamekusikia, by the way kwa nini mkuu unafikiri Lipumba anafaa na hata aungwe mkono na wapinzani wote?

es!
 
- Mkuu naomba kurudia tena CCM ni chama changu, record yangu hapa JF na nje ya hapa iko wazi, taifa kwanza chama baadaye,

- mengine siwezi kukusaidia maana najua una matatizo mengi sana, pole sana! ila mchawi wako sio mimi ni wewe mwenyewe na tabia zako, sasa mkuu naomba kurudi kwenye kujadili taifa!

Respect.

FMEs!

Mkuu mbona unataka kuharibu mada uliyoianzisha mwenyewe kwa nia nzuri tu?
 
Sasa Pasco nifanyeje nianze kumpamba Lucifer eti kwa sababu tu anawafuasi?
.
Shalom, kwenye maslahi ya taifa, siasa za vyama weka nyuma, don't call names vyama vya watu, twende kwenye mada maslahi ya taifa bila kujali vyama.

Huyo huyo unayemuita Lucifer, ndiye atatawala milele, sasa wewe peponi utakwenda kupitia wapi?.
 
Thanks Mkuu kwa kujaribu ku-moderate!!! NI mada nzuri sana lakini tusipoangalia itaishia kulekule
 
Mimi naanza na nafasi ya U-Rais

Napendekeza Mh. John Pombe Magufuli

kama kuna baadhi ya watu wanaoifanya CCM iwe na heshima ni pamoja na kazi anayoifanya huyu Mheshimiwa....watu wapende wasipende huo ndio ukweli wenyewe.

Sababu
Ni mchapakazi na rekodi yake inajulikana kokote kule alikofanyia kazi

Ana nia ya kweli kumpigania mtanzania, in some issues anahitaji guidance though

Ni Msomi aliyebobea (PhD Scholar) pale UDSM

...

- Heshima mbele sana Mkulu Ogah, maneno yenye nyekundu ni mazito sana, vipi mkuu kuhusu vita against mafisadi, huyu kiongozi anafaa? Ipo record?

Respect.

Field Marshall Es!
 
Sina tatizo na Prof Lipumba, ila tunajiuliza tunamhitaji mgombea mshindani au mshiriki, kama ni mshiriki its fine, kama ni mshindani, ashindanishwe kwa sifa na ma presidential materials, apite chekecheke tuje nyuma yake.

Kwa maoni yangu kwenye urais, tusipendekeze ngombea wa CCM maana its a fact yupo, ni JK, huo ndio utaratibu wao. Hivyo tunapomtafuta mgombea wa upinzani atakaekubalika na wote, lazima awe na sifa za kumzidi JK, vinginevyo tunajadili washiriki sio washindani.
 
Back
Top Bottom