Wakuu,
Ni wazi sasa baada ya kumpumzisha mwenzetu-(R.I.P) jimbo litakuwa wazi.
Ninaomba niwaambie wazi wenzetu wa CDM kwamba wananchi wana imani kubwa na aliyekuwa mgombea wenu Joshua Nassary. Msije mkajidanganya mkamteua mtu mwingine.Ni wazi kwa nguvu ya CDM sasa wenye pesa watajipenyeza kugombea ili waukwae ubunge.
Nawaambia wazi kamati kuu ya CDM mkimchakachua Joshua Nassary tutakuja huko makao makuu na mabango na tutawafungia ndani ya ofisi kwa kufuli.
Dr Slaa najua uko huku jamvini.Hakikisha wajanja hawatapenyeza pesa kwa ajili ya kumtosa kijana wetu Nassary.Tuna imani kubwa na huyu kijana.Kamati kuu hakikisheni mnamtendea haki huyu kijana.
Huyu kijana ni machachari mfano wa Lema, Mnyika, Zitto nk.
Hayo ni mawazo yangu kwenu kamati kuu.Tupeni chaguo tunalolitaka.